Friday, December 7, 2012

UNIQUE MODELS NDO HABARI YA MJINI DESEMBA HII

 

Washiriki wa shindano la unique model wakiwa katika hali ya kujifua catwalk ikiwa ni maandalizi ya fainali za shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwezi huu.
Washiriki Zenaath Unique na Sandra Unique katika mtanange wa miondoko ya kimaonyesho,hapa ni sehemu ya uwazi katika Hotel ya Giraffe ocean view,hotel bora na huduma za ukarimu.
 

UZINDUZI WA MBIO ZA UHURU MARATHON




Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akiwasili katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont, Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam tayari kwa kuendesha hafla hiyo ya Uzinduzi.akizindua rasmi tovuti ya Mbio hizo ya http://www.uhurumarathon.com pamoja nae ni Mkurugenzi wa Intelecture Communication Ltd, Waandaaji wa Mbio hizo, Innocent Meleck.
Msanii Maarufu wa Nyimbo za Mashaili hapa nchini,Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba akionyesha umahiri wake wa Mashairi yake yenye ujumbe mzito wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) ambazo zitakuwa zikifanyika kila Mwaka.hafla hii imefanyika katika Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon), Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akimtunza Mjomba Mrisho Mpoto wakati akiimba nyimbo zake za Mashairi yenye Ujumbe Mzito kwa Taifa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam
Muongozaji wa Hafla hiyo usiku huu, alikuwa ni MC Ephrahim Kibonde.
Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akisoma hotuba yake wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) ambazo zitakuwa zikifanyika kila Mwaka.hafla hii imefanyika katika Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akisoma hotuba yake aliyoiandaa wakati wa Uzinduzi wa Uhuru Marathon uliofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) uliofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam
Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akitoa ufafanuzi wa mdogo wa nembo na kauli mbiu zitakazo tumika kwenye Mbio hizo kwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara.
Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akimuelezea Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara juu ya Tovuti ya mbio hizo ambayo ni http:// www.uhurumarathon.com muda mfupi baada ya kuzinduliwa.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akikabidhiwa fulama Maalum yenye jina la Rais Jakaya Kikwete.
Mratibu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akifafanua jambo kwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara.
 
Wadau mbali mbali kutoka makampuni tofauti tofauti hapa nchini pia walikuwepo kwenye uzinduzi huo.
Mjomba Band ikifanya vitu vyake.
Wanahabari.
Wadau kibao walikuwepo kwenye uzinduzi huo.

BARABARA YA DAR LINDI KUKAMILIKA JUNI MWAKANI


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

 
 
 
 
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Barabara ya Dar-Lindi kukamilika Juni mwakani

                   Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameambiwa juzi, Jumatano, Desemba 5, 2012, kuwa ujenzi wa Barabara ya Dar es Salaam-Lindi utakamilika katika miezi sita ijayo kuanzia sasa.

                   Rais Kikwete alipewa maelezo hayo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Mhandisi Gerson Hosea Malangalila Lwenge wakati aliposimama kukagua maendeleo ya ujenzi kwa akiwango cha lami wa kilomita 56 kati ya  Nyamwage, Mkoa wa Pwani na Somanga, Mkoa wa Lindi.

                   Rais Kikwete alisimama kukagua ujenzi wa Barabara hiyo wakati akirejea Dar es Salaam kutoka Lindi ambako alifanya ziara yenye mafanikio makubwa ya siku tatu kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi.

                   Akipewa maelezo ya ujenzi wa Barabara hiyo kwenye eneo la Somanga, Rais Kikwete aliambiwa kuwa kati ya kilomita hizo 56 tayari kilomita 30 zimeshatiwa lami. Barabara hiyo inajengwa na Kampuni ya MS Karafi.

                   Naibu Waziri huyo alimwambia Rais Kikwete: “Mjenzi anajenga kiasi cha mita 250 kila siku na kama hapakuwepo na kuharibika kwa lolote ama mvua isipokuwa nyingi kupita kiasi, basi ujenzi wa Barabara hii utakuwa umekamilika katika miezi sita ijayo kuanzia sasa.”

                   Naibu Waziri alimwambia Rais Kikwete kuwa ni kweli ulikuwepo ucheleweshaji kwa upande wa mjenzi, lakini sasa maendeleo ni mazuri. Barabara hiyo ilipangwa kukamilika Juni, mwaka jana, 2011.

                   “Kwa jumla ujenzi wa Barabara nzima umekamilika kwa asilimia 78, njia ya awali ambako lami itawekwa imekamilika kwa asilimia 98, madaraja madogo kiasi cha 55 tayari yamejengwa na vifaa vyote ikiwa ni pamoja na kokoto viko kwenye eneo la ujenzi.”

                   Barabara ya Dar es Salaam-Lindi ina urefu wa jumla ya kilomita 452 na kukamilika kwa kipande cha Nyamwage-Somanga una maana kuwa mtu yoyote anaweza kusafiri kwa lami tupu kutoka Mtwara hadi Kagera ama Mwanza ama Arusha ama Tunduma.

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

07 Desemba, 2012