Bendi maarufu ya muziki jijini Dar es salaam ya African Stars "Twanga pepeta" inatarajia kufanya onesho lake la mwanzo wa juma siku ya Ijumaa tahehe 16.06.2011 katika ukumbi wa Massae gardaen view uliopo Kawe Tanganyika peckers.
Kwa mujibu wa mratibu wa onesho hilo bw. Albert Kawogo,onesho hilo linatarajiwa kuanza saa 3.00 usiku ambapo kiingilio kitakuwa 5000/=.
Kawogo amewataka mashabiki wa Twanga pepeta kujitokeza kwa wingi hasa wakazi wa kawe na maeneo ya jirani kwa kuwa hilo ni onesho maalum kwa wakazi wa maeneo hayo ambao huifuata bendi hiyo maeneo mengine.
Ninawahakikishia wapenzi wa burudani ya muziki kuwa kutakuwa na burudani ya kutosha na usalama wa kutosha hivyo waianzie wikiendi yao Kawe kwa kusugua kisigino ,alisema Kawogo.
Blog ya kimkeventertainment inawatakia msuguo mwema.