Tuesday, August 30, 2011

HERI YA EID MUBARAK 2011

Blog yenu ya kimkev entertainment inawatakia kila la heri katika sikukuu ya Eid Mubarak itakayofanyika kesho na  kesho kutwa na kuwataka muisheherekea kwa amani na utulivu

BALOZI WA LIBYA NCHINI,AITWA SERIKALINI KUJIELEZA KWA NINI AMEBADILISHA BENDERA YA LIBYA DAR BILA KUTOA TAARIFA SERIKALINIWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe, akizungumza na Balozi wa Libya nchini, Prof. Ahmed El Ash'hab baada ya Balozi huyo kuitwa Wizarani,Dar es Salaam juzi. kufuatia Ubalozi huo kubadilisha Bendera ya nchi hiyo bila kufuata taratibu. (PICHA NA TAGIE MWAKAWAGO WA WIZARA HIYO)

FAMILIA YA GADDAFI YATOROKEA ALGERIA


Mke wa Gaddafi, wanawe wa kiume na wa kike

Mke na watoto watatu wa kiongozi wa Libya aliye mafichoni Muammar Gaddafi wako nchini
Algeria, maafisa wa Algerian wamesema.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema mke wa kanali Gaddafi, Safia, binti yake Ayesha na watoto wa kiume Muhammad na Hannibal waliondoka Libya mapema Jumatatu.

Balozi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa amesema walipokelewa kwa misingi ya kibinadamu.

Waasi wa Libya wamesema kuwapa hifadhi familia ya Gaddafi ni kitendo cha uchokozi, na wametaka warejeshwe nchini Libya.

Haijulikani mahali alipo Kanali Gaddafi.

Wakati huo huo waasi wamesema mtoto mwingine wa kiume wa Kanali Gaddafi, Khamis, huenda aliuawa katika mapigano karibu na Bani Walid.

waasi washambulia Sirte

Taarifa hizo zimetolewa wakati waasi wa Libya wakijaribu kumaliza upinzani uliopo katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo yanayomtii Gaddafi, na kujiandaa kuendelea kwenda katika mji aliozaliwa kanali Gaddafi wa Sirte ili kumalizia upinzani unaonekana kuwa ngome yake ya mwisho.

Kuwasili kwa mke wa kanali Gaddafi na watoto watatu nchini Algeria kuliripotiwa Umoja wa Mataifa na kwa viongozi wa waasi wa Libya, wizara ya mambo ya nje ya algeria imesema katika taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la Algeria, APS.

Taarifa hiyo imesema familia ya Gaddafi walivuka mpaka kati ya Libya na Algeria Jumatatu, saa Mbili na dakika arobaini na tano za huko.

Algeria ni mahali dhahiri pa kukimbilia familia ya Gaddafi kutokana na nchi mbili hizo kuwa na mpaka mrefu na serikali ya Algeria bado halijalitambua Baraza la Mpito la Taifa la Libya.Mke na watoto watatu wa kiongozi wa Libya aliye mafichoni Muammar Gaddafi wako nchini Algeria, maafisa wa Algerian wamesema.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema mke wa kanali Gaddafi, Safia, binti yake Ayesha na watoto wa kiume Muhammad na Hannibal waliondoka Libya mapema Jumatatu.

Balozi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa amesema walipokelewa kwa misingi ya kibinadamu.

Waasi wa Libya wamesema kuwapa hifadhi familia ya Gaddafi ni kitendo cha uchokozi, na wametaka warejeshwe nchini Libya.

Haijulikani mahali alipo Kanali Gaddafi.

Wakati huo huo waasi wamesema mtoto mwingine wa kiume wa Kanali Gaddafi, Khamis, huenda aliuawa katika mapigano karibu na Bani Walid.

waasi washambulia Sirte

Taarifa hizo zimetolewa wakati waasi wa Libya wakijaribu kumaliza upinzani uliopo katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo yanayomtii Gaddafi, na kujiandaa kuendelea kwenda katika mji aliozaliwa kanali Gaddafi wa Sirte ili kumalizia upinzani unaonekana kuwa ngome yake ya mwisho.

Kuwasili kwa mke wa kanali Gaddafi na watoto watatu nchini Algeria kuliripotiwa Umoja wa Mataifa na kwa viongozi wa waasi wa Libya, wizara ya mambo ya nje ya algeria imesema katika taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la Algeria, APS.

Taarifa hiyo imesema familia ya Gaddafi walivuka mpaka kati ya Libya na Algeria Jumatatu, saa Mbili na dakika arobaini na tano za huko.

Algeria ni mahali dhahiri pa kukimbilia familia ya Gaddafi kutokana na nchi mbili hizo kuwa na mpaka mrefu na serikali ya Algeria bado halijalitambua Baraza la Mpito la Taifa la Libya.


ANSWAAR SUNNA WASWALI IDD LEO

Waumini wa dini ya Kiislamu wa madhehebu ya Answaar Sunna wakiswali swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo asubuhi

Monday, August 29, 2011

NAIBU SPIKA MH. JOB NDUGAI AONGELEA UVUMI AMBAO UMEZAGAA KUHUSU KUTOFAUTIANA NA SPIKA


Mh. Job Ndugai (Naibu Spika)
     Taarifa ambayo imeibuka kuhusu Spika na Naibu Spika kutofautiana kuhusu maamuzi ya kuunda Kamati maalum ya kumchunguza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg. David Jairo si ya kweli.
     Mh. Job Ndugai ameyaongea haya katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM cha leo na amekana huo ni uvumi tu wa watu ambao wasiolitakia mema taifa letu na wasioutakia mema ushirikiano wao mzuri ambao wanao yeye na Mh. Spika Anna Makinda, na vile vile Mh. Ndugai alilielezea pia uvumi ambao watu wameuzusha kuhusu yeye kuonekana ana nguvu zaidi ya Spika Anna Makinda; Mh. Ndugai amekana hilo na kusema ni maneno tu yale yale! ambayo watu wasioutakia mema ushirikiano wao na kusema kwamba Mh. Spika Anna Makinda anamuamini sana na anamtuma katika shughuli nyingi tu ambazo ni muhimu lakini anaenda yeye Mh. Job Ndugai.     Clouds Fm walimuuliza maswali mawili matatu naye akayaongelea kwa ufasaha na kutaka wananchi waelewe hivyo anavyosema yeye, kuliko kusikiliza watu ambao wanazusha tu mambo ambayo sio mazuri

REDD'S YATOA ZAWADI KWA AKINA MAMA WAZAZI HOSPITALI YA MWANANYAMALA


Jenifer kakolaki,mshiriki wa Miss tanzania akimbembeleza mtoto
 Warembo wakimsikiliza Mganga mkuu katika hospitali ya mwananyamala jijini Dar.
Mrembo akisaini kitabu cha wageni kwa niaba ya warembo wenzake.
 Miche ya sabuni na nepi kwaajili ya watoto wachanga waliozaliwa, zawadi hizo zilikabidhiwa hospitalini hapo na warembo kupitia kinywaji cha REDD'S.
Mrembo akionyesha upendo kwa mama na mtoto.

VOTE FOR MT.KILIMANJARO


MT. KILIMANJARO NOMINATED AS CANDIDATE FOR THE NEW SEVEN NATURAL WONDERS OF THE WORLD
Mount Kilimanjaro which is the highest peak in Africa and the highest free standing mountain in the world has been nominated as a candidate for the seven natural wonders of the world, in a competition organised by an organisation known as Seven Natural Wonders in which tourist attractions from all over the world are voted to nominated as The Seven Natural wonders of The World.

Tanzania will gain much publicity from being listed in the new list of Seven Natural wonders of the World and will be able to use this opportunity to promote Mt. Kilimanjaro as being in Tanzania.
Out of the 28 contestants which have made it to this stage, only two nominations are from Africa, these being Mt. Kilimanjaro (Tanzania) and Table Mountain (South Africa). There is fierce competition between the two African destinations. 

Voting trends have shown that most people who are voting for Mount Kilimanjaro are those residing outside the country and that very few Tanzanian residents are voting for Mt. Kilimanjaro unlike the case for Table Mountain where large numbers of South Africans are taking participation in voting for Table Mountain.
We (TTB) would like to urge Tanzanians (in and out of Tanzania), friends and patrons worldwide to vote for Mount Kilimanjaro so that it becomes one of the New Seven Natural Wonders Of The World.
Votes are being collected at the following website: www.new7wonders.com
Note that the competition is open until November 11th, 2011.
For more information contact:
The Managing Director,
Tanzania Tourist Board,
Dar-es-salaam
Tel: 255-22-2111244/5
Email: md@tanzaniatouristboard.go.tz

Mpigie kura yako Nelly Kamwelu


Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu, akiwa amepozi wakati wa zoezi la upigwaji picha muda mfupi baada ya kuwasili katika mji wa São Paulo, Brazil. 

Kamwelu atakuwa katika mji huo kwa wiki 3 akishiriki katika matukio mbalimbali na kujiandaa na shindano la 2011 MISS  UNIVERSE linalotaraji kufanyika September 12 kuanzia majira ya saa  9:00 p.m. 

Shindano hili litatangazwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha NBC kutoka katika ukumbi wa  Credicard Hall uliopo mjini São Paulo, Brazil. 

Mtanzania popote pale ulipo duniani unaombwa kumpigia kura mshiriki huyu na mwakilishi wa taifa ili aweze kufuzu hatua ya nusufainali.


Kumpigia Nelly Kamwelu kura yako ingiahapa chini:-

Wateja wa Vodacom kushindania zaidi ya Bilioni moja kupitia Promosheni ya Mega


Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba akiongea na waandishi wa habari kuhusu promosheni Mpya ya Mega inayowawezesha wateja kushiriki na kushinda bila kutozwa fedha. Mazungumzo hayo yalifanyika Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wateja, Charity Safford.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba akielezea namna ya kushiriki katika promosheni Mpya ya Mega inayowawezesha wateja kushiriki na kushinda bila kutozwa fedha. Mazungumzo hayo yalifanyika Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wateja, Charity Safford

Sunday, August 28, 2011

Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wajimwaga katika michezo Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011 jana walikutana na kushiriki michezo ya aina mbalimbali na hapa nawaletea baadhi ya michezo hiyo ukiwepo wa kuogelea. Hawa walionesha kushinda lakini baade walivutwa.
 upande wa pili mambo yalikuwa hivi na timu hii iliibuka washindi. Licha ya kamba kukatika mara mbili.
 furaha ya ushindi kwa timu ya wavuta kamba.
 Jamaa alikuwa mgeni rasmi na alizindua mpira wa miguu.
 Warembo wa Vodacom walifungua dimba na kati ya timu za M Pesa na Voda Jamaa.
 Eko India akifanya makeke na kumtoka Shafii Dauda
 Hashimu Lundenga nae alishiriki katika soka na hapa akifanya vitu vyake.
Ulifika wakati wa kucheza mziki na mshindi wa hapa alikabidhiwa kitita cha 50,000/= aliyekwenda msamba aliibuka mshinda.

Warembo wa Vodacom Miss Tanzania washiriki siku ya michezo

Na Mwandishi Wetu
Washiriki 30 wa Vodacom Miss Tanzania leo (jana)  walichuana vikali katika siku ya michezo ya Miss Tanzania iliyofanyika kwenye ufukwe wa bahari  wa Hoteli ya Jangwani See Breeze iliyopo Mbezi Kilongawima jijini Dar es Salaam.

 Wakiadhimisha siku hiyo washiriki hao wa shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa tasnia ya urembo nchini walichuana kwenye michezo mbalimbali ikiwemo Volleball, kuruka kamba, kukimbia na magunia, mbio za vijiti, kuvuta kamba na michezo mingine ya kuvutia.

Akizungumzia siku hiyo Meneja Uhusiano na Habari kwenye Mtandao Matina Nkrulu alisema lengo la siku hiyo ni kuwaunganisha warembo pamoja wakiwa tayari kuelekea kwenye hatua ya mwisho ya shindano hilo.

Akifafanua Nkurlu alisema kwamba mbali ya kuwaunganisha michezo pia imesaidia kuibua vipaji vya warembo hao mbali na fani ya urembo wanayojihusisha nayo.

“Tukiwa kwenye siku ya michezo ya Vodacom Miss Tanzania warembo wameonesha vipaji vyao vya kimichezo jambo lililowafanya pia kuendelea kuwa pamoja kama ilivyo tasnia hiyo kwamba inawaunganisha watu wote bila kujali dini rangi au kabila.

Kwa wake mrembo Glory Lory amesema siku hiyo ni ya faida kwao kwani wameweza kujifunza michezo mbalimbali ambayo walikuwa hawajawahi hata kuipitia.

Akifafanua Glory alisema mbali ya kujenga afya pia wamepanua mtazamo wa kiakili kwani ni moja ya fani zinazoenda kushindaniwa katika shindano la Miss World kwa atakayebahatika kuliwakilisha taifa.

“Michezo ni moja ya vipengele kwenye shindano la urembo la dunia, hivyo kwa atakayebahatika atafanya vizuri kwani mazoezi haya yamempika tayari kwa kwenda kushiriki michuano hiyo ya urembo ya dunia.

Nae Mkuu wa kitengo cha Itifaki wa Kamati ya Vodacom Miss Tanzania Albert Makoye alisema ari waliyonayo warembo inaonesha utayari wao katika kuliwakilisha taifa katika medani za kimataifa.

“Mmejionea wenyewe washiriki wetu walivyochuana katika michezo mbalimbali katika kuadhimisha siku ya michezo kwa warembo. Hili tu linadhihirisha kwamba shindano la mwaka huu litakuwa na changamoto kubwa ikilinganishwa na mengine yaliyopita,” alisema Makoye.

Tayari washiriki hao wanaoishi ndani ya jumba la Vodacom wameanza kupigiwa kura na watazamaji wa vituo vya televisheni  Star tv na Clouds TV baada ya maisha yao ndani ya nyumba kuoneshwa moja kwa moja na vituo hivyo

Saturday, August 27, 2011

VODACOM MISS TANZANIA KUCHUANA KATIKA MICHEZO LEO

Warembo wanaowania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011, leo wanatarajia kuchuana katika kuonyesha vipaji vyao katika michezo, kwenye ufukwe wa Jangwani Sea Breeze, Dar es Salaam.
Tukio hilo litakaloanza saa 3:00, ni miongoni mwa vipengele (fast tracks) vitano vya awali vya kinyang’anyiro hicho ambapo washindi hutinga moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali.
Tayari warembo wawili wameshapata tiketi ya kuingia nusu fainali ya mashindano hayo ambao ni Mwajabu Juma aliyeshinda taji la Top Model na Tracy Sospeter aliyeshinda taji la Miss Photogenic.
Mbali ya vipengele hivyo, vingine vilivyobaki ni Kipaji (Talent) na Mvuto (Personality) ambapo mshindi wake hutangazwa kila wiki kabla ya fainali za taifa zilizopangwa kufanayika Septemba 10, mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundenga, michezo itakayohusishwa leo ni riadha, mbio za magunia, kuogelea, kuruka chini, mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba na mingineyo.
Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, limedhaminiwa na Vodacom, Redd’s Original, New Habari (2006) Ltd, Star TV, Giraffe Hotel na Papa Zee Entertainment.

JIJI LA DAR LAENDELEA KUPIGA HATUA
Jengi jipya la Uhuru Peak lililopo makutano ya mitaa ya Ohio na Bibi Titi Mohamed, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Mtaa wa Ohio unazidi kupendeza baada majengo mapya ujenzi waka kukamilika

NBC yaipa Tiketi timu ya Walemavu itakayoshiriki All Africa Games


Meneja Uhusiano wa Benki ya NBC Tanzania, Robi Matiki-Simba  (kulia) akikabidhi tiketi saba za ndege za kwenda na kujrudi Msumbiji  kwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezom la Taifa (BMT) Kanali Iddi  Kipingu kwa ajili ya timu ya Tanzania ya wanamichezo wenye ulemavu  inayotarajiwa kushiriki michuano ya Afrika ya  nchini  Msumbiji kuanzia Septemba 3 mwaka huu. Hafla ya makabidhiano  ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati  ya Paralimpiki Tanzania, Iddi Kibwana.
Baadhi ya timu ya Tanzania ya Paralimpiki wakipozi kwa picha na  Kanali Kipingu, Meneja Uhusiano wa NBC, Bi. Robi na Katibu Mkuu wa  TPC, Iddi Kibwana katika hafla hiyo.

Dola Milioni 777 zatengwa kukamilisha Mpango wa UNDAP 2011-2015

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akiwakaribisha wadau na waandishi wa habari katika semina hiyo.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akifungua rasmi semina ya waandishi wa habari na wataalamu mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania nchini,  juu ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) Semina imefanyika kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Ukuaji Uchumi kutoka FAO Dkt. Vedasto Rutachokozibwa akibadilishana mawazo na waandishi wa habari katika Semina ya UNDAP iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa watumishi wa IAGG Bi. Salome Anyeti akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya masuala ya Haki na Jinsia katika mwendelezo wa semina iliyoandaliwa na UN Tanzania kwa lengo la kuhamasisha waaandishi wa habari kuandika na kuelimisha jamii juu ya mpango wa MKUKUTA  na MKUZA  kwa kipindi cha miaka 4 ijayo. Kushoto ni Bw. Robert Basil Mwenyekiti wa IAGG upande wa Jinsia na Maambukizo ya Ukimwi kutoka kitengo cha Chakula na Kilimo UN.
Waliokaa Kushoto ni Afisa Mipango wa Taifa (Elimu) kutoka UNESCO Godfrey Mnubi na anayefuata Bi. Maria Westergren wa UNESCO wakitoa ufafanuzi juu ya Mpango wa miaka 4 ya UNDAP kwa upande wa Sekta ya Elimu.
Afisa Program wa WFP Said Johari na Afisa Uhusiano wa michango wa WFP Fizza Moloo wakizungumza na mwandishi wa habari alitembelea kitengo hicho wakati wa semina ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assitance Plan 2011-2015 (UNDAP).

Dola Milioni 777 zatengwa kukamilisha Mpango wa UNDAP 2011-2015

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akiwakaribisha wadau na waandishi wa habari katika semina hiyo.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akifungua rasmi semina ya waandishi wa habari na wataalamu mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania nchini,  juu ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) Semina imefanyika kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Ukuaji Uchumi kutoka FAO Dkt. Vedasto Rutachokozibwa akibadilishana mawazo na waandishi wa habari katika Semina ya UNDAP iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa watumishi wa IAGG Bi. Salome Anyeti akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya masuala ya Haki na Jinsia katika mwendelezo wa semina iliyoandaliwa na UN Tanzania kwa lengo la kuhamasisha waaandishi wa habari kuandika na kuelimisha jamii juu ya mpango wa MKUKUTA  na MKUZA  kwa kipindi cha miaka 4 ijayo. Kushoto ni Bw. Robert Basil Mwenyekiti wa IAGG upande wa Jinsia na Maambukizo ya Ukimwi kutoka kitengo cha Chakula na Kilimo UN.
Waliokaa Kushoto ni Afisa Mipango wa Taifa (Elimu) kutoka UNESCO Godfrey Mnubi na anayefuata Bi. Maria Westergren wa UNESCO wakitoa ufafanuzi juu ya Mpango wa miaka 4 ya UNDAP kwa upande wa Sekta ya Elimu.
Afisa Program wa WFP Said Johari na Afisa Uhusiano wa michango wa WFP Fizza Moloo wakizungumza na mwandishi wa habari alitembelea kitengo hicho wakati wa semina ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assitance Plan 2011-2015 (UNDAP).

Thursday, August 25, 2011

TMTV kurusha Muziki wa Kitanzania

TUNAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WOTE WANAOISHI NDANI NA NJE YA TANZANIA KATIKA SIKU ZIJAZO ZA KARIBU TUTAFUNGUA TELEVISHENI. CHANELI YA MUZIKI WA KITANZANIA, KWA JINA LA TANZANIA MUSIC TELEVISION {TMTV} (WWW.TMTV.CO.TZ) AMBAYO
ITAKUWA INAPATIKA KWENYE MTANDAO,SETILATI,SIMU ZA MKONONI NA
VING'AMUZI(DECODER)

CHANELI HII ITAKUWA NA VIPINDI VIFUATAVYO:

1.BONGO BOX
2.SALAMU BOX
3.BENDI ZETU
 4.TAARABU
5.ZILIPENDWA
6.NYIMBO ZA DINI
7.VIPAJI
8. HABARI ZA MUZIKI
9.SWAHILI HIP-POP
10.NYIMBO ZA UTAMADUNI

ILI KUBORESHA UFANISHI WA CHANELI TUNAOMBA MAPENDEKEZO YENU KUPITIA:
info@tmtv.co.tz
BONYEZA HAPA KWA KUANGALIA CHANELI
www.tmtv.co.tz
KWA KOMPYUTA NYINGINE UTALAZIMIKA KUDOWNLOD  SOFTWARE YA MICROSOFT SILVER LIGHT KWA AJILI YA KUANGALIA TV.
SOFTWARE ITAJITOKEZA KTK SCREEN KWA AJILI YA KUDOWNLOD. 

WENU

UTAWALA
TANZANIA MUSIC TELEVISION

Warembo wa Miss Tanzania 2011 wapata elimu ya M Pesa kutoka Vodacom

 

Meneja Huduma wa Bidhaa za Vodacom, Elihuruma Ngowi akifafanua jambo juu  ya huduma ya M Pesa kwa washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika kambi yao iliyopo jumba la Vodacom jijini Dar es Salaam juziAfisa Utawala wa Huduma ya M Pesa kutoka Vodacom, Emmanuel Pallangyo akitoa mada juu ya huduma ya M Pesa kwa washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika kambi yao iliyopo jumba la Vodacom jijini Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakijisajili katika huduma ya M Pesa baada ya kupata semina juu ya faida na umuhimu wa kuwa umejisajili katika huduma hiyo juzi wakiwa Kambini katika Jumba la Vodacom

SILIMA AZIKWA NA MAELFU


Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya Viongozi, kubeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja jana Agosti 24.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif na baadhi ya viongozi wakiwa katika dua ya kumuombea aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Unguja, marehemu Mussa Hamis Silima, aliyefariki Agosti 23 katika hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam, alikolazwa baada ya kupata ajali Agosti 22. Marehemu Silima amezikwa jana Agosti 24 katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja.
Rais wa Zanzibar,Dkt.  Ali Mohamed Shein, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakiwa katika shughuli ya mazikonya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Silima.
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima.
 Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Mambo ya nje ya Bunge Edward Lowasa akiweka odongo.
 Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe akiweka udongo.
Wakazi wa Kijiji cha Kiboje na vitongoji vyake wakijumuika katika shughuli ya maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja jana