Wednesday, October 13, 2010

Mapacha watatu kuzindua album yao ya kwanza Ijumaa hii

Habari za kazi wadau,

Natumaini mtakuwa mnawajua vijana wa Mapacha Wa3 ambao ni Khalid Chuma a.k.a Chokoraa, Kalala Hamza a.k.a Kalala Junior wote kutoka bendi ya Twanga Pepeta na mimi mwenyewe Joseph Mponezya a.k.a Jose Mara wa FM Academia Tunatarajia kuzindua album yetu ya kwanza iitwayo "Jasho la Mtu" Album itazinduliwa tarehe 15 Octoba 2010 katika ukumbi wa Travertine - Magomeni kuanzia saa 3 usiku kwa kiingilio cha Tshs. 10,000/- tu.

 pia tutasindikizwa na The African Stars (Twanga Pepeta) Full squad na Mfalme wa Taarab nchini Mzee Yusuf.

Naombeni msaada wenu wa kunitangazia kwenye blog zenu.

Shukrani.

Jose Mara

MAHAFALI YA DARASA LA VII 2010 SHULE YA MSINGI NIANJEMA MJINI BAGAMOYO 8 OCTOBER 2010

 Mkuu wa shule ya msingi Nianjema Bi Anna Ngondya akifuatia maonesho(katikati mbele) akiwa na mgeni rasmi wa mahafali ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Campaigne for good governance(CCG) ya jiini Dar es salaam bw Walace Mayunga
 Mgeni rasmi (aliyevaa suti)akifuatilia maonesho ya mahafali,kushoto kwake ni mwakilishi wa afisa elimu(w) bw.Frank kwayu
 Mzee Samahani Kejeli(aliyevaa kofia) mhifadhi wa zamani wa kituo cha mambo ya kale cha Kaole Bagamoyo akiwa miongoni mwa wageni waalikwa.
 Mkuu wa shule ya msingi nianjema akimuongoza mgeni rasmi kutoa vyeti na zawadi kwa wahitimu
 Mstahiki Kim akiwa mmoja kati ya wageni waalikwa wa mahafali
 Mwalimu Grace Peter(aliyevaa suti ya manjano)akiwa na mkuu wa shule ya msingi Bwilungu - Chalinze wakati wa chakula cha mchana kwa ajili ya mahafali.
 Mkuu wa shule ya msingi Nianjema Bi Anna Ngondya(kushoto) akiwa pamoja na mkuu wa shule ya msingi kizuiani ya mjini Bagamoyo mama Joyce Haule wakati wa chakula cha mchana kwa ajili ya mahafali
 Mshereheshaji wa "After party" mwalimu Maine akila kilauri kwenye kiwanja cha Dolphin Bagamoyo
 Mkuu wa shule ya msingi Nianjema(katikati) akiwa na wadau wakati wa "After party" kushoto ni mhasibu Michael kauruda kwenye kiwanja cha Dolphin Bagamoyo
Mkurugenzi wa gazeti la Sauti huru(kulia) akiteta jambo na mstahiki wakati wa After party iliyofanyika kiwanja cha Dolphin Bagamoyo.

Tuesday, October 12, 2010

MAHAFALI YA SHULE YA MSINGI JITEGEMEE MJINI BAGAMOYO TAREHE 7 OCTOBER 2010

 Mkuu wa shule Jitegemee(mbele kushoto) akiwaongoza walimu wa shule hiyo kukabidhi zawadi kwa mgeni rasmi wa mahafali,Meneja wa benki ya NMB tawi la Bagamoyo bi Elizabeth Chawinga.
 Mkuu wa shule ya msingi Jitegemee Bi Dinna Mjema(kulia) akifurahia maonesho akiwa pamoja na mgeni rasmi Meneja wa benki ya NMB tawi la Bagamoyo bi Elizabeth Chawinga
Mstahiki Kim akijumuika na walimu wa shule ya msingi Jitegemee na wageni wengine kuzungusha mduara kwa agizo la mshereheshaji

Saturday, October 9, 2010

kufanya kampeni kwa kutumia udini na ukabila ni kuhatarisha amani - mama salma kikwete

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete

NA MWANDISHI MAALUMU, KIGOMA

MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, amesema kufanya kampeni kwa kutumia udini na ukabila ni kuhatarisha amani.

Alisema hayo juzi na jana alipozungumza kwa nyakati tofauti na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoani hapa, alipokuwa akiwaombea kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Mama Salma alisema kuwagawa Watanzania kwa misingi ya udini na ukabila ni kutaka kutowesha amani ambayo imedumu nchini kwa miaka mingi.

“Udini na ukabila utatutenganisha, tutahasimiana kwa sababu huyu ni mkristo na yule ni muislamu, haya ni yale yale ya huyu ni Mtutsi na yule ni Mhutu, jamani kina mama huko ndiko tunataka kwenda ?” Alihoji na kujibiwa “hapana”.

Mama Salma alisema, wanachama wa vyama vya siasa wana dini zao, lakini usajili wa vyama hivyo haufanyiki kwa kuangalia dini na kabila, hivyo kufanya kampeni kwa vigezo hivyo ni ukiukaji wa sheria.

Wakati akizungumzia hilo, kina mama hao walikuwa wakimwitikia kwa kusema “sema mama usiogope” kuashiria kuna baadhi ya watu wanafanya kampeni za kibaguzi kwa kutumia udini na ukabila.

Mwenyekiti huyo wa WAMA ambaye ni mke wa mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alitahadharisha kwamba, amani kuvunjika ni rahisi, kuirejesha ni kazi kubwa na mifano ipo katika baadhi ya nchi za Afrika ambazo ziliichezea na haijarejea.

Aliwaambia wananchi wa Kigoma kwamba wao ni mashahidi wa namna nchi jirani zilivyoathirika kutokana na machafuko chanzo kikiwa ni siasa za kibaguzi zilizojiegemeza kwenye udini na ukabila.

Mama Salma aliwaombea kura wagombea ubunge kwa tiketi ya CCM; Injinia Christopher Chiza (Buyungu), Jamal Tamimu (Muhambwe), Daniel Nsanzugwanko (Kasulu Vijijini), Raphael Neka (Kasulu Mjini), Robson Lembo (Kigoma Kaskazini), Peter Serukamba (Kigoma Mjini) na Gulamuhussein Kifu (Kigoma Kusini).

MISS TANZANIA EASTERN ZONE 2009 - TASUBA BAGAMOYO

                                        Vitalis Maembe akifanya vitu vyake kwenye onesho hilo.
 Mkurugenzi wa Kimkev entertainment waandaaji wa Miss eastern zone akisoma neno la kumkaribisha mgeni rasmi.

 Mgeni rasmi bw.Magesa Mulongo mkuu wa wilaya ya Bagamoyo akitoa baraka zake ili onesho liweze kuanza.

 Aliyekuwa mmiliki wa hoteli ya Lindi Oceanic ya mjini Lindi marehemu kanali Fusi (kati)akifuatilia onesho,kushoto mratibu wa Miss Lindi bw.Shah na kulia mjane wa Fusi.

 Warembo wakiwa kwenye  vazi la ufukweni kushoto Tory Oscar kutoka Morogoro na kulia Khadija Amir kutoka Mtwara.

                                     Barnaba na Pipi wakiburudisha kwa wimbo wa Njia panda.

 Mrembo Tory Oscar kutoka Morogoro akiwa kwenye vazi la jioni ,yeye ndiyo aliyekuwa Miss talent katika shindano miss Tanzania 2009.

 Mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania mjomba Makoye akinena jambo,hapa akiwa Jaji mkuu wa shindano hili.

 Top five wakiwa kwenye maswali na majibu kutoka kushoto ni Stawa Simba kutoka Mtwara,Lightness Makaya kutoka Lindi,Gloriablanca Mayowa kutoka Lindi,Tory Oscar kutoka Morogoro na Precious Donald kutoka Pwani.

 Tatu bora kati Gloriablanca Mayowa Miss eastern zone 2009 kutoka Lindi,kulia mshindi wa pili Tory Oscar kutoka Morogoro na kushoto ni  Precious Donald Kutoka Pwani    
                                                                           
                                                                              
MC Mary akisherehesha onesho. kwa wakati huo akiwa mwanachuo wa Tasuba

Thursday, October 7, 2010

FERRE GOLLA AFANYA SHOW DIAMOND JUBILEE

 Madada wakipata picha ya pamoja na Feree Golla
 Ferre akiimba wimbo wa Vita Imana live jukwaani
Mwanamuziki kutoka Demokrasia ya watu wa Congo Ferre Golla amekonga nyoyo za mashabiki baada ya kufanya bonge la show akiwa sambamba na Shikito

Sunday, October 3, 2010

MISS BAGAMOYO 2008 ILIYOANDALIWA NA KAMPUNI YA KIMKEV ENTERTAINMENT KWENYE HOTELI YA KIROMO VIEW RESORT- BAGAMOYO


Mkurugenzi wa Kimkev entertaiment bw.Kim Kimenya(kulia) akiteta jambo na bw.James Nicolaus(kushoto) mmiliki wa hoteli ya Kiromo,  kabla ya shindano la kumtafuta mrembo wa Bagamoyo 2008 kuanza  lililofanyika hotelini hapo,kati ni bw Patrice Kandokando mkuu wa itifaki wa shindano hilo.
 Mwenyekiti wa kamati ya miss bagamoyo 2008 bw. Cosmas Kadenge akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi. 

 Mgeni rasmi wa shindano la kumtafuta mrembo wa Bagamoyo 2008  Mh.Serengo Mrengo(mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kwa wakati huo) akiongea neno la ufunguzi.

 Wanenguaji wa bendi ya Akudo impact wakishambulia jukwaa wakati wa shindano.
 Chaijaba wa Akudo impact wakati huo akifanya vitu vyake wakati wa shindano hilo.
 Top five ya Miss Bagamoyo 2008 wakati wa maswali na majibu kuanzia kushoto Wilhelmina,Rose,Ashura,Zena ,na Jackline.
Baadhi ya majaji wa miss bagamoyo 2008 Ben kinyaiya kulia na Che mundu gwao.
 mkufunzi wa Miss bagamoyo 2008 Neema Chande ambaye pia ni Miss Ruvuma 2007. 
 Tatu bora ya Miss Bagamoyo 2008.


 Miss bagamoyo 2008 Jackline chuwa ambaye pia ni muandaaji wa miss kilimanjaro 2010 akiwa kwenye pozi mara baada ya kutangazwa mshindi.
 Tatu bora ya Miss Bagamoyo kati Jackline Chuwa (mshindi),kulia Zena Mohamed mshindi wa pili na kushoto Ashura Mbwana mshindi wa tatu
 Washindi wa Miss Bagamoyo wakiwa na washabiki wa urembo. 
 Mgeni rasmi akiwa kwenye pozi na Jackline Chuwa na na mama Mrengo. 
 Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kwa wakati huo mh.Serengo Mrengo akimkabidhi zawadi ya sofa seti Jackline Chuwa.
 Mgeni rasmi akimkabidhi mshindi wa nne Wilhelmina zawadi.
 Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya Miss Bagamoyo 2008 na wadau wengine.
 Mmiliki wa Hoteli ya Kiromo bw,James Nicolaus akinena jambo wakati wa shindano.
Mmoja wa majaji wa Miss Bagamoyo 2008 bw. Che mundu gwao (kati) kulia ni Maimatha aliyekuwa MC wa shindano hilo na shoto ni mkufunzi  wa warembo Neema Chande Mohamed.
 Ben na Maimatha  wakibadilishana mawazo na mgeni rasmi wa shindano.
 Mrembo Wilhelmina akiwa kwenye vazi la jioni wakati wa shindano.