Hii ndio hali halisi ya mafuriko yaliyotokea jana jijini Dar es Salaam na kuathiri kwa kiasi kikubwa wakazi wa Mabondeni hasa maoneo ya Jangwani, Mto Msimbazi na bonde la Mpunga kule Msasani. Pia Mvua hizo zilisababisha kuharibika kwa miundombinu kadhaa ya barabnara, maji, na umeme katika maeneo ya jijini la da es Salaam.
Hivi ndivyo hali halisi ilivyokuwa kwa eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam ambapo nyumba zilizopo katika mkondo huo wa maji zilifunikwa kwa maji na kusababisha watu kukosa makazi.
Wakazi wa magomeni wakishangaa mafuriko hayo katika barabara ya morogoro eneo la Jangwani.
Hii ni yard ya Kajima pale Janwani.
Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ilifunikwa kabisa na maji kama inavyoonekana pichani na kufungwa kwa saa kadhaa. hali haikuwa nziri. Serikali mara kadhaa ilikuwa ikihamasisha watu kuhama katika maeneo ya mabondeni kama haya lakini wananchi mara zote walikuwa wakaidi na matokeo yake ni kama haya. mamlaka ya Hali ya hewa inasema mvua hizo zimevunja rekodi. Lakini wapo watu waliodai kuwa mara ya miwosho kuona mafuriko kama hayo jijini Dar es salaam ni miaka ya 50.
No comments:
Post a Comment