Friday, July 29, 2011

SALHA ISRAEL ANYAKUA TAJI LA REDDS MISS ILALA 2011

 Salha katikati mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano lililofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.Kushoto ni mshindi wa pili Alexia William na kulia ni Jenipher Kakolaki mshindi wa tatu.
 Afisa wa udhamini wa Vodacom bw. Ibrahim Kaude akimpongeza Salha
Alexia William akijibu swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Wednesday, July 27, 2011

KAMANDA KOVA MGENI RASMI MISS ILALA 2011

Warembo wanaotarajiwa kuwania taji la Miss Ilala  2011 wakiwa kwenye pozi la pamoja.Shindano linatarajiwa kufanyika tarehe 29.07.2011 kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi anatajiwa kuwa kamanda  wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam bw. Suleiman Kova.

MNUSO WA HARUSI YA JOHNSON NA TUNU NDANI YA M ALAIKA BEACH RESORT -BAGAMOYO

 Hightable ya Johnson na Tunu siku ya mnuso
 Katibu wa kamati wa mnuso bw.Michael Mihayo akitoa maelezo kwa wageni waalikwa.
 Mstahiki kushoto akiwa miongoni mwa wageni waalikwa kati Jackline na kulia mwenye suti nyeusi Msuya
 Wageni waalikwa wakiwa na dada Nuru kushoto wakijadili jambo wakati wa mnuso
 Alex Rwezaula mshauri wa blog hii akiwa na kitu chake
 Wageni waalikwa kabla kipenga cha mnuso hakijapulizwa
 Johnson na Tunu wakiingia ukumbini
 Mwalimu Mbilinyi wa Marian girls High school akiwasalimu maharusi
Maharusi wakiwa na kamati ya maandalizi

Monday, July 25, 2011

AROBAINI YA MAREHEMU MZEE MSAFIRI HASSAN KALIPENI KUFANYIKA TAREHE 29.07.2011-30.07.2011

Familiya ya marehemu mzee Msafiri Hassan Kalipeni wa mtaa wa Kanazi Kinondoni B, Dar es Salaam inapenda kuwataarifu ndugu,jamaa na marafiki kuwa arobaini ya marehemu  baba yao mpendwa itafanyika nyumbani kwao siku ya Ijumaa ijayo tarehe 29.07.2011 na kisomo kusomwa siku ya Jumamosi tarehe 30.07.2011 asubuhi.

MBWANA MATUMLA NA FRANCIS MIYEYUSHO KUZICHAPA DIAMOND JUBILEE TAREHE 30 OKTOBA 2011

Mbwana Matula bingwa mtetezi wa UBO kulia akiwa na mpinzani wake Francis Miyeyusho wakiwa na muaandaji ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Darworldlink ltd Moddy Bawazir mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya mpambano huo.