Tuesday, February 28, 2012

MAKOCHA POULSEN (TAIFA STARS), ANGELS (MAMBAS)

Makocha Jan Poulsen wa Tanzania (Taifa Stars) na Gert Josef Angels wa Msumbiji (Mambas) kesho (Februari 28 mwaka huu) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya timu zao. Taifa Stars na Mambas zitapambana Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni katika mechi ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini. Mkutano huo na waandishi wa habari ambapo makocha hao pia watajibu maswali ya waandishi wa habari utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Mambas iliwasili nchini jana (Februari 26 mwaka huu) ikiwa na wachezaji 19 na viongozi kumi. Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho ni Francisco Muchanga, Clesio Bauque, Almiro Lobo, Manuel Fernandes na Francisco Massinga. Wengine ni Joao Rafael, Nelson Longomate, Joao Mazive, Zainadine Chavango, Osvaldo Sunde, Luis Vaz, Carlos Chimomole, Joao Aguiar, Edson Sitoe, Jeremias Sitoe, Stelio Ernesto, Elias Pelembe, Eduardo Jumisse na Simao Mate. 

MECHI YA YANGA, ZAMALEK KUCHEZWA SAA 12

Mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Zamalek na Yanga itachezwa Machi 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jeshi jijini Cairo kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Misri. Kwa mujibu wa maelekezo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mechi hiyo itachezwa bila washabiki  kwa vile Zamalek inakabiliwa na adhabu ya kucheza mechi hiyo bila washabiki. Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco ambao ni Jihed Redouane, Rouani Bouazza na Bekkali Mimoun wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Gihed Greisha wa Misri. Kamishna wa mchezo huo ni Ben Khadiga wa Tunisia. 

 WASOMALI KUCHEZESHA SIMBA, KIYOVU

Mwamuzi i Yabarow Hagi Wiish na wasaidizi wake Aweis Ahmed Nur na Abdirahman Omar Abdi, wote kutoka Somalia ndiyo watakaochezesha mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Kiyovu Sport ya Rwanda. Kwa mujibu wa orodha ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), mwamuzi wa akiba kati mechi hiyo namba 14 itakayochezwa Machi 4 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam atakuwa Waziri Sheha wa Tanzania.  Kamishna wa mechi hiyo ya raundi ya awali atakuwa Jean Marie V. Hicuburundi kutoka Burundi.  CAF imeziingiza moja kwa moja kati raundi ya kwanza timu 16 kutokana na ubora wake. Timu hizo ni ES Setif (Algeria), Interclube (Angola), Asec Mimosas (Ivory Coast), Enppi (Misri), AS Real Bamako (Mali), CO de Bamako (Mali) na CO Meknes (Morocco). Nyingine ni WAC (Morocco), Warri Wolves (Nigeria), Heartland (Nigeria), St. Eloi Lupopo (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Us Tshinkunku (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Amal Otbara (Sudan), Al Ahly Shandy (Sudan), CSS (Tunisia) na CA (Tunisia).

No comments:

Post a Comment