Monday, January 30, 2012

GABON YASONGA MBELE ROBO FAINALI

Gabon ilifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2 katika dakika ya mwisho, ilipocheza dhidi ya Morocco siku ya Ijumaa, na kufuzu kuingia robo fainali katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Mechi hiyo ilichezewa mjini Libreville.
Kwa muda mrefu, Morocco ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 katika mchezo huo, bao ambalo lilikuwa limepatikana kupitia nahodha Houssine Kharjah katika kipindi cha kwanza.
Lakini kupitia magoli ya Pierre-Emerick Aubameyang na Daniel Cousin, wenyeji Gabon waliweza kuongoza, hadi mkwaju wa Kharjah ulipoiwezesha Morocco kupata nafasi ya kwanza, na ilielekea mechi itaishia kwa sare ya 2-2.
Lakini Morocco walipoadhibiwa kwa kucheza vibaya, Bruno Zita Mbanangoye alipiga mkwaju kwa ufundi mkubwa, na mpira ulipinda hadi kuingia wavuni, na bao hilo la wakati wa majeruhi likawa ndio kwaheri kwa timu ya Morocco.
Gabon sasa inajiunga na wenyeji wenzao Equatorial Guinea, katika hatua ya robo fainali.
Equatorial Guinea walifanikiwa kuiondoa Senegal siku ya Jumatano, taifa ambalo lilitazamiwa na wengi kuwa miongoni mwa nchi ambazo zilikuwa katika nafasi nzuri ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mwaka huu.
Katika mechi ya awali siku ya Ijumaa, ambayo pia ilichezewa mjini Libreville, Niger iliondolewa na Tunisia, kwa kufungwa magoli 2-1.
Hata hivyo Niger ilikuwa bado na matumaini ya kusonga mbele, ikitazamia Morocco kuwafanyia kazi yao, kama ingeliweza kuishinda Gabon.
Lakini hayo hayakuwezekana, na hivyo basi Niger inajiunga na Morocco katika safari ya kurudi nyumbani.
Mechi za Jumamosi pia zinatazamiwa kuwa za kusisimua, wakati Botswana itakapokutana na Guinea, na Ghana nayo itacheza na Mali.
Mechi zote mbili ni za kundi D, na zote zitachezewa mjini Franceville.

               chanzo kamanda wa matukio

WEMA AMZODOA DIAMOND MCHANA KWEUPEE..!!

Hatimaye mrembo na msanii Wema Sepetu, ameweka wazi kuwa hataki tena kutembea na masharobaro kwani mapenzi yao yanakuwa hayana malengo zaidi ya kuchezeana.

Akizungumza hivi karibuni msanii huyu alisema kuwa msanii anayemfananisha na sharobaro ni aliyekuwa mpenzi wake
Nassib Abdul ‘Diamond’, kwani endapo angekuwa hayuko hivyo basi anaamini mapenzi yao yangedumu kwa muda mrefu.

Alisema kwa sasa anahitaji kutoka na mwanaume aliyemzidi umri kwani anaamini watu hao wanakuwa na mapenzi ya dhati tena hawana wivu kama watoto wadogo ambao muda wote hupenda kuwa karibu na wapenzi wao badala ya kufanya kazi.


“Kila kitu kina muelekeo wake, mapenzi yangu mimi na Diamond yangeweza kudumu lakini kutokana na usharobaro alionao ndiyo uliosababisha yote yaliyotokea, na ndiyo maana nasema kwamba ni bora kutembea na mwanaume aliyekuzidi umri mnaweza kufika mbali,”
alisema.

Msanii huyu alisema hata hivyo ni bora afunge ndoa na mwanaume atakayempata ambaye anajua maana ya mapenzi kuliko kutembea na vijana wadogo ambao hawajui nini maana ya mapenzi na hawana muelekeo wa maisha.
 
                                               chanzo unique entertainment

SERENGETI LAGER YAZINDUA NEMBO YENYE MUONEKANO MPYA WA DHAHABU, LAKINI BURUDANI ILEILE.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko B. Joyce Mapunjo katikati akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Kampuni ya bia ya Serengeti mara baada ya kuzindua rasmi bia ya Serengeti katika muonekano wa Dhahabu, uzinduzi uliofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam na kuhudguriwa na wadau mbalimbali na wageni waalikwa.
Kutoka kulia ni Emilian Rwejuna meneja masoko (SBL) Mark Tyro Mkurugenzi wa Usambazaji, Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko, Mgeni rasmi Katibu Mkuu Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo, Mkurugenzi mtendaji wa (SBL) Richard Wells na kushoto ni Zohra Moore Meneja wa Huduma IPP wakipozi kwa picha huku wakiwa wameshikilia chupa mpya ya Serengeti Lager iliyo katika muonekano wa Dhahabu
Chupa mpya ya Serengeti Lager yenye muonekano wa wa Dhahabu ikiibuka kutoka katika maji mara baada ya kuzinduliwa rasmi jana usiku.
Shamrashamra zikiendelea wakati nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager ikizinduliwa jana.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko B. Joyce Mapunjo akizungumza katika uzinduzi huo
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza katika uzinduzi huo wakati alipomkaribisha mgeni rasmi.
Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti akizungumzia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika taifa kupitia bia ya Serengeti Lager.
Mark Tyror Mkurugenzi wa Usambazaji kulia na Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti wakionyesha nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager.
Mkurugenzi wa Usambazaji Mark Tyro kushoto akipozi kwa picha na marafiki zake Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells, Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti na Mwisho ni Meneja wa Mahusiano kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela
 
Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti akiongea na mkurugenzi wa Extra Bongo Kamalade Ali Choki , kulia ni Meneja Masoko wa (SBL) Emilian Rwejuna.
Hapa mzuka ukapanda kidogo lakini yote ilikuwa burudani na uzinduzi wa muonekano wa Dhahabu katika burudani ileile ya Serengeti Lager.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Kikundi cha ngoma za asili kikitoa burudani katika uzinduzi huo.
Dada Ritah Mchaki meneja wa bia ya Tusker katikati akipozi na wadau kutoka kampuni ya bia ya Serengeti hebu wacheki pozi lao.
Mdau Bahati Singh kutoka kampuni ya bia ya Serengeti yeye ilikuwa mishemishe tu ili kuhakikisha mambo ya uzinduzi yanakwenda sawa.
Mikakati ikipangwa hapa Meneja wa kiinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo katikati anaonekana akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Richard Wells kushoto, huku akimsikiliza pamoja na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Emilian Rwejuna kulia.
Rapa mahili wa Extra Bongo Maarufu kama Furgason akighani huku akmsikilizia mnenguaji mahiri wa bendi hiyo Aisha Madinda wakati alipokuwa akicheza.
Huo ndiyo muonekano wa dhahabu wenyewe kama unavyoonekana.
Wanenguaji wa bendi ya Extra Bongo wakifanya vitu vyao jukwaani.
Wadau kutoka R$R wakiwajibika kazini.
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo

DK HARRISON MWAKYEMBE AIBUKIA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA KAWE

Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lilloko Kawe Tanganyika Pakers akimkaribisha Dk Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na Naibu Waziri wa Ujenzi katika ibada iliyofanyika jana kwenye kanisa hilo na kuhudhuriwa na Waziri wa Afrika Mashariki mzee Samwel Sitta na baadhi ya wabunge kadhaa, Mzee Samwel Sitta amesema Mwakyembe amekwenda kanisani hapo ili kutoa ushuhuda kuhusu ugonjwa wake kwa ujumla ambapo FULLSHANGWE ilishuhudia tukio hilo. Dk. Harrison Mwakyembe ametoa ushuhuda akimshukuru mungu kwa kumbariki na kuendelea kumpa nguvu juu ya afya njema, Mwakyembe ambaye alikuwa amevalia kofia na Glovu katika mikono yake, ameongeza kwamba tangu alipokuwa ameondoka kwenda nchini India kwa matibabu Oktoba 9 mwaka jana hakuwahi kuvaa viatu, lakini leo amevaa, hivyo akamshukuru mungu kwa miujiza yake.
Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akiongea katika ibada hiyo na kumkaribisha Dk Harrison Mwakyembe ili kuzungumza machache na waumini wa kanisa hilo na kutoa ushuhuda wake.
Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli kushoto , akizungumza na Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa ibada hiyo jana.
Dk Harrison Mwakyembe akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo jana.
Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada jana.
Dk. Harrison Mwakyembe wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge, kushoto ni Mbunge wa Same Mashariki Mama Anne Kilango Malecela, Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta na Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli.
Mchungaji Maximilian Machumu wa kanisa la Ufufuo na Uzima akiwa katika ibada hiyo jana.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakitawanyika baada ya kumalizika kwa ibada hiyo jana huko Kawe jijini Dar es salaam.

JENGO JIPYA LA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) ADDIS ABABA.

Jengo jipya la Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) lililozinduliwa leo na Rais wa China Bw Hu Jintao jijini Addis Ababa leo January 29,2012 Jengo hilo, ambgalo limegharimu dola milioni za Kimarekani, limejengwa kwa udhamini wa China (PICHA NA IKULU)

TWIGA STARS YAICHAPA NAMIBIA MAGOLI 5-2 UWANJA WA TAIFA

Mchezaji Mwanahamisi Omari a.k.a Gaucho akihojiwa na mwandishi wa habari wa BBC Eric David Nampesya baada ya kumalizika kwa mpira kati ya Twiga Stars na Namibia , Mwanahamis Omari 'Gaucho' ni mfungaji pekee wa mabao 2 kati ya 5 ya Twiga, katika mchezo wa kutafuta kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake, zinazotarajia kufanyika mwezi Juni mwaka huu.
Mchezo huo umemalizika muda mchache katika uwanja wa Taifa.
Mabao ya Twiga yalifungwa na Mwnahamisi Omar katika dakika 21, Asha Rashid 'Mwalala', bao la pili dakika 46, bao la tatu Etoe Mlenzi, dakika ya 84, Asha Rashid,bao la nne dakika ya 88, na bao la tano, likifungwa tena na Mwanahamis, dakika ya 90. Mabao ya Namibia mawili ya yamefungwa na Beki wa Twiga, Etoe, aliyejifunga dakika ya 29 na bao la pili likifungwa na Juliana Skrywer, dakika 73.
Kwa matokeo hayo sasa Twiga Stars inatarajia kukutana na mshindi kati ya Misri au Ethiopia ambapo Misri ilikuwa inaongoza kwa mabao 4-2 dhidi ya Ethiopia.
Mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars Asha Rashid akimtoka beki wa timu ya taifa ya Namibia ya wanawakeLovisa Mulunga, katika mchezo wa kuwania fainali za kombe la dunia kwa wanawake unaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii,
Wachezaji wa Twiga Stars wakishagilia mara baada ya mchezaji wa timu hiyo Asha Rashid kufunga goli la pili katika kipindi cha pili.
Mashabiki wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mpambano huo kwenye uwanja wa Taifa.

Monday, January 16, 2012

SIMBA NA TUSKER YA KENYA


Mshambuliaji wa Simba akichuana na kiungo wa timu ya Tusker ya Kenya, Joseph Mbugi wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika jana Kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1.

Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu akipata matibabu baada ya kuumia.

Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu akichuana na beki wa Tusker ya Kenya, Brian Mandela

Timu ya Tusker ya Kenya
Timu ya Simba ya Tanzania

ILIMANJARO PREMIUM LAGER NA BASATA WAZINDUA RASMI MCHAKATO WA TUNZO ZA MUZIKI TANZANIA 2012(KILI MUSIC AWARDS).


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) leo wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kuwa tunza wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri kupitia kazi zao za Muziki kwa mwaka wa 2012.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam meneja wa bia ya Kilimanjaro bwana George Kavishe alisema Mwaka jana Tunzo hizi za Muziki nchini Tanzania zilifanyiwa mabadiliko makubwa ambayo kwa mwaka huu yataendelezwa na kuboreshwa zaidi. Ambapo Mchakato wa kuwapata vinara hao utapitia hatua kuu zifuatazo:
1. ACADEMY:
ACADEMY ya Tunzo za Muziki Tanzania ni mkusanyiko wa wadau wa muziki kati ya hamsini hadi mia moja( 50 mpaka 100)kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambao huwekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua na hatimae kupata wateule (Nominees) wa kinyang’anyiro hicho baada ya majaji kujiridhisha kuwa washiriki waliopendekezwa wamekizi vigezo vyote muhimu ambapo zoezi hili kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika tarehe 27 na 28 Jan 2012.
2. Majaji:
Hatua ya pili ni Majaji ambapo huwa ni hatua muhimu sana ambapo majaji huwa na kazi moja kubwa ya kupiga kura wakizingatia vigezo muhimu vya kiufundi zaidi na vile vile kuhakiki uteuzi wa washiriki uliofanywa katika hatua ya awali kwenye Academy husika ikiwa ni pamoja na kura zitakazopigwa na wananchi. Wao hutumia zaidi vigezo halali vinavyopatikana na mkusanyiko wa rekodi za wasanii zilizotoka kwa mwaka 2011, kazi zao za mwaka 2011, Mafanikio n.k. Jopo hili hujumuisha wadau wa tasnia ya musiki kumi na tano (15).
3. KURA:
Hii ni ni hatua ya mwisho ambapo wapenzi wa musiki waliopiga kura zao Kura hizo hujumuishwa katika kuchangua washindi ambapo kwa shindano la mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitabeba asilimia sabini (70%) na kura za majaji asilimia thelasini (30%.) na katika kufanikisha upigaji kura kutakuwa njia kuu Njia kuu nne za upigaji wa kura :
  • Njia ya ujumbe mfupi (sms).
  • Njia ya barua pepe (Email).
  • Njia ya kujaza sehemu maalum katika Magazeti.
  • Na njia ya mwisho ni njia ya vipeperushi (Fliers.)
Kwa upande wake mwakilishi wa baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Mzee Luhaja amewataka wasanii wa tasnia hiyo nchini kutumia vyema fursa ya tunzo za Kili Music Award kama sehemu ya kuweza kujitangaza katika anga za muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
Alisema msanii mzuri ni Yule anaeweza kutunga nyimbo zenye lengo la kuelimisha jamii na kuburudisha kwa kuzingatia maadili na hayo hujidhihirisha kupitia kwenye tunzo kama hizi ambazo hutoa fursa kwa wasikilizaji kutoa michango yao juu ya mwanamuziki gani aliyeweza kukonga mioyo yao kupitia tungo zake.

Mkuu wa Mkoa DSM (kulia) Sadick Mecky apokea msaada wa waathirika wa mafuriko


Mkuu wa Mkoa wa DSM Sadick Mecky Sadick (kulia) akipokea leo rasmi msaada kupitia kivuli kinachoonyesha vitu mbalimbali na thamani kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara wa kichina Tanzania ZHU JINFENG (katikati) kwaajili ya waathirika wa mafuriko jijini , Msaada huo umekabidhiwa jana kwa Makamu wa Rais Dkt, Gharib Bilal wakati wa sherehe za maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina wenye thamani ya shilingi milioni10. Pamoja na kukabidhi jan 15,2012 lakini leo wamewasilisha rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa DSM Meck Sadick jumla ya milioni 12.5 baada ya kuendelea kuchangia vitu vyengine vikiwemo mabati na saruji, (kushoto) Ni Mmoja wa ofisa kutoka chama cha wafanyabiashara wa kichina nchini Janson Huang . Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Mkuu wa Mkoa wa DSM Said Mecky Sadick (kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Fadhili Manongi (kushoto) leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM kwaajili ya waathirika wa mafuriko wa mkoa wa Da r es Salaam (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO),
Mkuu wa Mkoa DSM (kulia) Sadick Mecky (katikati) Ofisa kutoka chama cha wafanyabiashara wa kichina nchini Janson Huang pamoja na Katibu tawala wa Mkoa wa DSM Theresia Mmbando (kushoto) wakijadiliana leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM baada ya kukabidhi rasmi msaada huo wa kivuli cha mchango wenyethamani ya shilingi milioni 10 ambapo michango hiyo imeongezeka hadi kufikia 12.5/- (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).