Monday, January 16, 2012
KOZI YA UKOCHA WA MASUMBWI YA KIMATAIFA YAANZA LEO KIBAHA MKOA WA PWANI
Serikali yapewa saa 72 kuwarejesha madaktari Muhimbili
CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT), kimeipa Serikali saa 72, kuwarejesha Hospitali ya Taifa Muhimbili, Wanafunzi waliofuzu udaktari waliondolewa hapo baada ya kugoma wakidai malipo yao. Tamko hilo lilitolewa na Rais wa chama hicho, Dk Namala Mkopi katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana. Chama hicho kimemuomba Rais Jakaya Kikwete, kuwatafutia kazi nyingine, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa kwa kosa la kumshauri vibaya Waziri wa wizara hiyo, Dk. Hadji Mponda. Alisema Dk. Mponda anasamehewa kwani hajui alitendalo ila inatakiwa awaombe radhi kwa kuwaita madaktari wenzao kuwa si madaktari bali bado wangali wanafunzi. Rais wa MAT, Dk. Mkopi, pia alitangaza kuwa kimefutia uanachama kwa mwaka mmoja, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mtasiwa kwa kosa lake la kuusaliti udaktari kutokana na kukiuka kiapo cha udakatari kinachosema kuwa Madaktari wote ni ndugu na nitawatendea haki kama dada na kaka. Alisema endapo Dk. Mtasiwa atanendelea na tabia hiyo ya kudharau taaluma ya udakatari, basi chama kitaamua kumfukuza kabisa na kumuweka kwenye mtandao wa madaktari duniani, ili iwe fundisho kwa madaktari wengine wenye tabia hiyo. Dk. Mkopi alisema kuwa chama kimesikitishwa sana na kwamba hawaoni ni kwa nini Serikali imeamua kuwaadhibu madaktari wenzao waliokuwa wakidai haki ya msingi, na kuwaacha kuwaadhibu watu waliosababisha ucheleweshaji wa makusudi wa kutowalipa malipo yao madaktari. Kwa habari zaidi soma hapa: http://richard-mwaikenda.blogspot.com/
Mwanafunzi ajiua Arusha kwa kosa la kusingiziwa kuiba dola 1500
Na Gladness Mushi wa Fullshangwe- Arusha Mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la John Justine(17) mkazi wa makao mapya amefariki dunia jana katika hospitali ya mount meru wakati akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwa risasi. Akizungumza na wandishi wa habari kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa arusha Thobias Andeng'enye amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa moja na nusu jioni ambapo siku hiyo mama wa marehemu aitwaye Betty John alikuwa akitoka kwenye sherehe mara baada ya kufika nyumbani alikuta geti limefungwa ndipo alipowaomba majirani kumsaidia kufungua. Andeng'enye amesema kuwa mama huyo amesema kuwa mara baada ya kuingia ndani akiwa na mtoto wa jirani alimkuta mtoto wake akiwa chini amelala chini huku akihema kwa tabu huku damu zikimtoka kifuani ndipo alipotoka nje na kuomba msaada kwa majirani. Aidha kamanda alisema kuwa mma huyo pamoja na majirani walisaidina kumkimbiza hospitali ya Dkt.Mohamed iliyopo eneo la Tank la maji Ilboru kwa matibabu ambapo ilishindikana na kumpeleka hospitali ya mkoa ya mount meru ambapo ailipatiwa msaada lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia. Hata hivyo andeng'enye amesema kuwa baada ya polisi kituo kikuu wilaya kupata taarifa walikwenda eneo la tukio kufanya ukakuzi ambapo walikuta bunduki aina ya shortgun Pump Action pamija na ujumbe unaosema"ANASIKITIKA KULAUMIWA NA WAZAZI WAKE PIA ANAWAPENDA SANA" Vilevile walikuta michirizi ya damu kutoka chumbani hadi alipoangukia. Kamanda ameongeza kuwa inasemekana kuwa marehemu alituhumiwa na baba yake mzazi Jastine Kaizer kuwa aliiba fedha kiasi cha dola za marekani 1500 hivyo polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa kumhoji baba mzazi wa marehemu . Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha mount meru ukisubiri uchunguzi zaidi wa dakta
Sunday, January 15, 2012
SOFT LAUNCHING YA SKYREAD HOTEL YA BAGAMOYO KWENYE PICHA
Wageni waalikwa wakiwa kwenye eneo la mgahawa wa hoteli ya Skyread iliyopo mjini Bagamoyo mkoani Pwani, mara baada ya kupokelewa hotelini hapo kwenye hafla ya uzinduzi mdogo iliyofanyika siku ya Ijumaa tarehe 13.01.2012
Bw,Eden Tetee akitoa neno la kubariki shughili ili iweze kuanza.
Bibi Salum Shariff mfanyabiashara maarufu mjini Bagamoyo (alivaa nguo ya pinki) akiwa mmoja wa wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Meja generali Meela mwenye kofia akiwa mmoja kati ya wageni mashuhuri waliyohudhuria hafla hiyo.
Bw. Chrispine Meela akitoa salamu za Skyread kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi
Mzee Ephafla Ezra Tetee(mwenye miwani) mmiliki wa hoteli ya Skyread akifurahia jambo na mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Free voice Investiment ltd Bw.Albert Kawago(mwenye glasi) wakati hafla ikiendelea.Picha ya juu mzee Tetee akikaribisha wageni aalikwa.
Wageni waalikwa wakiburudika kwa kwaito lililokuwa likiporomoshwa na dj Rama wa kampuni ya Kimkev Entertainment iliyoendesha hafla hiyo.
Wafanyakazi wa hoteli ya Skyread wakiaandaa maanjumati.
Bi Elizabeth Chawinga meneja wa benki ya N.M.B tawi la Bagamoyo akiwapungia wageni waalikwa akiwa na mzee Tetee kulia
Wageni waalikwa walipopata nafasi ya kujua mandhari ya ndani ya ndani ya hoteli ya Skyread.
Huu ulikuwa wakati mmiliki wa hoteli mzee Tetee akiwa na bi Shumina mtaalamu wa keki na mapambo alipokata keki ya siku ya kuzaliwa kwake ambapo alitimiza miaka 74 sambamba na uzinduzi mdogo wa hoteli ya Syread.Blog ya hii inakutakia kila la heri mzee Tetee
WAKONGO WAMFUNIKA CHARLES BABA
Na Mwandishi Wetu MWIMBAJI nguli nchini aliyeihama bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' na kutua Mashujaa Musica, Charles Gabriel 'Chaz Baba', ameanza vibaya kutambulishwa katika bendi yake mpya, kutokana na 'kufikikwa' na wanamuziki wenzake ambao wengi wanatoka Jamhuri ya Kidemokarsia ya Congo. Onesho hilo lililoshirikisha bendi tatu mahasimu za Mashujaa Musica, Mapacha Watatu na Extra Bongo, lengo likiwa ni kuungana 'kuiua' Twanga Pepeta, lilifanyika jana usiku kwenye ukumbi wa Business, Dar es Salaam, likijaza mashabiki kochokocho ambao wengi walikwenda kumuona Chaz Baba kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na bendi hiyo. Hata hivyo, tofauti na matarajio ya mashabiki wengi kwamba Chaz Baba angeingia na mambo mapya, alijikuta akifunikwa na waimbaji wenzake wa Mashujaa waliotawala jukwaa. Waimbaji wa Mashujaa wakiongozwa na Jado Field Force, Mirinda Nyeusi, Pasia Budansi 'BlackBerry', Raja Radha, Kajo Litungu, Sauti ya Radi, Kelvin Ulaka, Maga One Star, Thelathini na Tatu '33' na wengine, ndio waliong'ara katikla hilo lililokuwa maalumu kumtambulisha Chaz Baba. Chaz Baba aliingia ukumbini kwa mbwembwe, huku akisindikizwa na mashabiki wake waliokuwa wamebeba bango la kumkaribisha katika bendi hiyo inayomilikiwa na Mkurugenzi wa Mashujaa Group, Sakina Mbange 'Mamaa Sakina' akishirikiana na mumewe, Hoseah Hopaje 'Maisha'. Awali, kabla ya Mashujaa kupanda jukwaani, bendi ya Extra Bongo chini ya Ally Chocky ilipanda jukwaani na kupiga nyimbo za Mtenda Akitendewa, Fisadi wa Mapenzi na Falsafa. Kivutio kikubwa kwa Extra Bongo alikuwa Ramadhan Masanja 'Banza Stone', aliyelimudu jukwaa vyema na kuwafanya mashabiki wa muziki wa dansi kupagawa kutokana na uimbaji wake. Bendi ya Mapacha Watatu, ilipanda jukwaani ikiwa na Khalid Chuma 'Chokoraa', Jose Mara, Kalala Junior na walimkaribisha Chaz Baba kuimba naye. Hata hivyo, mpangilio wa upangaji ratiba ulionekana 'kuwaboa' baadhi ya mashabiki, huku washereheshaji wakiongozwa na Meneja wa Mapacha Watatu, Hamis Dacorta, wakichombeza majigambo mengi na kuinyima Extra Bongo nafasi ya kutumbuiza kwa ufasaha, hali iliyomkera Chocky na kuondoka ukumbini mapema. Chaz Baba alijiengua Twanga Pepeta wiki iliyopita akidai kwamba alikuwa ikifanya kazi ya 'deiwaka', bila kuwa na mkataba, lakini kwa sasa amesaini mkataba wa miaka miwili Mashujaa inayodaiwa kumpatia sh. milioni 10 na gari aina ya Noah.
Gari lililosababisha kifo cha Mbunge Regia
Hili ndilo gari alililokuwa akisafiria Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Marehemu Regia Mtema na kupata nalo ajali. hapa likiwa katika Kituo cha polisi Mlandizi mkoani Pwani. Regia aliyekuwa akiendesha gari hili alipindukanalo jana mara tatu kwa mujibu wa mashuhuda na kusababisha kifo chake. Taratibu za mazishi bado zinaendelea kufanyika.
Warembo Miss Tanzania wala nondo za Kidiplomasia
Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu (kushoto) na 1999 na Miss Tanzania namba tatu 2004, Cecilia Assey wakiwa na furaha baada ya kula nondo zao kutoka Chuo cha Diplomasia jijini Dar es Salaam. Warembo wengine nchini inafaa waige mfano huu wa kujiendelea kielimu na kuacha kufanya mambo ambayo hayawaletei tija wao na jamii kwa ujumla.
Hoyce Temu na Mdau Sixtus Mapunda akiwa na familia yake.
Subscribe to:
Posts (Atom)


