Tuesday, June 14, 2011

TWANGA PEPETA KUSHAMBULIA KAWE

                     

Bendi  maarufu ya muziki  jijini Dar es salaam ya African Stars "Twanga pepeta" inatarajia kufanya onesho lake la mwanzo wa juma siku ya Ijumaa tahehe 16.06.2011  katika ukumbi wa Massae gardaen view uliopo Kawe  Tanganyika peckers.

Kwa mujibu wa mratibu wa onesho hilo bw. Albert Kawogo,onesho hilo linatarajiwa kuanza saa 3.00 usiku ambapo kiingilio kitakuwa  5000/=.

Kawogo amewataka mashabiki wa Twanga pepeta  kujitokeza kwa wingi hasa wakazi wa kawe na maeneo ya jirani kwa kuwa hilo ni onesho maalum kwa wakazi wa maeneo hayo ambao huifuata bendi hiyo maeneo mengine.

Ninawahakikishia wapenzi wa burudani ya muziki kuwa  kutakuwa na burudani ya kutosha na usalama wa kutosha hivyo waianzie wikiendi yao Kawe kwa kusugua kisigino ,alisema Kawogo.

Blog ya kimkeventertainment inawatakia msuguo mwema. 

Tuesday, May 31, 2011

MBWANA SAMATA ALIVYOPOKELEWA LUBUMBASHI

 Tajiri wa TP Mazembe Moise Katumbi Chapwe  aliyeshika kinasa sauti akimwita Mbwana Samatta i;li mtambulishe kwa viongozi na mashabiki.
 Mbwana Samatta akitoa mawili matatu kwa viongozi na mashabiki wa TP Mazembe.
 Mbwana Samatta akiingia uwanjani chini ya ulinzi mkali.
Rais wa TP Mazembe akiwa amewasili uwanjani.

Wednesday, May 25, 2011

BARABARA YA KIBITI - LINDI BADO KASHESHE

 Abiria waendao Lindi na Mtwara  wakiwa wameshuka baada mabasi kukwama  katika eneo la Malendego kilometa 18 kufika Somanga siku ya Ijumaa tarehe 20 Mei 2011.Kwa miaka ya karibuni eneo kati ya Kibiti hadi Somanga huleta usumbufu mkubwa kwa wasafiri wakati wa msimu wa mvua kwasababu ya eneo kutokuwa na lami, pamoja na ujenzi kuendelea kwa kipindi kirefu sasa.
Abiria wakibadilishana mawazo mara baada ya mabasi kukwama.

Thursday, May 19, 2011

WAREMBO WA MISS UNIVERSE 2011 WAINGIA KAMBINI

Mratbu wa shindano la urembo la Miss universe Maria Sarungi akitoa maelezo kwa warembo kwenya hoteli ya Golden Turip jijini Dar es salaam leo.Warembo 20 wanatarajia kupanda jukwaani ambapo shindano hilo linatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Wednesday, April 27, 2011

KARIBU ALPHA LODGE - BAGAMOYO





Apha lodge iliyopo mtaa wa wakojani (shopping centre) ni hoteli ya hadhi ya kati iliyofunguliwa upya hivi karibuni chini ya mkurugenzi Mwanaidi Katendasi ambaye pia ni mkufunzi wa Taasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo -Tasuba.Kwa mujibu wa meneja wa Alpha huduma za chakula ,vinywaji na malazi hupatikana hapo kwa viwango vya hali juu na kwa bei nafuu.Karibuni sana Bagamoyo karibuni Alpha.

Saturday, April 23, 2011

BENDI YA CHIKICHA ORIGINAL YAUSHIKA MJI WA BAGAMOYO

 Rais wa bendi na mwimbaji kiongozi wa bendi Masoud Kilimanjaro akiwajibika kwenye moja ya maonesho ya bendi kwenye ukumbi wa hoteli ya Skylight mjini Bagamoyo hivi karibuni.

 Zungu likipagawishwa na dansa wa Chikicha original
 Dansa namba moja wa Chikicha original akishambulia jukwaa
 Mpigaji wa gitaa la solo na mwimbaji, Kibugila a.k.a KB akiwajIbika.
 Mwimbaji Hassani Mabele akiwakonga roho mashabiki wa Chikicha original.
 Mwimbaji anayechipukia kwa kasi Amour Bebesi akishambulia jukwaa.
Mashabiki wa Chikicha original Dalla Zambo a.k.a mzee wa chenji kota( kushoto) akiwa na mashabiki wengine kwenye moja ya maonesho ya Chikicha original kwenye hotel ya Skylight hivi karibuni.