Sunday, January 15, 2012

SOFT LAUNCHING YA SKYREAD HOTEL YA BAGAMOYO KWENYE PICHA

 Wageni waalikwa wakiwa kwenye eneo la mgahawa wa hoteli ya Skyread iliyopo mjini Bagamoyo mkoani Pwani, mara baada ya kupokelewa hotelini hapo kwenye hafla ya uzinduzi mdogo iliyofanyika siku ya Ijumaa tarehe 13.01.2012
Bw,Eden Tetee akitoa neno la kubariki shughili ili iweze kuanza.
Bibi Salum Shariff mfanyabiashara maarufu mjini Bagamoyo (alivaa nguo ya pinki) akiwa mmoja wa wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Meja generali Meela mwenye kofia akiwa mmoja kati ya wageni mashuhuri waliyohudhuria hafla hiyo.
Bw. Chrispine Meela akitoa salamu za Skyread kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi
Mzee Ephafla Ezra Tetee(mwenye miwani) mmiliki wa hoteli ya Skyread akifurahia jambo na mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Free voice Investiment ltd Bw.Albert Kawago(mwenye glasi) wakati hafla ikiendelea.Picha ya juu mzee Tetee akikaribisha wageni aalikwa.
Wageni waalikwa wakiburudika kwa kwaito lililokuwa likiporomoshwa na dj Rama wa kampuni ya Kimkev Entertainment iliyoendesha hafla hiyo.
Wafanyakazi wa hoteli ya Skyread wakiaandaa maanjumati.
Bi Elizabeth Chawinga meneja wa benki ya N.M.B tawi la Bagamoyo akiwapungia wageni waalikwa akiwa na mzee Tetee kulia
Wageni waalikwa walipopata nafasi ya kujua mandhari ya ndani ya ndani ya hoteli ya Skyread.
Huu ulikuwa wakati mmiliki wa hoteli mzee Tetee akiwa na bi Shumina mtaalamu wa keki na mapambo alipokata keki ya siku ya kuzaliwa kwake ambapo alitimiza miaka 74  sambamba na uzinduzi mdogo wa hoteli ya Syread.Blog ya hii inakutakia kila la heri mzee Tetee
                                                                                                                                                      

No comments:

Post a Comment