Wednesday, April 18, 2012

Maximo ashauri jinsi ya kupata wachezaji bora wa timu ya taifa

                                                                                                                                                                                                                                                                                           Kocha Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akisalimiana na  Rais Jakaya Mrisho Kikwete   alipokwenda kumsalimia Rais katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo
Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akimsalimu mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete alipokwenda kuwasalimia  katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo

Na Anna Nkinda – Sao Paul, Brazil
18/04/2012 Vilabu vya soka nchini vimeshauriwa kuwa na timu nzuri kuanzia ngazi ya watoto wenye umri wa miaka nane, vijana  na kuendelea ili kupata timu bora ya Taifa.
 Wito huo umetolewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Star  Marcio Maximo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Sao Paul.
Maximo alisema kuwa timu nyingi ambazo ni bora na zinafanya vizuri katika mchezo wa soka zimekuwa zikiwaandaa watoto wenye vipaji vya mchezo huo wangali wadogo ili waweze kuwa wachezaji wazuri hapo baadaye.
Kocha Maximo pia alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho kikwete, ambapo alimnshukuru sana Rais kwa ushirikiano wa hali ya juu aliompa wakati alipokuwa akiifundisha Taifa Stars miaka takriban mitatu iliyopita.
Kwa upande wake Rais Kikwete alimpongeza Kocha Maximo kwa juhudi zake za kuendeleza soka la Tanzania, akimwambia uwepo kwake Tanzania kuliasidia sana kuiweka nchi katika ramani ya mchezo huo.
Rais Kikwete alikubaliana na kocha huyo kwamba ili timu ya Taifa ifanye vyema ni lazima maandalizi yaanzie ngazi za chini, ikiwemo vilabu kuwa na timu za watoto na vijana ambao baadaye watakuwa hazina ya Taifa Stars.
 Kuhusiana na uvumi ulioenea kuwa anataka  kwenda kufundisha timu za Taifa Stars, Azam na Yanga alisema kuwa siyo kweli na wala hajawasiliana na timu hizo na hawezi kwenda kufundisha  kwani hivi sasa anamkataba wa kufundisha timu ya Democrata iliyopo nchini humo.
Rais alimshukuru Kocha Maximo kwa kuja kumsalimia na kumpa zawadi ya jezi ya timu ya Democrata anayofundisha, na kumtakia heri na fanaka katika kazi yake hiyo.
 “Timu ya Taifa Star ina kocha mzuri ambaye ninamuheshimu na ninaukubali ufundishaji wake hivyo basi kupitia kocha huyo ninaamini watanzania watazidi kuendelea katika soka na kufika mbali zaidi”, alisema.
 Maximo alimalizia kwa kusema kuwa  anamawasiliano mazuri na watanzania na anawapenda ndiyo maana kila mahali anapopita anajivuna na kusema  kuwa Tanzania ni nchi yake ya pili.
 Hivi sasa Maximo ni kocha wa timu ya  Democrata iliyopo nchini humo ambapo wiki ijayo inatarajia kuanza mashindano ya taifa yatakayopelekea kupata wachezaji bora watakaoshiriki mashindano ya kombe la Dunia yanayotarajia kufanyika mwaka 2014 nchini Brazil.

RAIS KIKWETE MKUTANONI BRASILIA, BRAZIL

 Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Open Government Partnership ukibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012. kutoka kushoto ni  Waziri katika  ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mh  Mathias Chikawe,  Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Mahadhi J. Maalim na Msahuri wa Rais (Masuala ya Siasa) Dkt Laurian Ndumbaro
   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu na mwenyeji wake Rais wa Brazil Mama Dilma Rousseff  na wajumbe wengine katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership. Kulia ni Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Bi Hilary Clinton
 Wajumbe wa Tanzania kutoka taasisi mbalimbali za kiraia na serikali wakiwa katika  ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012 katika mkutano wa Open Government Partnership 
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais wa Brazil Mama Dilma Rousseff alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April 17, 2012 kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership 

Picha na ikulu

Monday, April 16, 2012

TOTO WAVUNJA UNDUGU NA YANGA - WAITANDIKA 3-2 . SIMBA YAIZIDI KUCHANUA

SIMBA SC wamejiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kufuatia ushindi wa 1-0 jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, dhidi ya Ruvu Shooting.
Shukrani kwake kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 80.
Simba sasa ina pointi 53, tatu zaidi dhidi ya azam FC inayoshika nafasi ya pili.

CCM KIRUMBA MWANZA
Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, wenyeji Toto African walifanya kile ambacho hakikutarajiwa na wengi.
Toto wamewafunga ‘baba zao’ Yanga mabao 3-2 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mabao ya Toto inayopigana kuepuka kushuka daraja, yalitiwa kimiani na Mussa Said aliyefunga mawili dakika ya 18 na 39, Kulwa Mobbi dakika ya 24 Iddi.
Hamisi Kiiza aliifungia Yanga mabao mawili dakika ya 43 na 65.
Yanga inabaki na pointi zake 46 katika nafasi ya tatu, dhahiri sasa inaelekea kupoteza matumaini ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu.
Kocha Mserbia, Kosradin Papic alizomewa na mashabiki wa Yanga mjini Mwanza kutokana na kiwango kibovu ambacho timu hiyo inacheza hivi sasa.
Kipigo cha leo kinamaanisha Yanga imepoteza mechi mbili mfululizo, kwani mechi iliyopita na Coastal Union mjini Tanga, japokuwa walishinda 1-0, lakini walipokonywa pointi hizo na Kamati ya Ligi Kuu.

SUNZU - SIMBA TUTACHUKUA KOMBE LA SHIRIKISHO NA KUWEKA HISTORIA


Mshambuliaji wa Simba raia wa Zambia, Felix Sunzu amesema kuwa Simba itatwaa ubingwa wa ombe la Shirikisho la soka Afrika, CAF yeye anataka kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa kombe hilo.

Sunzu alisema kuwa mbali na kutwaa Kombe la Caf, hana wasiwasi Simba itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu na ufungaji bora na ndivyo vitakavyompa nafasi ya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo kinachowania kucheza Fainali za Kombe 2014.

Sunzu aliliambia Gazeti la Daily Mail la Zambia, kuwa ameshafunga mabao matano ya Kombe la Shirikisha na 13 ya ligi hivyo anatafuta nafasi zaidi kuitumikia timu ya taifa.

 “Nitafurahi sana kutwaa ubingwa wa Bara tena tutauchukua mikononi mwa wapinzani wetu (Young Africans) nina uhakika na pia nataka kuibuka mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho,” Sunzu alisema.

Alisema kuwa kiwango chake kiko juu na ana imani kocha wa timu ya taifa ya Zambia, Herve Renard atamuita kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014 na mechi za kuwania kucheza Fainali za Afrika 2013.

 “Kuna ushindani mkubwa kupata namba Chipolopolo, hasa baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika, na hiyo ni sababu ya mimi kujituma, nataka kuitwa tena kwenye kikosi hiki,” alisema.

Sunzu mmoja wa wachezaji wanaocheza soka ya kuvutia, amekuwa akiwindwa pia na El Merreikh ya Sudan na Yanga na kusema kuwa pamoja na kuchezea Simba, amevutiwa na klabu nyingine na ndiyo maana wanataka kumchukua.

Simba wiki iliyopita, iliiondosha Entente Setif ya Algeria na sasa itakutana na  Al Ahly Shandy ya Sudan.

Setif, ilifungwa na Simba mabao 2-0 mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam na ikashinda mabao 3-1 mjini Setif na Simba kufuzu kwa faida ya bao la ugenini.

Mara ya mwisho, Sunzu kuitumikia Chipolopolo ilikuwa katika michuano ya 2010 ya Kombe la Chalenji la Cecafa lililofanyika Tanzania na alifunga mabao matano na kuibuka mfungaji bora. Mchezaji huyo ni kaka mkubwa wa beki wa TP Mazembe na Chipolopolo, Stopilla.

Sunday, April 15, 2012

KILI MUSIC AWARDS 2012 YABAMBA JIJINI DAR USIKU WA KUAMKIA LEO


 Msanii Ali Kiba akikabidhiwa tuzo yake ya Wimbo bora wa Zhouk/Rhoumba uitwao Dushelele.
Burudani ikiendelea jukwaani.
Msanii kutoka THT,Rachael akitumbuiza usiku huu.
Msanii Dyana akiimba kwa hisia jukwaani.
Alikiba akishukuru Watanzania kwa kumpigia kura na kuibuka na tuzo hiyo,kulia kwake ni mdogo wake
Ma Mc wa Kili Music Awarsd usiku huu.Millard Ayo na Vanessa.
Diamond na wasanii wenzake wakitumbuiza mbele ya umati mkubwa hapa Mlimani City usiku huu.
Meneja wa Tip Top Connection,Babu Tale akiwa tuzo ya video bora ya mwaka ya wimbo uitwao hakunaga  wa Sumalee
Mwakilishi wa Msanii Ben Paul wakiwa na tuzo ya msanii huyo ya wimbo wa
Msanii nyota wa Hip hop hapa nchini Roma akiibuka kwenda kuchukua tuzo yake.
Msanii Roma akiwa na tuzo yake ya msanii bora wa Hip Hop
Mmoja wa Wasanii akitumbuiza kwenye utoaji wa tuzo za Kili 2012
Msanii Queen Doreen akiimba jukwaani.
Wasanii mahiri katika Maigizo a.k.a vichekesho,Mzee King Majuto na Sharobalo Men
Ommi Dimpoz akikabidhiwa tuzo yake ya Msanii bora anayechipukia na pia amenyakua tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana.
Ommi Dimpoz akitoa shukurani kwa washabiki wake kwa kuzinyakua tuzo hizo mbili
Mwanamuziki Mkongwe wa taarab hapa nchini,Bi Shakila akiimba kwa umahiri mkubwa jukwaani.
Palikuwa hapatoshi leo Mlimani city.
Msanii AT pichani kulia kiwa na tuzo yake ya wimbo bora wenye vionjo vya asili uitwao Vifuu tundu.

Mwanamuziki mahiri wa taarabu nchini,Isha Mashauzi akiibuka kwenda kuchukua tuzo yake
Isha Mashauzi na tuzo yake ya wimbo bora wa taarabu uitwao mamaa mashauzi
Mwimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta,Luiza Mbutu akipokea tuzo ya wimbo wa kiswahili  (bendi) uitwao Dunia Daraja
Mwimbaji mkongwe wa taarabu hapa nchini,Bi Khadija Omar Kopa akiwa na tuzo yake ya mwimbaji bora wa kike.
Khadija Kopa akitumbuiza jukwani.
Msanii Roma kikabidhiwa tuzo yake ya Msanii bora wa Hip Hop,ambapo pia aliibuka na tuzo ya wimbo bora wa hip hop.
Msanii bora wa Rap (Bendi) khalijo Kitokololo akiwa na tuzo yake.
Khadija Kopa na bintize hapatoshi jukwaani .
Mwakilishi wa msanii Jaguar kutoka nchini Kenya akiwa na tuzo ya msanii huyo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki uitwao Kigeu geu.
Picha na JIACHIE BLOG.

Siku Nilipomsikia Nyerere Akilitangazia Taifa Kifo Cha Sokoine


Ndugu zangu,
KUNA wengi  tunaokumbuka tulikuwa wapi siku ile ya tarehe 12 Aprili, 1984 wakati Mwalimu Nyerere alipolitangazia taifa kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine kilichotokana na ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa  akiwa njiani kutoka Dodoma kwenda Dar.

Kwa bahati mbaya, vijana wengi waliozaliwa baada ya 1984 hawajui sana habari za Edward Moringe Sokoine . Mimi nilikuwa Kidato cha Pili tu pale Sekondari ya Tambaza. Nakumbua ilikuwa majira ya saa kumi jioni.  Nilikuwa natembea kwa miguu kutoka Kinondoni ’ A’ kuelekea nyumbani Kinondoni Biafra. Nilipofika maeneo ya jirani na Msikiti wa Mtambani nikasikia wimbo wa taifa unapigwa.

Nilihisi haraka kuna jambo kubwa la kitaifa limetokea. Nikasogea kwenye duka la jirani. Wapita njia wengine nao walisogea mahali hapo. Wimbo wa Taifa ulipomalizika, nikamsikia Mwalimu akianza kutamka kwa sauti ya huzuni; ” Ndugu Wananchi, leo hii…” Kilichofuata ni historia ambayo hapa nashiriki kuiandika.

Naam, Sokoine alikuwa kiongozi wa kweli ambaye daima alisimama upande wa umma. Ni Sokoine aliyetufanya hata tuliokuwa sekondari  wakati huo, tuwe na imani na uongozi wa nchi. Tuwe na matumaini ya maisha bora kwa siku za baadae.

Ndio, ukitoka kwa Mwalimu, ni Sokoine pia aliyechangia katika kutufanya watoto wa wakati huo, tuamini na tuipende siasa. Alikuwa mfano wa kuigwa. Alishi kama alivyohubiri. Siyo tu hakujilimbikizia mali, halipunguza hata mali zake ili apate nafasi zaidi ya kututumikia Watanzania.
Itakumbukuwa, kwenye kikao cha Bunge cha mwezi Aprili, 1984, Sokoine alikabiliana n ahoja za wabunge kutaka kuongezewa posho na marupurupu yao. Sokoine alitamka;

”  Ndugu Spika, niko tayari kuwaongezea wabunge posho ya chakula chao, lakini kamwe sitakuwa tayari kuwaongezea mishahara na marupurupu mengine.” Mwisho wa kunukuu. Huyo ndiye Edward Moringe Sokoine.  Alikuwa kiongozi wa kanuni na mwenye msimamo usioyumba.

Sokoine alielewa, kuwa ukiwalinganisha na wananchi walio wengi, wabunge walikuwa na hali bora zaidi kimaisha. Alikuwa tayari kuchukiwa na wabunge kwa kutetea maslahi ya wanyonge, kuliko kupendwa na wabunge kwa kujali zaidi maslahi yao. 

Baada ya kikao kile cha Bunge, Edward Sokoine, badala ya kupanda ndege ya Serikali kumrudisha Dar es Salaam, aliamua kurudi Dar Es Salaam kwa njia ya barabara, afanye hivyo ili mle anamopita apate nafasi ya kuona shughuli za maendeleo zifanywazo na wananchi. Sokoine hakufika Dar Es Salaam, mauti yakamchukua kwa ajali ya gari pale Wami- Dakawa, Morogoro.
Leo tuna viongozi wa wananchi wenye kutanguliza mbele maslahi yao binafsi. Viongozi wasiotosheka na posho ya elfu sabini ya kikao. Viongozi wenye kufikiria tu ’ kamuhogo kao’. Wanafikiri magari na marupurupu yao badala ya masuala yenye kuwahusu  wananchi wa kawaida.

Je, Sokoine angefufuka leo ingekuwaje?
Bila shaka angefufuka na kufa tena ndani ya siku saba. Maana, Sokoine angeshangaa kuwaona wabunge wa leo wakichukua posho  ya kikao cha siku moja sawa na mshahara wa miezi miwili au mitatu kwa Watanzania walio wengi. 

Sokoine angeshangaa kuona wabunge hawatembelei tena Landrover za bei nafuu bali magari ya kifahari huku wananchi walio wengi bado wanaishi kwenye nyumba za udongo na nyasi. Kwamba bado kuna wanyonge wengi wasio na hakika ya kula yao ya leo na kesho huku wananchi wakiambiwa, tena na Spika wa Bunge, kuwa Bunge ni eneo la umasikini!

 Sokoine angeshangaa kusikia kuwa uongozi siku hizi unanunuliwa, na hata yeye akijaribu tena kuingia Bungeni atalazimika agawe ’ Vimuhogo’ kwa watakaompitisha kwenye kura za maoni.  Sokoine angeshangazwa pia kusikia, kuwa kuna mawaziri na watendaji wakuu serikalini wanaokaa mahotelini kwa kukosa nyumba za serikali kwa vile umepitishwa uamuzi wa kuziuza, kisha kujenga nyingine na kuziuza tena! 

Lakini, Sokoine angeshangaa zaidi kuona Watanzania aliowaacha mwaka 1984 wamechelewa sana kuamka na kupambana kuibadili hali iliyopo. 

Naam, Sokoine angefufuka leo, angesononeka sana kuona pengo pana  lililopo kati ya wenye nacho na wasio nacho. Kati ya viongozi na wananchi. 

Edward Moringe Sokoine, Daima Tutakukumbuka.

Tuesday, April 10, 2012

Wabunge Nassari na Cecilia wa CHADEMA 'wasepa' kuapishwa hii leo

Wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, wote kutoka Mkoani Arusha waliokuwa waapishwe hii leo mjini Dodoma wajaripoti Bungeni hapo.

Taarifa iliyosomwa na Spika wa Bunge, Anna Makinda asubuhi hii baada ya kufungua Mkutano wa Bunge ulioanza leo mjini Dodoma inasema kuwa Wabunge hao Joshua Nasari wa Arumeru Mashariki na Mwingine wa Viti Maalum ambaye amemrithi Marehemu Regia Mtema Cecilia Daniel Pareso, hawajatokea Bungeni mjini Dodoma hii leo.


Cecilia kabla ya uteuzi huo wa Chadema alikuwa ni Diwani wa Kata ya Qurus, iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.


Kwa Mujibu wa Spika Wabunge hao watapaswa kukutana na Kamati ya Bunge ya Uongozi na watapangiwa tarehe nyingine ya kuapishwa.

Wabunge hao walipaswa kuapishwa hii leo kabla ya kuanza kwa shughuli za Bunge.
FK Blog itaendelea kufuatilia habarii hii ili kujua sababu za kuto kufikaa kwao Bungeni hii leo.