Monday, September 5, 2011
CHAMI AZINDUA BODI MPYA YA WAKALA WA VIPIMO
Mrembo Rose Albert anyakua taji la Vodacom Miss Talent 2011
Na Mwandishi Wetu
Mrembo anaeuwakilisha Mkoa wa Kilimanjaro na Kanda ya Kaskazini katika shindano la Vodacom Miss Tanzania Rose Albert usiku wa Septemba 3,2011 aliwabwaga baadhi ya Washiriki wenzake aliochuana nao vikali na kunyakua taji la vipaji "Vodacom Miss Talent" iliyofanyika kwenye hotel ya Giraffe iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam.
Wakiadhimisha siku hiyo washiriki hao wa shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa tasnia ya urembo nchini walichuana kwa kuonyesha vipaji vyao mbalimbali ikiwemo kuimba, kucheza miziki mbalimbali ya Bongo flava,nyimbo zetu za kiutamaduni,maigizo.
Akizungumzia siku hiyo Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao Matina Nkurlu alisema lengo la siku hiyo ni kutaka kutambua vipaji mbalimbali walivyonavyo warembo wakiwa tayari kuelekea kwenye hatua ya mwisho ya shindano hilo lenye hadhi ya kimataifa litakalofanyika mlimani city tarehe septemba 10.
Akifafanua Nkurlu alisema kwamba mbali ya kutaka kujua vipaji vyao pia imesaidia kuibua vipaji vya warembo hao mbali na fani ya urembo wanayojihusisha nayo.
“Tukiwa kwenye siku ya Vodacom Miss Talent warembo wameonesha vipaji vyao vya kipekee jambo lililowafanya pia kuendelea kuwa pamoja kama ilivyo tasnia hiyo kwamba inawaunganisha watu wote bila kujali dini rangi au kabila.Nae mrembo Rose Albert alienyakua taji hilo amesema siku hiyo ni ya faida kwake kwani ameweza kuonyesha vipaji vyake mbalimbali alivyonavyo na kujifunza mengi toka kwa washiriki wenza .
Akifafanua Rose alisema mbali ya kuonesha viapaji vyake pia amepanua mtazamo wa kiakili kwani ni moja ya fani zinazoenda kushindaniwa katika shindano la Miss World kwa atakayebahatika kuliwakilisha Taifa letu.“Vipaji ni moja ya vipengele kwenye shindano la urembo la dunia, hivyo kwa atakayebahatika atafanya vizuri kwani vipaji kitu muhimu tayari kwa kwenda kushiriki michuano hiyo ya urembo ya dunia.
Mrembo anaeuwakilisha Mkoa wa Kilimanjaro na Kanda ya Kaskazini katika shindano la Vodacom Miss Tanzania Rose Albert usiku wa Septemba 3,2011 aliwabwaga baadhi ya Washiriki wenzake aliochuana nao vikali na kunyakua taji la vipaji "Vodacom Miss Talent" iliyofanyika kwenye hotel ya Giraffe iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam.
Wakiadhimisha siku hiyo washiriki hao wa shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa tasnia ya urembo nchini walichuana kwa kuonyesha vipaji vyao mbalimbali ikiwemo kuimba, kucheza miziki mbalimbali ya Bongo flava,nyimbo zetu za kiutamaduni,maigizo.
Akizungumzia siku hiyo Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao Matina Nkurlu alisema lengo la siku hiyo ni kutaka kutambua vipaji mbalimbali walivyonavyo warembo wakiwa tayari kuelekea kwenye hatua ya mwisho ya shindano hilo lenye hadhi ya kimataifa litakalofanyika mlimani city tarehe septemba 10.
Akifafanua Nkurlu alisema kwamba mbali ya kutaka kujua vipaji vyao pia imesaidia kuibua vipaji vya warembo hao mbali na fani ya urembo wanayojihusisha nayo.
“Tukiwa kwenye siku ya Vodacom Miss Talent warembo wameonesha vipaji vyao vya kipekee jambo lililowafanya pia kuendelea kuwa pamoja kama ilivyo tasnia hiyo kwamba inawaunganisha watu wote bila kujali dini rangi au kabila.
Akifafanua Rose alisema mbali ya kuonesha viapaji vyake pia amepanua mtazamo wa kiakili kwani ni moja ya fani zinazoenda kushindaniwa katika shindano la Miss World kwa atakayebahatika kuliwakilisha Taifa letu.“Vipaji ni moja ya vipengele kwenye shindano la urembo la dunia, hivyo kwa atakayebahatika atafanya vizuri kwani vipaji kitu muhimu tayari kwa kwenda kushiriki michuano hiyo ya urembo ya dunia.
Nae Mkuu wa kitengo cha Itifaki wa Kamati ya Vodacom Miss Tanzania Albert Makoye alisema ari waliyonayo warembo inaonesha utayari wao katika kuliwakilisha Taifa katika medani za kimataifa.
“Mmejionea wenyewe baadhi ya washiriki wetu walivyochuana katika shindano hili la Vodacom Miss Talent 2011 katika kuadhimisha siku ya vipaji kwa warembo. Hili tu linadhihirisha kwamba shindano la mwaka huu litakuwa na changamoto kubwa ikilinganishwa na mengine yaliyopita,” alisema Makoye.

Friday, September 2, 2011
NGELEJA AZINDUA KAMATI KAMATI YA KUSIMAMIA MCHAKATO WA UAGIZAJI MAFUTA KWA PAMOJA
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kushoto), akiwapongeza baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kusimamia mchakato wa uagizaji mafuta wa pamoja, baada ya kuizindua rasmi , Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Charles Sangweni na Tumaini Massaro.
Baadhi ya wadau wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa kamati hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kamati ya kusimamia mchakato wa uagizaji mafuta wa pamoja, jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu na Mwenyekiti wa Bodi wa EWURA, Simon Sayore. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA)
Kutoka kulia ni Boss wa EWURA, Haruna Masebu , Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Simon Sayore, Mjumbe wa Bodi ya Ewura, na Mjumbe wa zamani wa Bodi hiyo, Vincent Gondwe
Ngeleja akisalimiana na baadhi ya wajumbe wapya wa Bodi ya Ewura
Waziri Ngeleja akisalimiana na kiongozi wa Umoja wa wauzaji mafuta nchini (TAOMAC), Salum Bisarara. Katikati ni wajumbe wa kamati mpya ya kusimamia mchakato wa uagizaji mafuta kwa pamoja
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kamati ya kusimamia mchakato wa uagizaji mafuta wa pamoja, Dar es Salaam
Waziri Ngeleja akitoka baada ya kuzindua kamati hiyo huku akisindikizwa na kiongozi wa Umoja wa wauzaji mafuta nchini (TAOMAC), Salum Bisarara (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA , Simon Sayore. Uagizaji wa mafuta kwa pamoja unatarajiwa kuanza kabla ya mwaka huu kwisha. Vodacom Miss Tanzania watembelea TBL leo
Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Tanzania 2011, wakiwasili katika viwanja vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zinazoendeleo katika kampuni hiyo ambayo ni mmoja wa wadhamini wa shindano hilo kupitia kinywaji cha Redds.
Warembo wakivaa miwani ya kujikinga na vitu vya kupasuka kabla ya kuingia kiwandani.
Warembo wakipatiwa maelezo ya namna shughuli za uzalishaji Bia unavyofanyika.
Victoria Kimaro Meneja wa Kinywaji Redds akizungumza baada ya ziara hiyo ya warembo.
Usichezee Magufuli kwa kujenga katikia hifadhi ya barabara
Kituo cha Mafuta cha MT Camel kilichokuwa kinajengwa sangasanga Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro katika kona ya kuingilia barabara ya Mzumbe-Mlali kilikubwa na dhoruba ya kubomolewa baada ya kujengwa katika hifadhi ya barabara. Jana Waziri wa Ujenzi alisema zoezi la kubomoa nyumba na vituo kama hivi vilivyojengwa barabarani litaanza kwa kasi na kushirikisha askari.
Sony Ericsson yaja na simu mpya sokoni
Wakuu wa Masoko Afrika wa Kampuni ya Sony Ericsson kulia Patricia Wand na Jorgen Berg wa pili kutoka kushoto pamoja na Upendo Richard kutoka kitengo cha mauzo Vodacom Tanzania wa pili kutoka kulia na Sandhya G kushoto wakionyesha kwa pamoja simu mpya ya Sony Ericsson iliyozinduliwa leo katika hoteli ya Kilimanajro Kempinski jijini Dar es salaam
Mkuu wa Masoko Afrika Kampuni ya Sony Ericsson Patricia Wand akizungumza na wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Simu mpya za kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski leo ukihudhuriwa na watu kutoka makampuni mbalimbali hapa jijini Dar es salaam.
Wageni kutoka kampuni kadhaa zilizohudhuria katika uzinduzi huo kutoka kulia ni Joseline Kamuhanda kutoka Vodacom, Victoria Lukindo Mejeja Masoko kutoka New Habari 2006 LTD, Januarius Maganga Mkurugenzi wa Biashara kutoka IPP na Prosper Vedasto Kutoka kitengo cha Masoko Africa Media Group.
Hawa ni warembo kutoka kampuni ya Sony Ericsson wakipamba uzinduzi huo kutoka kulia ni Diana Besha, Sandra Nakazibwe mna Isabela Shija.
Subscribe to:
Posts (Atom)