Wednesday, April 27, 2011

KARIBU ALPHA LODGE - BAGAMOYO

Apha lodge iliyopo mtaa wa wakojani (shopping centre) ni hoteli ya hadhi ya kati iliyofunguliwa upya hivi karibuni chini ya mkurugenzi Mwanaidi Katendasi ambaye pia ni mkufunzi wa Taasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo -Tasuba.Kwa mujibu wa meneja wa Alpha huduma za chakula ,vinywaji na malazi hupatikana hapo kwa viwango vya hali juu na kwa bei nafuu.Karibuni sana Bagamoyo karibuni Alpha.

Saturday, April 23, 2011

BENDI YA CHIKICHA ORIGINAL YAUSHIKA MJI WA BAGAMOYO

 Rais wa bendi na mwimbaji kiongozi wa bendi Masoud Kilimanjaro akiwajibika kwenye moja ya maonesho ya bendi kwenye ukumbi wa hoteli ya Skylight mjini Bagamoyo hivi karibuni.

 Zungu likipagawishwa na dansa wa Chikicha original
 Dansa namba moja wa Chikicha original akishambulia jukwaa
 Mpigaji wa gitaa la solo na mwimbaji, Kibugila a.k.a KB akiwajIbika.
 Mwimbaji Hassani Mabele akiwakonga roho mashabiki wa Chikicha original.
 Mwimbaji anayechipukia kwa kasi Amour Bebesi akishambulia jukwaa.
Mashabiki wa Chikicha original Dalla Zambo a.k.a mzee wa chenji kota( kushoto) akiwa na mashabiki wengine kwenye moja ya maonesho ya Chikicha original kwenye hotel ya Skylight hivi karibuni.

Wednesday, April 13, 2011

DINNER YA JUBILEE YA MIAKA 25 YA NDOA YA BW NA BIBI MSAFIRI ILIYOFANYIKA JUMAMOSI YA TAREHE 09.04.2011 KWENYE HOTELI YA COLLUBUS-KIJITONYAMA

 Bw na bibi msafiri mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa hoteli ya collubus.
 Bw  na bibi msafiri wakipata kilaji.
 Bw msafiri akiwa anatafakari jambo.
 Bi Zena  akiwa kwenye pozi la jubilee
 Bw na bibi Msafiri wakiwa ya jubilee.
 Mwaaa hii ndiyo staili ya jubilee.
 Mzee Chabanga Hassani Dyamwale akitoa neno la jubilee.


 `Wageni waalikwa Brenda kushoto Eveta kati na Maria kulia
 Bw na bibi Faraji wa E.A.D. wakiwa miongoni mwa wageni waalikwa.
 Mkufu akiwa ndani ya jubilee.
 Wageni waalikwa wakiwa wanapata kitu roho inapenda.
 MC Kim Kimenya akihosti mnuso.
Mariam kulia na Brenda kushoto wakitawala mchezo.

Monday, April 11, 2011

MAFUNZO YA KAMPENI DHIDI YA MAGONJWA YASIYOPEWA UMUHIMU YAANZA BAGAMOYO

 Mkufunzi wa mafunzo yaliyofanyika katika kituo cha shule ya msingi Mwambao ya mjini Bagamoyo kushoto Bw.karindima kutoka idara ya afya ya Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo akiwa na mwenyekiti wa mafunzo kulia wakifuatilia mafunzo siku ya Alhamisi tarehe7,Aprili,2011.
 Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mafunzo.Washiriki wa mafunzo hayo walikuwa watumishi kutoka idara za afya na elimu kwa ngazi za vijiji vya Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.
 Washiriki wa mafunzo wakati wa mapumzilko
Mkufunzi wa mafunzo Bibi Agness Manyama kutoka idara ya afya ya Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo akifafanua jambo kwa washiriki wakati  mafunzo hayo.Kwa mujibu wa taarifa ya Manyama kampeni hiyo itaanza kati ya mwezi Aprili na Mei 2011 baada ya mafunzo ya makundi mengine yatakayohusika katika kampeni kufanyika.