Monday, April 2, 2012

Watanzania waanza vema katika South Africa Fashion Week


Mwanamitindo mahiri Millen Magese akiwapungia mkono washabiki wake waliokuwa wakimshangilia wakati akiingiaa katika onesho hilo la mavazi ya Afrika Kusini. 
 Mwanamitindo ambae matunda yake yameanza kuonekana mapema Anastazia Gura akitengenezwa nywele kabla ya kupanda jukwaani.
Mwanamitindo Anastazia Gura akipita mbele ya watazamaji walioshiriki katika onesho la wiki ya mavazi ya Afrika Kusini jana usiku wakati alipokuwa akionesha  mavazi yaliyobuniwa na mbunifu mkubwa wa mvazi ndani na nje ya Afrika Kusini, Olive Clandle.

Wabunifu wa mavazi wa Tanzania wakiwa wamepozi katika picha pamoja na Olive Clandle muda mfupi baada ya kumalizika kwa onesho la mbunifu huyo.
********
MWANAMITINDO Anastazia Gura aliyechaguliwa na mbunifu  mkubwa wa mavazi wa Afrika Kusini Olive Clandle kuonesha mavazi yake ameeleza kufurahishwa na hatua hiyo.  Anastazia akihojiwa na waandishi wa habari wa hapa Afrika Kusini alisema kuwa akiwa kama mwanamitindo chipukizi kuchaguliwa kuonesha mavazi ya mbunifu huyo ni hatua kubwa kwake.
 Alisema kuwa kwa kitendo cha kuchaguliwa bila hata ya kuonekana katika jukwaa ni dhahiri kuwa anavya vigezo vya kutosha na hivyo amepania kufika mbali zaidi.  Anastazia alichaguliwa mara tu baada ya kuonekana akijaribisha nguo za wabunifu wa kitanzania wanaoshiriki katika onesho hilo la wiki ya mavazi.
 Alifika nchini Afrika Kusini kwa lengo la kuonesha mavazi ya wabunifu watatu wa kitanzania waliochaguliwa na mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese.  Lakini hata hivyo alijikuta akichaguliwa kuonesha na mavazi ya mbunifu Olive Clande huku akiwa ndio kwanza anaingia katika tasnia ya uanamitindo huku akiwa hajawahi hata kutembea jukwaani.
 Hatua hiyo imeonekana kuwashangaza waandishi wa habari wa mitindo na hata wanamitindo wengine waliopo hapa Afrika Kusini kwa kuwa mara zote mbunifu huyu hupendelea kuwatumia wanamitindo wenye majina makubwa.
 Akizungumzia hatua hiyo Millen alisema kuwa Anastazia na vigezo vyote vinavyotakiwa kuwa mwanamitindo na ndio maana ameweza kupatiwa nafasi hiyo kirahisi.  “Ni kwamba ili uweze kuchaguliwa inatakiwa angalau uwe na vigezo vya kimataifa ili kumwezesha mbunifu kuchagua mtu wa kumuoneshea nguo zake” alisema Millen.

Mbunge Arumeru Mashariki ni Joshua Nassari wa CHADEMA




MGOMBEA Ubenge Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amewashinda wagombea wenzake saba kutoka vyama vya CCM, AFP, DP, NRA, SAU, UPDP na TLP katika uchaguzi mdogo wa Ubunge uliofanyika Aprili 1, 2012.

Kwa Mujibu wa Matokeo ya liyotangazwa asubuhi hii yanaonesha kuwa Mgombea Ubunge wa Joshua Nassari CHADEMA amepata kura  32,972, na kumshinda Mgombea mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo, Sioi Sumari wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 26,757.

Kwamatokeo hayo inafanya kuwa idadi ya Kura zilizompa ushindi  Nassari wa Chadema kuwa kura 6,215 dhidi ya Sioi Sumari CCM.

Msimamizi wa huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw Joshua Nassari kuwa mshindi.

Gagenzi pia ametangaza matokeo ya wagombea wengine ambao walitoka vyama vya Siasa nchini kuwa kama yafuatavyo:-
AFP – 139, DP -77, NRA – 35, SAU – 22, UPDB – 18 na TLP – 18.

Kwa mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.

Aidha CHADEMA pia jana katika Uchaguzi wa Udiwani imepata Ushindi katika Kata za Kirumba mkoani Mwanza na Kiwira mkoani Mbeya.

Sunday, April 1, 2012

NADIR HAROUB ALISTAHILI JANA KUCHEZA AU LA ?



Kanuni  YA 25 ya udhibiti wa wachezaji :
Tff itadhibiti mienendo ya wachezaji kwa kuchukua hatua kama ifuatavyo.

A) MCHEZAJI ATAKAYETOLEWA NJE KWA KADI NYEKUNDU BAADA YA KUPATA KADI MBILI ZA NJANO, HATARUHUSIWA KUCHEZA MCHEZO MMOJA
B) MCHEZAJI ATAKAYEPEWA KADI NYEKUNDU ( STRAIGHT RED CARD ) ATAKOSA MICHEZO MIWILI. 
C) MCHEZAJI ATAKAYETOLEWA NJE KWA KADI NYEKUNDU KWA KOSA LA KUPIGA AU KUPIGANA ATASIMAMA KUSHIRIKI MICHEZO MITATU INAYOFUATA YA KLABU YAKE NA ATALIPA FAINI YA TSH 500,000
D) WACHEZAJI 5 WAKIPATA KADI KTK MCHEZO MMOJA KLABU ITALIPA FAINI  YA TSH 500,000
E) MCHEZAJI AKIPATA KADI JUMLA YA KADI TATU ZA NJANO ATASIMAMA MCHEZO MMOJA

PATRICK MAFISANGO IS BACK IN THE BUSINESS !

KIUNGO WA KIMATAIFA WA RWANDA MWENYE ASILI YA CONGO DRC MUTESA PATRICK MAFISANGO AMERUDISHWA KUNDINI KWA AJILI YA SAFARI YA ALGERIA,
KIUNGO HUYO ALIYEKUA AMESIMAMISHWA NA KLABU YAKE YA SIMBA AMERUDUSHWA KIKOSINI BAADA YA KUTAMBUA KOSA LAKE NA KUOMBA RADHI KWA MWALIMU,WACHEZAJI NA VIONGOZI.

Utoaji tuzo za EJAT kwa Waandishi Bora wa Habari Tanzania


 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda akikabidhi tuzo kwa mwandhishi wa habari wa Mlimani Radio Tuma Dandi mshindi wa habari za watu wenye ulemavu- Redio
 Rais Dkt. Jakaya Kiwete akimkabidhi tuzo Mshindi wa Jumla wa tuzo za Mwaka huu za EJAT, Nevile Meena ambayo ilienda sambamba na Hundi ya USD 4000.
 Fili Karashani akipokea tuzo kutoka kwa Rais Jakaya Kiwete na Hundi ya Sh Milioni 10.
 Mkurugenzi wa Executive Solution, Agrey Mareale (kushoto) akikabidhi tuzo, Cheti na zawadi ya Laptop, Mshindi wa tuzo ya Mpigapicha Bora, Hamis Hamad "Mkojani"  kutoka Magazeti ya Chama cha Mapinduzi.
 Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Ernest Sugura (kulia) nae akikabidhi moja ya tuzo hizo.
 Mwakilishi wa TBC Dodoma, Victoria nae alipokea tuzo yake.
 Rais Dkt. Jakaya Kiwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginal Mengi wakati walipokutana katika halfa hiyo ya utoaji tuzo za EJAT.
Muhidin Michuzi ambaye ni mpigapicha wa siku nyingi nchini akimpongeza Hamisi Hamad kwa kutwaa tuzo ya Mpigapicha Bora.

Elfu 55 ya Wema yakataliwa na Diamond amwaga Chozi ukumbini.


 Marafiki wa Wema Sepetu wakijaribu kumbembeleza wakati akimwaga chozi... huku watu wengine wakishangilia na kuimba aibu yetu au aibu yao???
 ...hapa mwanadada akijaribu kubembeleza bila matumaini.
 Msanii wa kizazi kipya, Ommy Dimpozzz akimpa sapoti Diamond...huku akitoa ushuhuda wa maisha yake na    ya Diamond walipotoka.
 ...baada ya ujumbe wa Ommy Dimpozz, Diamond alimwaga chozi na hapa 
 alikuwa akijifuta. Picha zaidi ingia http://kajunason.blogspot.com/

SEMINA YA MAWAKALA WA MISS TANZANIA 2012 YAKAMILIKA


 Wakala wa Miss Tanzania 2012, kutoka Ukonga jijini Dar es Salaam, Daudi Mambya akichangia mada wakati wa semina ya siku mbili ya Mawakala wa Redds Miss Tanzania 2012 iliyofanyika kwa siku mbili na kumalizika tarehe 29.03.201 jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majalkiwa (kulia) akizungumza wakati wa Semina ya Mawakala wa Mashindano ya Redds Miss Tanzania 2012 inayofanyika kwa siku mbili na kumaliza jana jijini Dar es Salaam. Pamoja nae ni  Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
 Wakala wa Miss Tanzania 2012, kutoka Mara, Godsos Mkama akichangia mada wakati wa semina ya siku mbili ya Mawakala wa Redds Miss Tanzania 2012 iliyofanyika kwa siku mbili na kumalizika tarehe 29.03.2012 jijini Dar es Salaam.
 Wakala wa Miss Tanzania 2012 kutoka Mkoa wa Shinyanga, Asela Magaka akichangia mada wakati wa semina ya siku mbili ya Mawakala wa Redds Miss Tanzania 2012 iliyofanyika kwa siku mbili  jijini Dar es Salaam.
Washiriki mbalimbali ambao ni Mawakala wa Miss Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali katika semina hiyo .