Saturday, September 7, 2013
MWALIKO WA TAMASHA LA 32 LA SANAA TaSUBA 2013
Mwaliko wa Tamasha la 32 la Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania, Bagamoyo
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBa)
TAMASHA LA 32 LA SANAA NA UTAMADUNI WA MTANZANIA BAGAMOYO KUANZIA TAREHE 23 – 28 SEPTEMBA 2013
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo imekuwa na utaratibu wa kuandaa Tamasha la Sanaa na Utamaduni kila mwaka. TaSUBa ikishirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wanakuletea Tamasha la 32 la Sanaa na Utamaduni na litaadhimishwa kuanzia tarehe 23 – 28 Septemba hapa Bagamoyo. Tamasha
litafunguliwa tarehe 23 Septemba kuanzia saa 3:00 asubuhi na kufungwa tarehe 28 Septemba.
Kati ya shughuli zitakazofanyika ni pamoja na maonesho ya sanaa za jukwaani (Muziki, Ngoma, Maigizo, Vichekesho, Sarakasi n.k), maonesho ya sanaa za ufundi, warsha, semina na mafunzo mbalimbali kwa siku zote za tamasha pamoja na kongamano litakalojadili kaulimbiu Sanaa na Utamaduni katika kukuza Utalii .
Tamasha hili la kimataifa la sanaa na utamaduni wa Mtanzania ambalo linategemea kukusanya wasanii, wadau na watazamaji wapatao 3,500 kwa siku kutoka sehemu mbalimbali za ndani ya nchi pamoja na nchi za nje.
Hivyo tunawakaribisha wasanii, vikundi vya sanaa, ofisi za balozi, wadau katika sekta ya Sanaa, Utamaduni na Utalii, wananchi wote kwa ujumla, taasisi na mashirika mbalimbali kuhudhuria na kushiriki katika Tamasha hili.
KARIBUNI SANA.
Kwa mawasiliano zaidi;
Mtendaji Mkuu,
TaSUBa,
S.L.P 32
BAGAMOYO
Email: taasisisanaa@yahoo.com
Au piga Simu;
0715472745
0655850405
0754310425
0712683408
Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/09/mwaliko-wa-tamasha-la-32-la-sanaa-na-utamaduni-wa-mtanzania-bagamoyo.html#i
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment