Tuesday, September 6, 2011
WIZARA YA ELIMU YAADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU
Alexia William ndie Miss Personality 2011
Mrembo Alexia Williams akibebwa na wenzake wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 baada ya kutajwa kuwa ndie mshindi wa Miss Personality na kupata tiketi ya kuingia nusu fainali ya Vodacom Miss Tanzania itakayofanyika September 10 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Tayari warembo wengine wa nne wameshafanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali.
Warembo wanne kati ya 30 wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 waliopata kura nyingi za shindano la Miss Personality wakipozi kwa picha baada ya kutangazwa. Kutoka kulia ni Dalilla Ghalib, Maua Kimambo, Alexia William na Cynthia Kimasha. fainali za Vodacom Miss Tanzania 2011 zitafanyika Septemba 11, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaa
Mrembo Alexia Williams akipozi mbele ya washiriki wenzake wa Vodacom Miss Tanzania 2011 baada ya kutajwa kuwa ndie mshindi wa Miss Personality na kupata tiketi ya kuingia nusu fainali ya Vodacom Miss Tanzania itakayofanyika September 10 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Tayari warembo wengine wanne wameshafanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali.

Monday, September 5, 2011
VODACOM TANZANIA YAPATA MKURUGENZI MTENDAJI MPYA
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom leo imemtangaza Rene Meza kuwa Mkurugenzi
Mtendaji mpya wa kampuni hiyo hapa nchini.
Rene ambae kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bharti Airtel Kenya ana uzoefu mpana wa kimataifa katika sekta ya mawasiliano ya simu wa zaidi ya miaka kumi na miwili akiwa ameshafanya kazi barani Afrika, Asia na Larin-Amerika.
Akizungumzia uteuzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Johan Dennelind amesema:
“Tunayo furaha kubwa kwa Rene kujiunga nasi. Rene analeta uzoefu mpana kutoka nchi
alizowahi kufanyia kazi ikiwemo Paraguay, Pakistan na Kenya na amewahi pia kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Millicom’s (Tigo) nchini Tanzania hivyo basi ni wazi majukumu yake mapya katika Vodacom hayatokuwa na ugumu na atayamudu ndani ya muda mfupi.”
Rene anachukua nafasi ya Dietlof Mare ambae ameomba kupangiwa kazi nyengine baada ya kuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne na nusu na hilo linafanyika kama sehemu ya programu ya Vodacom ya maendeleo ya uongozi. Taarifa ya kazi mpya atakayopangiwa itatolewa baadae.
“Napenda kumshukuru Dietlof,chini ya uongozi wake Vodacom Tanzania imepiga hatua kubwa, kwa sasa ni kampuni ya pili kwa ukubwa Afrika ikiwa na wateja zaidi ya milioni tisa ukiacha Vodacom Afrika Kusini. Amekuwa ni kiongozi wa kuhusudiwa na wengine, uendeshwaji wa huduma ya M-Pesa na nyengine zilizobuniwa na kusimamiwa nae zinaiweka Vodacom mahala pazuri kibiashara katika siku za usoni.”Alisema Dennelind.
Dennilend amesema Vodacom itautumia ujuzi wa Dietlof popote katika kundi la makampuni ya Vodacom.
Imetolewa na:Mtendaji mpya wa kampuni hiyo hapa nchini.

Mwamvita Makamba
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano
Vodacom Tanzania
JEEP LA MILIONI ZA TZ 72 NDIYO ZAWADI YA MISS VODACOM TANZANIA 2011
Mshindi wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania mwaka huu kujinyakulia gari hili hapa juu aina ya Jeep lenye thamani ya shilingi za kitanzania Milioni 72.
Meneja Masoko wa CFAO "DT Dobie", Alfeddy Minja na Mkuu wa Udhamini wa Vodacom George Rwehumbiza (kushoto) wakimkabidhi ufunguo wa gari Hilo Mkurugenzi wa Lino International Agency mwandaaji wa Miss Tanzania , Hashim Lundenga.
JOYCE KIRIA APATA ZALI TENA

Bw Henry John Kileo na Bi Joyce Kiria Walipofunga ndoa yao jana Jumapili(jana) na baadae bonge la pati lililofanyika katika hoteli ya Atrium pande za Afrika Sana - Mwenge.NI mara ya pili kwa Joyce kiria kuolewa ndani ya kipindi cha muda mfupi baada ya kutalakiana dj Nelly mumewe wa ndoa ya kwanza Dj.
SENEGAL, IVORY COAST WATANGULIA EQUATORIAL GUINEA AND GABON, MISRI WAVULIWA TAJI
Timu ya Senegal imefuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani shukrani kwa mabao mawili ya Moussa Sow na kuisaidia nchi yake kushinda 2-0 dhidi ya DR Congo, huku Misri ikiaga rasmini baada ya kufungwa 2-1 na Sierra Leone.
Mfungaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1 alionyesha thamani yake kwenye ardhi ya nyumbani baada ya kupachika mabao hayo mawili katika kipindi cha kwanza na kuamsha shangwe kwenye jiji la Dakar na kuifanya Senegal kuongoza Kundi E.
Wanaungana na Botswana, Burkina Faso na Ivory Coast kuunda timu 16 zitazocheza michuano hiyo pamoja na wenyeji wawili Equatorial Guinea na Gabon.
Burkina Faso ilifuzu hata kabla ya kuanza kwa mpira baada ya Namibia kuichapa Gambia 1-0 jijini Windhoek kwenye mechi iliyochezwa mapema.
Mafanikio ya Burkina Faso na Senegal yalifunika kwa ushindi wa Libya, ikicheza timu mpya chini ya bendera mpya ya taifa walifanikiwa kufufua matumaini yao.
Libya ilifanikiwa kuichapa Msumbiji kwa bao1-0 jijini Cairo katika mechi Kundi C iliyochezwa huku milango ya uwanja ikiwa imefungwa.

Cameroon ilitoa namachungu yake kwa kuinyuka Mauritius 6-0, nayo Ivory Coast walitoa salamu za pole kwa majeruhi Didier Drogba baada ya chipukizi Gervinho kuongoza mauaji ya mabao 5-0 dhidi Rwanda.
Mali ikiwa na kiungo wa Barcelona, Seydou Keita wamejiweka vizuri baada ya kushinda 3-0 nyumbani dhidi ya Cape Verde jijini Bamako huku Tunisia ikiweka njia panda baada ya kutoka suruhu na Malawi.
Subscribe to:
Posts (Atom)