Wednesday, August 24, 2011
JK ALIPOTEMBELEA MRADI WA UPANUZI WA MIUNDOMBINU YA MAJI LINDI
Rais Kikwete akiwa na mkuu wa mkoa wa Lindi bw. Meck Sadick nyuma yake mara alipofika kwenye maeneo ya mradi Jumapili iliyopita tarehe 21.08.2011.
Rais Kikwete akisikiliza maelezo toka kwa mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji mjini Lindi bw.Daudi Majani
Rais akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa maendeleo wa mji wa Lindi kwenye sekta ya elimu.
Rais Kikwete akiwa na meneja mradi wa kampuni ya Jandu plumbers wanaotekeleza mradi huo bw.Jite Kalsi.
Picha kwa hisani ya mdau Jite
JAIRO APOKELEWA KWA SHANGWE
Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakilisukuma gari lililokuwa limembeba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. David Jairo mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara hiyo.
Wafanyakazi kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakilisukuma kwa nyuma gari lililokuwa limembeba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw David Jairo mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo mapema leo asubuhi.
Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakimpokea Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. David Jairo kwa shangwe mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo mara baada ya kuripoti mapema leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Jairo akitafakari jambo mara baada ya kurejea ofisini kwake ili kuendelea na majukumu yake.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akiwa amemkumbatia kwa furaha kama moja ya mapokezi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. David Jairo mara baada ya kuripoti katika ofisi za Wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo asubuhi.
ADEBAYOR AJIUNGA NA SPURS KWA MKOPO

Tottenham wamefanikiwa kukamilisha usajili wa mkopo kutoka Manchester City na kuwapiku Inter Milan ambao walianza harakati za siri za kumnyakua mshambuliaji huyo.
Adebayor hatoruhusiwa kuichezea Spurs dhidi ya City weekend hii.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal, atafanyiwa vipimo jijini London Jumatano baada ya Tottenham kukubali kuchangia kwa kiasi kikubwa mshahara wa 170,000 kwa wiki.
Dili hilo lilichelewa kutokana na mshambuliaji huyo kukataa kupunguza mshahara wake baada ya kukatwa katika kikosi cha kwanza na kocha Roberto Mancini.
Wakati huo huo Inter Milan walitumia masaa 11 kufanikishampango wa kumchukua Adebayor, lakini kipindi hicho hicho Tottenham walikuwa katika hatua za mwisho straiker huyo aliyekuwa kwa mkopo Real Madrid msimu uliopita.
NASRI AFAULU VIPIMO VYA AFYA MAN CITY

SAMIR NASRI AKITOKA KATIKA HOSPITAL YA BRIDGEWATER-MANCHESTER
Samir Nasri amefaulu vipimo vya afya vya kujiunga na Manchester City leo jioni, anategemewa kusaini mkataba wa miaka 5 wa kuitumikia klabu hiyo ya Eastlands.
Nasri anategemea kupata mshahara wa £185,000 kwa wiki mara mbili zaidi ya aliokuwa akipata akiwa na Arsenal.
MBUNGE WA SINGIDA MJINI DEWJI ATOA UFAFANUZI JUU YA TUHUMA DHIDI YAKE
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mohammed Dewji, ametoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wakazi wa Singida za kwamba hajafanya chochote cha maendeleo katika jimbo lake tangu kuchaguliwa kwake .
Tuhuma na malalamiko hayo yaliyotolewa na baadhi ya wananchi wa Singida kupitia mtandao wa kijamii wa FACEBOOK, wakati wa kubadilishana mawazo na Mbunge huyo.
Wananchi hao ambao waliruhusiwa kutoa maoni na dukuduku zao kwa mheshimiwa DEWJI walidai kutoona maendeleo yoyote katika jimbo hilo kwa madai kwamba wananchi wa SINGIDA wamekuwa wakiteseka na maisha kwa kukosa maji, ajira na masuala ya maendeleo.
Katika ufafanuzi wake kuhusiana na Malalamiko hayo, Mheshimiwa Dewji amesema, Tangu kuchaguliwa kwake amekuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika maeneo ya Kero za Maji ambapo amefanikisha uchimbaji wa visima virefu zaidi ya 21, kwenye kata za Unyambwa, Mungu Maji, Unyamikumbi, Mwankoko, Mtamaa, Mandewa na Mtipa pamoja na baadhi ya kata za Mjini Kama Kindai, Mitunduruni na Utemini.
Aidha Mheshimiwa Dewji pia ameongeza kuwa bado anaendelea na jitihada za kukabiliana na tatizo hilo kwa kuibana Serikali itekeleze mradi Mkubwa wa Benki ya Dunia wa kuchimba visima 10 jimboni na anaendelea kuibana Serikali ifanye haraka kumalizia mradi mkubwa mwingine wa maji unaofadhiliwa na Benki ya BADEA na OPEC .
“Mradi huo ukikamilika ndio utakuwa ufumbuzi wa tatizo la maji katika manispaa ya Singida. Mradi huu utabadilisha miundombinu yote ya Maji safi ndani ya manispa yetu. Mradi huu unatarajia kukamilika 2013 na utagharimu takriban billion 20”.Amesema Mheshimiwa Mbunge Dewji.
Kuhusu ajira DEWJI ameeleza kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kutoa Ajira kwa vijana kupitia kampuni yake ya Mohamed Enterprises Limited(MeTL) sambamba na makampuni mengine mbalimbali.
Amefafanua zaidi kuwa yuko mbioni kuwekeza katika jimbo lake kwa kufungua kiwanda kitakachotoa fursa zaidi kwa vijana na wakazi wa Singida kujipatia maendeleo na ajira, na kwamba kwasasa anaendelea kuwasiliana na wataalamu mbalimbali wa uwekezaji ili kuona kama kuna fursa za kuweza kuwekeza katika manispaa ya hiyo.
Amepongeza kupokelewa kwa wito wa kuhamasisha michezo katika Jimbo lake na kusisitiza kuwa ataendelea kunyanyua na kuibua vipaji kupitia mashindano yake yajulikanayo kama Mohammed Dewji Cup yakiwa na takribani miaka SABA na yamekuwa na mafanikio makubwa kwa vijana wazaliwa wa Singida.
“Kuhusiana na Suala la Ujenzi wa Uwanja wa Namfua nilishaanza ukarabati katika eneo la Jukwaa kuu wewe mwenyewe ni shahidi kama ulikuwa unaufahamu uwanja ulivyokuwa mwanzo na wakati wa mashindano ya riadha Kitaifa niliweza kukarabati eneo la kukimbilia wanariadha na bado nitaendelea kukarabati kwa awamu mpaka tutakapoukamilisha. Ukumbuke ahadi hii haikuwa yangu peke yangu. Ila nimeshanunua nyasi za bandia ambazo zimenigharimu million 250. Natarajia kuziweka hizo nyasi 2012/13.”

VODACOM YATOA NAFASI KWA WATANZANIA KUWAPIGIA KURA WAREMBO
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetoa fursa kwa Watanzania kuweza kupiga kura na kuchagua mrembo anaevutia zaidi kati ya warembo 30 wanaoshiriki katika shindano la kumsaka Vodacom Miss Tanzania 2011.
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Bw. George Rwehumbiza alisema ili kupiga kura Watanzania watatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na namba ya mshiriki kwenda 15550 ambapo gharama kwa kila ujumbe ni shilingi 150 tu .
Aidha Bw, Rwehumbiza aliongeza kuwa kila ujumbe mfupi utakaotumwa utampatia Mtanzania pointi 10 ambapo wateja 20 watakaobahatika kuwa na pointi nyingi zaidi kila mmoja atajipatia TIKETI mbili za VIP zitakazomwezesha kwenda kushuhudia fainali ya Vodacom Miss Tanzania 2011 itakayofanyika tarehe 10 mwezi septemba katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dares salaam.
Pia kwa wale watakaohitaji kutoa maoni au mitazamo yao mbalimbali kuhusu Vodacom Miss Tanzania watapata fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na maoni kwenda namba 15550.
Akisisitiza hili Bw. Rwehumbiza alisema ili kuwafahamu warembo wanaoshindania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 Watanzania wote wanaweza kuangalia kituo cha STAR TV leo kuanzia muda wa saa moja jioni pamoja na CLOUDS TV muda wa saa tatu usiku kila siku pia soma magazeti ya Mtanzania, The African,Dimba,Rai na Bingwa.
Vodacom
kazi ni kwako
kazi ni kwako
Subscribe to:
Posts (Atom)