Friday, September 16, 2011

MISS TANZANIA 2011 ENZI ZA RUKSA


 Miss Tanzania 2011 Salha Izrael akiwa  katika pozi tofauti wakati wa utoto wake. Salha alivikwa taji la Miss Tanzania 2011 wiki iliyopita Septemba 10, 2011 katikashindano lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

SOKO LA MWANJELWA MBEYA LAUNGUA


Hii ndiyo hali halisi ya moto unaowaka katika soko la Mwanjelwa mjini Mbeya, moto aulioanza asubuhi leo majira ya saa tatu asubuhi, ambapo imedaiwa kwamba moto huo umesababishwa na hitilafu ya mfumo wa umeme katika soko hilo. Inasemekana kuwa hali ni mbaya na uwezekano wa vikosi vya zimamoto kuzima moto huo ni mgumu kutokana na kwamba umeshaenea maeneo mengi ya soko hilo kwani gari mbili zilizokwenda kujaribu kuzima moto huo zimeshindwa, Sokoni hapo kuna vibanda vingi vya wafanyabiashara ndogondogo na maduka ya wafanyabiashara wa kati. Shuhuda wetu ambaye yuko eneo la tukio anasema watu wanakimbia huku na kule ili kuokoa maisha na kuna wengine wanaaguka na kuzirai pia kuna akina mama wawili ambao wamevujika wakati wakikimbia kujiokoa ma moto huo. Taarifa zaidi za madhara ya kibinadamu na hasara ya mali tutawaletea kadiri tutakavyokuwa tukizipata kutoka eneo la tukio.
Moto mkubwa ukiwaka katika soko hilo kama linavyoonekana.
Watu wakihangaika huku na kule ili angalau kuokoa mali zao.
Umati wa watu ukiwa umekusanyika eneo la Mwanjelwa kituo cha mabasi Mwanjelwa.
Watu waengine wakiwa juu ya magari ili kushuhudia tukio hilo ambalo ni la tatu kutokea mkoani Mbeya.

Thursday, September 15, 2011

JK ATEUWA WAKUU WAPYA WA MIKOA



RAIS Jakaya Kikwete (pichani) amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa nchini.
Katika mabadiliko hayo, amewateua Wakuu wa Mikoa wapya 15, kuwabadilisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa watano na wengine saba wamestaafu kwa mujibu wa taratibu. Mkuu wa Mkoa wa Singida amebaki kwenye kituo chake cha kazi wakati Wakuu wa Mikoa wengine wanne watapangiwa kazi nyingine.
Aidha, Wakuu wa Mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika watatangazwa baadaye.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Wakuu wa Wilaya 11 wamepandishwa Vyeo na kuwa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo: Bw. John Gabriel Tupa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara; Bw. Saidi Thabit Mwambungu (Ruvuma); Bi. Chiku S. Gallawa (Tanga); Bw. Leonidas T. Gama (Kilimanjaro); Dk. Rehema Nchimbi (Dodoma); Bw. Elaston Mbwillo (Manyara); Kanali Fabian Massawe (Kagera); na Bibi. Fatma Abubakar Mwassa (Tabora). Wakuu wa Wilaya wengine walioteuliwa ni Bw. Ali Nassoro Rufunga, (Lindi); Eng. Ernest Welle Ndikillo, (Mwanza); na Bw. Magesa Stanslaus Mulongo Mkuu wa Mkoa (Arusha).
Walioteuliwa nje ya nafasi hizo ni Eng. Stella Manyanya (Rukwa); Bibi Mwantumu Mahiza, (Pwani); Bw. Joel Nkaya Bendera (Morogoro) na Bw. Ludovick Mwananzila (Shinyanga).
Waliobadilishwa vituo vya kazi ni Bw. Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza; Bw. Said Mecki Sadiki anayekwenda Dar es Salaam akitokea Lindi; Bibi Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma; Lt. Kanali Issa Machibya anayekwenda Kigoma akitokea Morogoro; na Kanali Joseph Simbakalia anayekwenda Mtwara akitokea Kigoma. Dk. Parseko Ole Kone ataendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Waliostaafu ni Bw. Mohammed Babu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera; Bw. Isidore Shirima aliyekuwa Arusha; Kanali (mst.) Anatory Tarimo aliyekuwa Mtwara; Bw. John Mwakipesile, aliyekuwa Mbeya. Wengine ni Kanali Enos Mfuru aliyekuwa Mara; Brig. Jen. Dk. Johanes Balele aliyekuwa Shinyanga; na Meja Jen. Mst. Said S. Kalembo aliyekuwa Tanga.
Wakuu wa Mikoa wanne waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni Bibi Amina Mrisho aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani; Dk. James Msekela aliyekuwa Dodoma; Bw. Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Bw. Daniel Ole Njoolay aliyekuwa Rukwa.
Wakuu wote wa Mikoa waliopo sasa wameagizwa kuandaa Hati za Makabidhiano (Handing Over Notes) katika muda wa siku 14 kuanzia siku ya kuapishwa kwa Wakuu wapya wa Mikoa. Aidha Wakuu wa Wilaya ambao wamepandishwa vyeo kuwa Wakuu wa Mikoa nao wanapaswa kufanya hivyo hivyo kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya watakaopangiwa vituo vitakavyokuwa vimeachwa wazi kutokana na uteuzi wao.
Wakuu wa Mikoa ile minne mipya na Wakuu wa Wilaya watakaoteuliwa hapo baadaye nao watatakiwa kuandaa Hati za Makabidhiano ndani ya siku 14 tangu kuapishwa.
Makabidhiano hayo lazima yahusishe pia kutembelea kwa pamoja baadhi ya maeneo na miradi ambayo ni muhimu kama sehemu ya makabidhiano yao.
Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa na Wakuu wa Mikoa minne mipya wakaoteuliwa pamoja na Wakuu wote wa Wilaya watakaoteuliwa baada ya zoezi kukamilika watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya wiki tatu kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kiuongozi na kiutendaji.
Wakuu hao wapya wa mikoa wataapishwa siku ya Ijumaa, Septemba 16, 2011 saa 4.00 asubuhi kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wakuu hao wapya wa mikoa; vituo wanavyokwenda na vituo walivyotoka ni kama ifuatavyo:




Na.
JINA LA MKUU WA MKOA
KITUO AENDAKO
KITUO ATOKAKO
1.
Bw. Saidi Mecki Sadiki
DAR ES SALAAM
RC - Lindi
2.
Bw. John Gabriel Tupa
MARA
DC - Dodoma
3.
Bw. Saidi Thabit Mwambungu
RUVUMA
DC - Morogoro
4.
Kanali Joseph Simbakalia
MTWARA
RC Kigoma
5.
Bi. Chiku S. Gallawa
TANGA
DC - Temeke
6.
Bw. Abbas Kandoro
MBEYA
RC Mwanza
7.
Bw. Leonidas T. Gama
KILIMANJARO
DC – Ilala
8.
Dkt. Parseko Ole Kone
SINGIDA
RC Singida
9.
Eng. Stella Manyanya
RUKWA
Mbunge V/Maalum
10.
Bibi Christine Ishengoma
IRINGA
RC Ruvuma
11.
Dk. Rehema Nchimbi
DODOMA
DC - Newala
12.
Bw. Elaston John Mbwillo
MANYARA
DC – Mtwara
13.
Col. Fabian I. Massawe
KAGERA
DC - Karagwe
14.
Bibi. Mwantumu Mahiza
PWANI
Mbunge/NW Mstaafu
15.
Bibi. Fatma A. Mwassa
TABORA
DC - Mvomero
16.
Bw. Ali Nassoro Rufunga
LINDI
DC - Manyoni
17.
Eng. Ernest Welle Ndikillo
MWANZA
DC - Kilombero
18.
Lt. Col. Issa Machibya
KIGOMA
RC Morogoro
19.
Bw. Magesa S. Mulongo
ARUSHA
DC - Bagamoyo
20.
Bw. Joel Nkaya Bendera
MOROGORO
Mbunge/NW Mstaafu
21.
Bw. Ludovick Mwananzila
SHINYANGA
Mbunge/NW Mstaafu
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM
JUMATANO, SEPTEMBA 14, 2011.

MISS ANGOLA LEYLA LOPES NDIYE MISS UNIVERSE 2011

We have a new Miss Universe from Angola, Africa and a soon-to-be household name: Leila Lopes.
Most of you may remember the south central African nation of Angola as taking a spanking from America's First Dream Team, but they now have a major victory thanks to the beautiful Leila Lopes.

Wednesday, September 14, 2011

DK BILAL AZINDUA JENGO LA MIHADHARA DUCE


Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal akikata utepe kuzindua jengo jipya la kisasa la mihadhara la Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) lenye uwezo wa kuchukua wanachuo 2,000 jana jijini Dar es salaam.Kulia kushoto ni makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam utawala Prof. Yunus Mgaya na Prof. Salome Misana (kushoto).

KAMATI YA MISS TANZANIA YAOMBA RADHI KWA WAZANZIBAR


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.

YAH: KUOMBA RADHI  KWA NDUGU ZETU WALIOPATWA NA MAAFA YA AJALI YA MELI HUKO ZANZIBAR .

Usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe 10 / 09 2011 tukio kubwa na la huzuni lilitokea huko Zanzibar ambapo wananchi wengi walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati walipopatwa na ajali ya kuzama kwa MELI iliyokuwa ikitoka Unguja kuelekea Pemba .

Kwa bahati mbaya siku hiyo ya Jumamosi taaasisi yetu ilikuwa inahitimisha Fainali za Taifa za Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2011.

Kama waandaaji wa Mashindano haya na wenye Mamlaka kamili ya maamuzi juu ya ama kuendelea au la kuahirisha jambo hili, tulipatwa na mshituko mkubwa sana juu ya tukio hilo .
 
Kamati yetu ilikaa na kutakafari katika tukio hilo kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
  • Taarifa kamili ya maafa haya tuliipata rasmi saa tisa na nusu mchana ( 9:30 ) siku ya jumamosi ambayo ilikuwa ni  masaa machache kabla ya Fainali za Miss Tanzania kuanza katika ukumbi wa Mlimani City .
  • Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo ya Yanga na Ruvu Shooting.
  • Katika kumbi za starehe ikiwemo mabaa na burudani za muziki wa bendi na kumbi za disco ziliendelea kama kawaida.
  •  Muda uliokuwa umebaki kuwakilisha jina la mshiriki wetu kwenye fainali za Miss World zilikuwa zimekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza nafasi hiyo
  •  Pia tamko rasmi la kusimamisha shughuli zote za burudani lilianza tarehe 11 septemba 2011 kuomboleza Kitaifa maafa hayo.
Hata hivyo kama waandaaji tulifanya shindano tukiwa katika maombolezo kwani kabla ya kuanza shindano Watu wote waliokuwepo ukumbini walisimama kimya kwa dakika moja na hata washiriki walipoingia kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza walikuwa wamevaa vitambaa vyeusi katika mikono yao ikiashilia maombolezo.

Hali hii imetupa mkanganyiko na kujikuta tukiendelea na mashindano kitu ambacho tunaona tumewakosea Watanzania wenzetu.

 Kama Waandaaji tunapenda kusistiza kwamba tunawajibika kwa hayo yaliyotokea na si Taasisi yeyote au Kampuni yeyote na tunaomba ichukuliwe kama ni makosa ya kibinaadamu hasa ukizingatia mazingira magumu tuliyokuwa nayo kwa wakati huo na mkanganyiko wa matukio na taarifa za tatizo hilo.
KUOMBA RADHI
Hata hivyo shughuli hiyo inawezekana imewakwaza watu wengi na kwa sababu hiyo na pia hali halisi ya janga hilo na kwa niaba ya viongozi wenzangu na wadau wa shughuli zetu tunatoa tamko la dhati kwa Familia za ndugu wote walikumbwa na maafa haya, wale wote walionusurika katika ajali hii na  Watanzania wote kwa ujumla, kwamba TUNAWAOMBA RADHI KWA MKANGANYIKO ULIOTUTOKEA HADI KUFIKIA HALI HII. Hatuna neno zaidi ya kusema na kusisitiza “TUNAOMBA RADHI”

Mwenyezi MUNGU  aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.

Hashim Lundenga
Mkurugenzi

Tuesday, September 13, 2011

MNUSO WA NICOLAUS NA CECILIA NDANI YA LUGALO BARACKS TAREHE 03 SEPTEMBA 2011

 Bw na bibi Nicolaus Mkini mara baada ya ndoa takatifu iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam.
 Mrs Cecila Mkini akiwa kwenye pozi.
 Nibebe nibembembeleze.
 Maharusi wakiwa na wapambe wao.
 Maids wakiwa wanaingia ndani ya ukumbi
 Mzee Mgaya akitambulisha familia ya bwana harusi
 Kijana wa siku nyingi Msitingongo akitoa nasaha kwa maharusi.
 Mc Kim Kimenya akifungua champaigne kwa ajili ya wageni waalikwa.
 Mama Mkini akiwa kwenye pozi.
 Mc Stan Mkini  akiwajibika.
 Dr. Mkini akiwa pamoja na mama Mkini wakitoa neno la baba na mama.
 Hawa ndiyo madada waliotawala mchezo kwa siku hiyo wakiwa kwenye pozi chini kuanzia kushoto Ninah,Diana,Grace,Suda.Juu kuanzia kushoto Anna,Asta,na rafiki wa karibu wa Asta.
 Katibu wa kamati ya maandalizi bw. Joel Mkini aliyeinamisha kichwa akiwa na somethingi yake kwa karibu kwenye picha ya pamoja na wanakamati.
 Shindano la kucheza twisti lililompa ushindi Msitingongo kijana wa siku nyingi likiendelea.
Kamati ya maandalizi sambamba na dada Mtage, aliyevaa gauni la buluu,Diana kushoto kwake na Anna Kivembele mwenye gauni jeusi wakielekea kwa maharusi kwa mkono wa pongezi .