Thursday, September 6, 2012
Friday, May 4, 2012
JK AFANYA MABADILIKOYA BARAZA LA MAWAZIRI
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU
MAWAZIRI
MAWAZIRI
1. OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,
2. OFISI YA MAKAMU WA
RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa,
Mb.,
3. OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,
4. WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa Ujenzi
Dr. John P. Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu
Bernard K. Membe, Mb.,
Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,
Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Waziri
wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,
Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza,
Mb.,
Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,
Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,
5. NAIBU MAWAZIRI
OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI
6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,
7. OFISI
YA WAZIRI MKUU
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,
8. WIZARA
MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu
Lazaro Nyalandu, Mb.,
Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid,
Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,
Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
Wataapishwa Jumatatu tarehe 7 Mei, 2012 saa 5.00 asubuhi katika viwanja vya
Ikulu
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
4
Mei, 2012
Tuesday, April 24, 2012
MISS REDD’S ARUSHA CITY CENTRE KUJULIKANA MEI 5, 2012 NDANI YA HOTELI YA NAURA SPRINGS
Washiriki wa kitongoji Kanda ya
kaskazini, Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja,
tayari kuchuana vikali Mei 5, 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura
Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.katika shindano hilo
kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti
vya kawaida ni sh 15,000/=
Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.
---
Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya
kitongoji Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012,yanatarajiwa
kufanyika Mei 5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel
iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.
Akizungumza leo jijini Arusha,Mratibu wa
shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka kampuni ya Tour Visual
Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, amebainisha kuwa
mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na kila kitu kimekwisha
kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo ambao mpaka sasa
wametimia 20.
Bi. Upendo Simwita amesema kuwa
wameishakamilisha mchakato wa kuwapata Warembo wenye mvuto na wenye
vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo hao wenye ari kubwa ya
ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa Miss Tanzania 2012
anatokea kwenye kitongoji hicho.
“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti
kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20, ambao
watachuana vikali jukwaani, na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha
City Center”, alisema Upendo. Amesema kuwa kiingilia katika shindano
hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh 25,000/= na kwa viti vya
kawaida sh.15,000/=
Kwa upande wa Burudani,Upendo amesema
kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam
wa Ukweli, Muziki wa Asili, Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na
burudani nyingine mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku
hiyo.
ZAIDI YA ABIRIA 40 WANUSURIKA KIFO MKOANI MBEYA, BAADA YA BASI LAO KUGONGWA NA KUPINDUKA
Basi
aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria abiria zaidi ya 40, lenye nambari
za usajili T 374 AVR, likiwa limepinduka baada ya kugongwa kwa nyuma na
basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG. Tukio
lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala
Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Basi la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG lililohusika katika ajali, baada ya kuligonga kwa nyuma basi aina ya Coaster enye nambari za usajili T 374 AVR ambapo zaidi ya abiria 40 kunusurika kifo. Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.
---
Picha na Habari: Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Abiria
zaidi ya 40 wamenusurika kifo baada ya basi waliokuwa wakisafiri aina
ya Coaster, lenye nambari za usajili T 374 AVR, kupinduka lilipogongwa
kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499
AVG.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa basi la El Saedy likiwa katika hali ya
mwendokasi liliharibika mfumo wa breki kutoka eneo la Mlima Nyoka na
kuligonga basi hilo dogo kwa nyuma katika mteremko wa Shule ya Sekondari
Imezu, hali iliyopelekea basi hilo dogo kupinduka.
Baada
ya Coaster kupinduka basi la El Saedy likiwa bado katika mwendokasi
liliendelea na safari, kabla ya dereva kufanikiwa kulichepusha kabla
halijavuka reli ya TAZARA katika Kijiji cha Inyala Wilaya ya Mbeya
Vijijini.
Aidha
baadhi ya abiria katika basi hilo dogo walikuwemo wanafunzi 28, wa kike
na kiume wakielekea shuleni majira ya saa moja asubuhi, Aprili 23 mwaka
huu katika Shule ya Sekondari Imezu.
Mara
baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya abiria walikuwemo katika basi
hilo dogo walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya, ambapo
kati yao wamelazwa ili kufanyiwa uchunguzi na wengine wakiruhusiwa
kurudi nyumbani.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mbeya Barakiel
Masaki,hakupatikana kuelezea ajali hiyo ingawa dereva wa basi la El
Saedy anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.
Picha na Habari: MbeyaYetu Blog.
YANGA YAOMBA RADHI MKUTANO MKUU
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga
ambaye pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF akiwakilisha klabu za Mkoa wa
Dar es Salaam, Mohamed Bhinda aliwaomba radhi wajumbe wa Mkutano Mkuu
kwa kitendo cha wachezaji wake kumpiga mwamuzi Israel Nkongo kwenye
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka
huu.
Pia alimuomba Rais wa TFF, Leodegar Tenga
kutoa msamaha wa adhabu ya kulipa faini iliyotolewa na Kamati ya Ligi ya
TFF kwa wachezaji wawili wa Yanga ambao mpaka sasa hawajalipa faini
hiyo.
Rais Tenga alimshukuru Bhinda kwa ujasiri alioonesha wa kuomba radhi mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa kitendo kile.
Aliongeza kuwa kwa vile yeye ni muumini wa
kanuni, na adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni hawezi kutoa
msamaha, hivyo wachezaji hao walipe faini hizo.
Pia Rais Tenga alisema binafsi haziingilia
kamati za TFF katika uamuzi ambao zinafanya kwa vile zina watu
waadilifu, na angekuwa yeye binafsi ndiye anayetoa adhabu, angetoa
adhabu kali zaidi kwa vile vitendo vya kupiga waamuzi havikubaliki
katika mchezo wa mpira wa miguu.
FRANCIS CHEKA NA JAPHET KASEBA KUPAMBANA TENA SIKU YA SABASABA
FRANCIS CHEKA NA JAPHET KASEBA KUPAMBANA TENA SIKU YA SABASABA
Na Mwandishi Wetu
BINGWA wa kick Boxing Japhet Kaseba
amesaini mkataba wa kucheza na Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda
unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro katika uzani wa KG 75
utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo
Kaseba amesema anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha
uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mapambano
;Najua mabondia wa hapa bongo wananikwepa
sana kwa kuwa nimeshakuwa bingwa wa ngumi za mateke lakini awajui mimi
ni bingwa katika mapigano yote alisema Kaseba;
Nitahakikisha naweka kambi ya kutosha na
kukata ngebe za cheka ni mtoto mdogo sana katika masumbwi kwa kweli
bingwa wa kweli ni Rashidi Matumla ambaye ninamuheshimu mpaka sasa cheka
kanikimbia mda mrefu tu tangia tupambane 3 October 2009 ambapo alipewa
ubingwa kwa kusingizia mshabiki wangu alikuja kumtupa nje ya uwanja
kazi yake yeye anarudiana na Mada Maugo kila siku lakini kwa sasa
kakanyaga miwaya zamu yake imefika,
Nae Promota wa mpambano huo Kaike Siraju
amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba
utakuwa ni mpambano ambao aujawai kutokea kwa kuwa mabondia hao
wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya Nchi
Mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae.
BAGAMOYO KUWAKA MOTO USIKU WA MKESHA WA MUUNGANO
KWANJA MAALUM KWA AJILI YA MKESHA WA SIKUKUU YA MUUNGANO LINATARAJIA
KUUSHIKA MJI WA BAGAMOYO KESHO TAREHE 26.04.2012 NDANI YA CLUB LUSONA
ILIYOPO KWENYE HOTELI YA MILLENIUM SEA BREEZE RESORT(OLD POST OFFICE).
KWA MUJIBU WA TAARIFA ZILIZOPATIKANA MJINI BAGAMOYO MCHANA WA LEO
KUTOKA KWA MMOJA WA WARATIBU WA BURUDANI HIYO MAALUMU BW.ALBERT KAWOGO,
BURUDANI HIYO YA AINA YAKE INATARAJIA KUANZA SAA 3:00 USIKU NA KIINGILIO
KITAKUWA 5000/= TU.
TUMEJIZATITI KUTOA BURUDANI YA AINA YAKE
KATIKA CLUB HII KWA KUONGEZA NGUFU YA MADJ MAARUFU KUTOKA MOJA YA KITUO
CHA REDIO CHA JIJINI DAR ES SALAAM ILI WATEJA WETU WAWEZE KUPATA
BURUDANI YA AINA YAKE NA NINAWAOMBA MASHABIKI WA BURUDANI YA DISKO
KUJITOKEZA KWA WINGI,ALISEMA KAWOGO.
HII ITAKUWA MARA YA KWANZA
KWA BURUDANI KAMA HII KUFANYIKA KATIKATI YA JUMA NDANI YA CLUB LUSONA
YENYE UBORA WA AINA YAKE,AMBAYO KWA PAMOJA IMEANDALIWA NA ALBERT
KAWOGO(MUKUBWA KAWOGO) WA FREE VOICE INVESTMENT NA KIMKEV
ENTERTAINMENT .
Subscribe to:
Posts (Atom)

