Monday, October 31, 2011

USIKU WA BAGAMOYO INTERCOLLEGES NIGHT 2011 WAIBAMBA BAGAMOYO

Mwakikishi kutoka taasisi ya sanaa na utamaduni Tasuba bibie Fatma Kihemba akitoa salam za chuo chake kwenye usiku wa Bagamoyo Intercolleges Night 2011 uliyofanyika kwenye ukumbi wa Tasuba mjini Bagamoyo siku ya Ijumaa tarehe 28.10.2001.
Mdau Rabia kulia akifuatilia matukio ya Bagamoyo Intercolleges Night 2011.

Bw.Kim Kimenya mkurugenzi wa kampuni ya Kimkev Entertainment akitoa neno la makaribisho.

Rais wa wanachuo wa Tasuba bw.Gasper Tesha akiwasilisha mada juu ya umuhimu wa kozi ya sanaa na utamaduni kwa jamii.
Mdau akiuliza swali kwa mtoa mada wa Tasuba.
Mtoa mada kutoka SLADS bw. Godfrey Assenga akiwasilisha mada juu ya umuhimu wa kozi ya ukutubi na utunzaji wa nyaraka.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya KG Son kutoka TMK wanaume halisi akishambulia jukwaa.
Shabiki wa burudani na taaluma akijaribu kujibu swali la usiku wa Bagamoyo Intercolleges Night 2011.
Mkurugenzi Kim Kimenya akimkabidhi fedha taslimu bibie Manka mshindi wa swali la usiku wa Bagamoyo Intercolleges Night 2011.
Haji Adam (Baba Haji) akihost shughuli nzima ya Bagamoyo Intercolleges Night 2011.

Mkurugenzi wa kampuni ya Mrimi Classic wear bw Gesase Mrimi akitanganza zawadi kwa "lady of the night" bibie Aisha Kiputula (kushoto) na Francis Kamuli "man of the night"(katikati) wote kutoka SLADS(walichaguliwa kwa kigezo cha kupendeza kwa nguo za rangi nyeupe).

Bw.Martin Mhando kutoka taasisi ya utafiti ya Ifakara mara baada ya kumtangaza Aisha Kiputula kuwa ndiye Lady of the night.

Picha ya pamoja ya washindi na waandaaji.Washindi walipata zawadi za fedha taslimu na kulala usiku mmoja katika hoteli ya Green pack village ya Bagamoyo.
Huu ulikuwa wakati wa wote yaani kwanja time.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA, BLANDINA NYONI AFUNGA KONGAMANO LA WANAHABARI LA UTAFITI WA HUDUMA ZA AFYA ZA NHIF


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni (kushoto) akizungumza na wanahabari baada ya kufunga kongamano la wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusu taarifa za tafiti za upatikanaji wa huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilifanyika mjini Morogoro.
Blandina Nyoni akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Clement Mshana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akitoa majumuisho ya mapendekezo yaliyotolewa na wadau kwenye kongamano hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni (kushoto), akipongezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk. Emmanuel Humba baada ya kufunga kongamano la wahariri na waandishi wa waandamizi wa habari la kujadili taarifa za tafiti za upatikanaji wa huduma za afya zinazotolewa na mfuko huo nchini.Kongamano hilo la siku mbili lilifanyika, mjini Morogoro. Katikati ni Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Lauden Mwambona akiongoza mijadala ya tafiti hizo. Kutoka kushoto ni Benny Mwaipaja wa TBC Manyara na Saiboko wa Daily News.
Mhariri Mtendaji wa New Habari, Deodatus Balile akichangia hoja wakati wa kongamano hilo. kushoto ni Mussa Juma wa Mwananchi Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana akichangia hoja wakati wa kongamano hilo
Joyce Mwakalinga wa Stars Tv na Margareth Tengule wa Star TV wakishiriki kongamano hilo
Cosmas Nadimi wa MSD, akijibu maswali mbalimbali ya wanahabari kuhusu usambazaji wa dawa nchini
Abdul Saiboko wa Daily News, akitoa taarifa ya utafiti wa bima ya afya Mkoa wa Kilimanjaro. Kushoto ni Mtafiti mwenzie, Masanja wa Star Tv, Kilimanjaro
Mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Cloudia Karedia akiwa kazini
Mtangazaji wa TBC Tabora Nico Mwaibale akitoa taarifa ya utafi huo kwa Mkoa wa Tabora. Kulia ni mtafiti mwenzie, Vedasto Msungu wa ITV.
George Marato wa ITV, Mara, akifafanua jambo wakati wa kongamano hilo
Baadhi ya washiriki wakiwa katika kongamano hilo mjini Moro.

SALHA AENDELEA VYEMA NA MISS WORLD 2011


Salha Izrael, Miss Tanzania 2011 akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Dunia. Hapa wakiwa Scotland.

Thursday, October 27, 2011

DULAYO D- TIMING KUSHAMBULIA BAGAMOYO INTERCOLLEGES NIGHT 2011 KESHO

 Dulayo D-timing


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdulrahman Kasembe a.k.a Dulayo D-Timing anatarajia kuwaongoza wasanii wengine kutoa burudani  katika usiku wa wanavyuo ujulikanao kama Bagamoyo Intercolleges Night.Pamoja na Dulayo kutakuwa na wasanii wengine wa muziki wa asili na muziki wa disko utakaoporomoshwa na dj Nature Skills.

Kwa mujibu wa bw. Kim Kimenya ,mkurugenzi wa kampuni ya Kimkev entertainment Dulayo anayetamba na nyimbo ya “twende mchumba” ataburudisha kwenye usiku huo unaotarajiwa kufanyika kesho Ijumaa tarehe 28.10.2011 kuanzia saa 2:00 usiku katika ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo (Tasuba),ambapo tiketi za tukio hilo zinapatikana kwenye duka maarufu la nguo za kiume liitwalo Mrimi classic wear liliopo mjini Bagamoyo.

Kimenya alisema kuwa usiku huo ambao unafanyika kwa mara ya kwanza mjini Bagamoyo unatarajia kuhudhuriwa na wanavyuo wasiyopungua 1500 kutoka vyuo vya Bagamoyo na utakuwa usiku wa rangi nyeupe, ambapo watakaopendeza  kwa mavazi ya rangi nyeupe watazawadiwa fedha taslimu pamoja na kulala kwa usiku mmoja kwenye hoteli maarufu za mjini Bagamoyo.Sambamba na zawadi za waliopendeza pia kutakuwa na zawadi kwa atakayejibu swali la usiku huo ambaye  atajipatia fedha taslimu.

Kimenya amewahakikishia wapenda taaluma na burudani kuwa usiku huu umeandaliwa kwa umakini mkubwa,hivyo wategemee tulizo la mioyo yao kwa kuwa kwenye mikono salama ya waandaji na kupata burudani ya kihistoria katika mji wa Bagamoyo.

Usiku wa Bagamoyo intercolleges night ni usiku wa taaluma na burudani wenye lengo la kuwaunganisha na kuwaburudisha wanavyuo wa mji wa Bagamoyo na nje ya Bagamoyo.Pamoja na burudani wanavyuo watapata nafasi ya kuelezea na kujadili juu ya umuhimu wa kozi wanazojifunza kwa jamii.

Tuesday, October 25, 2011

BADO SIKU MBILI KUFIKIA BAGAMOYO INTRCOLLEGES NIGHT 2011

WAMBURA AENGULIWA NA TFF KUGOMBEA UENYEKITI MKOA WA MARA

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka T anzania (FAT), sasa TFF, Michael Wambura akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kabla ya Kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kumwengua usiku huu kugombea uenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara, kwa madai kwamba si mkazi wa mkoa huo.

KOCHA PAPIC NA YANGA TENA

Kocha wa Yanga Kostadic Popic, akiomba dua na wachezaji wa timu hiyo, baada kuanza tena kuifundisha leo jioni kwenye Uwanja wa Kaunda, Jangwani, Dar es Salaam.
Papic akiwajibika uwanjani huku Kocha Msaidizi,Fred Minziro akiondoka
Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi chini ya Kocha Papic jana jioni

DK SHEIN AAPISHWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI


Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande (kushoto), akimwapisha Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam juzi.
Rais Jakaya Kikwete (mbele katikati), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu, Othman Chande pamoja na mawaziri baada ya kuapishwa kwa Shein Ikulu Dar es Salaam .

JK akimpongeza Dk. Shein
JK (wa pili kulia) akiwa na Dk. Shein (kulia kwake), Waziri Mkuu (kulia) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othaman Chande.
Jaji Mkuu, Othman Chande akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema wakati wa hafla hiyo.
JK akizungumza na Jaji Mkuu, Othman Chande (kushoto), Dk Shein (wa pili kulia) pamoja na Waziri Mkuu, Pinda. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO)

KAMATI ZA BUNGE ZAKUTANA DAR


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Kabwe Zitto na Katibu wa Kamati hiyo, Eric Maseke wakitafakari jambo wakati wakijadili utendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), katika kikao cha kamati hiyo, Dar es Salaam juzi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Idd Azzan akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Augustino Mrema.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi akijieleza mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Dar es Salaam jana. PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA

UTURUKI WATOA MSAADA WA INCUBATORS 10 WAMA


Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshukuru balozi wa Uturuki Nchini, Dkt Sander Gurbuz, baada ya kupokea msaada wa mashine 10 za kusaidia watoto waliozaliwa kabla ya muda wao. Mashine hizo, zenye thamani ya dola 30,000 (kama milioni 50), zimetolewa na kampuni ya madini na nishati ya Uturki iitwayo TPM ambapo Mkurugenzi Mkuu wake Bw Burak Buyuksaar (wa tatu kulia) alikuwepo kushuhudisa makabidhiano hayo. Kulia ni mke wa balozi, Mama Durhan Gurbuz.
Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania umetoa msaada wa incubators 10 zenye thamani ya Tsh. Mil 50/- kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mhe. Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. 

Akikabidhi msaada huo Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Dr. Sander Gurbuz amesema kuwa wametoa msaada huo kwa ajili ya kusaidia moja ya programu za Taasisi ya WAMA inayolenga kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto. Pamoja na kudumisha uhusiano mzuri ambao nchi yake ya Uturuki na Tanzania umekuwa nao. 
Mhe. Balozi aliambatana na Mke Wake Mama Durhan Gurbuz na Mkurugenzi Mkuu wa TPM Mining and Energy Co. Limited, Bw. Burak Buyuksarac. 
Akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mhe. Mama Salma Kikwete amesema kuwa msaada huo ni mkubwa sana na utasaidia kuokoa maisha ya watoto wachanga ambao wangeweza kufa kutokana na ukosefu wa vifaa hivi hasa maeneo ya vijijini. 
Mama Salma aliongeza kuwa pamoja mazingira ya Vijijini yanaweza yasiruhusu sana utumiaji wa vifaa hivi lakini kwa sababu siku hizi kuna umeme wa jua utasaidia matumizi ya vifaa hivi.

MBEYA WAMUAGA MKURUGENZI WA VODACOM DIETLOF MARE


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania anaemaliza muda wake hapa nchini,Dietlof Mare(katikati) Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga,wakiwa wameshikilia picha inayomuonyesha Mare akisimikwa na wazee wa kimila wa kabila la Wahehe mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa,wakati alipotembelea mkoa huo kuwaaga rasmi hivi karibuni.

JUDITH SANGU NDIYE MISS KIU 2011


Mrembo Judith Sangu usiku wa Jumamosi iliyopita aliibuka kidedea baada ya kuwabwaga warembo wenzake katika shindano la kumsaka mlimbwende wa  Chuo Kikuu cha Kampala International University(KIU) tawi la Dar es Salaam.
Warembo waliofanikiwa kuingia tatu bora ni Judith Sangu ndiye mshindi(katikati),Martha Kamanyola mshindi wa pili (kulia) na Asha Mohamed mshindi wa tatu(kushoto).