Sunday, January 15, 2012

Kada wa CCM aliyemwagiwa tindikali arejea kutoka India


MKAZI wa Igunga, Kada wa CCM, Mussa Tesha aliyekuwa katika matibabu India baada ya kumwagiwa tindikali usoni na watu wanaodaiwa kuwa wa CHADAEMA, wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo mwaka jana, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, baada ya kurejea nchini. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni za CCM jimboni humo.

KADA wa CCM, mkazi wa Igunga, Tabora, Mussa Tesha (24) aliyekuwa akipatiwa matibabu India, baada ya kuwagia tindikali na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema wakati wa kampeni za uchagfuzi mdogo jimboni humo mwaka jana, amerejea nchini.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba alisema leo kwamba, Tesha amerejea juzi, akiwa amepona kiasi cha kuweza kuzungumza na kuona jicho moja huku lingine likiwa bado halioni vizuri kutokana na athari alkizopata.

Akizungumza nyumbani kwake Tegeta Mwisho, Dar es Salaam, Mwigulu ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni za CCM Igunga, alisema amemhifadhi Tesha nyumbani kwake wakati akisubiri kwenda tena India kuendelea kuendelea na matibabu madogo yaliyosalia.

Mwigulu alisema, Chama Cha Mapinduzi ambacho kiligharamia matibabu yote, hadi sasa kinaendelea kumhudumia Tesha mpaka atakapopona kabisa na kuwa na uwezo wa kufanya kazi.

"Hadi sasa tunashukuru kwamba amepona anaweza kuzungumza, kusikia na kuona walau jicho moja, tofauti na mwanzo alivyokuwa mara alipomwagiwa tindikali, hata hivyo hali yake haijaweza kuwa ya kufanya kazi mbalimbali kama za juani, hivyo CCM tunaendelea kumsaidia mpaka ajenge uwezo wa kujitegemea", alisema.

Alisema, CCM imefanya mpango wa kuwaugnanisha wabunge wa CCM kumtayarishia mtaji ambao utamsaidia Tesha kuendesha maisha yake baada ya kukumbwa na madhara hayo.
Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu amwagiwe tindikali, Tesha amewashukuru Watanzania kwa kumuombea wakati wote alipokuwa mgonjwa na kwamba anaamini dua zao ndizo zimemwezesha kubakia hai hadi sasa.

Tesha alisema, baada ya kumwagiwa tindikali Septemba 9, mwaka jana, hakujitambua hadi alipokuwa katika hospitali ya KCMC ambako alipatiwa matibabu na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikaa wiki tatu kabla ya kupelekwa India.

Akiwa India kwenye Hospitali ya Apollo, Tesha alikuwa chini ya uangalizi wa baba yake mdogo, Samwel Bethwel ambaye pia gharama za kuwa huko zimebebwa na CCM. Anatarajia kwenda tena India baada ya miezi mitatu.

Thursday, January 5, 2012

Balozi wa Oman,akutana na Rais Dk. Shein


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Oman Ali Ahmed Saleh,aliyefika kujitambulisha na kumuaga Rais kutokana na wadhifa wake huo alioupata Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Oman Ali Ahmed Saleh,aliyefika kujitambulisha kwa Rais Ikulu Mjini Zanzibar.
Picha na Ramadhan Othman IKulu

Kundi la Boko Haram lashambulia mji wa Maiduguri


Mashambulio mawili ya mabomu yametokea katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria yakiwa ndio machafuko ya kwanza kutokea tangu kutangazwa kwa hali ya hatari mjini humo.
Hakuna majeruhi yaliyoripotiwa katika ghasia hizi zinazodhaniwa kutekelezwa na wapiganaji wa kundi la kiislam lilopigwa marufuku la Boko Haram.
Kundi hilo linawataka waumini wa dini ya kikristo kutoka kusini mwa nchi hiyo waishio kaskazini mwa nchi kuondoka mara moja.

Msichana auawa

Awali, msichana mmoja aliuawa wakati wa ufyatulianaji wa risasi katika ya wapiganaji wanaoaminika kuwa wa kundi hilo la Boko Haram na maafisa wa polisi katika jimbo la Jigawa.
Jumapili iliyopita kundi hilo la Boko Haram lilitoa makataa kwa watu kutoka jamii ya wakristo kusini mwa Nigeria, waondoke maeneo ya Kaskazini mwa nchi.
Rais Goodluck Jonathan ametangaza hali ya hatari katika majimbo manne nchini humo.

Mgomo juu ya ruzuku ya mafuta

Mashambulio hayo yanatokea huku maandamano kupinga kuondolewa kwa ruzuka ya mafuta ya petroli yakiendelea.
Katika eneo la Liberation Square mjini Kano , maafisa wa polisi nchini humu wametumia gesi ya kutoa machozi na virungu kuwatawanya wanafunzi waliokuwa wakiandamana katika eneo lilowazi kupinga kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yameshutumu kitendo hicho cha polisi.
Aidha, Raia nchini humo wamechukizwa na tangazo la serikali hapo Jumapili kwamba itaondolewa ruzuku hiyo ambayo inaigharimu serikali mamilioni ya dola katika mapato.

KAJIMA KUJENGA UPYA BARABARA YA KILWA

Sehemu ya Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam, ambayo kwa mujibu wa makubaliano ya Serikali ya Japan na Tanzania yaliyofikiwa Dar es Salaam, itajengwa tena upya na Kampuni ya Ujenzi ya Kajima baada ya awali kuvurundwa.
Waziri wa Ujenzi, John Magufuli (kushoto) akibadilishana hati za makubaliano na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada baada kutiliana saini mkataba ambapo Serikali ya Japan imekubali Kampuni ya Kajima kurudia tena kujenga upya Barabara ya Kilwa ambayo ilijengwa vibaya na kampuni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika, Dar es Salaam

ALIYETUHUMIWA KUMUUA MEJA WA JESHI AFIKISHWA KIZIMBANI

Mtuhumiwa wa mauaji ya mwanajeshi Meja John Tawete (58) wa Kikosi namba 603, Airwing, Aisha Hamis akitoka Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam jana, baada ya kusomewa shitaka la mauaji. Anayemsindikiza ni Koplo Khamisa.

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA BALOZI ATHUMANI MHINA KIJIJINI MNYUZI, KOROGWE, MKOANI TANGA JANA

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais Mstaafu Mh Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu Mh Frederick Sumaye, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Bara Mh Pius Msekwa na wao mbolezaji wengine kwenye mazishi ya Mwenyekitiwa Jumuiya ya Wazazi Taifa Balozi Athumani Mhina kijijini Mnyuzi, Korogwe, mkoani Tanga jana Jumatano January 4, 2012.
Rais Kikwete akiweka udongo kaburini
Waziri Mkuu Mstaafu Mh Frederick Sumaye akiweka udongo kaburini
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mh Pius Mzekwa akiweka udongo kaburini
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akiweka udongo kaburin
Rais Kikwete akiongozana na viongozi wengine kuelekea kaburini
Mwili wa balozi Athman Muhina ukihifadhiwa katika nyumba ya milele.
Wanafamilia ndugu jamaa na marafiki wakilia kwa uchungu mkubwa
   Mwili wa Balozi Balozi Athumani Mhina ukiombewa kabla ya kuelekea katika mazishi.Picha na Ikulu

HAMAD RASHID ATIMULIWA CUF

 
Mbunge wa Wawi kwa tikeri ya CUF, Hamad Rashid Mohammed (pichani) amefukuzwa katika chama hicho.          

Taarifa zilizopatikana jana, zimesema Hamadi ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu CUF, amefukuzwa pamoja na viongozi wengine kadhaa akiwemo Mjumbe wa Baraza Kuu mkoa wa Tanga, Doyo Hassani.

      Wengine waliokumbwa na fagio hilo la kutimuliwa ni Hamis Shoka (Mjumbe wa Baraza Kuu, Pemba), Juma Sanaani (Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama hicho, wakati Mjumbe wa Baraza Kuu Mbeya Yassin Mrotwa amepigwa bonge la karipio au karipio kali.

      Katika makali yake ya kujivua gamba, taarifa zimesema wanachama wengine ambao si wajumbe wa Baraza kuu, walitarajiwa kuhojiwa ili kuchukukiwa hatua.

        Kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Hamadi na wengine waliofukuzwa wanayo fursa ya kukata rufani  kwenye mkutano mkuu wa Taifa wa chama hicho.