Tuesday, April 10, 2012

Mama Salma Kikwete ahani Msiba wa Steven Kanumba

 Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya Msanii nguli wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba aliefariki Dunia siku usiku wa Ijumaaa iliyopita  nyumbani kwake Sinza Vatican,Jijini Dar es Salaam
  Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akikumbatiana na Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba wakati alipofika nyumbani hapo kwa ajili ya kuhani msiba huo,jioni ya jana.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa   Habari,Vijana,Utamaduni,Dkt. Fenella Mukangara wakati alipofika Nyumbani kwa Marehemu Steven Kanumba kwa kuhani Msiba huo.Kushoto ni Mama Mzazi wa Steven Kanumba.

Thursday, April 5, 2012

HABARI YA HIVI PUNDE: Godbless Lema avuliwa Ubunge Arusha Mjini

MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.

Taarifa kutoka jijini Arusha zinasema uamuzi huo umefikiwa leo asubuhi Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo. 


Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).



Lema katika Uchaguzi huo alikuwa akichuana vikali na Mgombea wa CCM, Dk. Batilda Salha Buruiani ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya.

Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cham hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.

Pia habari za ndani ya Chama cha Chadema zinasema kuwa tayari Chama hicho kilisha soma alama za nyakati mapema katika kesi hiyo miezi kadhaa nyuma na kujipanga endapo mbunge huyo atavuliwa wadhifa wake nani kimsimamishe kutetea kiti hicho.

Habari hizo zinadai kuwa Chadema kimepanga kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chama hicho na Mgombea Urais wa 2010, Dk. Wilbroad Silaa kutetea kiti hicho.


Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa  wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.

Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5 kujitetea.

ratiba ya Msondo Pasaka hii



BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ imetoa ratiba yao katika kusherekea Siku kuu ya Pasaka ambapo wamesema kuwa wataanza leo kutoa burudani ndani ya Wipes Bar Mivinjeni Kurasini, siku ya Ijumaa watakuwa Leanders Club Kinondoni, Jumamosi watakuwa TCC Club Chang’ombe, Pasaka watakuwa Kata ya 14 Temeke na Jumatatu ya Pasaka watakuwa sambamba na FM Academia ‘Wazee wa ngwasuma’.

Akingongea , Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa wameamua kutoa ratiba hiyo ili mashabiki wao waweze kujua nini kinachoendelea ndani ya bendi yao.

Alisema kuwa hata hivyo tayari wamajipanga vizuri katika suala zima la kuwapa burudani mashabiki wao katika kusherekea sikukuu hii  ya Pasaka.

“Msondo ipo kamili katika kutoa burudan na ndiyo maana imeamua kutoa ratiba, hivyo tunaamini mashabiki wetu watakuja kwenye matamasha yetukwani bila wao sisi hatuwezi kusimama na kuimba,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa wanahitaji mashabiki wao kjitokeza kwa wingi ili waone nini wanachowapa katika siku hizo zote kwani sikukuu ya pasaka ni muhimu kusherekea na msondo ngoma bendi hiyo inayotamba
  na vibao vyake vipya vya Suluhu wa Shabani Dede na Nadhiri ya Mapenzi wa
Juma Katundu pia watapiga nyimbo zao zote zilizotamba kipindi cha nyuma alisema Super D

Miss Dar City Centre, Ukonga kusindikiza utambulisho Miss Tabata Pasaka


Na Mwandishi Wetu
WASHIRIKI wa Dar City Centre na wale wa Ukonga watasindikiza Miss Tabata kwenye utambulisho wao ambao utafanyika siku ya Pasaka Da’ West Park, Tabata.

Mratibu wa Miss Tabata Godfrey Kalinga alisema jana kuwa washiriki kutoka vituo hivyo viwili pia watatumia fursa hiyo kujitambulisha kwa wapenzi wa urembo.

“Tumewaalika Dar City Centre na Ukonga kwa sababu washindi wao watakutana na washindi wetu kwenye mashindano ya kanda ya Ilala,” Kalinga alisema.     

Kalinga alisema onyesho la Pasaka litakuwa ni shamrashamra ya kusherekea miaka 10 ya Miss Tabata ambayo itaadhimishwa kwenye fainali za Miss Tabata mwezi ujao.

Katika utambulisho huo wa Jumapili, bendi za African Stars “Twanga Pepeta” na Mashauzi Classic “Wakali wa Kujiachia” watatumbuiza kwenye onyesho litakalofanyika katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata.

Bendi hizo mbili zitafanya maonyesho yao kabla ya warembo kutambulishwa na hata baada ya utambulisho zitaendelea kutoa burudani kali hadi majogo huku wapenzi wao wakisherekea sikuku ya Pasaka.

Onyesho hilo maalum imeandaliwa na Bpb Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi.
Washiriki wa Miss Tabata wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata chini ya wakufunzi watatu,  Beatrice Joseph, Neema Chaki na Bokilo. 

Warembo hao ni  Neema Saleh (18), Paulina Valentine (18), Khadija Nurdin  (19), Phillos Lemi (20) na Mercy Mlay (21).

Wengine ni  Neema Innocent (19), Ellen Sule (22),  Wikllihemina Mvungi (20), Queen Issa (20), Suzane Deodatus (19), Everline Andrew (21), Josephine Peter (20) na Jamila Omary (19).  Warembo hao wako
Zaidi ya warembo 10 kutoka Tabata watafuzu kushiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala,  Miss Ilala baadaye mwaka huu.

Mrembo anayeshikilia taji la Tabata ni  Faiza Ally.
Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds. Katika shindano la mwaka juzi Juliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.

MAMA PINDA AENDESHA KAMPENI YA SAIDIA TAIFA QUEENS




Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group ,Bw.Joseph Kusaga akimkaribisha mgeni wake, Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Tunu Pinda mara alipowasili mapema jana asubuhi kwenye ofisi hizo.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Mke wa waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (pili kulia) akiwa amepozi katika picha ya pamoja na Watangazaji wa kipindi cha Power breakfast kutoka Clouds FM mapema leo asubuhi, Mama Pinda alifika kwenye ofisi za redio hizo kwa ajili ya kuwahamasisha jamii mbalimbali kuisaidia timu ya Taifa Queens kwenye michuano yake inayotarajiwa kuanza hivi karibuni hapa jijini dar. Kutoka kulia ni Gerald Hando, Barbla Hassan pamoja na Paul James.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Mama Tunu Pinda akiwa ni mmoja wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali wameamua kushiriki kuihamasisha jamii na wadau mbalimbali kuisaidia timu ya mpira ya wanawake ya Netboli (Taifa Queens ) kuhakikisha inafanikisha malengo yake na pia kuhakikisha maandalizi yote yanakwenda sawa. Pichani ni Mama Tunu Pinda akizungumza leo kwenye kipindi cha Power breakfast kupitia redio ya Clouds FM jijini Dar kuhusiana na mchakato mzima wa kuisadia Taifa Queens,kulia ni Paul James a.k.a PJ.

Taifa Queens kwa sasa iko kambini kwa ajili ya maandalizi ya mashidano ya Netiboli ya Kombe la Afrika, ambapo Tanzania kupitia CHANETA imepewa heshima ya kuandaa Mashindano ya Netiboli ya Kombe la Afrika ambayo yanatarajiwa kuanza Mei 8-12, mwaka huu. Mama Tunu Pinda aliweka bayana kuwa gharama za kuendesha mashindano hayo ni zaidi ya sh. milioni 127.

Hivyo Mama Pinda amewaomba wadau mbalimbali kuisaidia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kufanya vyema kwenye michuano yake,aidha amewataka Wadau watakaokuwa na nia kuichangia timu hiyo basi watume michango yao kupitia namba ya simu 0779 000 808 (huduma ya Easy pesa),ambapo mtu ama kampuni anaweza kutuma kwenye namba hiyo kwa mitandano yote. 
Picha: Michuzijr Blog

AMINI AAMUA KUOA KIMYA KIMYA


 












 Msanii wa kizazi kipya, kutoka THT Amini hatimaye ameamua kuachana na ukapela kwa kuvuta jiko kimya kimya. Harusi hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania, Azania Front jijini Dar es Salaam. 
Picha hiyo inawaonyesha maharusi wakitoka kanisani kwa nderemo na vifijo.

 ...Hahahahahahahahahahahahaha
 












 Maharusi wakiingia katika gari lao mara baada ya kufunga pingu za maisha.

 .












..Ilikuwa ni nderemo na vifijo
 ....
 












 Picha ya ukumbusho kwa wazazi na maharusi

Wednesday, April 4, 2012

YANGA YAPINGA ADHABU YA TFF KUWAPOKA POINTI ZAO

Uongozi wa Yanga umepinga hatua ya Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF)  kuipora   pointi tatu na mabao matatu kutokana na kitendo chake cha kumtumia, beki Nadir Haroub'Canavaro' wakati wa mechi ya ligi kuu dhidi ya Coastal Union.

Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura  alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa,Kamati ya Ligi kuu iliyokutana April 2 ilifikia uamuzi huo kwa kuzingatia kanuni ya 25 ya udhibiti wa wachezaji.

Alisema kuwa  kamati hiyo ilibaini kuwa Canavaro alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumshambulia mwamuzi Israel Nkongo wakati wa mechi ya ligi kuu dhidi ya Azam iliyofanyika Machi 10,hivyo kwa kuzingatia kanuni ya 25,beki hiyo alipaswa kukosa mechi tatu.

Kutokana na uamuzi huo wa kamati ya ligi,Yanga  itaendelea kubakia katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi licha ya pointi zake kushuka mpaka 43 baada ya kushuka dimbani mara 21.

Simba ndio inaongoza ligi ikiwa na pointi 48 ikifuatiwa na Azam iliyojikita katika nafasin ya pili ikiwa na pointi 47.Katibu Mkuu wa Yanga,Selestine Mwesigwa alisema jana kuwa klabu yake imeshangazwa na uamuzi huo wa kamati ya ligi, na kudai kwamba  haukuwa halali  kwavile rufaa yao bado haijatolewa uamuzi na kamati ya nidhamu."Uamuzi wao unadhihirisha kwamba kamati ya ligi haina sifa za kushughulia masuala ya utovu wa nidhamu,ipo ipo tu haina  faida yoyote,"alisema Mwesigwa.   
Alisema kuwa wao walishakata rufaa kupinga adhabu ya vifungo kwa wachezaji wao,Jerryson Tegete,Stephano Mwasika, Omega Seme,Nurdin Bakar na Canavaro, lakini jambo lililowashangaza kamati ya ligi kuchukua uamuzi wao badala ya kusubiri ule wa kamati ya nidhamu

"Ukumbuke kwamba Yanga ilishakata rufaa baada ya kamati hiyo hiyo kuwafungia wachezaji wetu watano,Jerryson Tegete, Stephano Mwasika, Omega Seme, Nurdin Bakar na Canavaro."Tibaigan(Alfred,Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Maadali)akasimamisha adhabu kwa siku 14 na kuwaruhusu tuwatumie, leo wanatuhukumu kwa suala hilo hilo la Canavaro, hapo ni sawa?,"alisema Mwesigwa na kuongeza kuwa:

"Adhabu ya kadi nyekundu inayotolewa na mwamuzi ni kukosa kadi mbili hiyo ya tatu ni lazima iidhinishwe na kamati, sasa kama kamati ilitoa adhabu hiyo ambapo ilikuja kusimamishwa na kamati ya nidhamu uhalali upo wapi?,".

Aliongeza kwa kusema kilichowashangaza zaidi ni namna uamuzi huo ulivyotolewa wakati tayari Coastal Union walishakata rufaa ambayo badala ya kutolewa uamuzi na kamati ya nidhamu ama rufaa umetolewa na kamati ya ligi.

"Sisi tunasubiri barua rasmi baada ya hapo tutajua nini cha kufanya,Coastal walishakata rufaa ambayo kama ilifika TFF basi ni jana,sasa kazi ya kamati ya ligi ni kusikiliza rufaa na kutoa uamuzi?,".

Si sahihi kabisa je kamati ya nidhamu ikitoa uamuzi kwamba Canavaro hakumpiga mwamuzi nja na wao wametumia kigezo hicho itakuwaje,huku ni kuingilia uhuru  wa chombo kingine,"alisema Mwesigwa.