Wednesday, November 30, 2011

DROGBA AKATAA KUSAINI MKATABA MPYA NA CHELSEA - KUONDOKA MWISHONI MWA MSIMU




Didier Drogba yupo tayari kuondoka Chelsea baada ya kukataa kusaini mkataba mpya.

mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33, yupo katika siku za mwisho mwisho za mkataba wake unaomuingizia £120,000 kwa wiki na amekataa nyongeza ya miezi 12 katika mkataba wake.

Sasa anajiandaa kuondoka Stamford Bridge akiwa huru kipindi kijacho cha kiangazi kuelekea Russia au Qatar.

Agent wa Drogba Thierno Seydi, alisema jana usiku: “Didier alipewa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja na Chelsea. Lakini ameona haumfai.

“Tunajua nini tunataka, wapi tunataka kwenda na kwa ofa ya namna gani. AC Milan walikuja na dili la mkopo kwa Didier wakiwa na option ya kumnunua pia, lakini niliwaambia haiwezekani. Ofa yao haikutuvutia.

“Kwa umri huu wa Didier, hana kipya cha ku-prove kama mchezaji. Ataenda mahala ambapo watatoa mkwanja mrefu zaidi. Inaweza kuwa Marekani , Russia, Qatar au popote in Asia.

“Unapokuwa tayari katika umri wa miaka ya 30 unatakiwa uende katika timu ambayo una uhakika utapata pesa ya kuweza kukuwezesha kuishi vizuri. LA Galaxy ni moja ya timu ambazo Drogba anaweza kujiunga nazo. Pia Anzhi, wanalipa vizuri lakini sio mimi wala Didier tumepokea ofa kutoka kwa timu hizo.”

Drogba alisajiliwa na Jose Mourinho kutoka Marseille kwa ada ya £24million in 2004 na amefunga magoli 146 katika kipindi cha miaka 7 aliyokaa Chelsea.

Habari za Drogba kutaka kuondoka zimekuja siku chache baada ya mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Marcel Desailly kusema kwamba klabu hiyo sasa imegawanyika chini ya Andre Villas Boas, timu haina umoja.

No comments:

Post a Comment