Friday, September 9, 2011

LIUMBA AFIKISHWA KORTINI KWA KUKUTWA NA SIMU GEREZANI

Mfungwa anayeshitakiwa kwa kosa kukutwa na simu ya mkononi inayodaiwa kutoruhusiwa gerezani, Amatus Liyumba, akiongozwa na Askari Magereza kupelekwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam jana kwa ajili ya kusomewa shitaka lake hilo.

Amatus Liumba akiwa Mahakamani

Thursday, September 8, 2011

SIMBA BYEE YANGA TEE


Mshambuliaji wa Yanga, Davis Mwape (kulia) akiwania mpira dhidi ya beki wa Mtibwa Sugar, Salum Sued wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Yanga jana kwa mara ya kwanza walivaa jezi za mdhamini wa Ligi Kuu Vodacom, lakini zikiwa na alama nyeusi badala ya alama nyekundu. Picha na Juma Mtanda wa gazeti la mwananchi.

Mwandishi Wetu
MABINGWA watetezi Yanga wameendelea kung'ang'ania mkiani mwa Ligi Kuu huku mahasimu wao Simba wakipata ushindi wa tatu mfululizo kwenye ligi hiyo katika mechi zilizofanyika jana kwenye viwanja vya Jamhuri, Morogoro na Mkwakwani, Tanga.

Yanga walishuka kwenye Uwanja wa Jamhuri wakiwa na matumaini ya kupata pointi tatu, lakini walijikuta wakilazimishwa suluhu na Mtibwa Sugar, wakati Gervas Kago alifunga bao lake la kwanza tangu aanze kuichezea Simba na kuiwezesha timu hiyo kuilaza Villa Squad bao 1-0, huku Polisi Dodoma wakitoka suluhu na Ruvu Shooting.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi tisa na kupanda hadi nafasi ya pili nyuma ya kinara wa ligi JKT Ruvu kwa tofauti ya mabao.Mabingwa wa Kombe la Kagame Yanga waliokusanya pointi mbili katika michezo mitatu ya ligi waliyocheza mpaka sasa walilazimika kubaki ndani ya uwanja wa Jamhuri kwa dakika tano na kuondolewa na ulinzi mkali wa polisi FFU baada ya mashabiki wao wenye hasira kuanza kurushia mawe basi lililobeba wachezaji hao.

Kocha Sam Timbe akizungumzia pambano hilo alisema vijana wake walishindwa kutumia nafasi walizopata kwenye mchezo huo.

Mkenya Tom Olaba aliyeiwezesha Mtibwa Sugar kufikisha pointi nane mpaka sasa aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kutawala sehemu ya kiungo, lakini walipoteza nafasi chake walizopata.Mtibwa ilianza mchezo huo kwa kasi na katika dakika ya 17, kipa Yaw Berko alifanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Said Mkopi.

Yanga ikicheza bila ya nahodha wake, Shadrack Nsajigwa ilionekana kupwaya katika kiungo na kuruhusu mashambulizi mengi golini kwake shukrani kwa juhudi binafsi za kipa Berko.

Mshambuliaji Thomas Mourice wa Mtibwa Sugar alipoteza nafasi ya kufunga katika dakika ya 40 kwa kushindwa kuunganisha vema krosi ya upande wa kushoto iliyopigwa na Said Bahanunzi.

Washambuliaji wa Yanga, Davis Mwape na Jerryson Tegete walikosa mabao katika dakika ya 29 na 42 waliposhindwa kutumia nafasi zilizotengenezwa na winga Julius Mrope.

Shujaa wa Ngao ya Jamii mshambuliaji wa Ghana, Kenneth Asamoah alishindwa kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Rashid Gumbo na kutemwa na kipa Munishi katika dakika ya 70.

Tanga; Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba wamedhamiria kurudia rekodi yao ya msimu wa 2009/10 waliotwaa ubingwa bila ya kupoteza mchezo wowote baada ya kuichapa Villa Squad bao 1-0.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kago alifunga bao lake la kwanza Ligi Kuu ya Tanzania katika dakika ya 7 akipokea krosi ya Haruna Moshi na kuipa Simba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Villa Squad.

Katika mchezo huo beki Victor Costa alifanya kazi ya ziada kuokoa bao lililotaka kufungwa na Mohamed Kijuso katika dakika za mwisho kwa mpira wa kichwa uliompotea kipa Juma Kaseja.

Pia winga wa Simba, Ulimboka Mwakingwe alipewa kadi ya njano kwa kujiangusha kwenye eneo la penalti, huku Amri Ramadhan wa Villa Squad akipewa kadi ya njano kwa kuushika mpira kwa makusudi.

Dodoma; Polisi Dodoma wakiwa nyumbani kwenye uwanja wa Jamhuri walilazimishwa suluhu na Ruvu Shooting.

Wenyeji Polisi walitawala vizuri kipindi cha kwanza na washambuliaji wake, Bantu Admin na Kulwa Mobby kulifikia goli la Ruvu mara kadhaa, lakini kipa Benjamin Haule wa Ruvu Shooting alikuwa kikwazo kwao.

Shooting waliamka na kujibu mapigo kwa kushambulia kwa kushtukiza kupitia kwa washambuliaji wake Abdalah Juma na Abrahman Musa.

VIKOSI

Yanga: Yaw Berko, Godfrey Taita, Oscar Joshua, Bakari Mbegu, Chacha Marwa, Nurdin Bakari, Julius Mrope, Rashid Gumbo, Jerryson Tegete (Kenneth Asamoah), Davis Mwape, Kigi Makassi (Idrissa Rashid).

Mtibwa Sugar: Deogartius Munishi, Juma Abdul, Issa Rashid, Salvatory Ntebe, Salum Sued, Shabaan Nditi, Said Mkopi, Masoud Ali, Said Bahanunzi, Thomas Mourice na Ali Mohamed.

Simba: Juma Kaseja, Nasoro Chollo, Amir Maftah, Juma Nyoso, Victor Costa, Jerry Santo, Shija Mkina, Amri Kiemba, Gervas Kago, Haruna Moshi na Ulimboka Mwakingwe.

Villa Squad: Abbas Nassoro, Haruna Shamte, Yassin Majota, Shai Mpala, Menard Mbugunza, Zuberi Dadi, Lameck Mbonde, Mussa Nampaka, Mohamed Kijuso, Mohamed Binslum na Nsa Job.

OFFICIAL:MR & MRS BONIVENTURE KILOSA

Over the weekend one of the most popular DJs in the country,DJ Venture(Real name Boniventure Kilosa) wedded his fiancee,Bernadina Shirima. The wedding took place at St.Martha Church in Mikocheni and then followed by a superb reception at Kilimanjaro-Kempinsk Hotel Dar-es-salaam. We congratulate and wish them an ever happy marriage life.

Wednesday, September 7, 2011

Warembo wajinyakulia dola kutoka Papazi baada ya kuigiza


Mrembo Zubeda Seif aliyejinyakulia kitita cha Dola 1000 akimnanga muingizaji nguli Jacquline Wolpa wakati wa kutafuta mrembo wa Vodacom Miss Tanzania aliye na kipaji cha uigizaji.
Washindi wakionesha vitita vya kutoka kushoto ni  Christine Mwegoha aliyepata dola 200, Zubeda Seif dola 1000 na Husna Maulid, warembo hawa wa Vodacom Miss Tanzania pia watafabya kazi nba Kampuni ya Papazi Entertainment & Promotion katika uchezaji Filamu.
Maofisa wa Papazi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Papazi, Hans Zakaria (kulia) wakipiga picha ya pamoja baada ya washindi hao kukabidhiwa vitita vyao.
Husna Maulid akionesha makali yake katika kucheza filamu na hapa akiigiza kuwa na machungu.
Mshiriki wa Vodacom Miss Tanzania Glori Lory, akicheza kipande chake na Yusuf Mlela.
Vodacom Miss Tanzania Top Model, Mwajabu Juma (kushoto) akijibizana na Princess Mashonobo.
Majaji wa shindano hilo la kutafuta waigizaji.

NMB yazindua Business Club mkoani Shinyanga


Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Amina Masenza (hayupo pichani) aliyekuwa akiongea wakati wa uzinduzi rasmi wa Klabu ya Wafanbyabiashara wa Benki ya NMB mkoani humo jana. Klabu hiyo inalengo la kuboresha mahusiano na mawasiliano kati ya Benki na wateja wake.
Meneja wa NMB Mikopo Midogo, Mashaga Changarawe akitoa mada yake juu ya utoaji wa Mikopo.
Meneja wa NMB tawi la Manonga, James Subi, (wapili kulia) akimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Amina Masenza baada ya kuzindua rasmi klabu ya wafanyabiashara wa Benki ya NMB mkoani Shinyanga jana.  Klabu hiyo inalengo la kuboresha mahusiano na mawasiliano kati ya Benki na wateja wake. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Jamii wa Benki ya NMB, Shy-Rose Banji (kushoto) ni Meneja wa NMB Mikopo Midogo, Mashaga Changarawe.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Amina Masenza (kushoto) akizungumza jambo baada ya kuzindua rasmi klabu ya wafanyabiashara wa Benki ya NMB mkoani Shinyanga jana, pamoja nae ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Jamii wa Benki ya NMB, Shy-Rose Banji.  Klabu hiyo inalengo la kuboresha mahusiano na mawasiliano kati ya Benki na wateja wake

Magavana wakutana Arusha


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) Dkt .Frannie Leautier(katikati) akiongea na waandishi wa habari leo mjini Arusha kuhusu kuanza kwa Mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika(ACBF) unaotarajiwa kufunguliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete siku ya Alhamis (8.9.2011). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano(ACBF) Audrey Mpunzwana na kushoto ni Mtaalamu kutoka ACBF George Kararach.

MSAFARA WA LIBYA WENYE ULINZI MKALI WAINGIA NIGER


Waasi wa Libya
Mke wa Gaddafi, Safia na wanawe
Msafara wa magari wenye ulinzi na silaha kutoka Libya umevuka mpaka kuingia nchini Niger, ripoti zinasema.

Msafara huo unaaminika ni wa wapiganaji wa Tuareg waliopewa mafunzo na Kanali Muammar Gaddafi aliyekimbia nchi kupigania utawala wake ukielekea katika mji wa Agadez.

Haijafahamika wazi iwapo kuna mwanafamilia yeyote wa Kanali Gaddafi katika msafara huo. Msemaji wake alisema Gaddafi mwenyewe bado yuko Libya.

Kanali Gaddafi ameapa atapigana mpaka kufa, ingawa amepoteza sehemu kubwa ya udhibiti wake nchini Libya.

Nato, ambayo imekuwa ikiendesha harakati za kijeshi za anga kuunga mkono Maamuzi ya Umoja wa Mataifa kuwalinda ria wa Libya, imekataa kusema chochote katika ripoti yake.

'katika ari ya juu'
Msafara huo wenye silaha umevuka mpaka na kuingia Niger na kufika mji wa Agadez Jumatatu, taarifa za kijeshi kutoka Ufaransa na Niger zimelifikia Shirika la Habari la Reuters.

Wamesema msafara huo una magari kati ya 200 na 250 na unasindikizwa na jeshi la Niger.

Wasemaji kutoka Agadez wameiambia BBC kuwa kati ya magari hayo 200, 60 ni ya Libya na yaliyosalia ni kutoka Niger.

Baadaye afisa mmoja kutoka Baraz la Mpito la Taifa Libya (NTC) aliliambia Shirka la Habari la Reuters kuwa msafara huo umebeba dhahabu na fedha na umevuka kuingia Niger kutoka katika mji unaoshikiliwa na Gaddafi wa Jufra.

"Usiku wa Jumatatu, magar 10 yaliyokuwa yamebeba dhahabu, fedha za Euro na dola na kuvuka mpaka kutoka Jufra na kuingia Niger wakisaidiwa na wapiganaji wa Tuaregs kutoka kabila moja Niger," Fathi Baja alisema.

Madai haya hayajathibitishwa na vyombo huru.

Mwandishi wa BBC Kevin Connolly, aliyeko mjini Tripoli, anasema kuna tetesi kuwa msafara huo unaweza kuwa umebeba washirika wa karibu wa Kanali Gaddafi huku njia ya jangwani inaonekana kuwa ni pekee kuweza kukimbia vikosi vya waasi wanaounda utwawala mpito nchini Libya.

Nchi ya Burkina Faso iliyoko Afrika Magharibi, haina bandari, inachangia mpaka na Niger, imekubali kumpa hifadhi Kanali Gaddafi.

Waasi wengi wa zamani wa Tuareg kutoka Mali na Niger walipewa mafunzo nchini Libya kati ya miaka ya 1970 na 80.

Kanali Gaddafi alisaidia kufikiwa makubaliano ya amani mwaka 2000 kati ya serikali ya Niger na kundi la waasi wa Tuareg linaloongozwa na Rissa ag Boula, ambaye alikimbilia Libya.

Watu wengi walioshuhudia wanasema wamemuona Rissa ag Boula katika msafara huo, lakini amekanusha taarifa hizo akiiambia AFP: "Mimi niko Niamey [Mji mkuu wa Niger]."

Msemaji wa NTC mjini London, Guma el-Gamaty, ameiambia BBC kuwa Niger italipishwa faini iwapo itathibitika kuwa imemsaidia Kanali Gaddafi kutoroka.

"Niger ni jirani na Libya kutoka Kusini na haina budi kufikiria uhusiano wake na Libya siku za usoni," Bw Gamaty alisema. "Hili – iwapo litathibitishwa - litaathiri sana uhusiano kati ya Libya na Niger."

Mke wa Kanali Gaddafi na watoto wake wawili wa kiume na binti yake tayari wamekimbilia Algeria.

Mwandishi wa BBC Jon Leyne, mjini Benghazi, yalipo makao makuu ya waasi, anasema kwa msafara mkubwa kama huo usingeweza kukatisha jangwa bila ya Nato kutokuuona.

Nato imekataa kusema chochote kuhusu masuala yake ya kijasusi, msemaji wake ameiambia BBC.

Kanali Roland Lavoie amesema kazi kubwa ya muungano wa Nato ni kuwalinda raia sio kufuatlia ‘viongozi wa zamani wanaokimbia nchi, mamluki,makamanda wa jeshi na watu waliopoteza makazi yao ".

Wakati waasi wanaimarisha ngome yao nchini Libya, Nato imeendelea na harakati zake za kijeshi za anga na uangalizi kama ilivyopewa majukumu na UN ya kuwalinda raia wa Libya.

Mapema Jumatatu, msemaji wa Kanali Gaddafi Moussa Ibrahim alisema kiongozi wa Libya ‘yuko vizuri na mwenye ari kubwa’

‘Yuko mahali ambako hataweza kufikiwa na vikundi cha watu tu walioasi na b ado yuko’ Bw Ibrahim ameiambia televisheni ya ya Arrai.