Tuesday, September 30, 2014

KIKWETE KUFUNGUA BARABARA YA MWENGE-TEGETA LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta utakaofanyika leo tarehe 1 Oktoba 2014.

 

Kwa mujibu wa taaria iliyotolewa na kitengo cha Mawasilano serikalini(GCU) cha Wizara ya Ujenzi,ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta wenye urefu wa Kilomita 12.9, utafanyika kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe.

 

Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Sunday, September 28, 2014

JIHAN DIMACHK NDIYE REDD'S MISS TANZANIA TOP MODEL 2014


Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2014, Jihan Dimachk (katikati) akipozi kwa picha na mshindi wa pili Doreen Robert (wapili kulia), mshindi wa tatu Evelyn Baasa ambaye pia ni Miss Tanzania Photogenic 2014 (wapili kushoto), mshindi wa nne, Lilian Timothy (kulia) na Mshindo wa tano Nasreen Abdul, mara baada ya kushinda taji hilo jana ambapo Jihan amekuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2014 baada ya Miss Photogenic. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha na kuwashirikisha warembo 30..Picha/Father Kidevu Blog




 Warembo wakipita jukwaani wakiwa wamevalia nguo za mbunifu Zakia Disign wakati wa shindano hilo.




Washiriki wakipita jukwaani na mavazi maridhawa kutoka Trecy Fashion ya jijini Arusha. 
Jopo la majaji wakiwa katika meza yao tayari kwa kutoa hukumu kwa walicho kiona.
Wadau wa urembo kutoka, Chuo cha Chuo Kikuu Iringa (Tumaini)  na Makumira jijini Arusha wakifuatilia shindano hilo ambapo mwenzao Martha  John alikuwa akitupa karata yake jukwaani.
 Mwana dada Vanesa Mdee na kikosi kazi chake walishambulia jukwaa vilivyo wakati wakisindikiza shindano hilo usiku huu.


Wadau mbalimbali wa sanaa ya urembo na mitindo jijini Arusha wakiwa wamejumuika katika shindanohilo.
 Mbunifu wa mavazi, Zakia akipozi kwa picha.
Mtangazaji wa kipindi cha burudani cha Funika Base kutoka Radio 5 ya Mjini Arusha , Julius Kamafa ndiye alikuwa mshereheshaji katika shindano hilo.

Mwanasheria Machachari wa Jijini Arusha, Albert Msendo (kulia) akiwa na mkali wa Bongo Fleva, Mwana FA wakifuatilia shindano hilo. 

SIRI YA POLISI MORO KUINYAMAZISHA SIMBA SC HII HAPA...


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
NAHODHA wa Polisi Morogoro Nicholas Kabipe amefichua siri ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Simba katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu soka Tanzania bara iliopigwa jana uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Simba walikuwa kwa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza kupitia kwa Emmanuel Okwi, lakini Danny David Mrwanda aliisawazishia Polisi katika dakika ya 50 kipindi cha pili.
Kabla ya mechi ya jana, Polisi walifungwa 3-1 na Azam fc katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa wikiendi ya septamba 20 mwaka huu uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Baada ya mechi ya jana dhidi ya Simba, Kabipe alisema: “Kwa matokeo haya sisi tumefurahi kwasababu tulipoteza mchezo wa kwanza. Kuna makosa yalikuwa yanatugharimu na Azam wakatufunga magoli matatu.
“Tumerekebisha hayo makosa na tumeweza kupata sare. Wakati wa mapumziko tukiwa nyuma kwa goli moja kwa bila, mwalimu alituelekeza kuwa Simba wana kasi sana sehemu ya kiungo”.

“Kwahiyo akasema tunatakiwa tuwe wengi katikati ili tusiwape nafasi ya kucheza, tuwe tunaenda kukaba watu watatu na tulifanya hivyo, ikawezekana na tukaweza kupata sare hiyo”.

Friday, September 26, 2014

SIMBA, YANGA SASA KUMALIZANA OKTOBA 18...NI JAJA AU OKWI?


MECHI ya Simba na Yanga iliyopangwa kuchezwa Oktoba 12 kwenye Uwanja wa Taifa sasa imesogezwa mbele mpaka Oktoba 18 kupisha mechi ya kirafiki ya Taifa Stars na Benin.Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza jana kwamba Stars itacheza Oktoba 12 na leo watatangaza mabadiliko mapya ya ratiba ya Ligi kupisha mechi hiyo ya kalenda ya Fifa na ni rasmi kwamba Simba na Yanga ni wikiendi ya Oktoba 18.
Benin itakuja nchini Oktoba 10 na msafara wa watu 28. Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo kati ya viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu.
Wakati huo huo, kutokana na mechi hiyo ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom inafanyiwa marekebisho madogo, na marekebisho hayo yatatangazwa leo Ijumaa siku ambayo pia Rais wa TFF, Jamal Malinzi atafunga mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Mafunzo hayo ya siku tano yalishirikisha viongozi 34 wakiwemo baadhi ya waandishi wa habari na Meneja wa Twiga Stars, na yaliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau.
Chanzo: Mwanaspoti

EVELYN BAASA NDIYE REDD'S MISS TANZANIA PHOTOGENIC 2014


 
Miss Tanzania Photogenic 2014, Evelyn Baasa.

 Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2014, wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa taji hilo, Evelyn Baasa (katiakti) jana. Wengine kutoka kushoto ni Nicole Sarakikya, Lilian Kamazima, Lilian Timothy na Dorice Mollel.
 Warembo wakilisakata rumba kabla ya kuatangzwa kwa matokeo hayo.
 Baadhi ya warembo wakipiga picha ya pamoja na mshindi huyo wa Taji la Miss Tanzania Photogenic 2014
Father Kidevu Blog, Arusha
Mlimbwende Evelyn Baasa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende wenzake 30 na kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2014.

Kwa kushinda taji hilo Baasa ambaye alinzania mbio za taji la Miss Tanzania katika Kitongoji cha Karatu naabadae kuingia Miss Arusha na Kanda ya Kaskazini amekuwa mrembo wa kwanza kuingia Nusu Fainali ya mashindano Miss Tanzania 2014.

Shindano hilo ni moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya shindano hilo litakalo fanyika mapema mwezi ujao.

Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga 'Uncle' amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha na wadau wa masuala ya urembo  wa masuala ya urembo Tanzania walikaa na kumchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.

Majaji waliowezesha kupatikana kwa mshindi huyo ni Mpigapicha mkongwe wa masuala ya urembo nchini Mroki Mroki ambaye anafanyakazi na Magazeti ya Serikali ya Daily News na Habarileo, Mtayarishaji wa vipindi Elliud Pemba wa True Vision na Afisa Itifaki Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Mukhsin Kassim.
Taji la Redd's Miss Tanzania Photogenic lilikuwa linashikiliwa na Redd’s Miss Tanzania 2013 Happyness Watimanywa.

 
Warembo wengine waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Miss Photogenic ni Dorice Mollel, Nicole Sarakikya, Lilian Timothy na Lilian Kamazima.
 
Kesho warembo hao watachuana tena kuwania taji la Miss Top Model katika shindano litakalofanyika Triple A jijini Arusha.