Thursday, July 31, 2014

MAZINGIRA WAZINDUA TOVUTI YA MABADILIKO YA TABIA NCHI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira  Dk.Binilith Mahenge akizindua rasmi tovuti ya mabadiliko ya tabianchi itakayotumika kutoa taarifa mbalimbali za utunzaji wa Mazingira.Kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dk. Julius Ningu.
 

SERIKALI kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, leo imezindua tovuti ya mabadiliko ya tabia nchi.

Akizindua tovuti hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira  Dk.Binilith Mahenge amesema mbali na mambo mengine lakini itakuwa ikitoa habari mbalimbali za masuala ya madiliko ya tabia nchi lakini pia itakuwa ikitoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo ya tabia nchi.

Katika hotuba yake fupi ya uzinduzi wa tovuti hiyo, aliyoandaliwa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark, Mhenge amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi huangaliwa kwa muda wa miaka 30 hivyo kwa kipindi hiki chote kumekuwa na madhara mengi yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia Nchi ikiwa ongezeko la joto, kina cha bahari kuongezeka pamoja na ongezeko la majanga ya mvua zisizo na viwango,  kutoka na shughuli za binadamu katika uzalishaji hasa viwanda vikubwa

Alisema kwa tovuti inayozinduliwa ina umuhimu mkubwa kwani inaelezea maeneo ya hali ya mabadiliko ya tabia  nchi na juhudi za serikali katika kukabiliana na athari zinazoletwa na mabadiliko hayo.

“ziko sababu za kuungana na wenzetu ili kuondoa      tatizo hili la mabadiliko ya nchi ambapo tovuti hii www.climatechange.go.tz inatuunganisha na tovuti mbali mbali katika kupunguza gesi joto hapanchini pia inaelezea fursa zilizopo katika miradi na program mbali mbali. Alisisitiza”

Alibaini kuwa tovuti hii itachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uelewa na weledi kuhusu mabadiliko ya tabia  nchi nchini kwa wananchi na wadau kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment