Friday, September 2, 2011

Vodacom Miss Tanzania watembelea TBL leo

 Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Tanzania 2011, wakiwasili katika viwanja vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zinazoendeleo katika kampuni hiyo ambayo ni mmoja wa wadhamini wa shindano hilo kupitia kinywaji cha Redds.
 Warembo wakivaa miwani ya kujikinga na vitu vya kupasuka kabla ya kuingia kiwandani.
 Warembo wakipatiwa maelezo ya namna shughuli za uzalishaji Bia unavyofanyika.
Victoria Kimaro Meneja wa Kinywaji Redds akizungumza baada ya ziara hiyo ya warembo.

Usichezee Magufuli kwa kujenga katikia hifadhi ya barabara

Kituo cha Mafuta cha MT Camel kilichokuwa kinajengwa sangasanga Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro katika kona ya kuingilia barabara ya Mzumbe-Mlali kilikubwa na dhoruba ya kubomolewa baada ya kujengwa katika hifadhi ya barabara. Jana Waziri wa Ujenzi alisema zoezi la kubomoa nyumba na vituo kama hivi vilivyojengwa barabarani litaanza kwa kasi na kushirikisha askari.

Sony Ericsson yaja na simu mpya sokoni

Wakuu wa Masoko Afrika wa Kampuni ya Sony Ericsson kulia Patricia Wand na Jorgen Berg wa pili kutoka kushoto pamoja na Upendo Richard kutoka kitengo cha mauzo Vodacom Tanzania wa pili kutoka kulia na Sandhya G kushoto wakionyesha kwa pamoja simu mpya ya Sony Ericsson iliyozinduliwa leo katika hoteli ya Kilimanajro Kempinski jijini Dar es salaam
Mkuu wa Masoko Afrika Kampuni ya Sony Ericsson Patricia Wand akizungumza na wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Simu mpya za kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski leo ukihudhuriwa na watu kutoka makampuni mbalimbali hapa jijini Dar es salaam.
Wageni kutoka kampuni kadhaa zilizohudhuria katika uzinduzi huo kutoka kulia ni Joseline Kamuhanda kutoka Vodacom, Victoria Lukindo Mejeja Masoko kutoka New Habari 2006 LTD, Januarius Maganga Mkurugenzi wa Biashara kutoka IPP na Prosper Vedasto Kutoka kitengo cha Masoko Africa Media Group.
Hawa ni warembo kutoka kampuni ya Sony Ericsson wakipamba uzinduzi huo kutoka kulia ni Diana Besha, Sandra Nakazibwe mna Isabela Shija.
Kutoka kulia ni Meneja wa Masoko wa Sony Ericsson Alex Ristic Gonesh B, Romo M. na Sampath K kutoka Krishna Interantional Ltd.
Kutoka kushoto ni Sandhya Kutoka Krishana Internation Ltd na Venkat M wakiwa katika uzinduzi huo.
Wadau mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Hawa ni warembo kutoka kampuni ya Sony Ericsson wakipamba uzinduzi huo kutoka kulia ni Diana Besha, Sandra Nakazibwe mna Isabela Shija.

Tuesday, August 30, 2011

HERI YA EID MUBARAK 2011

Blog yenu ya kimkev entertainment inawatakia kila la heri katika sikukuu ya Eid Mubarak itakayofanyika kesho na  kesho kutwa na kuwataka muisheherekea kwa amani na utulivu

BALOZI WA LIBYA NCHINI,AITWA SERIKALINI KUJIELEZA KWA NINI AMEBADILISHA BENDERA YA LIBYA DAR BILA KUTOA TAARIFA SERIKALINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe, akizungumza na Balozi wa Libya nchini, Prof. Ahmed El Ash'hab baada ya Balozi huyo kuitwa Wizarani,Dar es Salaam juzi. kufuatia Ubalozi huo kubadilisha Bendera ya nchi hiyo bila kufuata taratibu. (PICHA NA TAGIE MWAKAWAGO WA WIZARA HIYO)

FAMILIA YA GADDAFI YATOROKEA ALGERIA

Mke wa Gaddafi, wanawe wa kiume na wa kike

Mke na watoto watatu wa kiongozi wa Libya aliye mafichoni Muammar Gaddafi wako nchini
Algeria, maafisa wa Algerian wamesema.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema mke wa kanali Gaddafi, Safia, binti yake Ayesha na watoto wa kiume Muhammad na Hannibal waliondoka Libya mapema Jumatatu.

Balozi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa amesema walipokelewa kwa misingi ya kibinadamu.

Waasi wa Libya wamesema kuwapa hifadhi familia ya Gaddafi ni kitendo cha uchokozi, na wametaka warejeshwe nchini Libya.

Haijulikani mahali alipo Kanali Gaddafi.

Wakati huo huo waasi wamesema mtoto mwingine wa kiume wa Kanali Gaddafi, Khamis, huenda aliuawa katika mapigano karibu na Bani Walid.

waasi washambulia Sirte

Taarifa hizo zimetolewa wakati waasi wa Libya wakijaribu kumaliza upinzani uliopo katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo yanayomtii Gaddafi, na kujiandaa kuendelea kwenda katika mji aliozaliwa kanali Gaddafi wa Sirte ili kumalizia upinzani unaonekana kuwa ngome yake ya mwisho.

Kuwasili kwa mke wa kanali Gaddafi na watoto watatu nchini Algeria kuliripotiwa Umoja wa Mataifa na kwa viongozi wa waasi wa Libya, wizara ya mambo ya nje ya algeria imesema katika taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la Algeria, APS.

Taarifa hiyo imesema familia ya Gaddafi walivuka mpaka kati ya Libya na Algeria Jumatatu, saa Mbili na dakika arobaini na tano za huko.

Algeria ni mahali dhahiri pa kukimbilia familia ya Gaddafi kutokana na nchi mbili hizo kuwa na mpaka mrefu na serikali ya Algeria bado halijalitambua Baraza la Mpito la Taifa la Libya.Mke na watoto watatu wa kiongozi wa Libya aliye mafichoni Muammar Gaddafi wako nchini Algeria, maafisa wa Algerian wamesema.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema mke wa kanali Gaddafi, Safia, binti yake Ayesha na watoto wa kiume Muhammad na Hannibal waliondoka Libya mapema Jumatatu.

Balozi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa amesema walipokelewa kwa misingi ya kibinadamu.

Waasi wa Libya wamesema kuwapa hifadhi familia ya Gaddafi ni kitendo cha uchokozi, na wametaka warejeshwe nchini Libya.

Haijulikani mahali alipo Kanali Gaddafi.

Wakati huo huo waasi wamesema mtoto mwingine wa kiume wa Kanali Gaddafi, Khamis, huenda aliuawa katika mapigano karibu na Bani Walid.

waasi washambulia Sirte

Taarifa hizo zimetolewa wakati waasi wa Libya wakijaribu kumaliza upinzani uliopo katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo yanayomtii Gaddafi, na kujiandaa kuendelea kwenda katika mji aliozaliwa kanali Gaddafi wa Sirte ili kumalizia upinzani unaonekana kuwa ngome yake ya mwisho.

Kuwasili kwa mke wa kanali Gaddafi na watoto watatu nchini Algeria kuliripotiwa Umoja wa Mataifa na kwa viongozi wa waasi wa Libya, wizara ya mambo ya nje ya algeria imesema katika taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la Algeria, APS.

Taarifa hiyo imesema familia ya Gaddafi walivuka mpaka kati ya Libya na Algeria Jumatatu, saa Mbili na dakika arobaini na tano za huko.

Algeria ni mahali dhahiri pa kukimbilia familia ya Gaddafi kutokana na nchi mbili hizo kuwa na mpaka mrefu na serikali ya Algeria bado halijalitambua Baraza la Mpito la Taifa la Libya.

ANSWAAR SUNNA WASWALI IDD LEO

Waumini wa dini ya Kiislamu wa madhehebu ya Answaar Sunna wakiswali swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo asubuhi