Tuesday, August 26, 2014

DKT. FRANCIS MICHAEL ATOA UFAFANUZI KUHUSU SUALA LA UTUNGAJI WA KATIBA

         

index
Na Magreth Kinabo, Dodoma
26/08/2014.
 
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Namba  Tatu  ya Bunge hilo, Dkt. Francis  Michael  ametoa ufafanuzi kuhusu suala la utungaji wa Katiba ambalo hufanyika kwa mifumo miwili, na kuwataka wananchi wasipotoshwe na mfumo unaotumika.
 
 Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti huyo, ambaye pia ni mtaalam wa sheria  wakati akizungumza katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na  Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
 
Akifafanua kukuhusu mifumo hiyo, amema kuwa kuna mfumo wa kwanza ,ambao hutumia Tume kama ilivyokuwa Tume ya Jaji Joseph Warioba yenye watu  ambayo ilikuwa na kazi  ya kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi na kutengeneza  Rasimu ya Katiba   Mpya , baadaye  Bunge Maalum la Katiba linapitia maoni ya Rasimu hiyo, ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2014 linaweza kubadilisha na kuongeza kwa ajili ya kuiboresha.
 
“Katika  mfumo huu lazima Bunge liwepo kwa ajili ya kuiboresha kabla ya kwenda kupigiwa kura na wananchi,” alisema Dkt. Michael .
 
Dkt. Michael aliutaja mfumo wa pili ni ule wa   kutumia  Tume  Maalum ya Wataalam, ambao wanawajibu wa kuandika Katiba na  hakuna chombo chochote kitakachokuwa na wajibu wa kuibadilisha, bali itakwenda moja kwa moja kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.
 
“Wananchi wasichanganywe na mfumo unaotumika,” alisisitiza Dkt. Michael.
 
Akizungumzia kuhusu uwasilishaji wa nyongeza ya mapendekezo yaliyowasilishwa na makundi mbalimbali hivi karibuni kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta yamepokelewa kwa mujibu wa sheria hiyo, kipengele cha 25 ambapo Bunge hilo lina nguvu kufanya  marekebisho au kuongoza vifungu vingine  pale linapoona inafaa.
 
Aidha, Dkt. Michael amefafanua kuwa  wanatumia nafasi hiyo kisheria na kikanuni, kupokea nyongeza ya mapendekezo hayo kutoka  kwa watu mbalimbali.
 
Akizungumzia kuhusu suala hilo, Mjumbe wa  Kamati hiyo, Mhe, Ridhiwani Kikwete alisema linafanyika kisheria hivyo mtu au kikundi kinaweza kuwasilisha mapendekezo ya nyongeza.
 
Mhe, Ridhiwani alisema nyongeza ya mapendekezo hayo, uwasilishwa kwenye Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo, ambayo nayo hupeleka kwa Kamati 12 za Bunge hilo kwa ajili ya kuratibu mambo ya msingi na kuyachukua .
 
Aliongeza kuwa suala hilo pia linaweza kufanyika wakati wa mjadala wa Bunge hilo,mjumbe anaweza  kulishawishi Bunge hilo, kwa kuwa sheria , kanuni na miongozo inaruhusu

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUFANYA KIKAOCHAKE CHA BUNGE KARIMJEE DAR ES SALAAM, JK KUUFUNGUA

 


Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa  akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam leo juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaotaraji kuanza kesho katika ukumbi wa Karimjee na kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete kesho kutwa. 

 Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam jana juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Amantius Msole, wabunge wa EALA kutoka Tanzania Twaha Taslima na Shy Rose Banji
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Wabunge kutoka Tanzania, Adam Kimbisa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam leo, juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee. Kushoto ni Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa,wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Twaha Taslima na Shy Rose Banji.
 Mbunge wa EALA kutoka Tanzania, Twaha Taslima akizungumza na wabunge wenzake.
 Mkutano ukiendelea
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Amantius Msole akifafanua jambo. Kulia ni Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa
 Wanahabari wakichukua dondoo za mkutano huo.
 Mbunge Shy Rose Banji akifafanua jambo
 Wabunge wakibadilishana mawazo baada ya kumaliza kwa mkutano huo ambapo walisifu kupata idadi kubwa ya waandishi kuliko nchi nyingine.
Ofisa wa Bunge la Tanzania  Prosper Minja (katikati) akizungumza jambo na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Adam Kimbisa (kulia) na Angela Kiziga.
Wabunge wakitoka nje ya chumba cha mkutano.
********

MKUTANO WA KWANZA – KIKAO CHA TATU – BUNGE LA TATU
(IMETOLEWA NA MH. (Dk.) MARGARET NANTONGO ZZIWA – SPIKA, EALA)


Ndugu Waandishi wa Habari,
 
Napenda kuwakaribisha wote kwenye mkutano huu wa waandishi wa habari ulioitishwa ili kuwafahamisha kuhusu mkutano wa kwanza wa kikao cha tatu cha Bunge la Tatu la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) unaonza tarehe 27 Agosti 2014 mpaka tarehe 5 Septemba 2014 kwenye ukumbi wa Karimjee hapa jijini Dar es Salaam.

Kwa niaba ya Bunge la EALA na kwa niaba yangu mimi binafsi, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, na Serikali nzima ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kukubali kuwa mwenyeji wa EALA kwenye nchi hii kubwa na kwa kukubali kutufungulia rasmi mkutano wetu.

Tunatoa shukrani za pekee kwa uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dk. Kikwete kwa nchi ya Tanzania na vilevile kwa mchango wake kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kama mwanachama wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hii (Summit).

 Hii ni mara ya kwanza kwa Bunge la Tatu kufanya mkutano wake Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wetu mahsusi tuliojiwekea wa kufanya vikao kwa zamu kwenye nchi zote wanachama ili kuliweka Bunge hili liwe karibu zaidi na wananchi ili wapate fursa kufahamu kuhusu shughuli za EALA. Vikao vya Bunge hili sasa hufanyika mara kwa mara kwenye nchi wanachama kwa mujibu wa Ibara ya 55 ya Mkataba (Treaty) wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tunapenda kumshukuru mwenyeji wetu, Spika wa Bunge la Tanzania, Mh. Anna Makinda, kwa kutupa nafasi ya kutumia nyenzo za Bunge la Tanzania na ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya mkutano wetu. Hii inaendelea kudhihirisha uwepo wa mahusiano ya karibu ya kikazi kati ya Bunge la Tanzania na EALA.

Katika kipindi kijacho cha wiki mbili, ratiba ya shughuli za kazi za Bunge la EALA ni kama ifuatavyo:

·        Ufunguzi rasmi wa mkutano wa Bunge na Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete;
·        Kupokea na kujadili ripoti kutoka Kamati mbalimbali za Bunge. Ripoti hizi ni pamoja na ya Kamati ya Masuala ya Jumuiya na Upatanishi wa Migogoro (Committee on Regional Affairs and Conflict Resolutions) and Kituo cha Uongozi cha Afrika cha Taasisi za Afrika Mashariki na Usalama wa Jumuiya (African Leadership Centre on East African Societies and Regional Security); Ripoti ya Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili (Committee on Agriculture, Tourism and Natural Resources) kuhusu semina ya Wabunge wa Jumuiya juu ya Misitu na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Ripoti ya Kamati ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji (Committee on Communication, Trade and Investment) kuhusu Sekta ya Urafiri wa Anga ya EAC.

·        Aidha, kuna Miswada kadhaa ambayo iko mbele ya Kamati mbalimbali za Bunge. Hii ni pamoja na:

a)  Muswada wa Elimu -- the EAC Integration (Education) Bill – ambapo Bunge linatarajia kupokea taarifa kutoka Kamati ya Masuala ya Jumuiya na Upatanishi wa Migogoro (Committee on Regional Affairs and Conflict Resolution) kuhusu hatua waliofikia;

b) Muswada wa Masuala ya Ushirika -- the EAC Co-operatives Societies Bill – huu uko mbele ya Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili (Committee on Agriculture, Tourism and Natural Resources), ambayo hivi karibuni inatarajiwa kuanza vikao vya wazi;

c)  Muswada wa Masuala ya Biashara -- the EAC Joint Trade Negotiations (Repeal) Bill – ambao uko mbele ya Kamati ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji (Committee on Communication, Trade and Investments).

·        Hatimaye, Bunge la EALA litapitia Hoja, Maazimio na Maswali mbalimbali ambayo yatakuwa yameletwa kwenye mkutano.

Kwa ujumla, EALA inatoa mchango wake kwenye mchakato wa utengamano kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na mfumo rasmi wa kisheria na usimamizi ili kuwepo na  kipaumbele kwa ajenda ya utengamano.

Ni muhimu kuhakikisha kuwa wananchi wa Afrika Mashariki wanahusishwa kwenye mchakato huu. Kama EALA tutaendelea kuwa karibu na wananchi wa Jumuiya hii na kuhakikisha kuwa maoni yao yanasikilizwa wakati wa kutunga Sheria.

Siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita, EALA ilifanya ziara mahsusi kwenye vyombo vya habari vya IPP Media jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo, Dk. Reginald Mengi. Tunapenda kutoa shukrani kwa IPP Media kwa kuamua kutuunga mkono kwenye urushwaji wa moja kwa moja (live broadcast) wa ufunguzi rasmi wa mkutano wa Bunge letu. Hii ni hatua ya kwanza ya jitihada zetu za kuhakikisha kuwa tunajenga mahusiano ya karibu kati ya vyombo vya habari na Wabunge wa EALA ili tuweze kutangaza ajenda ya utengamano na kuelimisha wananchi kuhusu majukumu ya Bunge letu. Tutaendelea kufanya majadiliano haya na vyombo vya habari vingine kwenye nchi zote wanachana wa EAC.

Taasisi nyingine ambazo tutazitembelea wakati wa kikao chetu ni pamoja na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) mnamo tarehe 29 Agosti 2014, na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TASUBA) iliyopo Bagamoyo tarehe 30 Agosti 2014. Ziara hizi zinatarajia kuongeza ushirikiano kati ya EALA na washikadau husika kwa upande mmoja na kuboresha kazi zetu za utungaji wa sheria kwa upande mwingine.

Jumuiya ya EAC hivi sasa inapitia katika kipindi muhimu cha mchakato wa utengamano. Tunatoa pongezi kwa nchi zote wanachama kwa kuonesha moyo wa dhati wa kuimarisha mchakato wa utengamano kwa kutekeleza Itifaki mbalimbali.

Umoja wa Forodha (Customs Union) sasa uko kwenye hatua nzuri ya utekelezaji. Ndani ya umoja huu, bidhaa zinazozalishwa kwenye Jumuiya hazitozwi kodi na nchi wanachama na zinafaidika na kodi sawasawa ya nje, pamoja na utaratibu na nyaraka za pamoja. Kuanzishwa kwa Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory) ni jambo jingine kubwa kwenye EAC, kwani kutawezesha bidhaa ziweze kusafiri kwa kasi zaidi.  Lengo la kuwa na Himaya Moja ya Forodha ni kuhakikisha kuwa nchi wanachana zinanufaika kwa pamoja kwa kuunganisha uchumi wa nchi hizi kwa lengo la kuunga mkono jitihada za maendeleo ya uchumi.

Mwaka wa nne wa utekelezaji wa Soko la Pamoja umeanza. Itifaki ya Soko la Pamoja (Common Market Protocol) inahakikisha kuwa kunakuwa hakuna vikwazo vyovyote kwa bidhaa, huduma, ajira, mitaji na uanzishaji wa biashara miongoni mwa wananchi wa nchi wanachana wa Jumuiya. Kwa ujumla, nchi wanachama zimeonesha utashi mkubwa wa kusimamia utekelezaji wa Itifaki hii. Jumuiya ya EAC pia imesaini Itifaki ya kuanzisha Umoja wa Fedha (Monetary Union), ambayo ni hatua ya tatu muhimu kwenye mchakato wa utengemano ambao unapitia kwenye hatua kubwa nne.

Nimetaarifiwa kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari imeshatia saini kupitisha Itifaki ya Umoja wa Fedha (Monetary Union Protocol).

Utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Fedha unatarajia kuanza mara baada ya nchi zote wanachama kuidhinisha itifaki hiyo na kukabidhi nyaraka hizo kwenye ofisi ya Katibu Mkuu wa EAC. Hii ni hatua muhimu sana ambayo itasimika mchakato huu wa utengamano. Hata hivyo, utekelezaji rasmi wa Itifaki hii utahitaji kuwepo kwa sheria mbalimbali. Kama EALA, tumejidhatiti kuhakikisha kuwa tunatunga sheria hizi na hapa tungependa kutoa wito kwa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Council of Ministers) kuleta hii Miswada kwenye Bunge haraka iwezekanavyo.

Pamoja na hatua hizi kubwa ambazo tumepiga, bado kuna changamoto. Kama ilivyoelezwa awali, hatuna budi kuhakikisha kuwa vikwazo vya kibiasha visivyo vya kiforodha (Non-Tariff Barriers) vinashughulikiwa kikamilifu. Utaratibu mahsusi ni lazima uwekwe na utekelezwe kuondoa hivi vikwazo na kama EALA tutatoa wito kwa Kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (Summit) kuharakisha mchakato huu. Changamoto nyingine ni pamoja na kusuasua kwenye utekelezaji wa ajenda ya EAC kwenye sera za taifa za nchi wanachama wa Jumuiya. Tutaendelea kushirikiana na Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki na washikadau wengine kutimiza wajibu wetu kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba ili kuhakikisha kuwa Jumuiya yetu ya kiuchumi inatengemaa.

Ni muhimu kuzingatia kuwa sheria ambazo zinapitishwa na EALA kwa niaba ya EAC zina nguvu ya kisheria na zinatakiwa kupewa kipaumbele kuliko sheria nyingine zilizopo kwenye nchi wanachana kuhusiana na masuala ya Jumuiya. Hivyo basi, tunatoa wito kwa nchi zote wanachama kuharakisha mchakato wa kuhakikisha kuwa sheria za nchi zao zinaoanishwa ili ziweze kuendana na sheria za Jumuiya.

Napenda kutoa wito kwa vyombo vya habari vyote kuwa vishirikiane na EALA katika kutangaza vikao vya Bunge letu katika kipindi hiki cha wiki mbili ambapo tutakuwa tunakutana Dar es Salaam. Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.

KIMENUKA BUNGE LA KATIBA--- MWANDISHI KUBENEA, AKIMBILIA MAHAKAMANI KUOKOA PESA ZA WATANZANIA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI




Pichani niSaed Kubenea,
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited - wachapishaji wa gazeti la MwanaHALISI, lilosimamishwa na serikali kwa muda usiojulikana, MSETO, MwanaHALISI Online.com na mtandao wa MwanaHALISI Forum ambaye amefungua kesi Mahakama kuu kushinikiza Bunge Maalum la Katiba livunjwe picha na Maktaba

 Karoli Vinsent na Mwanahalisi Forum
MWANDISHI mwandamizi wa Habari nchini  Saed Kubenea ameamua kuwa Mzarendo na Nchi yake Baada ya Kufungua kesi Mahakamani kwa lengo la Kuzuia Bunge la Katiba lisiiendelee haya ndio aliyasema mwenyewe Kubenea kuhusu hilo 

“Kwa muda wa siku tatu mfululizo sasa, kumekuwa na mjadala hapa MF kuhusu mimi kufungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Niseme wazi kwamba ni kweli nimefungua kesi hiyo; tayari kesi hiyo imepewa Na. 28/ 2014.

         Katika kesi hiyo, pamoja na mengine, nimeomba mahakama itoe tafsri sahihi juu ya mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba, chini ya vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka 2011.


         Aidha, nimewasilisha maombi nikitaka mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri.

          Kinyume na inavyoelezwa na kutaka kuaminishwa na baadhi ya watu, kuwa nimetumwa kufungua kesi hii; ukweli ni kwamba shauri hili nimelifungua kwa utashi wangu binafsi.

            Katika maisha yangu yote, sijawahi kutumika kwa maslahi ya mtu binafsi. Nimetumika kwa maslahi ya umma. Hivyo basi, sijasukumwa na kundi lolote kufanya kazi hii. Wala siwakilishi matakwa ya yoyote; zaidi ya maslahi ya taifa langu.

        Nimefungua kesi hii, baada ya kuona Rais wa Jamhuri, Dk. Jakaya Kikwete ambaye kwa mujibu wa katiba, amepewa mamlaka ya kusimamia rasimali za taifa, akiendelea kuruhusu mabilioni ya shilingi za walipa kodi yakitumika kwa jambo ambalo halina manufaa kwa taifa.

                 Nimefungua kesi hii, baada ya kukiona chama tawala – Chama Cha Mapinduzi – ambacho ndicho kilichopewa ridhaa na wananchi kusimamia rasimali zao, kikimuoga Samwel Sitta, mwenyekiti wa bunge hilo hivyo kumuacha akitafuna fedha za wananchi kama mchwa.

            Ninawaahidi Watanzania wenzangu, popote walipo – ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano – nitasimama katika shauri hili hadi mwisho. Sitayumba wala kuyumbishwa. Siko tayari kusikiliza yoyote zaidi ya kusimamia maslahi ya nchi yangu.

Saed Kubenea,
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited - wachapishaji wa gazeti la MwanaHALISI, lilosimamishwa na serikali kwa muda usiojulikana, MSETO, MwanaHALISI Online.com na mtandao wa MwanaHALISI Forum.



         Leo, Tarehe 25 August 2014 kwa niaba ya mteja wangu Saed Kubenea ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe wa gazeti ya Mwanahalisi, nimefungua shauri Mahakama Kuu ya Tanzania nikiomba yafuatayo;
            1. Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi ya Kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
       2. Mahakama Kuu itoe tamko iwapo Bunge Maalum la Katiba lina uwezo wa kubadili Misingi Mikuu ya Rasimu.
           3. Mahakama Kuu itoe amri ya kusimamisha Bunge Maalum la Katiba lisiendelee na vikao mpaka pale tafsiri sahihi ya Mamlaka yake itakapotolewa na Mahakama Kuu.

Kwa kuwa muda unakwenda na mabishano yanaendelea, na hakuna anayechukua hatua, nimeona ni vyema kukishirikisha chombo chenye mamlaka kamili ya Kikatiba kutoa tafsiri sahihi ya Kisheria.

Peter Kibatala, Wakili

DIEGO SIMEONE ASHIKISHWA ADABU NA SHIRIKISHA LA SOKA NCHINI HISPANIA, ATASUGUA BENJI MECHI NANE MFULULIZO NA ADHABU NYINGINE JUU

Shirkisho la kandanda nchini Hispania limemsimamisha meneja wa Atletical De Madrid, Diego Simeone kutokuwa kwenye benji la ufundi la timu yake katika michezo minane ijayo kwa sababau ya utovu wa nidhamu aliyo onyesha wakati timu yake ikipepetana dhidi ya mtani wake wa jadi, Real Madrid katika dimbani Vicent Calderon siku ya Ijuma ya Agosti 22 mwaka huu ambapo Atletical walishinda kwa goli 1-0.

Diego Simeone
Diego simeone ndiye kocha anaye ongoza kwa ubwatukaji katika ligi ya Hispania kwa sasa

Katika mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kuashiria kufunguliwa kwa ligi kuu ya Hispania amabayo hufahamika kwa jina SUPER CUP, Diego Simeone alitolewa nje ndani ya dakia 24 ya mtanange huo baada ya kumfokea aliyekuwa mwamuzi wa mchezo huo, David Fernando akitaka amruhusu mchezaji wake, Juanfran Torres kurudi uwanjani haraka baada ya kumaliza kutibiwa jeraha la mdomo alilolipata baada ya kugonga na Ronaldo uwanjani.

Mchanganuo wa adahabu hiyo ni kama ifuatavyo; kwanza Simeone amesimamishwa mechi nne kwa kosa la kumgonga mwamuzi msaidizi kwenye kisogo wakati wa maabisahano, kosa la pili ni lile la kutaka kugoma kutoka nje baada ya kuamriwa kufanya hivyo kosa ambalo limemsimamisha mechi mbili , kosa la tatu ni lile la kufoka wakati akitoka nje ya uwanja ambapo kosa hili limemuweka nje mechi moja na kosa la nne ni lile la kubaki kwenye jukwaa la mashabiki badala ya kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kama ambavyo sheria inasema, kosa ambalo pia limememfanya kuwa nje ya dimba mechi moja.

Mbali na kupewa adhabu ya kuwa nje ya benji la ufundi kwa jumla ya mechi nane, Diego Simeone pia ameamuriwa kulipa kiasi cha dola za kimarekani 6,339, wakati huhuo klabu yake ya Atletical yenyewe ikiamriwa kulipa kiasi cha dola za kimarekani 3,694