Washiriki wa kitongoji Kanda ya
kaskazini, Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja,
tayari kuchuana vikali Mei 5, 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura
Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.katika shindano hilo
kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti
vya kawaida ni sh 15,000/=
Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.
---
Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya
kitongoji Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012,yanatarajiwa
kufanyika Mei 5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel
iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.
Akizungumza leo jijini Arusha,Mratibu wa
shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka kampuni ya Tour Visual
Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, amebainisha kuwa
mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na kila kitu kimekwisha
kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo ambao mpaka sasa
wametimia 20.
Bi. Upendo Simwita amesema kuwa
wameishakamilisha mchakato wa kuwapata Warembo wenye mvuto na wenye
vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo hao wenye ari kubwa ya
ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa Miss Tanzania 2012
anatokea kwenye kitongoji hicho.
“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti
kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20, ambao
watachuana vikali jukwaani, na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha
City Center”, alisema Upendo. Amesema kuwa kiingilia katika shindano
hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh 25,000/= na kwa viti vya
kawaida sh.15,000/=
Kwa upande wa Burudani,Upendo amesema
kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam
wa Ukweli, Muziki wa Asili, Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na
burudani nyingine mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku
hiyo.
No comments:
Post a Comment