Monday, September 9, 2013

BALAA LA MADAWA YA KULEVYA... RIPOTI MPYA!

BALAA  LA MADAWA YA KULEVYA... RIPOTI MPYA!

 
Na Waandishi Wetu

SAKATA la madawa ya kulevya kusafirishwa nje au kuingizwa nchini na
kuwafikia vijana wanaoharibika kila kukicha, limezidi kuchukua nafasi ya
kipekee baada ya ripoti mpya kabisa kutoka juzi,
 Ijumaa Wikienda limesheheni mambo.
 
Kwa wiki iliyopita, Ijumaa Wikienda lilipekenyua maeneo yote muhimu
kukumbana na mambo mapya kuhusu habari za ‘unga’ huku taarifa
zikionesha kuwa, hali katika viwanja vye ndege duniani kote ni tete.… 

Kwa wiki iliyopita, Ijumaa Wikienda lilipekenyua maeneo yote muhimu na kukumbana na mambo mapya kuhusu habari za ‘unga’ huku taarifa zikionesha kuwa, hali katika viwanja vye ndege duniani kote ni tete.
 
Madawa ya kulevya.
MNIGERIA ALIYEKAMATWA NA ‘UNGA’ ALITAHADHARISHWA MAGOMENI
Anthonie Ojo, raia wa Nigeria aliyekamatwa Septemba 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar (JNIA), akijaribu kusafirisha kete 99 za unga na ndege ya Shirika la Ethiopian Airways alinaswa.
Mwanamke huyo aliyevalia baibui akidai anakwenda kuhiji Maka, anadaiwa aliununua mzigo huo Magomeni-Mapipa jijini Dar. Aliziweka kete hizo kwenye makopo yaliyokuwa na poda ya Johnson.
 
Mnigeria Anthonie Ojo (25) aliyekamatwa na dawa za kulevya wenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, wenyeji waliomuuzia unga mwanamke huyo walimtahadharisha kuhusu hali ya ulinzi iliyopo sasa JNIA hasa baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kushikia bango udhibiti wa unga lakini mtuhumiwa huyo alidaiwa kusema atapita kwa anavyojua yeye.
MTANZANIA AFA DUBAI AKIWA NA UNGA TUMBONI
Ukiachilia mbali tukio la mwanamke huyo, habari zilizolifikia gazeti hili juzi zilidai kwamba Mbongo aliyejulikana kwa jina moja la Chambuso amefariki dunia katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kutokana na unga alioubeba tumboni kuyeyuka kabla ya kufika kwenye kituo husika.
Habari za uhakika kutoka chanzo chetu jijini Dar zinasema kuwa marehemu Chambuso alikuwa na ‘mlinzi’ wake ndani ya Ndege ya Emirate huku akiwa hamjui.
 
Masogange.
Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kushuka jijini Dubai, hali ya Chambuso ilianza kubadilika akilalamikia zaidi maumivu ya tumbo, ndipo ‘mlinzi’ huyo alipombeba na kumpeleka hospitali (haikutajwa jina).
“Baada ya kufariki dunia, jamaa (mlinzi) alijiweka mbele akitaka kufanya maarifa kwa madaktari ili tumbo la jamaa lipasuliwe atoe mzigo. Akashtukiwa, akakimbia na mpaka sasa maiti hiyo iko chini ya ulinzi wa serikali,” kilisema chanzo.
Tuachane na kifo cha Chambuso huko Dubai. Septemba 2, mwaka huu zilitufikia taarifa kwamba, mchumba wa mwigizaji Pendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’ aliyejulikana kwa jina moja la Tasha amedakwa na unga nchini China.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tasha alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing nchini humo akiwa na unga aina ya heroin (kiasi na thamani hakikutajwa).
 
Melisa.
Ili kupata uhakika wa madai hayo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta Pendo kwa njia ya simu ya mkononi na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri.
“Yeah, ishu ni kweli. Mimi nilizipata hizo taarifa kutoka kule nikawaambia ndugu zake. Kwa mujibu wa mtu wake aliyekuwa naye kule (China) jamaa (Tasha) ameshapandishwa kortini,” alisema Pendo huku akisema uchumba wake na Tasha ulishakufa.
AISHA BUI ETI KAFUNGWA BRAZIL!
Wiki mbili sasa, mapaparazi wa Global Publishers wamekuwa wakifuatilia kwa undani kuhusu kusambaa kwa madai kwamba, staa wa filamu za Kibongo, Aisha Bui eti kafungwa miaka 5 jela katika gereza moja nchini Brazil baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye kibegi.
Pendo akiwa na mchumba wake.
Kwa mujibu wa madai ya habari hizo, eti Aisha alidakwa kwenye uwanja wa ndege wa jijini Brasilia akirejea Bongo kupitia Dubai.
Septemba 2 na 5, mwaka huu, waandishi wetu walifika nyumbani kwa baba wa Aisha, Kigamboni, Dar kutaka kujua ukweli.
Septemba 2, mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema Aisha yupo Brazil lakini hakuna mawasiliano naye na alikwenda siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Julai mwaka huu.
Septemba 5, hakukutwa mtu ila majirani walielekeza eneo analopatikana mzee huyo ambapo ni ufukweni. Hata hivyo, sehemu hiyo hakupatikana na waandiishi waliacha namba zao za simu.
Jioni, mzee Bui alizipata namba zilizoachwa, saa 9:00 usiku wa kuamkia Septemba 6 alimpigia simu mwandishi wetu na kumvurumishia matusi huku akisema akome kumfuatafuata akidai yeye hana mawasiliano na binti yake tangu mwaka 2007.
Mzee huyo alikwenda mbele zaidi kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwenye simu ya paparazi akitumia lugha ya Kiarabu ambapo kwa mujibu wa wataalam wa lugha hiyo ni dua ya kumwombea mabaya mwandishi huyo.
NZOWA AMZUNGUMZIA
Ili kwenda mbele zaidi, mapaparazi wetu walikwenda ofisini kwa Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ili kutaka kujua kama amesikia lolote kuhusu Aisha Bui.
Alisema: Eee, kuna habari kama hiyo lakini si rasmi kwangu, bado nafuatilia Brazil ikiwa tayari nitawajulisha tu.
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Aisha kwenye mitandao, hasa Facebook, Instagram na Twitter bila mafanikio. Gazeti hili limemwachia ujumbe kwa kuamini kwamba akirudi hewani ataukuta na kujibu lakini wapi!
Mbwana Matumla.
UZUSHI WA MBWANA MATUMLA KUNASWA NA UNGA HISPANIA WAWASHANGAZA WENGI
Wiki iliyopita ilihitimika kwa redio moja kutangaza habari kwamba mmoja wa wanafamilia ya mzee Matumla, Mbwana Matumla amenaswa na unga nchini Hispania na kuwashangaza wengi.
Watu waliozungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki walisema kwamba walishangaa kusikia habari hiyo huku wakiwa wanamwona Mbwana mitaani.
“Sasa huyu kakamatwa Hispania huku tukiwa tunamwona mitaani, maana yake nini jamani? Alihoji msomaji wetu mmoja na kuongeza kwamba, yeye alikutana na bondia huyo siku tano nyuma.
Ijumaa Wikienda lilimsaka Mbwana kwa njia ya simu yake ya mkononi bila mafanikio, lakini lilipomtafuta kaka mtu, Rashid Matumla, Jumamosi iliyopita alisema Mbwana amejaa tele nyumbani kwake, Gongo la Mboto, Dar.
Imeandikwa na Shakoor Jongo, Hamida Hassan, Gladness Mallya, Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’.  

CHANZO; GLOBAL PUBLISHERS.

Saturday, September 7, 2013

TAMASHA LA 'MTAKUJA' SEPT 14


Usikose tamasha la “Mtakuja” kwa Wanafunzi Jumamosi, Septemba 14

 Picture
Baada ya muda mrefu kupita bila kuwa na tamasha lolote la wanafunzi hasa wa shule za Sekondari, uongozi wa Mtakuja Secondary School ya Kunduchi kwa kushirikiana na mtangazaji maarufu Allan Lucky 'Rais wa Wanafunzi' wa kipindi maarufu cha Skonga ambacho hurushwa kupitia televisheni ya vijana ya EATV umeandaa tamasha la wanafunzi linalotarajiwa kuhudhuriwa na wanafunzi zaidi ya 3,000 kutoka katika shule zaidi ya 20 za jijini Dar-es-Salaam.

Tamasha hilo lenye lengo la kuwakutanisha wanafunzi wa shule mbali mbali za Dar-es-Salaam kwa pamoja na kupata changamoto kimawazo na kiburudani, pia kuwakutanisha wadau mbalimbali wa elimu katika
kufanikisha uboreshwaji wa elimu na kusaidia katika kutekeleza mpango wa 'Matokeo Makubwa Sasa', linatarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo tarehe 14/09/2013 katika viwanja vya shule hiyo.

Miongoni mwa shule ambazo zitashiriki ni: Mtakuja, Kondo, Jordan, St. Gasper, Mbezi Beach, Boko, Goba, Twiga, Maendeleo, Mwambao, Kisauke, Kinzudi, londa, Makongo, Kawe Ukwamani, Tegeta, Mbweni, Teta, Hananasif na Mtongani, zote ni za sekondari.

Tamasha hilo linatarajiwa kuhusisha wadau mbali mbali wa elimu watakaokutana katika kubadilishana mawazo na kupata burudani kwa kushuhudia vipaji lukuki walivyo navyo wanafunzi kutoka shule mbali mbali.

Miongoni mwa shughuli zitakazoendeshwa ni pamoja na maswali na majibu, fashion show, uimbaji, ufokaji, na wanafunzi wenye vipaji mbali mbali maalum watapewa nafasi.

Msemaji wa tamasha hilo ambaye pia ni mwalimu wa michezo wa Mtakuja Beach Sekondari Bw Misonji Charles amewataka wadau mbali mbali wa elimu kuhudhuria na kushuhudia vipaji vya wanafunzi mbali mbali na pia amewataka waandishi wa habari kujitokeza kwa wingi katika kuchukua habari na matukio mbali mbali yatakayojitokeza. Pia amewaomba wadau mbali mbali wenye uwezo wa kuchangia katika kufanikisha tamasha hili wajitokeze, kwa kuwa linaandaliwa kwa nguvu za shule na kamati maalum ya maandalizi pekee.

Kwa maelezo na kama unataka kushiriki, tafadhali wasiliana na Msemaji wa Tamsha Bw Misonji Charles kupitia 0714642442

MWALIKO WA TAMASHA LA 32 LA SANAA TaSUBA 2013


Mwaliko wa Tamasha la 32 la Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania, Bagamoyo
 Picture              Picture      
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBa)

TAMASHA LA 32 LA SANAA NA UTAMADUNI WA MTANZANIA BAGAMOYO KUANZIA TAREHE 23 – 28 SEPTEMBA 2013
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo imekuwa na utaratibu wa kuandaa Tamasha la Sanaa na Utamaduni kila mwaka. TaSUBa ikishirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wanakuletea Tamasha la 32 la Sanaa na Utamaduni na litaadhimishwa kuanzia tarehe 23 – 28 Septemba hapa Bagamoyo. Tamasha
litafunguliwa tarehe 23 Septemba kuanzia saa 3:00 asubuhi na kufungwa tarehe 28 Septemba.

Kati ya shughuli zitakazofanyika ni pamoja na maonesho ya sanaa za jukwaani (Muziki, Ngoma, Maigizo, Vichekesho, Sarakasi n.k), maonesho ya sanaa za ufundi, warsha, semina na mafunzo mbalimbali kwa siku zote za tamasha pamoja na kongamano litakalojadili kaulimbiu Sanaa na Utamaduni katika kukuza Utalii .

Tamasha hili la kimataifa la sanaa na utamaduni wa Mtanzania ambalo linategemea kukusanya wasanii, wadau na watazamaji wapatao 3,500 kwa siku kutoka sehemu mbalimbali za ndani ya nchi pamoja na nchi za nje.

Hivyo tunawakaribisha wasanii, vikundi vya sanaa, ofisi za balozi, wadau katika sekta ya Sanaa, Utamaduni na Utalii, wananchi wote kwa ujumla, taasisi na mashirika mbalimbali kuhudhuria na kushiriki katika Tamasha hili.

KARIBUNI SANA.

Kwa mawasiliano zaidi;
Mtendaji Mkuu,
TaSUBa,
S.L.P 32
BAGAMOYO

Email: taasisisanaa@yahoo.com
   
Au piga Simu;

0715472745
0655850405
0754310425
0712683408

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/09/mwaliko-wa-tamasha-la-32-la-sanaa-na-utamaduni-wa-mtanzania-bagamoyo.html#i

Fuse ODG kuicheza style ya Azonto leo Dar



Mkali wa Azonto na Antenna Nana Richard Abiona aka Fuse ODG anatarajiwa kutoa burudani kali siku ya leo katika viwanja vya Ustawi Jamii.
Katika burudani hiyo 'Fuse ODG' atasindizwa na wasanii mbalimbali wa hapa Tanzania wakiwemo,Wakazi,Vanessa Mdee,Gosby,Janjaro,Deddy,Menina,Wakali Dancers,Madee na wengine kibao.
Ticket zinapatikana katika vituo mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam
 Kwa shilingi 10000/=
 1.Zizzo Fashion-Africa Sana
 2.Nyumbani Lounge
 3.TCC Club-Chang'ombe
 4.Dar Live
 5.Samaki Mlimani City
 6.Zantel Makao Makuu
 7.Coco Beach
 8.Zantel Ilala
 9.Jay Hustle Unique
Mlangoni ni shilingi 15000

AZONTO KULINDIMA DAR LEO






Nana Richard Abiona aka Fuse ODG ( Pichani kulia) ...Hitmaker huyo wa 'Azonto na Antenna' Fuse ODG ambaye anatarajiwa kutoa burudani nzuri siku ya leo katika viwanja vya Ustawi wa Jamii alisema ikiwa ni mara yake ya kwanza kutoa burudani hapa Tanzania basi aahidi kuwasha moto mkubwa wa AZONTO..

Burudani hiyo inatarajiwa kuanza saa mbili usiku hadi majogoo kwa kiingilio cha Shilingi elfu kumi kwa kununua ticket kabla na elfu kumi na tano wataonunua ticketi mlangoni.
Fuse ODG atasindizwa na wasanii wengi wakiwemo,Wakazi,Banana Zorro,H Baba,Wakali Dancer, Menina, Dojo Janja, B Hit's Music Group, Madee na wengine kibao.

WABUNGE WATWANGANA NGUMI

WANAUSALAMA WA BUNGE WAKIWA WAMEMDHIBITI MHE SUGU.

UKUMBI wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, jana uligeuka ulingo wa masumbwi, baada ya wabunge wa kambi ya upinzani kupigana hadharani na askari wa Bunge.


Wabunge hao walichapana ndani na nje ya ukumbi, hali iliyosababisha tafrani kubwa, huku maofisa usalama na askari polisi kutoka kituo kikuu mjini Dodoma, wakilazimika kuitwa kwenda kuongeza nguvu ili kukabiliana na hali hiyo.

Hatua ya vurugu hizo, ilikuja baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kunyanyuka ili kutaka kutoa hoja, ambapo Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alimtaka kukaa chini hali iliyowafanya wabunge wote wa upinzani kunyanyuka wakiashiria kumuunga mkono.

Mbowe, alisimama bungeni baada ya kutangazwa matokeo ya kutaka kuendelea na hoja iliyotolewa na Mbunge wa Mkoani, Ali Khamis Seif (CUF), kuomba mwongozo wa Spika wa kutaka Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, uahirishwe hadi pale yatakapopatikana maoni ya wadau kwa upande wa Zanzibar.


Hoja hiyo, ilionekana kuwa mwiba mkali, baada ya Seif pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu kutoa taarifa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, Pindi Chana (CCM), kuwa amelidanganya Bunge kwa kutoa taarifa ya uongo.

Baada ya hoja hizo, Naibu Spika Ndugai, aliamuru kupigwa kura za kutaka kuendelea na mjadala huo ambapo wabunge 157 wakitaka kuendelea na mjadala huo, huku 59 wa kambi ya upinzani wakitaka usiendelee.

“Baada ya kutangazwa kwa matokeo haya ya kuamua kuendelea na mjadala ama laa kama alivyowasilisha mheshimiwa Ali, sitataka kupokea taarifa yoyote.

“Ninachotaka kuwahakikishia kiti changu kinatenda haki kwa kila upande wa vyama humu ndani, ila ninachotaka kusema hakilali kitu hapa,” alisema Ndugai.

Wakati Ndugai, akiwa amemtaka mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP), ili aweze kuendelea na hoja hiyo ndipo aliposimama Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akitaka kutoa taarifa huku Naibu Spika akimzuia kwa kumtaka akae chini hali iliyowafanya wabunge wote wa upinzani kunyanyuka ndani ya Bunge kama njia ya kupinga hali hiyo.

Wabunge hao waliosimama ni wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, hali iliyomfanya Naibu Spika Ndugai kutoa amri kwa askari wa Bunge kumtoa nje Mbowe.

Agizo hilo la Ndugai liliibua hisia kutoka kwa wabunge wa vyama hivyo na kwenda karibu na kiti cha Mbowe kama njia ya kumlinda ili asiweze kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge na askari hao kama ilivyoamuriwa.

Mvutano huo, ulioanza saa 6:35 mchana hadi saa 7 mchana, ilimlazimu Ndugai kutoa agizo tena mara ya pili kwakumtaka kiongozi wa askari hao kutekeleza agizo hilo kwa kumtoa nje Mbowe.

WANAUSALAMA WA BUNGE WAKIWA WAMEMUANGUSHA CHINI MHE SUGU KATIKA HARAKATI ZA KUMDHIBITI
                                            ***
Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anadaiwa kumpiga kichwa Askari wa Bunge na kumchania sare na kung’oa kipaza sauti.
Mbilinyi jana alisema alikuwa anatafutwa na polisi huku akisema hilo limemshangaza akidai kwamba yeye ndiye aliyeshambuliwa na askari huyo.
                                            ***

Mbowe alisema wameamua kususia majadiliano hayo kuonyesha msimamo wao wa kupinga kupitisha mambo yasiyo na masilahi kwa nchi.
Mnyaa alisema kitendo cha wadau wa Zanzibar kutoshirikishwa katika kutoa maoni yao katika muswada huo wa marekebisho ni dharau kubwa.

Mbatia alisema Tanzania haiwezi kuingia Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kutumia Katiba ya sasa kwa sababu tayari kuna mgongano wa kikatiba kati ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alimtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kutoa ushahidi kama Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kulingana na mapendekezo ya taasisi zao.

 UKITAKA UTATOKA USIPOTAKA UTATOKA TU,NDIVYO WANAVYOONEKANA WAKISEMA WANAUSALAMA WA BUNGE WAKATI WAKIMTOA NJE KINGUVU MHE SUGU BAADA YA KUKAIDI AMRI YA NAIBU WA SPIKA WA BUNGE.

DUNIA IMEISHA...ATAFUNWA USO



 

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Susuluka (16) anadaiwa kujeruhiwa vibaya usoni na bosi wake, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa ng’atwa usoni na kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje, kama ambavyo anaonekana pichani ukurasa wa mbele.


Tukio hilo ambalo tunaweza kulifananisha na dunia kuelekea kufika mwisho, limegusa hisia za watu wengi hasa wakazi wa Kibondo, huku wengine wakitokwa na machozi kutokana na kuguswa na ukatili ambao amefanyiwa kijana huyo.Tunaweza kufikiria kuwa tukio hilo ni sinema, lakini Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamotto, ameliambia Majira kuwa tukio hilo limetokea miezi miwili iliyopita. 
 

Akizungumza katika mahojiano maalumu, Mwamotto, alisema kuwa kabla ya kijana huyo kujeruhiwa na bosi wake, alimtuma dukani ili akamnunulie soda.Alisema kuwa baada ya kufika nyumbani alimkuta bosi wake akiwa amemkaba koo mbwa na kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata mbwa huyo, alianza kuhema akitoa ulimi nje. 
 

DC Mwamotto alisema kuwa mtuhumiwa huyo ghafla alianza kuung’ata ulimi wa mbwa na kisha kumeza vipande jambo lililosababisha mbwa huyo kupiga kelele kutokana na maumivu.Aliongeza kuwa aliendelea kula vipande vya ulimi huo wa mbwa hadi alipoumaliza. 
 

“Unaweza kusema kuwa ni uongo, lakini ni tukio la kweli kabisa kwani mshtakiwa huyo aliendelea kula ulimi wote wa mbwa, huku kijana huyo akiendelea kumshangaa bosi wake kutokana na kitendo hicho kilichosababisha mbwa huyo kufa,”Wakati akiendelea kumshangaa bosi wake ghafla alimrukia na kumkamata kwa nguvu na kuanza kumng’ata kama mtu anayetafuna hindi la kuchoma. 
 

“Mshtakiwa huyo alianza kumtafuna jicho moja na kufuatia jicho la pili na kisha kumeza vipande vya macho huku akiendelea kumshika kwa nguvu,” alisema DC

Baada ya kumaliza kitendo hicho alisema kuwa mshtakiwa huyo alianza kumng’ata pua na kisha kumeza na vipande. 

Alisema kuwa wakati anaendelea na kitendo hicho majeruhi huyo alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada, lakini mshtakiwa huyo alianza kumng’ata tena kipande cha mdomo wa chini na kisha kusababisha meno kubaki nje.“Kutokana na kelele hizo wananchi waliamua kusogea karibu, lakini walikuta tayari, Susuluka amejeruhiwa vibaya usoni huku damu zikimtoka kwa wingi,” alisema. 
 

Mwamotto alisema kuwa kutokana na hali hiyo wananchi walimvamia na kumpiga na kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Kibondo na majeruhi walimkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo. 

Mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya na kufunguliwa mashtaka ya kudhulu mwili.“Hivi sasa mshtakiwa yupo katika Gereza la Nyamisivi Kibondo, lakini cha kusikitisha tena akiwa huko alimng’ata na kula vipande vya nyama vya mguu mshtakiwa mwenzake,” alisema. 
 

Alisema kuwa mshtakiwa mwenzake alimjeruhi vibaya na kupelekwa hospitalini hali iliyosababisha mshtakiwa huyo kutengwa na washtakiwa wenzake.“Mimi nimelazimika kwenda hadi gerezani na kufanya mahojiano na mshtakiwa huyu, kwani hili tukio linasikitisha sana lakini cha ajabu alitaka kufahamu je ameshtakiwa kwa makosa gani ya kuua mbwa au kumng’ata mtu,” alisema. 
 
Alisema kuwa pia amelazimika kwenda kumjulia hali majeruhi huyo ambapo madaktari katika hospitali hiyo walishindwa kumtibia.“Nimeomba msaada kutoka Wizara ya Afya ili mgonjwa huyu akatibiwe India na tayari maandalizi yameanza kufanyika kwa kushirikiana na Hospitali ya Kibondo,” alisema.

Habari na vyanzo mbalimbali vya habari nchini...