Thursday, March 31, 2011

MASHUJAA MUSICA KUKAMUA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO

Kiongozi wa bendi ya Mashujaa Musica Edward Antony a.k.a Jado F.F.U akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana kuhusu onesho lao linalotarajiwa kufanyika kijiji cha Makumbuso siku ya Aprili mosi 2011,na kusindikizwa na Mapacha watatu.Kati ni meneja wa bendi Mujibu na kulia kabisa ni Yanick Sauti ya radi.

Saturday, March 26, 2011

KASHESHE KUELEKEA KWA BABU

Abiria wa basi la kukodi kutoka wilayani Nzega wakisukuma gari lililokwama kwenye mpaka wa Serengeti na Loliondo siku ya Jumatano iliyopita kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katIka maeneo hayo.Hii ni safari ya kuelekea kijiji cha Samunge kwa mchungaji Ambilikile Mwasupile kwa ajili ya kupata kikombe.

Friday, March 25, 2011

MKAPA AOMBOLEZA WAJAPANI

Rais mstaafu wa Tanzania Bw.Benjamin Mkapa akipeana mkono na balozi wa Japani nchini leo asubuhi alipokwenda kwa maombolezo ya wajapani waliyokosa makazi na waliyokufa kutokana na maafa ya tsunami yaliyotokea majuma mawili yaliyopita.

Saturday, March 19, 2011

KIMKEV ENTERTAINMENT KUTOANDAA MISS TANZANIA KANDA YA MASHARIKI 2011

Kwa masikitiko makubwa nasikitika kuwataarifu kuwa hatutoandaa na kuratibu mashindano ya Miss Tanzania kanda ya Mashariki 2011 kutokana na kuzidiwa na majukumu mbalimbali.

Taarifa hii inahusu pia kutoandaa  na kutoratibu mashindano ya ngazi yoyote ya Miss Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2011.

Tunatambua kutowafurahisha mashabiki na wenye mapenzi mema nasi wanaotambua uwezo wetu wa kupanga na kusimamia matukio kwa maamuzi haya.

Tunatoa shukurani zetu kwa wote waliotuunga mkono kwa kipindi chote hasa kamati ya Miss Tanzania, waandaaji wa mikoa na wilaya ndani ya kanda ya Mashariki,warembo,wasanii,wadhamini (Vodacom,Redds Hillside Bagamoyo, Clouds redio,blog ya Michuzi,blog ya Michuzijr,blog ya OthmaniMichuzi,City style hotel,na Lindi oceanic hotel),Marafiki wetu(Albert Kawogo wa Free voice Investment Company Ltd,Mbunge wa Bagamoyo Dr.Shukuru kawambwa na wengi ambao ni vigumu kuwataja kwa sasa.

Kimkev Entretainment bado ni mwana familia ya Miss Tanzania.Tunawatakia maandalizi mema waandaji wa taifa na waandaaji wa ngazi zote kwa mwaka 2011,tupo pamoja nanyi kwa ushauri na mengine yote yatakayokuwa ndani ya uwezo wetu.


Kim H.J.Kimenya
Mkurugenzi

02Januari,2011