Tuesday, June 14, 2011

TWANGA PEPETA KUSHAMBULIA KAWE

                     

Bendi  maarufu ya muziki  jijini Dar es salaam ya African Stars "Twanga pepeta" inatarajia kufanya onesho lake la mwanzo wa juma siku ya Ijumaa tahehe 16.06.2011  katika ukumbi wa Massae gardaen view uliopo Kawe  Tanganyika peckers.

Kwa mujibu wa mratibu wa onesho hilo bw. Albert Kawogo,onesho hilo linatarajiwa kuanza saa 3.00 usiku ambapo kiingilio kitakuwa  5000/=.

Kawogo amewataka mashabiki wa Twanga pepeta  kujitokeza kwa wingi hasa wakazi wa kawe na maeneo ya jirani kwa kuwa hilo ni onesho maalum kwa wakazi wa maeneo hayo ambao huifuata bendi hiyo maeneo mengine.

Ninawahakikishia wapenzi wa burudani ya muziki kuwa  kutakuwa na burudani ya kutosha na usalama wa kutosha hivyo waianzie wikiendi yao Kawe kwa kusugua kisigino ,alisema Kawogo.

Blog ya kimkeventertainment inawatakia msuguo mwema. 

No comments:

Post a Comment