Saturday, September 7, 2013

DUNIA IMEISHA...ATAFUNWA USO



 

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Susuluka (16) anadaiwa kujeruhiwa vibaya usoni na bosi wake, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa ng’atwa usoni na kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje, kama ambavyo anaonekana pichani ukurasa wa mbele.


Tukio hilo ambalo tunaweza kulifananisha na dunia kuelekea kufika mwisho, limegusa hisia za watu wengi hasa wakazi wa Kibondo, huku wengine wakitokwa na machozi kutokana na kuguswa na ukatili ambao amefanyiwa kijana huyo.Tunaweza kufikiria kuwa tukio hilo ni sinema, lakini Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamotto, ameliambia Majira kuwa tukio hilo limetokea miezi miwili iliyopita. 
 

Akizungumza katika mahojiano maalumu, Mwamotto, alisema kuwa kabla ya kijana huyo kujeruhiwa na bosi wake, alimtuma dukani ili akamnunulie soda.Alisema kuwa baada ya kufika nyumbani alimkuta bosi wake akiwa amemkaba koo mbwa na kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata mbwa huyo, alianza kuhema akitoa ulimi nje. 
 

DC Mwamotto alisema kuwa mtuhumiwa huyo ghafla alianza kuung’ata ulimi wa mbwa na kisha kumeza vipande jambo lililosababisha mbwa huyo kupiga kelele kutokana na maumivu.Aliongeza kuwa aliendelea kula vipande vya ulimi huo wa mbwa hadi alipoumaliza. 
 

“Unaweza kusema kuwa ni uongo, lakini ni tukio la kweli kabisa kwani mshtakiwa huyo aliendelea kula ulimi wote wa mbwa, huku kijana huyo akiendelea kumshangaa bosi wake kutokana na kitendo hicho kilichosababisha mbwa huyo kufa,”Wakati akiendelea kumshangaa bosi wake ghafla alimrukia na kumkamata kwa nguvu na kuanza kumng’ata kama mtu anayetafuna hindi la kuchoma. 
 

“Mshtakiwa huyo alianza kumtafuna jicho moja na kufuatia jicho la pili na kisha kumeza vipande vya macho huku akiendelea kumshika kwa nguvu,” alisema DC

Baada ya kumaliza kitendo hicho alisema kuwa mshtakiwa huyo alianza kumng’ata pua na kisha kumeza na vipande. 

Alisema kuwa wakati anaendelea na kitendo hicho majeruhi huyo alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada, lakini mshtakiwa huyo alianza kumng’ata tena kipande cha mdomo wa chini na kisha kusababisha meno kubaki nje.“Kutokana na kelele hizo wananchi waliamua kusogea karibu, lakini walikuta tayari, Susuluka amejeruhiwa vibaya usoni huku damu zikimtoka kwa wingi,” alisema. 
 

Mwamotto alisema kuwa kutokana na hali hiyo wananchi walimvamia na kumpiga na kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Kibondo na majeruhi walimkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo. 

Mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya na kufunguliwa mashtaka ya kudhulu mwili.“Hivi sasa mshtakiwa yupo katika Gereza la Nyamisivi Kibondo, lakini cha kusikitisha tena akiwa huko alimng’ata na kula vipande vya nyama vya mguu mshtakiwa mwenzake,” alisema. 
 

Alisema kuwa mshtakiwa mwenzake alimjeruhi vibaya na kupelekwa hospitalini hali iliyosababisha mshtakiwa huyo kutengwa na washtakiwa wenzake.“Mimi nimelazimika kwenda hadi gerezani na kufanya mahojiano na mshtakiwa huyu, kwani hili tukio linasikitisha sana lakini cha ajabu alitaka kufahamu je ameshtakiwa kwa makosa gani ya kuua mbwa au kumng’ata mtu,” alisema. 
 
Alisema kuwa pia amelazimika kwenda kumjulia hali majeruhi huyo ambapo madaktari katika hospitali hiyo walishindwa kumtibia.“Nimeomba msaada kutoka Wizara ya Afya ili mgonjwa huyu akatibiwe India na tayari maandalizi yameanza kufanyika kwa kushirikiana na Hospitali ya Kibondo,” alisema.

Habari na vyanzo mbalimbali vya habari nchini...

Thursday, August 29, 2013

MWENGE WA UHURU 2013 WAZINDUA MIRADI BAGAMOYO


Kiongozi mbio za Mwenge ahimiza umoja na mshikamano
Na bloger team,Bagamoyo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Juma Ally Simai amewahimiza watanzania kuwapuuza watu wanaotaka kuwatenga wananchi kwa itikadi za kidini au za kisiasa na kusema kuwa watu hao sio wema kwa sababu wanataka kuingiza nchi kwenye machafuko kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amesema hayo leo wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa mkuu wa mkoa wa Pwani, Mwantumu Maiza aliyepokea Mwenge huo kutokea mkoa wa Morogoro.
Simai aliyasema hayo kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara wilayani hapa alipozindua miradi ya madarasa mawili ya shule ya sekondari Bwawani,Nyumba ya mganga wa  Zahanati ya Ubena Zamozi zote za Kata ya Ubena, Kituo cha Upimaji na ushahuri nasahaĆ .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya bagamoyo.  Ahmed Kipozi alisisitiza ushirikiano na kureta tija kwa wilaya kwa kuwataka wananchi kulinda miradi inayozinduliwa na mwenge huo.

mwenge huo pia ulizindua miradi mbalimbali ikiwemo yaWodi ya wazazi kituo cha afya chalinze,jengo la madarasa 2 sekondari ya Mboga,kuweka jiwe la msingi ofisi ya kata msata na miradi mingine mingi.
Aidha Mwenge huo kesho unatarajiwa kukabidhiwa Wilayani Kibaha. na pwani unakuwa mkoa wa 23 kupitiwa na mwenge huu

Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Maiza akipokea Mwenge wa Uhuru 2013. ..ulipoingia Bagamoyo kutokea Morogoro asubuhi ya Agost 29.

Friday, December 7, 2012

UNIQUE MODELS NDO HABARI YA MJINI DESEMBA HII

 

Washiriki wa shindano la unique model wakiwa katika hali ya kujifua catwalk ikiwa ni maandalizi ya fainali za shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwezi huu.
Washiriki Zenaath Unique na Sandra Unique katika mtanange wa miondoko ya kimaonyesho,hapa ni sehemu ya uwazi katika Hotel ya Giraffe ocean view,hotel bora na huduma za ukarimu.
 

UZINDUZI WA MBIO ZA UHURU MARATHON




Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akiwasili katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont, Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam tayari kwa kuendesha hafla hiyo ya Uzinduzi.akizindua rasmi tovuti ya Mbio hizo ya http://www.uhurumarathon.com pamoja nae ni Mkurugenzi wa Intelecture Communication Ltd, Waandaaji wa Mbio hizo, Innocent Meleck.
Msanii Maarufu wa Nyimbo za Mashaili hapa nchini,Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba akionyesha umahiri wake wa Mashairi yake yenye ujumbe mzito wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) ambazo zitakuwa zikifanyika kila Mwaka.hafla hii imefanyika katika Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon), Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akimtunza Mjomba Mrisho Mpoto wakati akiimba nyimbo zake za Mashairi yenye Ujumbe Mzito kwa Taifa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam
Muongozaji wa Hafla hiyo usiku huu, alikuwa ni MC Ephrahim Kibonde.
Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akisoma hotuba yake wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) ambazo zitakuwa zikifanyika kila Mwaka.hafla hii imefanyika katika Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akisoma hotuba yake aliyoiandaa wakati wa Uzinduzi wa Uhuru Marathon uliofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) uliofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam
Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akitoa ufafanuzi wa mdogo wa nembo na kauli mbiu zitakazo tumika kwenye Mbio hizo kwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara.
Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akimuelezea Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara juu ya Tovuti ya mbio hizo ambayo ni http:// www.uhurumarathon.com muda mfupi baada ya kuzinduliwa.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akikabidhiwa fulama Maalum yenye jina la Rais Jakaya Kikwete.
Mratibu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akifafanua jambo kwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara.
 
Wadau mbali mbali kutoka makampuni tofauti tofauti hapa nchini pia walikuwepo kwenye uzinduzi huo.
Mjomba Band ikifanya vitu vyake.
Wanahabari.
Wadau kibao walikuwepo kwenye uzinduzi huo.

BARABARA YA DAR LINDI KUKAMILIKA JUNI MWAKANI


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

 
 
 
 
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Barabara ya Dar-Lindi kukamilika Juni mwakani

                   Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameambiwa juzi, Jumatano, Desemba 5, 2012, kuwa ujenzi wa Barabara ya Dar es Salaam-Lindi utakamilika katika miezi sita ijayo kuanzia sasa.

                   Rais Kikwete alipewa maelezo hayo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Mhandisi Gerson Hosea Malangalila Lwenge wakati aliposimama kukagua maendeleo ya ujenzi kwa akiwango cha lami wa kilomita 56 kati ya  Nyamwage, Mkoa wa Pwani na Somanga, Mkoa wa Lindi.

                   Rais Kikwete alisimama kukagua ujenzi wa Barabara hiyo wakati akirejea Dar es Salaam kutoka Lindi ambako alifanya ziara yenye mafanikio makubwa ya siku tatu kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi.

                   Akipewa maelezo ya ujenzi wa Barabara hiyo kwenye eneo la Somanga, Rais Kikwete aliambiwa kuwa kati ya kilomita hizo 56 tayari kilomita 30 zimeshatiwa lami. Barabara hiyo inajengwa na Kampuni ya MS Karafi.

                   Naibu Waziri huyo alimwambia Rais Kikwete: “Mjenzi anajenga kiasi cha mita 250 kila siku na kama hapakuwepo na kuharibika kwa lolote ama mvua isipokuwa nyingi kupita kiasi, basi ujenzi wa Barabara hii utakuwa umekamilika katika miezi sita ijayo kuanzia sasa.”

                   Naibu Waziri alimwambia Rais Kikwete kuwa ni kweli ulikuwepo ucheleweshaji kwa upande wa mjenzi, lakini sasa maendeleo ni mazuri. Barabara hiyo ilipangwa kukamilika Juni, mwaka jana, 2011.

                   “Kwa jumla ujenzi wa Barabara nzima umekamilika kwa asilimia 78, njia ya awali ambako lami itawekwa imekamilika kwa asilimia 98, madaraja madogo kiasi cha 55 tayari yamejengwa na vifaa vyote ikiwa ni pamoja na kokoto viko kwenye eneo la ujenzi.”

                   Barabara ya Dar es Salaam-Lindi ina urefu wa jumla ya kilomita 452 na kukamilika kwa kipande cha Nyamwage-Somanga una maana kuwa mtu yoyote anaweza kusafiri kwa lami tupu kutoka Mtwara hadi Kagera ama Mwanza ama Arusha ama Tunduma.

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

07 Desemba, 2012