Monday, September 9, 2013

BALAA LA MADAWA YA KULEVYA... RIPOTI MPYA!

BALAA  LA MADAWA YA KULEVYA... RIPOTI MPYA!

 
Na Waandishi Wetu

SAKATA la madawa ya kulevya kusafirishwa nje au kuingizwa nchini na
kuwafikia vijana wanaoharibika kila kukicha, limezidi kuchukua nafasi ya
kipekee baada ya ripoti mpya kabisa kutoka juzi,
 Ijumaa Wikienda limesheheni mambo.
 
Kwa wiki iliyopita, Ijumaa Wikienda lilipekenyua maeneo yote muhimu
kukumbana na mambo mapya kuhusu habari za ‘unga’ huku taarifa
zikionesha kuwa, hali katika viwanja vye ndege duniani kote ni tete.… 

Kwa wiki iliyopita, Ijumaa Wikienda lilipekenyua maeneo yote muhimu na kukumbana na mambo mapya kuhusu habari za ‘unga’ huku taarifa zikionesha kuwa, hali katika viwanja vye ndege duniani kote ni tete.
 
Madawa ya kulevya.
MNIGERIA ALIYEKAMATWA NA ‘UNGA’ ALITAHADHARISHWA MAGOMENI
Anthonie Ojo, raia wa Nigeria aliyekamatwa Septemba 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar (JNIA), akijaribu kusafirisha kete 99 za unga na ndege ya Shirika la Ethiopian Airways alinaswa.
Mwanamke huyo aliyevalia baibui akidai anakwenda kuhiji Maka, anadaiwa aliununua mzigo huo Magomeni-Mapipa jijini Dar. Aliziweka kete hizo kwenye makopo yaliyokuwa na poda ya Johnson.
 
Mnigeria Anthonie Ojo (25) aliyekamatwa na dawa za kulevya wenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, wenyeji waliomuuzia unga mwanamke huyo walimtahadharisha kuhusu hali ya ulinzi iliyopo sasa JNIA hasa baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kushikia bango udhibiti wa unga lakini mtuhumiwa huyo alidaiwa kusema atapita kwa anavyojua yeye.
MTANZANIA AFA DUBAI AKIWA NA UNGA TUMBONI
Ukiachilia mbali tukio la mwanamke huyo, habari zilizolifikia gazeti hili juzi zilidai kwamba Mbongo aliyejulikana kwa jina moja la Chambuso amefariki dunia katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kutokana na unga alioubeba tumboni kuyeyuka kabla ya kufika kwenye kituo husika.
Habari za uhakika kutoka chanzo chetu jijini Dar zinasema kuwa marehemu Chambuso alikuwa na ‘mlinzi’ wake ndani ya Ndege ya Emirate huku akiwa hamjui.
 
Masogange.
Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kushuka jijini Dubai, hali ya Chambuso ilianza kubadilika akilalamikia zaidi maumivu ya tumbo, ndipo ‘mlinzi’ huyo alipombeba na kumpeleka hospitali (haikutajwa jina).
“Baada ya kufariki dunia, jamaa (mlinzi) alijiweka mbele akitaka kufanya maarifa kwa madaktari ili tumbo la jamaa lipasuliwe atoe mzigo. Akashtukiwa, akakimbia na mpaka sasa maiti hiyo iko chini ya ulinzi wa serikali,” kilisema chanzo.
Tuachane na kifo cha Chambuso huko Dubai. Septemba 2, mwaka huu zilitufikia taarifa kwamba, mchumba wa mwigizaji Pendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’ aliyejulikana kwa jina moja la Tasha amedakwa na unga nchini China.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tasha alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing nchini humo akiwa na unga aina ya heroin (kiasi na thamani hakikutajwa).
 
Melisa.
Ili kupata uhakika wa madai hayo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta Pendo kwa njia ya simu ya mkononi na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri.
“Yeah, ishu ni kweli. Mimi nilizipata hizo taarifa kutoka kule nikawaambia ndugu zake. Kwa mujibu wa mtu wake aliyekuwa naye kule (China) jamaa (Tasha) ameshapandishwa kortini,” alisema Pendo huku akisema uchumba wake na Tasha ulishakufa.
AISHA BUI ETI KAFUNGWA BRAZIL!
Wiki mbili sasa, mapaparazi wa Global Publishers wamekuwa wakifuatilia kwa undani kuhusu kusambaa kwa madai kwamba, staa wa filamu za Kibongo, Aisha Bui eti kafungwa miaka 5 jela katika gereza moja nchini Brazil baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye kibegi.
Pendo akiwa na mchumba wake.
Kwa mujibu wa madai ya habari hizo, eti Aisha alidakwa kwenye uwanja wa ndege wa jijini Brasilia akirejea Bongo kupitia Dubai.
Septemba 2 na 5, mwaka huu, waandishi wetu walifika nyumbani kwa baba wa Aisha, Kigamboni, Dar kutaka kujua ukweli.
Septemba 2, mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema Aisha yupo Brazil lakini hakuna mawasiliano naye na alikwenda siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Julai mwaka huu.
Septemba 5, hakukutwa mtu ila majirani walielekeza eneo analopatikana mzee huyo ambapo ni ufukweni. Hata hivyo, sehemu hiyo hakupatikana na waandiishi waliacha namba zao za simu.
Jioni, mzee Bui alizipata namba zilizoachwa, saa 9:00 usiku wa kuamkia Septemba 6 alimpigia simu mwandishi wetu na kumvurumishia matusi huku akisema akome kumfuatafuata akidai yeye hana mawasiliano na binti yake tangu mwaka 2007.
Mzee huyo alikwenda mbele zaidi kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwenye simu ya paparazi akitumia lugha ya Kiarabu ambapo kwa mujibu wa wataalam wa lugha hiyo ni dua ya kumwombea mabaya mwandishi huyo.
NZOWA AMZUNGUMZIA
Ili kwenda mbele zaidi, mapaparazi wetu walikwenda ofisini kwa Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ili kutaka kujua kama amesikia lolote kuhusu Aisha Bui.
Alisema: Eee, kuna habari kama hiyo lakini si rasmi kwangu, bado nafuatilia Brazil ikiwa tayari nitawajulisha tu.
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Aisha kwenye mitandao, hasa Facebook, Instagram na Twitter bila mafanikio. Gazeti hili limemwachia ujumbe kwa kuamini kwamba akirudi hewani ataukuta na kujibu lakini wapi!
Mbwana Matumla.
UZUSHI WA MBWANA MATUMLA KUNASWA NA UNGA HISPANIA WAWASHANGAZA WENGI
Wiki iliyopita ilihitimika kwa redio moja kutangaza habari kwamba mmoja wa wanafamilia ya mzee Matumla, Mbwana Matumla amenaswa na unga nchini Hispania na kuwashangaza wengi.
Watu waliozungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki walisema kwamba walishangaa kusikia habari hiyo huku wakiwa wanamwona Mbwana mitaani.
“Sasa huyu kakamatwa Hispania huku tukiwa tunamwona mitaani, maana yake nini jamani? Alihoji msomaji wetu mmoja na kuongeza kwamba, yeye alikutana na bondia huyo siku tano nyuma.
Ijumaa Wikienda lilimsaka Mbwana kwa njia ya simu yake ya mkononi bila mafanikio, lakini lilipomtafuta kaka mtu, Rashid Matumla, Jumamosi iliyopita alisema Mbwana amejaa tele nyumbani kwake, Gongo la Mboto, Dar.
Imeandikwa na Shakoor Jongo, Hamida Hassan, Gladness Mallya, Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’.  

CHANZO; GLOBAL PUBLISHERS.

No comments:

Post a Comment