Wachezaji wa timu ya mpira wa pete ya Ikulu wakiwa wamejipanga tayari kuanza mechi yao dhidi ya timu ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali uliochezwa jana uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mchezaji wa timu ya Ikulu Monica Kassy akiwa katika harakati za kuwania mpira katika mechi yao dhidi ya Ukaguzi jana katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Baadhi viongozi wa benchi la ufundi la timu ya Ikulu.
Baadhi ya wanamichezo wa timu ya Ikulu wakiishangilia na wakishudia timu yao ikiwasasambua vilivyo timu ya ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa kuwafunga magoli 48 kwa 13 jana mjini Morogoro.
(Picha
zote na Eleuteri Mangi –MAELEZO
Na Eleuteri Mangi
–MAELEZO
01/10/2014
Timu ya mpira wa pete
ya Ikulu imeendeleza kichapo kwa timu pinzani inyokutana nazo katika mashindano
ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.
Ikiwa imekamilika katika
idara zote, timu ya Ikulu imetakata vilivyo kwa kuwafunga Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa magoli 48 kwa 13.
Ushindi huo umekuja
baada ya safu ushambuliaji kutekeleza wajibu wao vilivyo wakiongozwa na Monica
Kassy anayechezea nafasi ya (GS) wakati nafasi (GA) amecheza Irene Elias na
nafasi ya (WA) Mwadawa Twalibu ameitendea haki ambapo timu yake imefanikiwa
kuibuka kwa ushindi huo mnono.
Kiungo mchezeshaji wa
timu ya Ikulu Sophia Komba (C) aliipanga vilivyo timu yake na kuhakikisha timu
inaelewana na klucheza kwa umahiri mkubwa mbele ya wapinzani wao timu ya
Ukaguzi ambao hawakufurukuta vipindi vyote viwili vya mchezo ambapo kipindi cha
kwanza hadi mapumziko Ikulu walikuwa wanaongoza kwa magoli 25 kwa 05 dhidi ya
Ukaguzi.
Safu kamili inayounda
kikosi cha mpira wa pete kinawajumuisha wachezaji saba na wawili wakiwa
wachezaji wa akiba.
Wacheazji hao ni Monica
Kassy (GS), Irene Elias (GA), Mwadawa Twalibu (WA), Sophia Komba (C), Paskalia
Kibayasa (WD), Lilian Syilidion (GD) na Tatu Kalembo (GK).
Wachezaji wengine wa
akiba katika mchezo huo walikuwa Jenifer Mwandupe na Nyamaina Magesa.
Mashindano ya SHIMIWI
mwaka huu yanachezwa kwa mara ya 34 tangu kuasisiwa kwake na mkoa wa Morogoro
umeepewa heshima ya kuandaa mashindano hayo kwa mara nyingine ambapo iliwahi
kuandaa mashindano hayo mwaka 2009, 2012 na 2014.
No comments:
Post a Comment