Tuesday, February 28, 2012

Jose Mourinho aweka rekodi ya LA LIGA


FASTEST RUN TOWARDS 50 VICTORIES IN LA LIGA
CoachTeamPWDL
MourinhoReal Madrid625066
GuardiolaBarcelona6750116
Miguel MuñozReal Madrid70501010
VillalongaReal Madrid / At. Madrid78501018
Van GaalBarcelona79501217
CapelloReal Madrid80501812
CruyffBarcelona80501614
BruReal Madrid8250626
RijkaardBarcelona85502213
E.FernandezBarcelona / Real Madrid85501520

FASTEST REAL MADRID COACHES TO REACH 50 VICTORY MARK IN LA LIGA
CoachGames
Mourinho62
Miguel Muñoz70
Beenhakker74
Capello80
Boskov81
Bru82
Molowny91
Del Bosque92
Miljanic92
FASTEST RUN TOWARDS 50 VICTORIES IN LA LIGA
CoachTeamPWDL
MourinhoReal Madrid625066
GuardiolaBarcelona6750116
Miguel MuñozReal Madrid70501010
VillalongaReal Madrid / At. Madrid78501018
Van GaalBarcelona79501217
CapelloReal Madrid80501812
CruyffBarcelona80501614
BruReal Madrid8250626
RijkaardBarcelona85502213
E.FernandezBarcelona / Real Madrid85501520

FASTEST REAL MADRID COACHES TO REACH 50 VICTORY MARK IN LA LIGA
CoachGames
Mourinho62
Miguel Muñoz70
Beenhakker74
Capello80
Boskov81
Bru82
Molowny91
Del Bosque92
Miljanic92

MAKOCHA POULSEN (TAIFA STARS), ANGELS (MAMBAS)

Makocha Jan Poulsen wa Tanzania (Taifa Stars) na Gert Josef Angels wa Msumbiji (Mambas) kesho (Februari 28 mwaka huu) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya timu zao. Taifa Stars na Mambas zitapambana Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni katika mechi ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini. Mkutano huo na waandishi wa habari ambapo makocha hao pia watajibu maswali ya waandishi wa habari utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Mambas iliwasili nchini jana (Februari 26 mwaka huu) ikiwa na wachezaji 19 na viongozi kumi. Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho ni Francisco Muchanga, Clesio Bauque, Almiro Lobo, Manuel Fernandes na Francisco Massinga. Wengine ni Joao Rafael, Nelson Longomate, Joao Mazive, Zainadine Chavango, Osvaldo Sunde, Luis Vaz, Carlos Chimomole, Joao Aguiar, Edson Sitoe, Jeremias Sitoe, Stelio Ernesto, Elias Pelembe, Eduardo Jumisse na Simao Mate. 

MECHI YA YANGA, ZAMALEK KUCHEZWA SAA 12

Mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Zamalek na Yanga itachezwa Machi 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jeshi jijini Cairo kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Misri. Kwa mujibu wa maelekezo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mechi hiyo itachezwa bila washabiki  kwa vile Zamalek inakabiliwa na adhabu ya kucheza mechi hiyo bila washabiki. Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco ambao ni Jihed Redouane, Rouani Bouazza na Bekkali Mimoun wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Gihed Greisha wa Misri. Kamishna wa mchezo huo ni Ben Khadiga wa Tunisia. 

 WASOMALI KUCHEZESHA SIMBA, KIYOVU

Mwamuzi i Yabarow Hagi Wiish na wasaidizi wake Aweis Ahmed Nur na Abdirahman Omar Abdi, wote kutoka Somalia ndiyo watakaochezesha mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Kiyovu Sport ya Rwanda. Kwa mujibu wa orodha ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), mwamuzi wa akiba kati mechi hiyo namba 14 itakayochezwa Machi 4 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam atakuwa Waziri Sheha wa Tanzania.  Kamishna wa mechi hiyo ya raundi ya awali atakuwa Jean Marie V. Hicuburundi kutoka Burundi.  CAF imeziingiza moja kwa moja kati raundi ya kwanza timu 16 kutokana na ubora wake. Timu hizo ni ES Setif (Algeria), Interclube (Angola), Asec Mimosas (Ivory Coast), Enppi (Misri), AS Real Bamako (Mali), CO de Bamako (Mali) na CO Meknes (Morocco). Nyingine ni WAC (Morocco), Warri Wolves (Nigeria), Heartland (Nigeria), St. Eloi Lupopo (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Us Tshinkunku (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Amal Otbara (Sudan), Al Ahly Shandy (Sudan), CSS (Tunisia) na CA (Tunisia).

Thursday, February 23, 2012

Matumizi ya Digitali katika Televisheni


Waziri wa wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu usitishwaji wa matangazo ya Televisheni kwa kutumia Technolojia ya analogia na kuhamia teknolojia ya utangazaji ya dijitali  ambao utasitishwa rasmi tarehe 31 Disemba mwaka 2012 saa sita kamili usiku. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dk. Frorens Turuka.

Pinda ziarani Meatu


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akialimana na Wananchi wa  na viongozi wa wilaya ya Meatu baada ya kuwasili katika kijiji cha Mwandoya akiwa katika ziara ya Mkoa wa Shinyanga Februari 22, 2012.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Ally Nasoro Rufunga na  wapili kushotoni  Mkuu wa Wilaya ya Meatu Abihudi Saideya.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Afisa Biashara wa  Wilaya ya Bariadi, Leonard   Batigashaga akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Febeuari 22, 2012. Kulia ni Mkewe Tunu.
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina ikoa katika hatari ya kuvunjwa kwa vile imejengwa kwenye eneo la akiba la barabara. Picha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akionyeshwa  na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Nasoro Rufunga alama inayoonyesha  sehemu ya ukuta wa ofisi hiyo unatakiwa kuvunjwa. Nyumba hiyo imejengwa kwenye kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu.

Usalama wa watoto


 
Wanafunzi wa Shule za Msingi Mjini Moshi wakikimbia kuvuka barabarwakati wa mchana jana. Watoto kama hawa wamekuwa wakigongwa na magarai marakwa mara katika maeneo mengi nchini kutokana na umakini mdogo wa waendesha magari na vyombo vingine vya usafiri. Jamii haina budu kuwalinda watoto na kuwajali popote wanapokuwa.

POLISI WATUMIA SILAHA ZA MOTO KUTAWANYA WAANDAMANAJI


Polisi wakiwatawanya na kuwakamata baadhi ya waandamanaji hao katika manispaa ya Songea baada ya wakazi wa manispaa hiyo wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki kuandamana hadi ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma kupinga mauaji ya watu yanayoendelea kwa kasi mjini humo ambao hadi sasa jeshi la polisi halijafanikiwa kuwakamata wauaji.
Madereva pikipiki wakiwa wamefunga barabara ya songea kwenda tunduru karibu na mlango wa kuingilia ofisi ya mkuu wa mkoa wa ruvuma,wakilitaka jeshi la polisi mkoa huo kuchukua hatua dhidi ya mauaji ya watu yanayoendelea mjini songea ambapo hadi sasa zaidi ya watu 8 wameuawa na watu wasiojulikana wengi wao wakiwa ni madereva wa pikpiki.
 
======    ======    =====

JESHI la polisi mkoani Ruvuma limelazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya wananchi waliokuwa wakiandamana kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma na kituo kikuu cha polisi Songea mjini hali iliyopelekea shughuli mbalimbali kusimama.

Hali hiyo ilianza kujitokeza majira ya asubuhi ambapo wananchi wa mtaa wa Lizaboni wengi wakiwa ni madereva wa pikpiki walianza kujikusanya na kuanza maandamano kuelekea kituo kikuu cha polisi kilichopo karibu na uwanja wa majimaji mjini hapa.

Wananchi hao walikuwa wakiimba nyimbo za kulaumu jeshi la polisi wakidai kuwa limeshindwa kudhibiti mauaji yanayoendelea kujitokeza mjini hapa kila mara ambapo hadi sasa zaidi ya watu kumi wameshauawa na watu wasiojulikana. “Tumeamua kuandamana kwani kimsingi mauaji yamezidi kutokea mjini hapa jana ameuwawa mtu,juzi na usiku wa kuamkia leo ameuwawa mwendesha pikipiki na abiria wake”walisikika wakisema.

Baada ya wananchi hao kukaribia kituo cha polisi walianza kurusha mawe na ndipo polisi walijihami kwa kutumia mabomu ya machozi ambapo wananchi hao na waendesha pikipiki walianza kukimbia ovyo na kupeleka maduka kufungwa kwa hofu ya kuibiwa.

Licha ya biashara mbalimbali kusimama pia ofisi za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa na ya mkuu wa wilaya Songea zilifungwa kwa kuhofia waandamanaji kuingia kwenye ofisi hizo na kufanya uharibifu.

Kabla ya maandamano ya leo februari 20 mwaka huu wananchi kutoka kata ya Lizabon waliandamana hadi kwa mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Ole Sabaya kulalamikia kukithiri kwa mauaji katani humo ambayo yamekuwa yakifanywa na watu wasiojulikana. Akijibu malalamiko hayo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa serikali itahakikisha ulinzi unaimarishwa na kwamba aliwataka kuimarisha ulinzi shirikishi ili kukabiliana na matukio hayo maovu.

Februari 19 mwaka huu mkazi wa Lizaboni Bakary Ally(20) aliuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiojulikana ambapo februari 20 mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku mtu mmoja mkazi wa mtaa wa Kipera shekhe Jamari(65) alikutwa ameuwawa kwa kukatwa mapanga kichwani na watu wasiojulikana wakati alipokuwa akielekea nyumbani kwake.

Marehemu Jamari alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wa msikiti uliopo katika eneo hilo la Kipera.Mauaji hayo yameendelea kujitokeza ambapo mwendesha pikipiki ambaye jina lake halikufahamika mara moja ameuwawa na watu wasiojulikana katika mtaa wa Mji Mwema mjini hapa usiku wa februari 22 mwaka huu na kupelekea wananchi mjini hapa kuishi kwa hofu kubwa. Habari na Picha kwa hisani ya Muhidin Amri-Songea (wa Globu ya Jamii).

Friday, February 17, 2012

Nembo ya Redds Miss Tanzania 2012 yazinduliwa

 Miss Tanzania 2011, Salha Izrael akiwa amesimama mbele ya nembo mpya ya REDDS MISS TANZANIA 2012 muda mfupi baada ya yeye na warembo wenzake kuizindua usiku wa kuamkia Februari 16,2012 jiji Dar es Salaam.
 Meneja wa Kinywaji cha Redds, Vick Kimaro(kushoto) na Mkurugenzi wa Mahusiano na Sheria wa TBL, Stephen Kilindo wakiungana na warembo wa Miss tanzania 2011 kugonganisha vinywaji vyao vya REDDS kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Msimu mpya wa mashimndano ya Urembo 2012.
 Warembo walipokuwa wakifungua pazia kuzindua nembo ya Mdhamini mpya wa Miss Tanzania 2012.
 Waliyarudi mangoma baada ya kuzindua...
 Meneja wa Chapa ya Kilimanjaro George Kavishe alikuwepo kumpa tafu Meneja wa Chapa ya REDDS, Vick Kimaro wote kutoka TBL.
 Mzee wa Jahazi, Epraim Kibonde akitoa Asalam Alekhum kwa Miss Tanzania 2011, Salha Izrael
 warembo mbalimbali walijumuika katika tafrija hiyo pale Mlimani City, hapa ni warembo wa Miss tanzania na marafiki zao katika zulia jekundu. 

 Wadau wa Mavazi Asia Idarus (shoto) na Shamim Mwasha wa 8020 blog na rafiki yao wakila pozi.
 wadau mbalimbali walikuwepo wakiwapo waandaaji wa masjhindano hayo ngazi ya vitongoji.
 Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga akiteta jambo na Mkurugenzi wa masoko wa TBL, Fimbo Butala.
.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Prashant Patel akiwa na wadau wa urembo nchini, Odhiambo, Mchata, Innocent na wengineo.
 Mdau kutoka Zantel akibadilishana mawazo na marafiki.
 Hadija Kalili na Somoe Ng'itu (kulia)  nao walifuatilia kwa ukaribu tukio hilo
 Christina Manongi (Sinta) ama J Lo wa bongo (kulia) na marafiki zake nao walikuwepo
Wazee wa taswira nao walichukuliwa taswira yao...hapa wakivizia tukio muhimu.