Wednesday, August 10, 2011

TUSKER ALL STARS YABAMBA




KAMANDA MAYUNGA AAGWA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha Luteni Jenerali mstaafu, Silas Peter Mayunga, aliyefariki hivi karibuni. Shughuli ya kugwa kwa mwili ya marehemu Mayunga imefanyika leo Agost 10, katika Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha Luteni Jenerali mstaafu , Silas Peter Mayunga, aliyefariki hivi karibuni. Shughuli ya kugwa kwa mwili ya marehemu Mayunga imefanyika leo Agost 10, katika Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwiny, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Shimbo na Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakiwa katika shughuli ya mazishi kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali mstaafu,  Silas Mayungi kwenye Viwanja vya Kambi ya Jeshi Lugalo leo Agost 10.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Mawaziri wastaafu, Joseph Sinde Warioba na Salim Ahmed Sailm, wakiwa katika shughuli ya mazishi kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali mstaafu,  Silas Mayungi kwenye Viwanja vya Kambi ya Jeshi Lugalo leo Agost 10
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Mayungi, wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Viongozi wa Serikali, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo Agosti 10.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Peter Mayunga, wakati wa shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo Agost 10.

Tuesday, August 9, 2011

VODACOM YATOA SUPPORT YA KUJIWEKA FIT

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakifanya mazoezi kwenye viwanja vya chuo, cha simu Kijitonyama jijini leo.Mazoezi yamedhaminiwa na Vodacom

VIMWANA WA MISS TANZANIA 2011 WAPIGWA MSASA

 Warembo wanao wania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakifuatilia mafunzo katika semina maalum ya warembo hao inayoendelea katika Hotel ya Giraffe Ocean View iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Warembo hawa baada ya kumalizika semina hii watahamia katika Jumba la Vodacom House.

Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Miss Tanzania, Hasim Lundenga (katikati) akifafanua jambo wakati wa semina maalum kwa washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2011. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Nsao Shalua na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel.

Warembo wakiunga mkono hoja kwa kuipigia makofi. Warembo 30 wapo kambini kwaajili ya kujifua na mchuano huo utakao fanyika mwezi Septemba jijini Dar es Salaam.

Wanyange hawa leo watapandaa jukwaani katika shindano dogo la kumsaka Miss Top Model. Mrembo ambaye moja kwa moja atapata tiketi ya kuingia nusu fainali za Miss Tanzania.

JK AMPOKEA RAIS WA SOMALIA

 Rais Kikwete kulia akiwa na mgeni wake  rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Kikwete akisalimiana na mgeni wake mara baada ya kuwasili .
 Askari wa JWTZ wakiwa kwenye gwaride rasmi la kumpokea mgeni.

Wasanii wa JKT wakitoa burudani kabla ya ujio wa mgeni.

Tuesday, August 2, 2011

SALAMU ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Ally Mohamedi Sheini akisoma salamu za mwezi mtukufu wa ramadhani,ambapo aliihasa jamii kutenda mema ndani ya mwezi kwa kutii yote yaliyoagizwa  na mwenyezi mungu.

Aidha blog ya KIMKEV inawatakia kila la kheri waislmu wote katika mwezi huu wa toba.

HAMIA AIRTEL NGWASUMA YASHIKA MJI WA SONGEA

 Kiongozi wa FM Academia Nyoshi Elsadat(wa pili kushoto) akiwaongoza wanamuziki wenzake waliposhambulia jukwaa mjini Songea mwishoni  mwa wiki iliyopita kwenye onesho lililodhaminiwa na Airtel.
 Pablo Masai wa FM Academia akishambulia jukwaa.
 Wanenguaji wa FM Academia wakiwapagawisha wakazi wa mjini Songea .
Wakazi wa mjini Songea wakiserebuka.