Monday, December 5, 2011

MBUNGE VITI MAALUM VICK KAMATA AZINDUA FILAMU YA MR PRESIDENT


Mbunge wa Viti Maalum CCM ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Filamu ya Mpya ya Mr. President, Vicky Kimata akionyesha baadhi ya cd za filamu hiyo mara baada ya kuizindua rasmi na kuanza kuiuza kwa mnada.Wasanii wa Filamu nchini,Ray,Steve Nyerere na JB wakitoa burudani katika uzinduzi huo. ZAIDI ya Milioni 18 zimekusanywa kwenye uzinduzi wa filamu ya Mr President uliofanyika kwenye ukumbi wa Serena hoteli zamani Moven Pick usiku wa juzi. Fedha hizo ambazo asilimia 20 zitaelekezwa kwenye hospitali ya Mwananyamala kusaidia Wodi za Wanawake na Watoto zimepatikana kwa njia ya mnada wa CD za filamu hiyo inayoonyesha maisha halisi ya Rais Jakaya Kikwete. Katika mnada huo vibopa na wasanii mbali mbali nchini walijitoza kununua Cd hizo kwa njia ya mnada ambapo wasanii kama JB, Ray walijitosa kunua CD hiyo kwa shilingi 200,000 wakati mratibu wa Miss Tanzania Hashimu Lundenga alijitosa kwa kununua CD hiyo kwa shilingi 300,000. Funika bovu ilikuwa kwa wafanyabiashara maarufu hapa nchini ambao walinunua Cd hiyo kwa Shilingi Milioni 1,000,000 mpaka Shilingi milioni 5.5 wakiongozwa na kundi la Freinds of Simba na wale wa Yanga Family. Awali akizindua filamu hiyo mbunge wa Viti Maalum CCM ambaye alikuwa mgeni rasmi Mwambata, Vicky Kimata alisema ni muda muafaka kwa wasanii kuungana na kuwa na umoja ili waweze kushinda vita ya maharamia wa kazi zao. "Kuna sheria mpya ya haki miliki itatungwa na Bunge ili kulinda kazi za wasanii kutokana na kuibiwa kazi zao muda mrefu,hii itakuwa na nguvu kuliko ile ya mwaka 99 ambayo imepitwa na wakati,"alisema. Kamata Alisema sanaa ni kazi nzuri ambayo imekuwa ikiwasaidia wasanii wa nje kuishi maisha mazuri, lakini pia kufanya maendeleo katika maisha yao,tofauti na hapa nchini wasanii wamekuwa ndio mafukara wa kutupwa huku watu wachache wakinufaika na kazi zao . Vick Kamata amezindua filamu hiyo kwa niaba ya Waziri Mathias Chikawe ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo amabye hata hivyo hakuudhuria huku awali kampuni ya Papa-Z ambao ndio waandaaji wa filamu hiyo walitangaza kuwa Rais wa awamu ya tatu Ali Hassan Mwinyi ndio atakuwa mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment