Sunday, August 14, 2011

KAMANDA MAYUNGA AZIKWA


Maafisa wa Jeshi la Wananchi wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Luteni Jenerali Silas Mayunga kuelekea kaburini tayari kwa mazishi yaliyofanyika Agosti 12, 2011 Nyumbani kwake Maswa Mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwepo Rais Jakaya Kikwete.
Maafisa kutoka Jeshi la Wananchi wakishusha jeneza lililohifadhi mwili wa Marehemu Luteni Jenerali Silas Mayunga kaburini.
Rais Jakaya Kikwete akiongoza mamia ya waombolezaji waliohudhuria mazishi ya marehemu Luteni Jenerali Silas Mayunga nyumbani kwake huko Maswa mkoani Shinyanga.
Rais Jakaya Kikwete na mkewe Salama Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la Luteni Jenerali Silas Mayunga

Saturday, August 13, 2011

NELLY NDIYE MWAKILISHI WETU MISS UNIVERSE 2011

Unayemuona pichani ni Nelly Kamwelu,Miss Universe Tanzania 2011.Nelly ndiye atakayebeba bendera yetu akituwakilisha katika mashindano ya dunia ya Miss Universe ambayo kwa mwaka huu yatafanyikia huko Sao Paulo,Brazil ndani ya Credicard Hall kunako tarehe 12 September,2011.Tunamtakia kila la kheri Nelly katika maandalizi yake.
Close to perfection

KCB YAAGWA VIONGOZI WAKE


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Edmund Mndolwa (kushoto) akimkabidhi zawadi ya ngao Mkurugezi wa Benki hiyo anayemaliza muda wake, Joram Kiarie baada ya kuitumikia wa kipindi cha miaka 6 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCB  Kenya, Peter Muthoka (kulia)  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCB Tanzania, Edmund Mndolwa na Mkurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Joram Kiarie wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya kuwaaga  baadhi ya Wakurugenzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Edmund Mndolwa akizungumza.
Mwenyekiti wa Bodi  ya Wakurugenzi wa Benki ya KCB na Baadhi ya Wakurugenzi wa benki hiyo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kuwaaga baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye  akiwa na moja ya zawadi ambayo alikabidhiwa mmoja ya Wakurugenzi  wa benki hiyo  wakati wa hafla ya kuwaaga baadhi ya wakurugenzi wa benki  jijini Dar es Salaam

Friday, August 12, 2011

WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA UN

Waziri Mkuu, MIzengo Pinda akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro kwenye makazi yake Mjini Dodoma Augost 11, 2011.
Waziri Mkuu, MIzengo PInda na mkewe Tunu wakiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Taifa, Dk. Asha Rose Migiro kwenye makazi ya Waziri Mkuu Mjini Dodoma Augost 11, 2011 baada ya mazungumzo yao

WASHIRIKI WA MISS VODACOM TANZANIA 2011 NDIYO HAWA



Leyla Juma
 Jeniffer Kakolaki
 Mwajabu Juma "Top Model"
Mariaclara Mathayo
Cynthia Kimasha
Christine William
Hamisa Hassan
 Alexia William
Stacy Alfred
 Asha Salehe
Zubeda Seif
Rose Hulbert
 Maua Kimambo
Glory Samuel
Neema Mtitu
Atu Daniel
Blessing Ngowi
Weirungu David
Chiaru Masonobo
Irene Karugaba
Delillah Ghalib
 Tracy Sospeter
Husna Twalibu
Loveness Flavian
Christine Mwegoha
Husna Maulid
Zerulia Manonko
Salha Israel
Glory Lori
Stella Mbuge.

Wednesday, August 10, 2011

MWAJABU ATWAA TAJI LA VODACOM TOP MODEL 2011

 Mshindi wa Taji la Top Model Vodacom Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma akipozi mbele ya camera baada ya kutajwa kuwa ndiye mshindi na mrembo wa kwanza kuingia Nusu Fainali itakayokuwa na warembo 15 bora wa Vodacom Miss Tanzania 2011
 Usipokubali kushindwa we si mshindani...warembo wenzake walioingia 5 bora ya Top Model wakishangilia na kukubaliana na matokeo baada Mwajabu Juma kutangazwa.
 Mwajabu Juma akionesha makeke yake baada ya kutangazwa..
 Top Model wa Vodacom Miss Tanzania 2011 Mwajabu Juma akipongezwa na warembo wenzake.
Kutoka kushoto ni Jeniffer Kakolaki, Alexia William, Zerulia Manonko, Cynthia Kimath na Mwajabu Juma wakiwa katika pozi kabla ya kutangazwa mshindi