Monday, October 13, 2014

STARS YAMSHIKISHA ADABU BENIN KWA KUMCHARAZA MAGOLI 4-1 KAMA VILE WALIKUWA WAMESIMAMA


Ushindi wa leo, utaifanya Tanzania  kupanda katika viwango vya soka dunia kwa kiasi fulani.
Watu wengi walikuwa wakiibeza sana Stars kuelekea katika mchezo wa jana dhidi ya Benin, lakini ndiyo hivyo Wahenga walisema, "mdharau mwiba, mguu huota tende" na ndicho kilichowakuta Wa Benin jana katika dimba la taifa licha ya kusheheni nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya kama vile, Stephane Sesegnon anayekipa kunako West Bromwich Albion. 

Magoli ya Stars yalifungwa na beki Haroub Canavaro, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, pamoja naye Juma Luizio. Goli la kufutia kijasho la Benin Lilifungwa na mshambuliaji Sadel akipokea pasi maridadi kutoka kwake kiungo mshambuliaji, Stephane Sesegnon dakika ya 90 ya mchezo huo.

Ushindi huo ni furaha kubwa kwa watanzania ambao walikuwa wamekata tamaa na timu yao ya taifa iliyopo chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij kufuatia matokeo mabovu ya hivi karibuni katika michuano ya kuwania tiketi za kupangwa katika makundi ya michuano ya AFCON yatakayo fanyika mwakani nchini Moroco..

Sunday, October 12, 2014

SITI MTEMVU NDIYE REDD'S MISS TANZANIA 2014

 

 
Miss Tanzania 2014, Siti Abass Zuberi Mtemvu akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia leo katika shindano lililoshirikisha warembo 30 na kufanyika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Siti Mtemvu ametwaa taji hilo lililokuwa likishikiliwa na Happyness Watimanywa.

Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili,Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu,Jihhan Dimachk mara baada ya kutawazwa rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.
Picha zote na Othman Michuzi.
Redd's Miss Tanzania aliyemaliza muda wake,Happiness Watimanywa akimpisha crown,Redd's Miss Tanzania wa sasa,Sitti Mtemvu.














































Wednesday, October 8, 2014

RAIS DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE APOKEA RASIMU YA MWISHO YA KATIBA INAYOPENDE​KEZWA OKTOBA 08,2014 – UWANJA WA JAMHURI DODOMA

 

 Mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba Mhe.Samuel Sitta akikabidhi rasimu ya katiba inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.1mohamed Ali Shein katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
Rais jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Alli Mohamed Shein wakionesha Katiba hiyo iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Mabadiliko ya Katiba.

MFUMUKO WA BEI NCHINI WAPUNGUA.

Thursday, October 2, 2014

Timu ya mpira wa pete Ikulu yawapa kichapo Ukaguzi


  Wachezaji wa timu ya mpira wa pete ya Ikulu wakiwa wamejipanga tayari kuanza mechi yao dhidi ya timu ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali uliochezwa jana uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Mchezaji wa timu ya Ikulu Monica Kassy akiwa katika harakati za kuwania mpira katika mechi yao dhidi ya Ukaguzi jana katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.


              Baadhi   viongozi wa benchi la ufundi la timu ya Ikulu.



Baadhi ya wanamichezo wa timu ya Ikulu wakiishangilia na wakishudia timu yao ikiwasasambua vilivyo timu ya  ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa kuwafunga magoli 48 kwa 13 jana mjini Morogoro.
 

(Picha zote na Eleuteri Mangi –MAELEZO



Na Eleuteri Mangi –MAELEZO

01/10/2014

Timu ya mpira wa pete ya Ikulu imeendeleza kichapo kwa timu pinzani inyokutana nazo katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.

Ikiwa imekamilika katika idara zote, timu ya Ikulu imetakata vilivyo kwa kuwafunga Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa magoli 48 kwa 13.

Ushindi huo umekuja baada ya safu ushambuliaji kutekeleza wajibu wao vilivyo wakiongozwa na Monica Kassy anayechezea nafasi ya (GS) wakati nafasi (GA) amecheza Irene Elias na nafasi ya (WA) Mwadawa Twalibu ameitendea haki ambapo timu yake imefanikiwa kuibuka kwa ushindi huo mnono.

Kiungo mchezeshaji wa timu ya Ikulu Sophia Komba (C) aliipanga vilivyo timu yake na kuhakikisha timu inaelewana na klucheza kwa umahiri mkubwa mbele ya wapinzani wao timu ya Ukaguzi ambao hawakufurukuta vipindi vyote viwili vya mchezo ambapo kipindi cha kwanza hadi mapumziko Ikulu walikuwa wanaongoza kwa magoli 25 kwa 05 dhidi ya Ukaguzi.

Safu kamili inayounda kikosi cha mpira wa pete kinawajumuisha wachezaji saba na wawili wakiwa wachezaji wa akiba.

Wacheazji hao ni Monica Kassy (GS), Irene Elias (GA), Mwadawa Twalibu (WA), Sophia Komba (C), Paskalia Kibayasa (WD), Lilian Syilidion (GD) na Tatu Kalembo (GK).

Wachezaji wengine wa akiba katika mchezo huo walikuwa Jenifer Mwandupe na Nyamaina Magesa.

Mashindano ya SHIMIWI mwaka huu yanachezwa kwa mara ya 34 tangu kuasisiwa kwake na mkoa wa Morogoro umeepewa heshima ya kuandaa mashindano hayo kwa mara nyingine ambapo iliwahi kuandaa mashindano hayo mwaka 2009, 2012 na 2014.