Monday, September 19, 2011

Moto mwingine wateketeza soko la Forest Magorofani mjini Mbeya


Moto mkali uliozuka majira ya saa 9 usiku wa kuamkia jana umeteketezabaadhi ya vibanda vya biashara na mali katika soko dogo la Forest jijini Mbeya kabla ya vikosi vya zima moto vikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Evans Balama kufanikiwa kuuzima moto huo. Moto huu umezuka tena ikiwa ni siku chache tu baada ya moto  mwingine kuteketeza soko jijini humo wiki hii.

Tanzanian Shillings (TZS) to 1 US Dollar (USD)


Tanzanian Shillings (TZS) to 1 US Dollar (USD)



 The graph above displays historical exchange rates between the Tanzanian Shilling and the US Dollar.Between 21/3/2011 & 16/9/2011

Friday, September 16, 2011

MKENYA AINGIA UWANJANI AKIWA UCHI WA MNYAMA




Jamaa mmoja mwenye asili ya kenya aliingia uwanjani akiwa uchi wa mnyama kwenye mechi kati ya England na Argentina kwenye michuano ya Rugby World Cup - 2011 inayofanyika nchini New Zealand .

Inasemekana jamaa ni mzaliwa wa Kenya ana miaka 23 na alikua hajavaa kitu zaidi ya kuchora uso wake,na alikatiza kwenye uwanja wa Otago na kuonekana na mamilioni ya watazamaji wa television duniani,baadaye alikamatwa na wana usalama na huenda akakabiliwa na kifungo che miezi 3 jela au faini ya dola 5,000.
Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa jamaa huyo aliamua kufanya hivyo ili kujizolea umaarufu duniani.

AIRTEL RISING STAR KUANZA KESHO

AIRTEL RISING STARS KURINDIMA JUMAMOSI

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Airtel, Jackson Mbando (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam juzi, kuhusu maandalizi ya michuano ya Aitel Rising Stars, inayotarajia kuanza Jumamosi kwenye Uwanja wa Karume jijini.Kutoka kulia ni Ofisa Tawala wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Idd Mshangama na OIfisa Habari wa TFF, Boniface Wambura. (NA MPIGAPICHA WETU)

MISS UNIVERSE TANZANIA AREJEA


Miss Universe Tanzania 2011,Nelly Kimwelu akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam jana, baada ya kuwasili akitokea Brazil alikoshiriki fainali za Dunia za mashindano hayo, ambapo alifanikiwa kuingia katika 16 bora na kushika nafasi ya saba katika vazi la kitaifa. (NA MPIGAPICHA WETU)

YANGA TEE YAFUFUKA NA KUCHABANGA AFRICAN LYON 2-1


Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kupata bao la pili la ushindi dhidi ya African Lyon katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Azam, eneo la Chamazi, Mbagala, Dar es Salaam jana jioni.

JK AWAAPISHA WAKUU WAPYA WA MIKOA LEO


 Rais Jakaya Kikwete leo amewaapisha wakuu wapya wa mikoa aliowateua hivi karibu katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Pichani ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Morogoro, JoelNkaya Bendera akipokea nyenzo zake za kufanyia kazi baada ya kula kiapo mbelea ya Rais.
Rais Jakaya, akimwapisha, Saidi Thabiti Mwambungu, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi mamlaka Fatuma Abubakar Mwassa, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Abbas Hussein Kandoro, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Leonidas Tutubert Gama, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza jambo na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati washerehe hizo za kuwaapisha wakuu wapya wa mikoa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wa zamani, Daniel Ole Njoolay (kushoto) akiteta na Mkuu wa mkoa huo wa sasa, Stella Manyanya katika sherehe za kuwaapisha wakuu wa mikoa zilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
 Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo za kuwaapisha wakuu wapya wa mikoa.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa walioteuliwa kushika nyadhifa hizo baada ya kuwaapisha katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo