Tuesday, October 25, 2011

WAMBURA AENGULIWA NA TFF KUGOMBEA UENYEKITI MKOA WA MARA

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka T anzania (FAT), sasa TFF, Michael Wambura akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kabla ya Kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kumwengua usiku huu kugombea uenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara, kwa madai kwamba si mkazi wa mkoa huo.

KOCHA PAPIC NA YANGA TENA

Kocha wa Yanga Kostadic Popic, akiomba dua na wachezaji wa timu hiyo, baada kuanza tena kuifundisha leo jioni kwenye Uwanja wa Kaunda, Jangwani, Dar es Salaam.
Papic akiwajibika uwanjani huku Kocha Msaidizi,Fred Minziro akiondoka
Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi chini ya Kocha Papic jana jioni

DK SHEIN AAPISHWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI


Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande (kushoto), akimwapisha Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam juzi.
Rais Jakaya Kikwete (mbele katikati), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu, Othman Chande pamoja na mawaziri baada ya kuapishwa kwa Shein Ikulu Dar es Salaam .

JK akimpongeza Dk. Shein
JK (wa pili kulia) akiwa na Dk. Shein (kulia kwake), Waziri Mkuu (kulia) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othaman Chande.
Jaji Mkuu, Othman Chande akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema wakati wa hafla hiyo.
JK akizungumza na Jaji Mkuu, Othman Chande (kushoto), Dk Shein (wa pili kulia) pamoja na Waziri Mkuu, Pinda. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO)

KAMATI ZA BUNGE ZAKUTANA DAR


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Kabwe Zitto na Katibu wa Kamati hiyo, Eric Maseke wakitafakari jambo wakati wakijadili utendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), katika kikao cha kamati hiyo, Dar es Salaam juzi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Idd Azzan akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Augustino Mrema.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi akijieleza mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Dar es Salaam jana. PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA

UTURUKI WATOA MSAADA WA INCUBATORS 10 WAMA


Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshukuru balozi wa Uturuki Nchini, Dkt Sander Gurbuz, baada ya kupokea msaada wa mashine 10 za kusaidia watoto waliozaliwa kabla ya muda wao. Mashine hizo, zenye thamani ya dola 30,000 (kama milioni 50), zimetolewa na kampuni ya madini na nishati ya Uturki iitwayo TPM ambapo Mkurugenzi Mkuu wake Bw Burak Buyuksaar (wa tatu kulia) alikuwepo kushuhudisa makabidhiano hayo. Kulia ni mke wa balozi, Mama Durhan Gurbuz.
Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania umetoa msaada wa incubators 10 zenye thamani ya Tsh. Mil 50/- kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mhe. Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. 

Akikabidhi msaada huo Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Dr. Sander Gurbuz amesema kuwa wametoa msaada huo kwa ajili ya kusaidia moja ya programu za Taasisi ya WAMA inayolenga kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto. Pamoja na kudumisha uhusiano mzuri ambao nchi yake ya Uturuki na Tanzania umekuwa nao. 
Mhe. Balozi aliambatana na Mke Wake Mama Durhan Gurbuz na Mkurugenzi Mkuu wa TPM Mining and Energy Co. Limited, Bw. Burak Buyuksarac. 
Akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mhe. Mama Salma Kikwete amesema kuwa msaada huo ni mkubwa sana na utasaidia kuokoa maisha ya watoto wachanga ambao wangeweza kufa kutokana na ukosefu wa vifaa hivi hasa maeneo ya vijijini. 
Mama Salma aliongeza kuwa pamoja mazingira ya Vijijini yanaweza yasiruhusu sana utumiaji wa vifaa hivi lakini kwa sababu siku hizi kuna umeme wa jua utasaidia matumizi ya vifaa hivi.

MBEYA WAMUAGA MKURUGENZI WA VODACOM DIETLOF MARE


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania anaemaliza muda wake hapa nchini,Dietlof Mare(katikati) Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga,wakiwa wameshikilia picha inayomuonyesha Mare akisimikwa na wazee wa kimila wa kabila la Wahehe mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa,wakati alipotembelea mkoa huo kuwaaga rasmi hivi karibuni.

JUDITH SANGU NDIYE MISS KIU 2011


Mrembo Judith Sangu usiku wa Jumamosi iliyopita aliibuka kidedea baada ya kuwabwaga warembo wenzake katika shindano la kumsaka mlimbwende wa  Chuo Kikuu cha Kampala International University(KIU) tawi la Dar es Salaam.
Warembo waliofanikiwa kuingia tatu bora ni Judith Sangu ndiye mshindi(katikati),Martha Kamanyola mshindi wa pili (kulia) na Asha Mohamed mshindi wa tatu(kushoto).