Friday, December 7, 2012

UNIQUE MODELS NDO HABARI YA MJINI DESEMBA HII

 

Washiriki wa shindano la unique model wakiwa katika hali ya kujifua catwalk ikiwa ni maandalizi ya fainali za shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwezi huu.
Washiriki Zenaath Unique na Sandra Unique katika mtanange wa miondoko ya kimaonyesho,hapa ni sehemu ya uwazi katika Hotel ya Giraffe ocean view,hotel bora na huduma za ukarimu.
 

UZINDUZI WA MBIO ZA UHURU MARATHON
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akiwasili katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont, Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam tayari kwa kuendesha hafla hiyo ya Uzinduzi.akizindua rasmi tovuti ya Mbio hizo ya http://www.uhurumarathon.com pamoja nae ni Mkurugenzi wa Intelecture Communication Ltd, Waandaaji wa Mbio hizo, Innocent Meleck.
Msanii Maarufu wa Nyimbo za Mashaili hapa nchini,Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba akionyesha umahiri wake wa Mashairi yake yenye ujumbe mzito wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) ambazo zitakuwa zikifanyika kila Mwaka.hafla hii imefanyika katika Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon), Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akimtunza Mjomba Mrisho Mpoto wakati akiimba nyimbo zake za Mashairi yenye Ujumbe Mzito kwa Taifa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam
Muongozaji wa Hafla hiyo usiku huu, alikuwa ni MC Ephrahim Kibonde.
Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akisoma hotuba yake wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) ambazo zitakuwa zikifanyika kila Mwaka.hafla hii imefanyika katika Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akisoma hotuba yake aliyoiandaa wakati wa Uzinduzi wa Uhuru Marathon uliofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) uliofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam
Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akitoa ufafanuzi wa mdogo wa nembo na kauli mbiu zitakazo tumika kwenye Mbio hizo kwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara.
Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akimuelezea Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara juu ya Tovuti ya mbio hizo ambayo ni http:// www.uhurumarathon.com muda mfupi baada ya kuzinduliwa.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akikabidhiwa fulama Maalum yenye jina la Rais Jakaya Kikwete.
Mratibu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akifafanua jambo kwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara.
 
Wadau mbali mbali kutoka makampuni tofauti tofauti hapa nchini pia walikuwepo kwenye uzinduzi huo.
Mjomba Band ikifanya vitu vyake.
Wanahabari.
Wadau kibao walikuwepo kwenye uzinduzi huo.

BARABARA YA DAR LINDI KUKAMILIKA JUNI MWAKANI


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

 
 
 
 
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Barabara ya Dar-Lindi kukamilika Juni mwakani

                   Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameambiwa juzi, Jumatano, Desemba 5, 2012, kuwa ujenzi wa Barabara ya Dar es Salaam-Lindi utakamilika katika miezi sita ijayo kuanzia sasa.

                   Rais Kikwete alipewa maelezo hayo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Mhandisi Gerson Hosea Malangalila Lwenge wakati aliposimama kukagua maendeleo ya ujenzi kwa akiwango cha lami wa kilomita 56 kati ya  Nyamwage, Mkoa wa Pwani na Somanga, Mkoa wa Lindi.

                   Rais Kikwete alisimama kukagua ujenzi wa Barabara hiyo wakati akirejea Dar es Salaam kutoka Lindi ambako alifanya ziara yenye mafanikio makubwa ya siku tatu kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi.

                   Akipewa maelezo ya ujenzi wa Barabara hiyo kwenye eneo la Somanga, Rais Kikwete aliambiwa kuwa kati ya kilomita hizo 56 tayari kilomita 30 zimeshatiwa lami. Barabara hiyo inajengwa na Kampuni ya MS Karafi.

                   Naibu Waziri huyo alimwambia Rais Kikwete: “Mjenzi anajenga kiasi cha mita 250 kila siku na kama hapakuwepo na kuharibika kwa lolote ama mvua isipokuwa nyingi kupita kiasi, basi ujenzi wa Barabara hii utakuwa umekamilika katika miezi sita ijayo kuanzia sasa.”

                   Naibu Waziri alimwambia Rais Kikwete kuwa ni kweli ulikuwepo ucheleweshaji kwa upande wa mjenzi, lakini sasa maendeleo ni mazuri. Barabara hiyo ilipangwa kukamilika Juni, mwaka jana, 2011.

                   “Kwa jumla ujenzi wa Barabara nzima umekamilika kwa asilimia 78, njia ya awali ambako lami itawekwa imekamilika kwa asilimia 98, madaraja madogo kiasi cha 55 tayari yamejengwa na vifaa vyote ikiwa ni pamoja na kokoto viko kwenye eneo la ujenzi.”

                   Barabara ya Dar es Salaam-Lindi ina urefu wa jumla ya kilomita 452 na kukamilika kwa kipande cha Nyamwage-Somanga una maana kuwa mtu yoyote anaweza kusafiri kwa lami tupu kutoka Mtwara hadi Kagera ama Mwanza ama Arusha ama Tunduma.

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

07 Desemba, 2012

 

Friday, May 4, 2012

JK AFANYA MABADILIKOYA BARAZA LA MAWAZIRI

 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI


MAWAZIRI

1.      OFISI YA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,


2.      OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H.  Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,


3.      OFISI  YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri  Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,


4.      WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi
Dr.  John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof.  Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof.  Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe,  Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa  Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,


Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,5.      NAIBU MAWAZIRI


 OFISI YA RAIS

HAKUNA NAIBU WAZIRI


6.      OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,


7.      OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,
8.      WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,


Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,

Wataapishwa Jumatatu tarehe 7  Mei, 2012 saa 5.00 asubuhi katika viwanja vya Ikulu

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Mei, 2012

Tuesday, April 24, 2012

MISS REDD’S ARUSHA CITY CENTRE KUJULIKANA MEI 5, 2012 NDANI YA HOTELI YA NAURA SPRINGS 

 
 Washiriki wa kitongoji Kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja, tayari kuchuana vikali Mei 5, 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.katika shindano hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000/=
Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.
---
Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012,yanatarajiwa kufanyika Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.

Akizungumza leo jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka  kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, amebainisha kuwa mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na kila kitu kimekwisha kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo ambao mpaka sasa wametimia 20.

Bi. Upendo Simwita amesema kuwa wameishakamilisha mchakato wa kuwapata Warembo wenye mvuto na wenye vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo hao wenye ari kubwa ya ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa Miss Tanzania 2012 anatokea kwenye kitongoji hicho.

“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20, ambao watachuana vikali jukwaani, na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”, alisema Upendo. Amesema kuwa kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh 25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=

Kwa upande wa Burudani,Upendo  amesema kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli, Muziki wa Asili, Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine  mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.

ZAIDI YA ABIRIA 40 WANUSURIKA KIFO MKOANI MBEYA, BAADA YA BASI LAO KUGONGWA NA KUPINDUKA


Basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria abiria zaidi ya 40, lenye nambari za usajili T 374 AVR, likiwa limepinduka baada ya kugongwa kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG. Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.


Basi la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG lililohusika katika ajali, baada ya kuligonga kwa nyuma basi aina ya Coaster enye nambari za usajili T 374 AVR ambapo zaidi ya abiria 40 kunusurika kifo. Tukio lililotokea Aprili 23 mwaka huu saa moja asubuhi eneo la Imezu na Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini. 
---

Picha na Habari: Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Abiria zaidi ya 40 wamenusurika kifo baada ya basi waliokuwa wakisafiri aina ya Coaster, lenye nambari za usajili T 374 AVR, kupinduka lilipogongwa kwa nyuma na basi jingine la kampuni ya El Saedy lenye nambari T 499 AVG.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa basi la El Saedy likiwa katika hali ya mwendokasi liliharibika mfumo wa breki kutoka eneo la Mlima Nyoka na kuligonga basi hilo dogo kwa nyuma katika mteremko wa Shule ya Sekondari Imezu, hali iliyopelekea basi hilo dogo kupinduka.

Baada ya Coaster kupinduka basi la El Saedy likiwa bado katika mwendokasi liliendelea na safari, kabla ya dereva kufanikiwa kulichepusha kabla halijavuka reli ya TAZARA katika Kijiji cha Inyala Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Aidha baadhi ya abiria katika basi hilo dogo walikuwemo wanafunzi 28, wa kike na kiume wakielekea shuleni majira ya saa moja asubuhi, Aprili 23 mwaka huu katika Shule ya Sekondari Imezu.

Mara baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya abiria walikuwemo katika basi hilo dogo walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya, ambapo kati yao wamelazwa ili kufanyiwa uchunguzi na wengine wakiruhusiwa kurudi nyumbani.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mbeya Barakiel Masaki,hakupatikana kuelezea ajali hiyo ingawa dereva wa basi la El Saedy anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.

Picha na Habari: MbeyaYetu Blog.

YANGA YAOMBA RADHI MKUTANO MKUU


Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga ambaye pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF akiwakilisha klabu za Mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Bhinda aliwaomba radhi wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kitendo cha wachezaji wake kumpiga mwamuzi Israel Nkongo kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu.

Pia alimuomba Rais wa TFF, Leodegar Tenga kutoa msamaha wa adhabu ya kulipa faini iliyotolewa na Kamati ya Ligi ya TFF kwa wachezaji wawili wa Yanga ambao mpaka sasa hawajalipa faini hiyo.

Rais Tenga alimshukuru Bhinda kwa ujasiri alioonesha wa kuomba radhi mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa kitendo kile.

Aliongeza kuwa kwa vile yeye ni muumini wa kanuni, na adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni hawezi kutoa msamaha, hivyo wachezaji hao walipe faini hizo.

Pia Rais Tenga alisema binafsi haziingilia kamati za TFF katika uamuzi ambao zinafanya kwa vile zina watu waadilifu, na angekuwa yeye binafsi ndiye anayetoa adhabu, angetoa adhabu kali zaidi kwa vile vitendo vya kupiga waamuzi havikubaliki katika mchezo wa mpira wa miguu.