Thursday, July 31, 2014

BUNGE LA KATIBA LAITISHWA,UKAWA WATIA MGOMO

                                                                     

         


mbowe_326e8.jpg
Bunge Maalumu la Katiba limeitishwa Agosti 5, mwaka huu, huku wajumbe wake wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiendelea na msimamo wao wa kutorejea bungeni hadi yatakapopatikana maridhiano ya msingi.
Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe jana, alisema kitakachowarudisha ndani ya Bunge hilo ni maridhiano ya msingi yatakayorejesha maoni ya wananchi kujadiliwa.
Mbowe alizungumzia msimamo huo wa Ukawa kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) alioutuma kwa mwandishi baada ya kutakiwa kueleza msimamo wa umoja huo kufuatia Bunge hilo kuitishwa.
"Hadi hatua ya sasa ninapoandika sms (ujumbe) hii, msimamo wetu Ukawa uko palepale. Hatutarejea Bunge la Katiba...Labda yawepo maridhiano ya msingi yatakayorejesha maoni ya wananchi kuheshimiwa kupitia Rasimu ya Katiba ya Tume ya Warioba na siyo vinginevyo," alisema Mbowe.(E.L)

No comments:

Post a Comment