Sunday, November 13, 2011

JAGUAR AWASILI TZ…TAYARI KWA BODA KWA BODA BEACH CONCERT @ MBALAMWEZI…!!


Mwanamuziki mahiri nchini Kenya ajulikanae kwa jina la Jaguar, awasili nchini Tanzania tayari kwa kuangusha bonge la shoo kwenye tamasha la Boda kwa Boda Beach Concert.

Kuzungumzia na uthibitisho wa ujio wa Mwanamuziki huyo Dar, Meneja wa Masoko wa kampuni ya
G5 Click Company, Desy Ernest amesema kuwa,Mwanamuziki Jaguar kutoka nchini Kenya anatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la Boda kwa Boda Beach Concert litalojiri pande za Mbalamwezi Beach Club, Mikocheni jijini Dar Es Salaam mnamo November 12 (LEO) majira ya saa moja jioni. Akisindikizwa jukwani na wasanii wakibongo wakiwemo Sumalee, GodZilla, Country Boy & Stamina,Young D,Beka na wengineo wengi tu.



Desy Ernest
amesema kuwa mpaka sasa mambo yanakwenda sawa bin sawia,na kwamba shamra shamra za Boda kwa Boda Beach Concert zitakuwa tofauti na wenye msisimko mkubwa, ambalo ni kubwa katika anga ya burudani ndani ya Tanzania. Jaguar awasii mashabiki wake kujitokeza kwa wingi ilikukamilisha mpango mzima wa Boda kwa Boda Beach Concert.

No comments:

Post a Comment