Thursday, February 23, 2012

Pinda ziarani Meatu


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akialimana na Wananchi wa  na viongozi wa wilaya ya Meatu baada ya kuwasili katika kijiji cha Mwandoya akiwa katika ziara ya Mkoa wa Shinyanga Februari 22, 2012.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Ally Nasoro Rufunga na  wapili kushotoni  Mkuu wa Wilaya ya Meatu Abihudi Saideya.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Afisa Biashara wa  Wilaya ya Bariadi, Leonard   Batigashaga akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Febeuari 22, 2012. Kulia ni Mkewe Tunu.
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina ikoa katika hatari ya kuvunjwa kwa vile imejengwa kwenye eneo la akiba la barabara. Picha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akionyeshwa  na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Nasoro Rufunga alama inayoonyesha  sehemu ya ukuta wa ofisi hiyo unatakiwa kuvunjwa. Nyumba hiyo imejengwa kwenye kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu.

No comments:

Post a Comment