Saturday, August 30, 2014

MWALIM WA VODACOM AWANIA UONGOZI CHADEMA ZANZIBAR


Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Zanzibar Bi Maryam Ahmed Omar akimkabidhi fomu Salum Mwalim fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho kundi la Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika ofisi Kuu za Chadema kisiwani humo. .
*******
Na Martin Kabemba, Zanzibar
Mmoja wa maafisa wa Kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacoma na mwanahabari, Salum Mwalim ameomba kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia nafasi za Zanzibar,

Uamuzi huo wa Mwalim ambae kwa sasa ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom tayari umeibua mjadala Zanzibar na kwamba unatarajiwa kubadili upepo wa uchaguzi wa Chadema Visiwani humo kutokana na ushawishi na mvuto alionao utakaomfanya kukubalika na kuaminika huku akifanya joto la uchaguzi kupanda.

Kwa sasa joto la uchaguzi ndani ya Chadema linaonekana kuwa juu zaidi Tanzania Bara.
Akichukua fomu ya kuomba kugombea kuingia kwenye chombo hicho kikuu cha maamuzi ndani ya Chadema, Mwalim amesema baada ya kushawishiwa na watu wa rika na wa aina mbalimbali kushauriana na makundi mbalimbali amejipima na kuona kuwa anatosha katika nafasi hiyo.

Mwalim amesema wakati wote wa maisha yake amekuwa akitembea na uzanzibari wake na kwamba alitambua kuwa siku moja atakuja kuwatumikia wazanzibar na hivyo kutoa mchango wake katika maendeleo ya visiwa hivyo ambako ndiko asili yake ilipo.

Mwalim amechukulia fomu hiyo mapema leo (Jumamosi Agosti 30) katika ofisi kuu za Chadema Zanzibar na kuirudisha majira ya mchana ikiwa leo ndio siku ya mwisho ya uchukuaji wa fomu na urejeshaji kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho,

"Nimechukua fomu na sasa nairudisha, kwa kuwa wakati wa kampeni bado sitoweza kuzungumza wala kujinadi naomba niheshimu taratibu na miongozo ya uchaguzi ya chama lakini nataka kuwaambia kuwa Zanzibar na U-zanzibari wangu ni jambo ninalojivunia kuliko kitu kingine chochote maishani mwangu."Alisema Mwalim 

"Ni uamuzi mgumu sana kuwahi kufanya katika maisha yangu lakini nimeufanya kwa kuzingatia masilahi mapana ya chama ninachokiamini na kwa nchi yangu ya Zanzibar na watanzania kwa ujumla,ninamuomba Mwenyezi Mungu anisimamie anipe nguvu,afya,hekima,busara, unyenyekevu na uadilifu katika safari hii ya siasa ninayoianza." Aliongeza Mwalim

Akiongea kwa kujiamini na kwa umakini mkubwa, amesema ana imani kubwa kuwa ataungwa mkono na kushinda nafasi hiyo kwa kuwa pande zote mbili za Visiwani na Bara wanamfahamu vizuri sana na wanatambua mchango wake kwa Chadema na kwa nchi kwa ujumla.

Mwalim ambae ni msomi wa masuala ya uandishi wa habari na mwenye shahada ya uzamii katika usimamizi wa Biashara ni mmoja wa vijana waliotokea kujizolea umashuhuri mkubwa nchini kutoka na uwezo wake na uchapaji kazi wake akiwa mtu mwenye misimamo na kukubalika hasa na vijana nchini.

Kamati kuu ya Chadema ndicho chombo kikuu cha maamuzi ndani ya Chama hicho, na iwapo Mwalim atafanikiwa kushinda na kuingia kwenye chombo hicho anatabiriwa kuwa atabadili upepo wa Chadema katika siasa za Zanzibar kutokana na Mwanahabari huyo kukubalika katika jamii na upya wake katika siasa unamfanya kuingia katika siasa pasi na kuwa na makundi hali itakayomwezesha kupewa ushirikiano na kila mtu ndani na nje ya Zanzibar.
Akimkabidhi fomu hiyo Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar wa Baraza la Wazee La Chadema Bi Maryam Ahmed Omar amempongeza Mwalim kwa uamuzi wake huo na kumtakia kila la kheri katika uchaguzi huo.

Bi Omar amesema Chadema ya sasa imeimarika kwa kiwango cha juu na kwamba uamuzi wa Mwalim ambae ni kijana mzaliwa wa visiwani humo wa kuamua kugombea nafasi hiyo utasaidia kuongeza nguvu ya kukiimarisha chama.

Tukio la uchukuaji wa Fomu wa Mwalim limehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Jumbe, mbunge wa wa viti maalum wa chama hicho Mwanamrisho Abama miongoni mwa viongozi na makada mbalimbali wa chama hicho

TBL YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA FYFES WHISKY JIJINI ARUSHA

 

100_8877
Meneja Masoko wa TBL Tanzania Bw.Joseph Chebehe akizindua kinywaji kipya cha FYFES WHISKY katika hotel ya Mt.Meru jijini ArushaMeneja wa Brand ya Tanzania Distilleries Limited kampuni tanzu ya Tanzania Breweries Limited ambayo ni sehemu ya kampuni mama ya SABMiller Group Bi.Martha Bangu akiwakaribisha wageni wageni katika uzinduzi wa FYES WHISKY
100_8900
Muonekano wa FYFES WHISKY
100_8878
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa FYFES WHISKY katika hotel ya Mt.Meru jijini Arusha
100_8880 100_8883
Katikati ni Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Ivestment Goodluck Kway na wadau wengine wakifatilia kwa ukaribu uzinduzi wa kinywaji kipya cha FYFES WHISKY katika hotel ya Mt.Meru jijini Arusha
100_8893
100_8894
 100_8902
Kulia ni Mtangazaji wa Redio 5 Arusha Ashura Mohamed naye alihudhuria uzinduzi huo
100_8905
Kushoto ni Mtangazaji maarufu wa choice fm ya jijini Dar es saalam Jimmy Kabwe ndiye aliyekuwa mshereheshaji wa uzinduzi wa kinywaji cha FYFES WHISKY katika hotel ya Mt.Meru Arusha
100_8907
100_8910
100_8917
100_8919
100_8921
Mkurugenzi wa Mwandago Investment kushoto Bw Mwandago akifurahia jambo ndani ya uzinduzi huo
100_8924
100_8929
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) imezindua kwa mara ya kwanza kinywaji ambacho kinatokana na malighafi halisi ya Whisky ya Scotch kutoka katika vilima vya Uscotchi huko Scotland ambayo itasambazwa nchini Tanzania na Tanzania Distilleries Limited ijulikanayo kwa jina la FYFES WHISKY
Akizindua rasmi uzinduzi huo katika hotel ya Mt.Meru jijini Arusha Meneja Masoko wa TBL Tanzania Bw.Joseph Chebehe alisema kuwa  pamoja na kuwapa watanzania vinywaji mbalimbali vile vile itaongeza ajira na fursa ya watanzania kujiajiri kupitia bidhaa zao(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

NI WAKATI WA JAPAN KUHAMIA AFRIKA – PINDA


PG4A3943 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Hirotaka Ishihara baada ya kukutana naye Ofisini kwake jijini Dar es salaam August 30, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 ………………………………………………..
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema umefika wakati wa Japan kuhamia barani Afrika na na kuwekeza kwa nguvu hasa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumamosi, Agosti 30, 2014) wakati alipokutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Bw. Hirotaka Ishihara na wafanyabiashara kutoka Japan kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu. Bw. Ishihara anaongoza ujumbe wa wafanyabiashara 70 kutoka makampuni makubwa 14 ya Japan.
Akizungumza na Bw. Ishihara na baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo, Waziri Mkuu alisema ni ukweli usiopingika kwamba Japan ni nchi yenye uchumi imara na kwamba licha ya kuwepo kwa mikutano ya TICAD ambayo hutoa fursa kwa Japan kushirikiana na nchi za kiafrika, bado kuna haja ya wao kuelekeza macho yao Afrika kipekee.
“Mikutano ya TICAD imekuwa ikifanyika kwa zaidi ya miaka 20 sasa lakini nchi za Afrika na hasa Afrika Mashariki tumefumba macho… tumeshindwa kutumia kwa kiasi kikubwa fursa zilizopo na kuchota utaalamu wa kiteknolojia kutoka Japan,” alisema.
Waziri Mkuu alisema Afrika Mashariki ni soko la uhakika kwa mtu yeyote anayetaka kuwekeza barani Afrika. “Kama nchi wanachama wa Jumuiya siyo soko la kutisha, lakini kutokana na mahali nchi zetu zilipo, tuna fursa kubwa ya kufungua milango ya soko kwa nchi zote jirani zinazotuzunguka na hiyo ni fursa kubwa kwa mwekezaji yoyote,” alisisitiza.
Kuhusu uwekezaji, Waziri Mkuu alisema Japan inaweza kuwekeza kwenye viwanda vya nguo na kusokota nyuzi, kuna fursa kwenye viwanda vya kusindika samaki kwani kuna aina nyingi za samaki waliopo katika bahari ya Hindi. Pia alisema amefarijika kusikia kwamba wameonana na wahusika kutoka Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan ambaye ndiye kiongozi wa msafara huo alimweleza Waziri Mkuu kuridhishwa kwake na mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili na kwamba katika kipindi cha miaka miwili kumekuwa na ongezeko la ziara za viongozi baina ya nchi hizi mbili.
“Nina furaha kuzuru Tanzania kwa mara ya pili nikiongoza Kamati ya Pamoja ya Umma na Sekta Binafsi ya Kukuza Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania… tumevutiwa na kasi ya ukuaji uchumi wa Tanzania, ndiyo maana makampuni ya Kijapani yameonyesha nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania,” alisema Bw. Ishihara.
Bw. Ishihara na msafara wake wamemaliza ziara yao ya siku ya tatu hapa nchini na wanaondoka Tanzania kurejea Japan leo jioni.

COASTAL UNION YASHUSHA MSHAMBULIAJI MPYA KUTOKA GORMAHIA YA KENYA

         
???????????????????????????????
Mshambuliaji mpya wa Coastal Union kutoka Gormahia
ya Kenya Itubu Imbem Guelor akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia
timu hiyo kwenye makao makuu ya klabu hiyo barabara kumi na moja jijini
Tanga kulia ni Meneja wa timu ya Coastal Union akida Machai na kushoto ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Salim Bawaziri  jana,Picha na ,Tanga. ???????????????????????????????
kulia ni Meneja wa Klabu ya Coastal Union Akida Machai
akimuonyesha kitu kwenye simu ya mkononi, Mshambuliaji Mpya wa timu hiyo
aliyesajiliwa kutoka Gormahia ya Kenya ,Itubu Imbem Guelor aliyesaini
mkataba wa kuichezea kwa kipindi cha miaka miwili,Picha na,Tanga.
…………………………………………………………………
UONGOZI wa Coastal Union umeonyesha nia ya kusaka ubingwa wa Ligi kuu soka
Tanzania bara kwa vitendo kwa kufanya usajili wa nguvu baada ya kumpa
mkataba wa miaka miwili aliyekuwa mshambuliaji wa Gormahia ya Kenya Itubu
Imbem Guelor .
Utiliaji wa Saini hiyo ulifanyika jana makao makuu ya Klabu hiyo mbele ya
Meneja wa Coastal Union Akida Machai na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili
Salim Bawaziri
Itubu ambaye pia aliwahi kuzichezea timu za FC Leopard ya Kenya,na Tusker
amehaidi kuipa mafanikio timu hiyo ambayo imedhamiria kurudisha histori
yake ya miaka 1988 waliochukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania.
Mchezaji huyo anakuwa  ni wa pili kutoka timu hiyo kusajiliwa na Coastal
Union ambapo kwanza aliyesajiliwa ni Rama Salum ambaye aliingia mkataba wa
kuichezea timu hiyo hivi karibu na tayari yupo visiwani Pemba kwa ajili ya
maandalizi ya msimu mpya wa Ligi kuu .
Akizungumza kabla ya kupanda ndege kuelelekea visiwani Pemba ambapo timu ya
Coastal Union imeweka kambi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi kuu soka
Tanzania bara,Itubu alisema amefurahishwa sana kusajiliwa na timu hiyo na
kuwahaidi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwa watafanya kila
liwezekanalo kuweza kunyakua ubingwa wa ligi hiyo.
Mshambuliaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Kongo Kinshasa alisema malengo yake
makubwa ni kuhakikisha anashirikiana na wachezaji wenzake katika kuipa
mafanikio timu hiyo.
“Kimsingi mimi mwenyewe binafsi nimefurahi sana kuja kuicheza Coastal Union
kwa sababu ni timu yenye historia kubwa ya soka hapa nchini hivyo naahaidia
kushirikiana na wachezaji wenzangu ili kutimiza ndoto walizojiweka za kuwa
mabingwa wapya Ligi kuu msimu ujao “Alisema Itubu.
Kwa upande wake, Meneja wa Coastal Union Akida Machai alisema kuwa usajili
huo ni ishara tosha ya kuwa timu hiyo itakuwa tishio kwenye michuano ya
ligi kuu Tanzania bara msimu ujao kwa kuweza kutimiza malengo yao ya muda
mrefu ya kunyakua bingwa wa Ligi kuu.

Kivumbi Miss Lake Zone kutimka CCM Kirumba leo

 Kivumbi Miss Lake Zone kutimka CCM Kirumba leoSHINDANO la Miss Lake Zone 2014, leo linakwenda kufikia tamati katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa kwa warembo 18 kujimwaga jukwaani kuwania taji la kinyang’anyiro hicho kilichovuta hisia za wengi.

Warembo hao waliokuwa wamepiga kambi ya siku 10 katika Lenny Hotel ya Mkoani Geita, leo watachuana kuwania taji linaloshikiliwa na Ruth Charles.

Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo, Flora Lauwo, warembo wote wapi vizuri wakiwa wamepikwa vizuri na kilichobaki ni muda tu.

“Nashukuru kila mrembo amejifunza na kuona mengi kwa kipindi chote cha kambi, hivyo ni jukumu lake kufanyia kazi yote alitojifunza,” alisema Flora.

Kuhusu ushindani, alisema ni maratajio yake kuwa utakuwa mkubwa kutokana na uwezo wa kila mshiriki ambaye atakuwa akitaka kubeba taji kutwaa zawadi ya gari yenye thamani y ash mil 10.
Alikiri kuwa zwadi hiyo iliyotolewa na mmoja wa wadhamini wa shindano hilo, Lenny Hotel chini ya Mkurugenzi wake Leonard Bugomola ambaye leo ni mgeni rasmi, imeongeza ushindani.

Warembo watakaopanda jukwaani na mikoa yao kwenye mabano ni Moshy Shaban; Doreen Robert; Christina Jilulu (Mwanza); Nikole Sarakikya, Mary Emanuel na Rachael Julika (Shinyanga).
Wengine ni Faudhia Haruna, Jackline Kimambo na Christina John (Kagera), huku Nyangi Warioba; Cecilia Kibada na Everlyn Charles (Simiyu). Wamo pia Martina John; Elinaja Nnko, Winfrida Nashon (Mara)huku Rose Msuya, Rachael Clavery na Faridha Ramadhani wakiwakilisha mkoa wa Geita.

Wakiwa kambini wilayani Geita, warembo hao walifanya shughuli za kijamii ikiwemo kutoa msaada kituo cha Yatima cha Moyo wa Huruma na kutembelea mgodi wa GGM na Hospitali ya Geita na Hifadhi ya Lubondo na kufanya usafi.

Kwa upande wa zawadi, Flora alisema mshindi wa kwanza atazawadiwa gari ya shilingi mil 10; mshindi wa pili ataondoka na bajaji yenye thamani ya sh. mil 4 huku mshindi wa tatu atapata pikipiki y ash mil 1.8.

Mratibu huyo ametoa pongezi kwa wadhamini wakuu, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Redd’s, Lenny Hotel, Crown Paint, Shule ya Rishor Pre & Primary English Medium na Benki ya CRDB ya Geita.

Flora ambaye ni mara ya tatu kuandaa shindano hilo la Kanda ya Ziwa, amewahi kutoa mara mbili mshindi wa Miss Tanzania (2008 na 2009), Nasrim Karim na Miriam Gerrard. Kwa upande wa kiingilio, Flora alisema viti maalum ni shilingi 30,000; viti vya jukwaa kuu ni sh 10,000 na viti vya kawaida ni sh 5,000.

Manji amgeuzia kibao Okwi

 

  • Aipa TFF siku 7, apanga kwenda FIFA, CAS
  • Asema kama jeuri ni fedha, Simba haiwezi

Manji amgeuzia kibao OkwiSAKATA la Mshambuliaji wa Kimataifa Emmanuel Okwi kuikacha timu yake ya Yanga aliyojifunga nayo mkataba wa miaka miwili na kurejea Simba, limechukua sura mpya baada ya Yanga kumtaka awalipe fidia ya dola 500,000 za Marekani.
Yanga chini ya Mwenyekiti wake Yusuf Manji, imetaka kulipwa kiasi hicho kutokana na kitendo chake nyota huyo kuibukia Simba wakati akiwa na makata wa kuicheza Jangwani alikotua kwa kishindo msimu uliopita akitokea Sports Club Villa ya Uganda.

Nje ya hilo, wameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais wake Jamal Malinzi, litoe uamuzi juu ya sakata la mchezaji huyo ndani ya siku saba kabla ya wao hawajaamua vinginevyo.
Juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharia Hanspope, ilimtangaza Okwi kurejea Simba baada ya nyota huyo kuuomba uongozi wa Simba afanye hivyo kutokana na Yanga kumpa barua ya kuvunja naye mkataba.

Wakati Okwi akijinadi hivyo mbele ya waaandishi wa habari katika mkutano huo wa juzi, Yanga wamekanusha wakisema hakuna kitu kama hicho kwa sababu nyota huyo bado ana mkataba wao.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji alisema jana mbele ya waandishi wa habari kuwa, hadi kufikia juzi asubuhi, Okwi alitakiwa awalipe wao (Yanga) fidia ya dola 200,000 za Marekani sawa na sh mil 300.

Manji aliongeza kuwa, kwa kitendo cha mchezaji huyo kujitangaza mbele ya vyombo vya habari kwamba ameondoka Yanga na yu tayari kujiunga na Simba, fidia yake kwa Yanga imeongezeka hadi kufukia kiasi cha dola hizo 500,000.

Kiongozi huyo alisema, kwa vile mchezaji huyo wa kimataifa anafanya hivyo akitambua kuwa yumo katika mkataba halali na Yanga, kadri siku zinavyoendelea baada ya juzi, fidia hiyo inaweza kuzidi kupanda.

Hata hivyo, Manji alihoji ukimya wa TFF juu ya vitendo vya ukiukwaji wa mkataba vinavyofanywa na mchezaji huyo kwani tayari walishawasilisha barua kwa Shirikisho hilo ikiwemo kutoroka, kufungiwa na kuingarimu Yanga katika mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.
Manji alisema kwa mazingira hayo, waliandika barua TFF kuomba mwongozo, lakini mpaka sasa hawajapata majibu, hivyo jana waliamua kuwasilisha barua nyingine ya malalamiko kutokana na nyota huyo kutimkia Simba.

Manji alisema ndio maana wameamua kuwapa TFF siku saba kutoa majibu juu ya mchezaji huyo, vinginevyo watalazimika kupeleka suala hilo katika ngazi za juu kwa maana ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na ikiwezekana Mahakama ya Usuluhishi wa Masuala ya Michezo (Cas).
Alisema katika barua waliyowasilisha TFF tangu jana, wamelitaka shirikisho hilo kuishusha daraja klabu ya Simba na kumfungia Okwi kujihusisha na masuala ya soka katika maisha yake ili kuwa funzo kwa wengine.

“Mimi sina kinyongo wala tatizo na Simba, lakini naona wao wanafanya fujo sasa, mimi ninachotaka tushindane uwanjani na tunaiomba TFF itende haki katika hili. Simba wakishuka Daraja wasije wakanilaumu kabisa,” alisema Manji.

Manji alikwenda mbali zaidi na kusema tatizo haliko kwao wanachama moja kwa moja, bali ni kuchagua watu wasio wa michezo bali wapenda sifa sizizo na tija kwa maendeleo ya mchezo wenyewe.

Aliongeza kuwa, kama hoja ni jeuri ya fedha, Yanga chini ya uongozi wake hawashindwi kufanya lolote ikiwezekana kumhamisha Amisi Tambwe na Kocha Mkuu Mzambia Patrick Phiri, lakini hawaoni mantiki ya kufanya hivyo ikiwemo kuheshimu kanuni na sheria za mchezo huo.
“Mimi nawashangaa wenzetu (Simba), wao kila mwanamke anayepita wanaona anafaa kuoa, kama ni jeuri ya fedha, mimi sishindwi.

Ninao uwezo wa kuchukua timu nzima ya Simba na kuwalipa mshahara bila hata kucheza soka wakiishia kufanya mazoezi tu katika ufukwe wa Coco,” alisema.

Chanzo Tanzania Daima

Friday, August 29, 2014

AFRIKA INACHANGIA ASILIMIA 3 TU YA HEWA CHAFU DUNIANI – WAZIRI MKUU


PG4A3658
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema tatizo la mabadilko ya tabianchi ni kubwa sana na kama hazitachukuliwa hatua stahiki Dunia itaisha.
Ametoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Agosti 29, 2014) wakati akifungua mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mazingira ambao ni wajumbe wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Barani Afrikainayosimamia Mabadiliko ya Tabianchi (Committee of African Heads of States and Governments on Climate Change-CAHOSCC) wanaokutana kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Alisema tatizola mabadiliko ya tabianchi linachangiwa kwa kiasi kikubwa na hewa chafu ambayo inazalishwa viwandani kutokana na matumizi makubwaya nishati.
“Kuna vyanzo vya nishati ambavyo si rafiki na kimojawapo ni makaa ya mawe. Ili uweze kupata nishati yakeni lazima uyaunguze nakwa kufanya hivyo unatoa hewa ukaa nyingi sana. Viko viwanda vinatumia mafuta mazito, vinginedizeli kwa wingi sana. Yote haya yanachangia hewa chafuambayo inafanya utando unaozuia hewa ya joto kurudi kwenye mfumo wa sayari na kutumika tena,”alisema.
Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari,  Waziri Mkuu alisema kiwango kikubwa cha hewa chafu inayozalishwa viwandani kutokanana matumizi ya nishati kinatoka nchi zilizoendelea wakati Bara la Afrika linazalisha asilimia tatu tu ya hewa hiyo.
“Sisi Afrika tunapaswa tusifiwekwa kupunguza kasi ya ongezeko la jotoduniani.Nchi tajiri zinapaswa kutupongeza kwa sababu bado tuna misitu ambayo inasaidia kunyonya hiyo hewa chafu,”aliongeza.
Waziri Mkuu alisema mkutano huo ni muhimu kwa sababu unaandaa kauli kwa ajili ya Wakuu wa Nchi watakayokwenda kuiwasilisha kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Kujadili masuala ya Tabianchi utakaofanyika New York, Marekani mwezi ujao.
“Ninatumaini Mawaziri wote watatoka na kauli moja itayowawezesha Wakuu wa Nchi zetu waende na kauli moja. Natumaini watafanikiwa,”alisisitiza Waziri Mkuu.
Akizungumza na washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Algeria,  Jamhuri ya Congo,  Misri, Kenya, Uganda,  Sudan,  Msumbiji, Ethiopia,  Ghana, Mauritania na wenyeji Tanzania,  Waziri Mkuu alisema suala la mabadiliko ya tabianchi yanaziathiri nchi zote duniani bila kujali kipato, umri, mahali nchi ilipo, matabakawala kazi za wananchi.
“Nchi za Afrika ambazo kazi za uchumi wa wananchi wake zinategemea zaidi hali ya hewa, ndizo zinaathirika maradufu zikichangiwa zaidi na kukosekana kwa mbinu za kujihami pamoja na misingi dhaifu ya kiuchumi,”alisema.
Alisema taarifa za hivi karibuni kutoka Intergovernmental Panel on ClimateChange zinaonyesha kwamba kiwango cha utoaji wa hewa chafu kila mwaka kimeongezeka kwa asilimia 2.2huku hewa chafu kutoka viwandani ikiongoza kwa kuchangia asilimia 80 ya hewa hiyo kwenye nchi zilizoendelea.
Mapema, Kamishna wa Umoja wa Afrika anayesimamia Kilimo na Uchumi wa Vijijini, Bibi Rhoda Tumusiime alisema bara la Afrika linapaswa lijipange vizuri na kutoa matamko mazito kwenye mikutano ya kimataifa ili kukemea matumizi matumkzi makubwa ya nishati yanayochangia uharibifu wa mazingira.
“Afrika lazima iendelee kutetea nafasi yake kwenye mikutano hii mikubwa. Lazima itoa kauli nzito kwani kuharibiwa kwa mazingira kunaathiri pia sektanyingine za utalii, maji, nishati na kadhalika,”alisema.

RAIS KIKWETE AZINDUA NYUMBA ZA NHC KONGWA DODOMA

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Abdulkarim Shah.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia jiwe la msingi mara baada ya kufungua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44.
Wageni waliokuwapo katika hafla hiyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoka ndani ya nyumba ya mfano baada ya kufungua nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa. 

HALMASHAURI nchini zimetakiwa kununua nyumba za bei nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba (NHC) ili kuwapangisha watumishi wake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua mradi wa nyumba nafuu katika eneo la Mnyakongo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya maeneo watumishi wa halmashauri kukaa mbali na sehemu zao za kazi kwa visingizio vya kukosa makazi.

Alisema sababu hiyo sasa haina msingi katika maeneo ambayo NHC imejenga nyumba zao kwani halmashauri inaweza kununua nyumba hizo na kuwapangisha watumishi wake.

‘’ Hawa NHC wana utaratibu kwa kupitia mabenki wanayoshirikana nayo hivyo kwa kutumia utaratibu huo halmashuri mnaweza kwenda katika hizo benki na kuingia mkataba na kukopa nyumba hizo na kisa kuwapangisha watumishi…’’ alisema.

Aidha Rais Kikwete alisema shirika hilo linafanya kazi nzuri katika ujenzi wa nyumba hizo za bei nafuu huku akilitaka kuongeza zaidi idadi ya nyumba. Alisema ni vyema sasa halmashuri zikaongeza maeneo ya kujenga nyumba hizo ili wananchi wengi zaidi waweze kuishi katika nyumba bora.

Akizungumza katika ufunguzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa NHC Nehemia Mchechu alisema mradi huo ni utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Alisema mradi huo wenye nyumba 44 hadi kukamilika utakuwa umegharimu Shilingi bilioni 1.2.

Alisema nyumba hizo zinauzwa kwa gharama kati ya Sh milioni 35 hadi 40 kulingana na ukubwa wa nyumba husika.

Hata hivyo alisema bado kuna tatizo la kodi katika uuzaji wa nyumba hizo na ndio kinachofanya kuuzwa kwa bei kubwa.

Alimuomba Rais kusaidia katika kusukuma nia ya kushusha kodi ili nyumba hizo ziuzwe kwa bei nafuu na kila mwananchi aweze kununua.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA SOKO LA NAFAKA LA KIMATAIFA LA KIBAIGWA, DODOMA

         

kb3 kb4
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea soko la nafaka la kimataifa la Kibaigwa mkoani Dodoma katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo Agosti 28, 2014 , ambapo alijionea shehena kubwa sana ya mahindi iliyoletwa kutoka mashambani na kusafirishwa kila pembe ya nchi. Mwaka huu, kama ilivyokuwa mwaka jana, mavuno ya mahindi yamekuwa makubwa kiasi hata cha kupatikana kwa mavuno ya ziada yanayolemea maghala yaliyopo, ikiwa ni muendelezo wa mafanikio ya sera ya kilimo kwanza ambayo imekuwa ikileta matokeo mazuri kila mwaka.
 
 kb5
 
PICHA NA IKULU
 kb6

PINDA AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAZINGIRA AFRIKA JIJINI DAR LEO

 

Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda leo amefungua mkutano wa Mawaziri wa Afrika wa Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ambao ufunguzi wake uliongozwa na agenda kuu iliyozungumzia mwongozo wa namna ya kushughulikia changamoto zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabianchi, na ambavyo nchi zaAfrika zitakavyoweza kunufaika na rasilimali zinazotolewa na nchi zinazoendelea ili kukabiliana na jangahilo.

Aidha Waziri mkuu Pinda alielezea kuwa mkutano huo pia una umuhimu kwa nchi za bara la Afrika piautahusisha namna ambavyo serikali za Afrika zinaweza kukabiliana athari zitokanazo na mabadiliko yaTabiachi. Pia alisema kuwa mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa mabadilikoya Tabianchi utakaofanyika mjini Newyork Marekani unaotegemewa kufunguliwa na Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa Bw. Baink Moon.

“Wote tunafahamu kwamba mabadiliko ya Tabianchi yanaathari kubwa kwa dunia nzima ila madharayake yanatofautiana kutokana na mabara, vizazi, umri, nafasi, matabaka pamoja na kipato” Aliongezakuwa kutokana na uchumi tegemezi wa nchi nyingi za Afrika nchi hizo zimekuwa zikiathirika zaidi
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kiwango kidogo cha kuhimili athari zitokanazo na mabadilikoya Tabianchi na kuwa na uchumi mbovu.

Aliendelea kusema kuwa Afrika na Jamii za kimataifa zinatakiwa kuwa na utashi wa kisiasa katikakuungana kwa pamoja ili kuweza kushirikiana katika kupunguza uzalishaji wa gesi joto pia katika kuhimilina kukabiliana na athari hizo.

Mkutano huo wa Mabadiliko ya tabianchi uliofanyika leo jijini Dar-es-salaam umehusisha baadhi yaMawaziri wa Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya nje ambao ni wajumbe wa kamati ya nchi za Afrika yaMabadikliko ya Tabianchi.

FM ACADEMIA KUTUA ARUSHA KWA KISHINDO KUZINDUA ALBAMU YAO MPYA

 

 wasanii wa bendi ya fm Academia wakiwa jukwaani wanaimba wapili kulia ni Rais wa bendi Nyoshi

Rapa wa bendi  ya Fm Academia akiwa anashambulia jukwaa wakati wa shoo
Wanenguaji wa bendi ya Fm wakiwa kazini  wote hawa watakuwepo katika  uzinduzi huu wa Albamu ya Chuki ya nini usikose ni balaa.
*******

Fm  Academia baada ya kukaa kwa muda wa miaka 4 (minne) yaani kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013 sasa wanatarajia kuzindua rasmi  album mpya kabisa inayojulikana kwa jina la Chuki ya nini ndani ya jiji la Arusha na vitongoji vyake .

 Album ya chuki ya nini imebeba nyimbo kumi ndani yake,nazo ni:-Chuki ya nini, Fataki ,Otilia ,Ndoa ya kisasa,Neema,Dai chako ulaumiwe,Maisha,Madudu,Miraessa.album ya chuki ya nini ni album yenye kiwango cha kimataifa ambapo nyimbo hizi zote zitazinduliwa rasmi septemba tano mwaka huu ndani ya viwanja vya  ukumbi wa Triple A jijini Arusha


Akizungumza na waandishi  wa habari jijini hapa mkurugenzi wa SB Intamenti Seif Manyota alisema kuwa bendi hiyo inatarajia kutua jijini Arusha kwa kishindo kwa ajili ya uzinduzi huu wa albamu mpya ambapo alibainisha kua tukio hilo litakuwa la kihistoria.

Alisema kuwa  hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii  kuzindua albamu  nje ya mkoa wa dar es salaam na kwa hivyo wameamua kuwapa heshima kubwa wapenzi wa bendi hiyo wa mkoa wa Arusha  pamoja na mikoa ya kanda ya kaskazini kwa ujumla hii ikiwa ni heshima ya kipekee.

"uzinduzi huu wa  albamu sio tu tunazindua  nyimbo mpya bali tunazindua pia vyombo vipya na staili mpya za kuicheza gwasuma kama vile mnavyojua bendi ya fm  ni wazee wa pamba wazee wa kushambulia jukwaa"alisema Manyota

Aidha alibainisha kuwa kwa mkoa wa Arusha wameamua kuwapa kipaumbele na pia kwakuwa kunawapenzi wengi wa ngwasuma wameamua kufanya shoo hii nje ambapo ,kutafugwa jukwaa la kisasa  kabisa.

Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika albamu ambayo inazinduliwa kuwa ni pamoja na Chuki ya nini,ndoa ya kisasa fataki  pamoja na nyinginezo.

Aidha kwa upande  mungine alisema uzinduzi huu autaishia Arusha tu bali wakazi wa Moshi na Tanga nao watapata burudani hii na kuzitambua staili mpya pamoja na nyimbo mpya zilizopo kwenye albamu hii.

Alisema kua pia kutakuwa na CD na DVD za albamu hiyo mpya iliyozinduliwa huku akisema kuwa kwa upande wa Arusha kiingili    akuwa 20000 na unapatiwa CD moja buru mlangoni.

kwa upande wa Rais wa bendi hiyo Nyoshi alisema kuwa timu  yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa Arusha  na kuwapa staili mpya ikiwemo ile ya vundesa  ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha  zaidi  na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu  pamoja na maneno matamu.
Alisema kuwa lengo lao kubwa la kuzindua albaimu hii apa jijini Arusha ni pamoja na kuwaelewesha wapenzi wao nyimbo mpya na kuakikisha wapenzi wao wanajua staili zao zote za  nyimbo hizo na  sio ivyo tu pia alisema kuwa kwa kipindi  hiki wanataka kuwa wakazi wa arusha zawadi ya kuwaletea wasanii wote wa bendi hiyo ambapo alisema wapo 32  na wote watafika jijini Arusha

NYOTA YA ROONEY YAZIDI KUNG'ARA, AWA NAHODHA WA TIMU YAKE YA TAIFA YA UINGEREZA.


Mshambuliajiwa Manchester utd na timu ya taifaya Uingereza, Wayne Rooney ametangazwa rasmi kuwa nahodha wa timu ya taifaya Uingereza kuchukua mikoba iliyo wachwa na Steven Gerrard aliye staafu kuchezea timu hiyo yataifa Julai mwaka huu mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.
Wayne Rooney has been given the England armband
Wayne Mark Rooney.

Rooney mwenye umri wa miaka 28 alitangazwa pia kuwa nahodha wa klabu yake ya Manchester utd mapema mwezi huu, amefanikiwa kuichezea timu yake ya taifa ya England mechi 95 huku akiifungia magoli 40. Uteuzi huo metangazwa na meneja wa timu hiyo Roy Hodgoson.
England inajiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Norway September 3 mwaka huu katika uwanja waWembley kablaya mechiya kufuzu kwa michuano ya mataifa ya ulaya dhidi ya Switzerland September 8 mwakahuu, michuano hiyo ya Ulaya yatafanyika mwaka 2016.

WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA NA MAJERUHI SABA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MBALIZI LEO.Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita 
Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga 
Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo
Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo
Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka 
Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea 
Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo  Haribika Baada ya ajali hiyo
Mashuhuda wakiwa wamelizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea 
 Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea , Askari wa usalama wa barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo
 Ilikuwa ni Ajali mbaya 
 
Mashuhuda 
Baadhi ya Majeruhi wakiwa wanatolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya 
……………………………………………………………..
WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani.
 
Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.
NA MBEYA YETU BLOG

Tuesday, August 26, 2014

DKT. FRANCIS MICHAEL ATOA UFAFANUZI KUHUSU SUALA LA UTUNGAJI WA KATIBA

         

index
Na Magreth Kinabo, Dodoma
26/08/2014.
 
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Namba  Tatu  ya Bunge hilo, Dkt. Francis  Michael  ametoa ufafanuzi kuhusu suala la utungaji wa Katiba ambalo hufanyika kwa mifumo miwili, na kuwataka wananchi wasipotoshwe na mfumo unaotumika.
 
 Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti huyo, ambaye pia ni mtaalam wa sheria  wakati akizungumza katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na  Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
 
Akifafanua kukuhusu mifumo hiyo, amema kuwa kuna mfumo wa kwanza ,ambao hutumia Tume kama ilivyokuwa Tume ya Jaji Joseph Warioba yenye watu  ambayo ilikuwa na kazi  ya kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi na kutengeneza  Rasimu ya Katiba   Mpya , baadaye  Bunge Maalum la Katiba linapitia maoni ya Rasimu hiyo, ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2014 linaweza kubadilisha na kuongeza kwa ajili ya kuiboresha.
 
“Katika  mfumo huu lazima Bunge liwepo kwa ajili ya kuiboresha kabla ya kwenda kupigiwa kura na wananchi,” alisema Dkt. Michael .
 
Dkt. Michael aliutaja mfumo wa pili ni ule wa   kutumia  Tume  Maalum ya Wataalam, ambao wanawajibu wa kuandika Katiba na  hakuna chombo chochote kitakachokuwa na wajibu wa kuibadilisha, bali itakwenda moja kwa moja kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.
 
“Wananchi wasichanganywe na mfumo unaotumika,” alisisitiza Dkt. Michael.
 
Akizungumzia kuhusu uwasilishaji wa nyongeza ya mapendekezo yaliyowasilishwa na makundi mbalimbali hivi karibuni kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta yamepokelewa kwa mujibu wa sheria hiyo, kipengele cha 25 ambapo Bunge hilo lina nguvu kufanya  marekebisho au kuongoza vifungu vingine  pale linapoona inafaa.
 
Aidha, Dkt. Michael amefafanua kuwa  wanatumia nafasi hiyo kisheria na kikanuni, kupokea nyongeza ya mapendekezo hayo kutoka  kwa watu mbalimbali.
 
Akizungumzia kuhusu suala hilo, Mjumbe wa  Kamati hiyo, Mhe, Ridhiwani Kikwete alisema linafanyika kisheria hivyo mtu au kikundi kinaweza kuwasilisha mapendekezo ya nyongeza.
 
Mhe, Ridhiwani alisema nyongeza ya mapendekezo hayo, uwasilishwa kwenye Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo, ambayo nayo hupeleka kwa Kamati 12 za Bunge hilo kwa ajili ya kuratibu mambo ya msingi na kuyachukua .
 
Aliongeza kuwa suala hilo pia linaweza kufanyika wakati wa mjadala wa Bunge hilo,mjumbe anaweza  kulishawishi Bunge hilo, kwa kuwa sheria , kanuni na miongozo inaruhusu