Friday, February 10, 2012

BEACH BORA RESORT “a new era of leisure & entertainment”KUZINDULIWA LEO



Kiwanja cha maraha cha Beach bora resort kinatarajiwa kuzinduliwa jioni ya leo tarehe 10.02.2012 baada ya kubinafsishwa na kupata uongozi mpya.Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mjini Bagamoyo asubuhi ya leo kutoka kwa mkurugenzi  wa Beach bora resort bw. Mussa Maganga uzinduzi huo utatawaliwa na burudani kutoka kwa madj wa maarufu wa mjini Bagamoyo.

“Tunatarajia shughuli yetu kuanza saa 12:00 jioni na ninawahakikishia wageni waalikwa wote huduma ya hali ya juu na usalama wa kutosha” alisema Maganga.

Beach bora resort yenye mandhari nzuri ipo kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi mjini  Bagamoyo na inapakana kwa karibu kabisa na Taasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo(Tasuba).

Wednesday, February 1, 2012

FRANCIS CHEKA MADA MAUGO KUGOMBEA UBINGWA WA IBF RAUNDI 12 APRIL 28 PTA SABASABA

 

Makamu mwenyekiti wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini, Madaraka Nyerer (Kushoto) akiwaelekeza mabondia Fransc Cheka kulia na Mada Maugo jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)

Bondia Mada Maugo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba uho leokupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)


Bondia Fransic Cheka akizungumza na waandishi wa habari leo kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

RATIBA YA UCHAGUZI NA NAFASI ZA UONGOZI BIAFRA SPORTS CLUB

RATIBA YA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA KWANZA WA VIONGOZI WA KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA UTAKAOFANYIKA TAREHE 11 MACHI, 2012.

Mara baada ya kupata usajili rasmi toka serikalini klabu ya michezo ya Biafra imejipanga kufanya uchaguzi mkuu wa kwanza wa viongozi ambao unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 11 Machi, 2011. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo Bw. Abdul Mollel, ratiba hiyo ya uchaguzi inafuatiwa na uchukuaji wa fomu za uanachama kwa mujibu wa ratiba inayoonekana hapa chini: -Ratiba ya uchukuaji na urudishaji fomu mbalimbali
1. Fomu za maombi ya uanachama zimeanza kuuzwa tarehe 28 Januari, 2012
2. Tarehe ya mwisho ya kurudisha fomu za uanachama ni 15 Februari, 2012
3. Fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zitaanza kutolewa tarehe 19 - 22 Februari, 2012
4. Mwisho wa kurejesha fomu za kugombea nafasi za uongozi ni tarehe 25 Februari, 2012
5. Uchaguzi mkuu wa viongozi utafanyika tarehe 11 Machi, 2012


Nafasi za uongozi zitakazogombewa katika uchaguzi huo ni kama ifuatavyo: -
1. Mwenyekiti
2. Makamu mwenyekiti
3. Katibu Mkuu
4. Katibu Mkuu Msaidizi
5. Mweka Hazina
6. Wajumbe watano (5) watakaoingia kwenye kamati ya utendaji
7. Wajumbe nane (8) wa kamati ya uchumi na mipango
8. Wajumbe saba (7) wa kamati ya ufundi
9. Wajumbe saba (7) wa kamati ya nidhamu na rufaa
Kwa maelezo, maoni na maswali wasiliana na katibu wa klabu kwa anuani ifuatayo: -
BIAFRA SPORTS CLUB,
SIMU: +255 715 253 653
EMAIL: biafra.jsclub@gmail.com
HQ: MTAA WA ISELE, 90 DEGREES PUB, KINONDONI
DAR ES SALAAM

BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LAANZA

 Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Kigoma Kusini, Davida Kafulila mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha kwanza cha Mkutano wa Sita wa Bunge mjini Dodoma jana
 Spika wa Bunge, Anne Makinda akitoka ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya kuahirisha Kikao cha kwanza cha Mkutano wa Sita wa Bunge la Tanzania mjini Dodoma jana Januari 31,2012.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha kwanza cha Mkutao wa sita wa Bunge mjini Dodoma jana
Spika wa Bunge, Anne Makinda akisalimiana na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha kwanza cha Mkutano wa sita wa Bunge mjini humo jana.

Airtel yafanya semina nchini kuhusu Airtel Money


 Mkurungezi wa fedha wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Kalpesh Mehta akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa mashirika na wadau mbalimbali walioalikwa na kuhudhuria seminar hiyo iliyofanyika leo na kuendeshwa kwa siku mbili katika makao  makuu ya Airtel , lengo likiwa
ni kuwaeleimisha wafanyabiashara na mashirika mbalimbali jinsi huduma ya Airtel money inavyoweza kutoa suluhisho la matatizo yanayowapata katika kuendesha biashara zao.
  Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi  ya Airtel Sam Elangallor akiongesha kwa vitendo jinsi gani huduma ya Airtel money inavyofanya kazi na kutoa shuluhisho kwa changamoto wanazozipata katika kuendesha biashara kwa wawakilishi kutoka katika makapuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo iliyofanyika Makao makuu ya Airtel, pichani anayefata ni Mkurungezi wa fedha Kalpesh Mehta na Meneja huduma Airtel money Asumpya Naligingwa.
 Mkurugenzi wa mahusiano wa Airtel Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa semina ya Airtel money inayotolewa kwa makapuni mbalimbali jana kwa muda wa siku mbili, uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na wadau wengi na waandishi wa habari
wadau waliohudhuria wakichangia hoja Mmoja wa wakilishi kutoka katika makampuni yaliyohudhuria semina ya huduma za Airtel money akichangia hoja wakati wa semina hiyo iliyozinduliwa rasmi leo na kuendesha na Mkurugenzi wa Airtel Sam Ellangallor na Mkurugenzi wa fedha Kalpesh Meltha katika ofisi za makao makuu ya Airtel.
 ==========  ============ =============== =========

Jumanne, 31 Januari 2012, Dar es saaalam, katika kuhakikisha huduma ya pesa mkononi inawafikia watanzania wengi Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel jana imeendesha semina ya huduma ya Airtel money kwa  wadau  na sekta mbalimbali wakiwemo wadau wa usafirishaji, asasi za kifedha, wakuu wa  shule na vyuo vya elimu ya juu kwa lengo la kupambanua faida za kutumia huduma  mpya ya Airtel Money katika shughuli zao zinazohusiana na maswala ya kulipa au kupokea fedha.


Akizungumza wakati wa semina iliyohudhuriwa na wadau hao na kufanyika katika makao makuu ya Airtel Tanzania Afisa Mkuu wa Biashara Walingo Chiruyi alisema "lengo la semina hii ni kutaka kujadiliana na wadau wetu faida za kuitumia huduma yetu hii mpya ya Airtel Money katika shughuli zao za kila siku.


Tumegundua huduma hii ni nyenzo muhimu sana katika kuweka urahisi usalama zaidi pamoja na kupunguza hatari zinazotokana na kutembea na fedha nyingi au kukaa ofisini na fedha nyingi kwa lengo la kuzitumia
katika shughuli za wiki nzima au kulipa mahitaji mbalimbali Airtel Money ni suluhisho la kufanya hayo yote na ndio maana leo hii tumekaa pamoja kwa lengo la kuweka kila kitu bayana kwa wadau hawa
muhimu kwetu! 

Aliendelea kusema Bw, Akitoa maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia huduma ya Airtel money ambapo kwa kupitia huduma hiyo wateja wanaweza kulipa Ankra kama vile Ada ya shule, Mishahara ya wafanyakazi au vibarua, Kufanya makusanyo ya mauzo ya siku, kulipia huduma za DSTV, Luku, bili ya Dawasco, kulipia visa ya USA, pamoja na kutuma na kupokea hela ndani na nje ya nchi.,


Aidha kwa wafanya biashara za usafirishaji huduma ya Airtel money itawasaidia katika kupunguza risk za wizi wa fedha na kuwaakikishia usalama madereva wakiwa safarini kwani malipo yote ya bidhaa baada ya
usambazaji hayatafanyika tena kwa pesa taslimu bali kwa kupitia huduma ya Airtel money.


Kwa mabasi ya abiria wateja sasa wataweza kufanya booking na kulipa nauli kwa kupitia huduma ya Airtel money ambapo mteja hatakuwa na ulazima wa kutembelea kituo cha basi kukata tiketi na kulipia gharama
za nauli .


Huduma ya Airtel money pia itapunguza gharama zilizopo katika kupata huduma za kifedha , na kwakupitia mtandao wetu ulioenea zaidi nchi nzima na mawaka waliosambaa kote tuna uhakika wa kuwafikia watanzania
wengi zaidi walioko mjini na vijijini aliongeza Bi, Kazimoto.


Airtel hivi karibuni ilizindua na kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamefaidi  kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania wengi  kwa kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hii, Huduma ya  Airtel money sasa ina mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa nchi nzima  hivyo ili kukamilsha upatikanaji wa huduma hii ya kisasa na rahisi zaidi .

MTUME NA NABII MWINGIRA ATIWA MBARONI DAR

KIONGOZI wa Kanisa la Efatha, Nabii na Mtume Josephat Mwingira amekamatwa na polisi  katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, akituhumiwa kuharibu mali za mfanyabiashara, Zain Sharifu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, ACP Charles Kenyela, Mwingira alikamatwa wiki iliyopita na kushikiliwa kituoni hapo.
Hata hivyo, Kenyela alisema, Mwingira alidhamiwa baada ya kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kuvunja na kuharibu mali ndani ya Kiwanda cha Uchapaji cha Afroplus kinachomilikiwa na mlalamikaji.

“Tumemkamata kiongozi huyo ili atoe ufafanuzi wa kina baada ya kupokea malalamiko hayo, “ alisema Kenyela alipozungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita ofisini kwake.
Kenyela alisema, mashtaka hayo yalifikishwa polisi na Zain, Januari 8, mwaka huu, akidai kwamba walinzi binafsi wa kiongozi huyo wa kanisa, walivamia kiwandani kwake na kuharibu mali baada ya kufanya fujo.

Aliongeza kuwa polisi baada ya kupata taarifa hizo, walikwenda eneo la tukio kushuhudia na kukuta mali zilizoharibiwa, hivyo walimtaka Mwingira kufika polisi ili atoe ufafanuzi lakini alikaidi ndipo polisi ikatumia nguvu kumkamata.

“Alipoulizwa Mwingira kuhusu madai hayo alijitetea uwa eneo hilo ni mali halali ya Efatha tangu Juni 17, 2005, baada ya kulinunua kutoka kwa mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Mangula, hivyo anasubiri tamko la Mahakama ya Ardhi Tanzania ambako shitaka limepelekwa,” alisema.
Baada ya Mwingira kuhojiwa kituoni hapo, Kenyela aliwakutanisha na Zain ambaye ni mlalamikaji na kuwataka wasiendelee kugombana, badala yake wasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu kesi hiyo.
Kamanda Kenyela alifafanua kuwa mwanamke aliyemshitaki Mwingira ni mmoja wa wamiliki 11 wa viwanda vilivyokuwa ndani ya Kitalu namba 90, Mwenge, Dar es Salaam.

Awali, Mwingira alisema, aliwataka wamiliki wa viwanda hivyo kuhama ili kupisha upanuzi wa kanisa na viwanda 10 vilitekeleza ombo hilo.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa makampuni 10 ambayo yalitakiwa kuhama na Mwingira na kutekeleza ni Metal Works, Timber Malt Tech, Auto Ran Makongo, Container Global, Simon Engineering, Safe Man, Profession Investigation, Elbe Ltd, Zana za Kilimo Mbeya na Kilimanjaro Machine Tools Ltd.

Januari 17 mwaka huu, katika toleo lake namba 721 gazeti hili liliripoti kusakwa kwa Mwingira na askari 20 waliofika kanisani kwake kwa lengo la kumkamata.
Askari hao waliokuwa katika magari mawili aina ya Land Rover ‘Difenda’ walifika kanisani kwa Mwingira baada ya kupata taarifa za kutokea kwa fujo kati ya wafuasi wa kanisa na wafanyakazi wa viwanda cha Afroplus kinachopakana na kanisa hilo, Mwenge, Dar lakini walimkosa.

Kamanda Kenyela alisema alimtuma mkuu wa polisi wa wilaya (OCD) kumpelekea Mwingira barua ya wito ili afike ofisini kwake na kutoa onyo kwamba kama akikaidi, wao polisi wasilaumiwe.
Baadhi ya wananchi waliokuwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay baada ya kumuona Mwingira walisema ni kitendo cha aibu kwa viongozi wa makanisa ya kiroho kufikishwa polisi.

“Siyo Mwingira tu, tumekuwa tukiona viongozi wengi wa makanisa ya kiroho wakifikishana polisi na watu au wao kwa wao, ningeshauri haya mambo wayamalize kwa kuelewana uraiani. Wana uwezo wa kuombea matatizo, hilo linawashinda nini? Zamani ilikuwa ni mwiko kuona kiongozi wa dini akifika polisi kulalamika au kulalamikiwa,” alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Frida Gabriel aliyedai kuwa ni mlokole.
 
chanzo unique entertainment