Thursday, July 31, 2014

MAZINGIRA WAZINDUA TOVUTI YA MABADILIKO YA TABIA NCHI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira  Dk.Binilith Mahenge akizindua rasmi tovuti ya mabadiliko ya tabianchi itakayotumika kutoa taarifa mbalimbali za utunzaji wa Mazingira.Kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dk. Julius Ningu.
 

SERIKALI kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, leo imezindua tovuti ya mabadiliko ya tabia nchi.

Akizindua tovuti hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira  Dk.Binilith Mahenge amesema mbali na mambo mengine lakini itakuwa ikitoa habari mbalimbali za masuala ya madiliko ya tabia nchi lakini pia itakuwa ikitoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo ya tabia nchi.

Katika hotuba yake fupi ya uzinduzi wa tovuti hiyo, aliyoandaliwa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark, Mhenge amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi huangaliwa kwa muda wa miaka 30 hivyo kwa kipindi hiki chote kumekuwa na madhara mengi yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia Nchi ikiwa ongezeko la joto, kina cha bahari kuongezeka pamoja na ongezeko la majanga ya mvua zisizo na viwango,  kutoka na shughuli za binadamu katika uzalishaji hasa viwanda vikubwa

Alisema kwa tovuti inayozinduliwa ina umuhimu mkubwa kwani inaelezea maeneo ya hali ya mabadiliko ya tabia  nchi na juhudi za serikali katika kukabiliana na athari zinazoletwa na mabadiliko hayo.

“ziko sababu za kuungana na wenzetu ili kuondoa      tatizo hili la mabadiliko ya nchi ambapo tovuti hii www.climatechange.go.tz inatuunganisha na tovuti mbali mbali katika kupunguza gesi joto hapanchini pia inaelezea fursa zilizopo katika miradi na program mbali mbali. Alisisitiza”

Alibaini kuwa tovuti hii itachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uelewa na weledi kuhusu mabadiliko ya tabia  nchi nchini kwa wananchi na wadau kwa ujumla.

BUNGE LA KATIBA LAITISHWA,UKAWA WATIA MGOMO

                                                                     

         


mbowe_326e8.jpg
Bunge Maalumu la Katiba limeitishwa Agosti 5, mwaka huu, huku wajumbe wake wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiendelea na msimamo wao wa kutorejea bungeni hadi yatakapopatikana maridhiano ya msingi.
Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe jana, alisema kitakachowarudisha ndani ya Bunge hilo ni maridhiano ya msingi yatakayorejesha maoni ya wananchi kujadiliwa.
Mbowe alizungumzia msimamo huo wa Ukawa kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) alioutuma kwa mwandishi baada ya kutakiwa kueleza msimamo wa umoja huo kufuatia Bunge hilo kuitishwa.
"Hadi hatua ya sasa ninapoandika sms (ujumbe) hii, msimamo wetu Ukawa uko palepale. Hatutarejea Bunge la Katiba...Labda yawepo maridhiano ya msingi yatakayorejesha maoni ya wananchi kuheshimiwa kupitia Rasimu ya Katiba ya Tume ya Warioba na siyo vinginevyo," alisema Mbowe.(E.L)

MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM

  
1a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Festus Mogae wa Botswana wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Africa Readership Forum ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia changamoto hizo.
2a
Rais mstaafu wa wa Afrika Kusin Thabo Mbeki akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
3a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini katikati ,Festus Mogae wa Botswana kushoo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa wakiwa wakiongoza mkutano huo.
4a
Baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
5a
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe katikati ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katik mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
6a
Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye kulia ni Mh. Balozi Ali Karume walikuwa ni miogoni wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo pia
 
source michuzijr.blogspot

MNYAMA TID ATIKISA DAR LIVE SIKU YA IDD PILI


 
 
Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Khalid Mohammed 'TID Mnyama' akizikonga nyoyo za mashabiki wa Dar Live katika Usiku wa Mnyama na Wanyama.
 
Mnyama TID akijiachia kwa mashabiki wake wa Dar Live.
Mwanamuziki Jafarai akipagawisha mashabiki waliofurika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Jay Moe akifanya makamuzi katika steji ya kupanda na kushuka ya Dar Live.
Inspector Haroun akiwapa hi mashabiki wake ndani ya Dar Live

Wednesday, July 30, 2014

SHAABAN KISSIGA AJIUNGA NA SIMBA


10
Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar msimu uliopita na sasa amejiunga na Simba sc, Shaaban Kisiga ‘Malone’  (kushoto) akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Yanga, Athuman Idd ‘Chuji’ (katikati)  na Mbuyu Twite (kulia)
 Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
 Miaka 12 iliyopita katika uwanja wa Nambole, jijini, Kampala, timu ya Simba SC ilikuwa katika kiwango cha juu katika michuano ya kombe la Kagame. Simba ambayo ilifika robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika mwaka mmoja baadaye chini ya Mwalimu, Mkenya, James Siang’a timu hiyo ilikuwa kamili kila idara na ilikaribia kuvunja rekodi yao mbaya kama mabingwa mara nyingi wa klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ( mabingwa mara sita) ambao hawajatwaa taji lolote nje ya ardhi ya Tanzania.
 Simba ilipoteza mchezo wa fainali mbele ya wenyeji, timu ya Sports Club Villa kwa bao 1-0. Shaaban Kisiga ‘ Malone’ aliwatesa viungo wa Simba kama Suleimani Matola, Shekhani Rashid, Kisiga akichipukia. Kiungo huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania alipiga pasi ya mwisho kwa Bernad Mwalala na mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Kenya akafunga bao pekee. Licha ya kuonyesha kiwango cha juu katika michuano, Kisiga hakutulia nchini Uganda kutokana na mambo ya kiusalama.
Siang’a alipendekeza mchezaji huyo pamoja na Primus Kasonso wasajiliwe kwa ajili ya msimu wa mwaka, 2003, ila hakufanikiwa kumpata, Kisiga na badala yake aliwapata Christopher Alex na Ulimboka Mwakingwe kutoka Reli FC ya Morogoro na Primus kutoka Tanzania Prisons ya Mbeya. Simba ilifanya kwa mwaka wote wa 2003, na wakati wa usajili ulipofika kwa ajili ya msimu wa mwaka 2004. Kisiga alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa wakati huo.
 Kisiga alicheza Simba kwa miaka miwili. Msimu wake wa kwanza ulikuwa na mafanikio makubwa, licha ya kuwa kiungo mbunifu katikati ya uwanja, Kisiga ni mshambuliaji mzuri wa pili, namaanisha namba 10. Kutokana na utitiri wa vipaji katika nafasi ya kiungo, Mwalimu, Siang’a mara nyingi alikuwa akimtumia kama mshambulizi wa pili sambamba na Athumani Machuppa. Alipoondoka, Siang’a alikuaja, Mzambia, Patrick Phiri ambaye alikuwa akimtumia zaidi Kisiga kama kiungo wa pembeni au mshambuliaji wa pili.
 Trott Moloto, kocha raia wa Afrika Kusini alipochukua nafasi ya Phiri kama kocha mkuu wa Simba mwanzoni mwa mwaka, 2005 alisema wazi kuwa hatowatumia Machuppa na Kisiga kama washambuliaji na katika mchezo wake wa kwanza wa mashindano dhidi ya Enyimba ya Nigeria katika klabu bingwa Afrika katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Moloto aliwaweka benchi Kisiga na Machuppa huku mshambulizi mwenye umbo kubwa, Nurdin Msiga akiongoza safu ya mashambulizi. Simba ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 huku Nurdin akifunga bao pekee la Simba ambalo lilikuwa la kusawazisha.
IMG_9835

  Mashabiki walikuja juu kutokana na kitendo cha wachezaji hao kuanzia benchi na kupangwa katika nafasi tofauti. Moloto alisema kama Simba ilikuwa ikihitaji kufanya vizuri katika michuano ya vilabu barani Afrika ni kutowachezesha, Kisiga na Machuppa kama washambuliaji pekee kutokana na maumbo yao madogo.
  Moloto alipangiwa timu katika mchezo wa marejeano, Aba, Nigeria huku Kisiga na Machuppa wakirudishwa katika majukumu ya ufungaji na Simba ikatandikwa mabao 4-0. Mwalimu huyo raia wa Afrika Kusini akaondoka zake lakini Simba haikuweza kunyanyuka hata ilipokuwa chini ya Mwalimu wa muda, Jamhuri Kiwelo ‘ Julio ‘. Kisiga aliondoka Simba na kwena kucheza soka la kulipwa nje ya nchi mara baada ya kumalizika kwa msimu wa mwaka, 2005.
 ARUDI SIMBA SC BAADA YA MIAKA TISA. ……
Kiwango cha juu ambacho alikionyesha katika msimu uliopita akiwa na timu ya Mtibwa Sugar bila shaka kimekuwa na mafanikio huku akipata heshima kama mmoja wa viungo bora wachezesha timu nchini. Aliwafunika chipukizi wa Simba kama Jonas Mkude na Said Ndemla katika mchezo wa Mwezi Februari na akaendelea kuwa bora katika mchezo dhidi ya Yanga, hiyo si sababu ya kusajiliwa tena na Simba, bali mchezaji huyo atatumika kuimarisha timu inayojipanga kwa kutumia wachezaji vijana zaidi. Kwa misimu miwili iliyopita Kisiga amekuwa mchezaji wa kiwango cha juu katika timu ya Mtibwa. Siku zote anacheza vizuri zaidi katika mechi kubwa jambo ambalo linafanya kuwepo na sababu muhimu ya kumsaini.
 Msimu uliopita, Simba haikupata ushindi wowote katika michezo sita dhidi ya timu za Azam FC, Yanga na Mbeya City FC hivyo ni wazi kuwa kuna maeneo timu hiyo ilikuwa ikizidiwa, eneo la kiungo ni sehemu ya kwanza. Kisiga hatocheza mechi zote, ila anaweza kucheza mechi zote muhimu na kutoa matunda mazuri. Kisiga amesajiliwa kwa sababu ya uwezo wake, pia maisha yake marefu katika soka, na jinsi anavyojiandaa na kupenda kwake mchezo wenyewe. Huyu ni sehemu ya mfano wa kuigwa kwa vijana wa Kitanzania,
 Kisiga si yule wa SS Villa vs Simba SC, 2002, ila amekuwa na mchezo uleule, wachache wamejitunza kwa muda mrefu kama huo. Kisiga ni mchezaji wa Simba, alivyo, kiuchezaji. Kisiga ni kiungo bora wa kupiga pasi za mwisho na mchezaji anayejiamini muda wote uwanjani.


      

TAIFA STARS KWENDA AFRIKA KUSINI LEO

 
TAIFA1
Msafara wa watu 27 wa kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinaondoka leo (Julai 30 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya Air Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kitapiga kambi ya siku mbili kabla ya kuingia Maputo kuikabili Msumbiji (Mambas).
 Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili saa 9 asubuhi kesho (Julai 30 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet kutoka Tukuyu mkoani Mbeya, na baadaye jioni kuunganisha safari ya Afrika Kusini.
 Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itachezwa Agosti 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa uliopo Zimpeto nje kidogo ya Jiji la Maputo.
 Msafara huo wa Taifa Stars kwenda Afrika Kusini unajumuisha wachezaji 19 na waliobaki ni maofisa wa Benchi la Ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij kutoka Uholanzi.
 Wakati kiungo Mwinyi Kazimoto ametua jana (Julai 29 mwaka huu) nchini kuungana na wenzake, washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wao wataungana na wenzao kesho (Julai 30 mwaka huu) jijini Johannesburg wakitokea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
 Wakati huo huo, Serengeti Boys imewasili salama juzi (Julai 28 mwaka huu) jijini Johannesburg kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi ya wenyeji Afrika Kusini (Amajimbos).
 Serengeti Boys imefikia hoteli ya Garden Court, na mechi hiyo itachezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto. Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa karibu wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam.
 BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

ROSE MUHANDO NA ALBAM YA PINDO LA YESU HIVI KARIBUNI

  
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili, Rose Muhando amelalamika kuwa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu Albamu anayotarajia kuizindua Jumapili wiki hii imeingizwa mtaani na wezi wa kazi za wasanii, hivyo kuonya wananchi wawe makini kwani albamu yake halisi itatoka Jumapili.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa Muhando jana, ilieleza kuwa albamu yake halisi bado haijaingia mtaani na kwamba hiyo wanayoiona wananchi sasa ni bandia na mtu atakayewauzia wamripoti polisi.
 
“Albamu ya Kamata Pindo la Yesu itaanza kuingia mtaani baada ya uzinduzi wangu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jumapili wiki hii. Albamu yangu ina nembo ya TRA (Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini).
 
“Hizi CD zinazouzwa hivi sasa si zangu, hao ni matapeli na nawaomba wananchi tushirikiane kudhibiti wizi. Hao ni maharamia wa kazi za wasanii wanataka kunyonyajasho langu, naomba sana wananchi mnisaidie.“Nasisitiza albamu yangu sijaiachia sokoni bado mpaka uzinduzi ukamilike, Watanzania wenzangu na mashabiki wangu kote duniani mnielewe na naomba tusaidiane katika hili maana CD feki zimezagaa,” alisema Muhando na kuongez akuwa tayari ameripoti taarifa hiyo kwa vyombo vya dola.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayoratibu uzinduzi huo, Alex msama naye katika taarifa hiyo ya pamoja alionya wote watakaobanika kuwa CD za albamu ya Rose Muhando watakumbana na mkono wa sheria.
 
“Inasikitisha sana kuona baadhi ya watu wanataka kutumia jasho la wengine kujinufaisha. Watanzania kuweni macho, msubiri albamu yenyewe ya Rose Muhando Jumapili pale ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam,” alisema Msama.
 
Albamu hiyo ya Muhando itakayozinduliwa Jumapili ina nyimbo za Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.
 
Hivi sasa Rose anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu, ambapo pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka na Wololo.
 
 
 
 
 

DIAMOND AREJEA NA TUZO

   Diamond Platnumz  akionesha tuzo yake aliyoshinda kwa baadhi ya vyombo vya habari  na mashabiki waliofika kumlaki,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.
 Mwanamuziki nyota wa miondoko ya Bongo Fleva Diamond Platnumz akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.Pichani akilakiwa na Mama yake Mzazi na baadhi ya washabiki na wapenzi wa muziki huo.

 Diamond Platnumz akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.

Tuesday, July 29, 2014

TIMU Y ATAIFA YA MCHEZO WA CHESS YAKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA KWA AJILI YA KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA NCHINI NORWAY

       

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (kulia), akimakabidhi Bendera ya Taifa, mmoja wa wachezaji wa timu ya Taifa wa mchezo wa Chess, Hemed Mlawa (wa pili kushoto), Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kuondoka kesho kwenda kushiriki mashindano ya kimataifa nchini Norway. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini, kushoto ni mchezaji Emmanuel Mwaisumbe. Safari hiyo imedhaminiwa na Tanzania Chess Foundation na Kasparov Foundation.
Hapa ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini (kulia), mchezaji Hemed Mlawa (kushoto) na Emmanuel Mwaisumbe (wa pili kushoto), wakifurahi baada ya kucheza mchezo huo wakati wakiwaonesha waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), akizungumza na wanahabri kabla ya kukabidhi bendera. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini na kulia mchezaji Hemed Mlawa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini, akizungumza na wanahabari. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini, akizungumza na wanahabari.
Wachezaji wa mchezo huo, Hemed Mlawa (kulia) na Emmanuel Mwaisumbe wakiwa kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa bendera ya Taifa. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania, Henry Lihaya.
Kulia ni Mratibu wa Chess Tanzania, Johnson Mshana akifuatilia kwa karibu tukio hilo. Kushoto ni Mwanahabari
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), akizungumza na wanahabri kabla ya kukabidhi bendera. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini na kulia mchezaji Hemed Mlawa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini na mchezaji wa mchezo huo, Hemed Mlawa wakionesha umahiri wa kucheza mchezo huo mbele ya wanahabari.Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi na mchezaji Emmanuel Mwaisumbe. (Imeandaliwa na www.habari za jamii.com- simu namba 0712-727062, 0786-858550)
…………………………………………………………………………………………..
Dotto Mwaibale
 
TIMU ya Taifa ya Chess imeagwa Dar es Salaam leo asubuhi kwajili ya kwenda kushiriki mashindano ya chess 41 ya kimataifa Olympiads yatakayofanyika nchini Norway.
 
Jumla ya wachezaji watano wataondoka nchini leo usiku kwenda kushiriki mashindano hayo.
 
Wachezaji hao ni Geofrey Mwanyika, Hemed Mlawa, Emmanuel Mwaisumbe, Nurdin Hassuji na Yusuph Mdoe.
 
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi timu hiyo bendera ya taifa, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania, Dioniz Malinzi alisema kuwa kuwakabidhi bendera hiyo ni ishara ya kuwatakia safari njema na ushindi katika mashindano hayo.
 
Malinzi alisema anashukuru wale wote ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kusimamia mchezo huo nchini hadi kufikia kushiriki mashindano ya kimataifa.
 
”Namshukuru sana Mr Vinay kwa msaada wake anaoutoa kusapoti mchezo huu Tanzania na kwa moyo wake wa kutoa, maana waswahili husema kutoa ni moyo na sio utajiri maana kuna matajiri wegi lakini sio watoaji” alisema
 
Aliongeza kuwa anamatumaini kuwa wachezaji hao watakwenda kufanya vizuri katika mashindano hayo na kuitangza Tanzania.
 
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet na Mwanzilishi wa Mchezo wa Chess Tanzania, Vinay Choudary alisema kwa yeyote atakayeweza kuibuka na ubingwa shilingi milioni mia moja zitatolewa kwa ajili yake.
 
Choudary alisema hadi sasa walipofikia ni pazuri kwa Tanzania kushiriki mashindano ya kimataifa hivyo anawatakia safari njema na ushindi katika mchezo huo.
 
Mchezaji Hemed Mlawa alisema wataiwakilisha vema Tanzania na watahakikisha wanafanya vizuri.
 
”Hii ni mara ya kwanza sisi kushiriki hivyo hatuwezi kusema kuwa tutarudi na ushindi moja kwa moja bali tutafanya vizuri na tunaamini tunaweza kuzishinda baadhi ya nchi”alisema
 
Mashindano hayo ni ya wiki mbili na yameratibiwa na Shirikisho la Chess Duniani(FIDE)
na kudhaminiwa na Tanzania Chess Association na Kasparov Association.

WAISLAMU WATAKIWA KUONESHA MSHIKAMANO NA MADHEHEBU MENGINE


Waumini wa dini ya kiislamu wakihitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani wakiwa kwenye ibada ya swala ya Iddy el Fitry kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid jijini Arusha.

 Sheikh wa mkoa wa Arusha Shaban bin Jumaa akitoa hutuba ya Idd kwa waumini wa dini ya kiislamu na kuwataka kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa waumini wa dini nyingine ilikuweka katika hali ya utlivu mkoa wa Arusha ilikuweza kujiletea maendeleo endelevu kama mafungisho ya dini yanavyowataka(picha zote na mahmoud ahmad wa blog ya jamii arusha.)